Sunday 30 September 2012

Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!

Mbilinyi, tuache siasa za kufanya dharau kwa amiri jeshi Mkuu wa nchi yetu aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi walio wengi! Tumpeni heshima yake tafadhali. Kama tumeshindwa kujadili hoja kwa heshima na taadhima basi tuache tu siyo kumtukana na kumdhalilisha JK kwa kuwa ni mpole na rahim!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Gaston Mbilinyi <mbilinyi.gaston49@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 30 Sep 2012 08:06:23 +0300
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!

HK,

Mimi nafikiri tumpe JK miaka mingine mitano au zaidi ya kuiongoza Tz maana ni kichwa au jembe zaidi ya Zitto aliye zaidi ya wote walio CDM na wote ndani ya ccm. Sijui hilo unalionaje? 

Pengine ni vema nikukumbushe tu kuwa urais ni taasisi ambamo kuna yote, majembe; visu; vichwa; n.k. Ndio maana hata wewe wakati mwingine umeshuhudia mkorogano kati ya JK na Pinda au Katibu Mkuu Kiongozi au n.k.

Kwahiyo CDM hata tungemweka Ikulu Mh. Nassari au Zitto unayempenda kiushabiki wako mambo bado yataenda kwani hatakuwa peke yake kama ambavyo hatakuwa peke yake Zitto wako! Kama ameweza JK nani ataishindwa Ikulu?

On Saturday, September 29, 2012, wrote:
Nimefurahi kuona kauli ya Zitto imewaibua wachambuzi makini na ninaowaheshimu kama akina Bart, Kunyaranyara na Mgamba kuchangia.

I endorse Zitto si kwa sbb nyingine yoyote ile, wala si kwa sbb ni scholar mwenzangu wa Livingstone, ama ni mwenye historia ya kupitia students politics kama mimi, ni kwa sbb ninaamini ana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo nafahamu kuna wengine mnamchukia kwa kuwa anawashinda uwezo watu mnaowataka ndani ya CDM na ndiyo maana mnaona kama anajivuna kwa kuwa ni maarufu kwa kutangaza nia yake mapema! Tukisema ukweli, Zitto ana akili sana kuliko wengi tu ndani ya CDM na yuko objective ila CDM hakuna demokrasia (jambo ambalo limewakimbiza wengi kutka CCM) kumbe bahati mbaya sana hata huko walikokimbilia NCCR (Kafulila), CUF (Hamad Rashid), CDM (Wangwe, Zitto na yule BAWACHA mama simkumbuki jina) hakuna demokrasia, inakuwa bora wangebaki tu huku huku CCM...!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
Date: Sat, 29 Sep 2012 02:40:19 -0700 (PDT)
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!

Nashukuru Mganda,
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa miaka 20 ni mingi.
 
Uchanga wa CHADEMA haupo katika umri wa tangu kuandikishwa mpaka sasa bali upo katika utendaji kazi wa chama chenyewe kama taasisi kuu inayojengwa na taasisi ndogondogo ndani yake. Vyama vingi vya upinzani Tanzania, licha ya kuandikishwa na kuruhusiwa kuanza kufanya kazi, kwa miaka mingi havikuweza kufanya kazi kama vyama. Hiyo, kwanza ilichangiwa na mazingira magumu waliyowekewa na CCM na serikali, na pili ni matatizo ya ndani ya vyama vyenyewe ambapo vingi viliendeshwa kama vikundi vya shughuli binafsi.
 
Ni kutokana na uchanga huo, ndiyo maana baadhi ya waanzilishi wa vyama hivi , mpaka leo, bado wanaviona kama ni mali zao ambapo kila mmoja ana hisa zake, na hivyo anaweza kuziondoa wakati anapotaka. Nimewahi kumsikia hata Zitto, mara kadhaa akisema kuwa yeye ni kati ya waanzilishi wa CHADEMA, na kuna wakati akiwataja wengine waliokuja baadaye. Hakusema kama wazi kama hiyo kuwa mwanachama mwanzilishi na mwanachama 'wa kuja' inakuwa na utofauti gani katika haki za uwanachama lakini ukimsikiliza kwa makini utaelewa anataka kusema nini. Huo ndiyo ninauita uchanga wa chama kama taasisi, ambapo watu bado wanakiona chama kwa sura za watu.
 
Miaka kadhaa iliyopita tulimwona Bwana Lyatonga akiingia na kutoka katika vyama kadhaa na kundi lake la watu. Kwenye hali hiyo, ni kwamba wale hawakuwa wanachama wa vyama bali wanachama wa Lyatonga.
 
Bart

From: RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, September 29, 2012 10:57 AM
Subject: Re: [wanabidii] ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Bart,

Kwanza karibu, maana umepotea sana. Chadema kina miaka 20 sasa tangu kisajiliwe rasmi mwaka 1992, na ninadhani kimeanza kukomaa. Kuna hatari pia ya chama kuwa kikongwe sana eti kikikua na kukomaa—kwani mwishowe huwa sugu kama KANU, CCM na vinginevyo.

<

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment