Friday 28 September 2012

Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Wanabidii,
Zipo hoja "ngumu" na zipo "laini"...kama mnataka zitumike nguvu, kama baadhi ya wachangiaji hapa; nadhani hakuna haja ya DEMOKRASIA au tutumie DEMOKRASIA YA KIJESHI. Kama mnapiga debe la "demokrasia" na watu waamue hatma yao, nadhani ni muafaka kuwapa watu UHURU, HAKI na USAWA katika kuamua hatma yao. Mifano ya uvamizi wa Kimarekani (kwa mtindo wa ki-cowboy) na mauwaji ya watu na kuteka maeneo yao si tu ni USHENZI bali pia ni UWENDAWAZIMU uliyopita mipaka.
 
Binadamu hawezi kuongozwa na ROHO YA UVAMIZI na uuwaji wa watu katika kuwakalia watu wengine; kama USHENZI wa aina hii utaruhusiwa DUNIA ITAGEUZWA uwanja wa harakati za KINYAMA na mateso ya kiakili na kimwili kwa watu wasiye na satwa (nguvu) za kujilinda. Hatuwezi kuruhusu nadharia ya SURVIVAL FOR THE FITTEST kama mwendo wa kuendesha siasa na memejimenti ya dunia. Hatuwezi, narudia; hatuwezi kuwa na maisha yenye staha na yanayozingatia kanuni ya utawala wa watu kama tutaacha kuwauliza watu nini wanataka. Lazima tukubali, kwamba binadamu lazima aishi kwa mujibu wa UTASHI wa kimaumbile bila ya kuvunja SHERIA, KANUNI na TARATIBU zinazokubaliana na maumbile. anamoishi
 
Zanzibar, lazima tukubali (hata tusipokubali) ni nchi na itabaki kuwa nchi; na Tanganyika ni nchi vilevile. Kama leo kila mmoja anataka demokrasia (sio DOMOKAYA) lazima awape watu UHURU, HAKI na USAWA katika kuamua hatma yao. Na wanodhani kwamba binadamu anaweza kulazimishwa akubali KUPIGA MAGOTI NA KUCHINJWA MBELE YA MTAWALA KATILI hii ni dhana ya muda mfupi; na si muda muda mrefu ujao hasira za watu zitaangukia mikononi mwa watawala wanaotumia nguvu kuwatawala watu wenye HAKI ya MAAMUZI kama watu huru. Sidhani kama ni sahihi kuchukua mifano ya USHENZI wa kuwavamia watu waliyeamua kuishi "watakavyo" na kuwatweza nguvu na kuwatawala...ati leo wanaitwa ndio "machampioni wa demokrasia",...EBO! Nani kasema [?]...na ni nani awezaye kudhani kwamba leo (wakati huu) kwamba watu wanaweza kuwaacha watu wachache wawaamulie wengi ati tu kwa vile wanatumia nguvu za kijeshi katika kutawala...[?]. Kama si USHENZI; huu ni nini?
 
Hivi; tunaandika historia gani kwa zama hizi? Haikuwa zamani enzi za watawala washenzi na katili waliyotumia "mkono wa chuma" kuwalazimisha watu vile wapendavyo WASHENZI hata kwa kumwaga damu za wahanga wasiyekuwa na hatia ya kuuawa. Ati watawaliwe kwa nguvu [?] kana kwamba watu hao ni mazezeta! Haiwezekani; lazima tuwe waungwana na tuheshimu UHURU wa watu kuamua hatma yao. Kama ni hivi; kuna haja gani ya kuwa na sheria inayotaka watu washiriki katika kutoa maoni yao [?]...na kama hakuna haja ya kuwa na Katiba Mpya, kwa nini watumie fedha za walipa kodi kwa kazi isiyokuwa na tija kwa maendeleo ya watu na nchi yao? Hivi; tunafikiri kwa kutumia nini? Vichwa au matumbo yetu [?] yaliyojaa UTUMBO?
 
Kama walivyo Wazanzibari, Watanganyika wana haki ya kudai nchi yao; na ni vema tuache UZEZETA na tutumie AKILI yenye kuongozwa na roho safi na UKWELI msadikivu juu ya kuona na kuchunguza maudhui ya MUUNGANO tangu awali. Hatusomi historia kwa kujifurahisha; na historia haisomwi kwa kukosa budi, lazima historia isomwe kwa matini na batini yake katika kutafuta UKWELI wa kindakikindaki katika kudadavua hoja zenye mashiko ya kitaaluma ili kwa UKWELI huo watu (wa sasa) waweze kujua yaliyopita kwa mustakabali wa siku zijazo. Hakuna FIKRA zinazoweza kudumu "milele" kama zilitokana na mtu au kikundi cha watu wenye "inda" na "taasubi" ya kuficha UKWELI wa kwa nini MUUNGANO ulikuwapo...na kwa nini ulifanywa HARAKA na watu WAWILI (NYERERE + KARUME) na ukafanya kafara (sacred) kana kwamba ni "AGANO LA MUNGU". Sidhani kama ni sahihi kudhani kwamba waliyounganisha nchi mbili walikuwa MALAIKA (au hata watu wasiyekuwa na dhambi - maasum)...wote walikuwa watu na kuna wakati waliongozwa na ROHO CHAFU pale walipokuwa wakiwauwa wenzao waliyewapinga kutokana na SERA KANDAMIZI dhidi ya demokrasia.
 
Hata kama; na kama baadhi ya watu wanavyotaka kutumia NGUVU dhidi ya wale wasiyoutaka muungano, bado wengi watashinda! Ushindi mara zote ni kwa wale wanaodhulumiwa, hata kama wanaodhulumu wataendeleza UBABE wa matumizi makubwa ya NGUVU za kijeshi na au kipolisi...mwisho, na kama ada; lazima hatma ya wale wote wanaokandamiza wengine ni TUMBO LA ARDHI na tumbo hilo ndilo linalowameza wote na hata kuwachukua wakati wenye wakitamani kuishi miaka mingi ili waendelee kutafuna NYAMA ZA WAHANGA na kufyonza (na kunyonya) DAMU ZA WATU...kama alivyosema Mwalimu Nyerere (yeye mwenyewe), "MTU AKIZOWEA KULA NYAMA ZA WATU HAACHI, ATAENDELEA KULA...." Kwa hivyo, kwa wale waliyozowea kuuwa watu na kuwalazimisha kutii utashi wao wa KISHENZI wanaweza kufanya hivyo, isipokuwa wajiulize suala hili: WAKO WAPI WALE WALIOKUWA WAKIWATESA NA KUWAUWA WENZAO? Nadhani majibu ni: (1) Wengi wameshakufa na kumezwa kwenye tumbo la ardhi; (2) Wengine wametweza nguvu na au kuuawa na wengine kwa mtindo uleule!
 
Tusizuwie FIKRA za kujitenga kwa vile HAKUNA (narudia, HAKUNA) awezaye kuzuwia kuvunjika kwa muungano! Kama uliweza kuvunjika MUUNGANO wa KISOVIET sueze huu wa TANGANYIKA na ZANZIBAR [?] sidhani; tukubali MUUNGANO uhojiwe na ikibidi UREKEBISHWE na uchukuwe sura ya watu wanavyotaka kwa UHURU, HAKI na USAWA tusilete dhana ya kutishana kwa kuwa VITISHO si sehemu ya UUNGWANA; na muungwana siku zote hutumia AKILI (ANGAVU), BUSARA na HEKIMA ya hali ya juu katika kufikia maamuzi yenye tija kwa manufaa ya watu wote. Hapa napenda nimalizie kwa maneno ya Marehemu Shaaban Robert alipoandika hivi:
 
"Majuju ni taifa lafi na litishalo kabisa. Kila kitu kigumu kijulikanacho duniani kilikuwa laini kama mkate kati ya meno ya majuju; na kilicho kichungu kilikuwa kitamu kama asali katika maonjo yao. Kwa ulafi uliokithiri viumbe hawa, walikuwa hawajui halali wala haramu."...........
  
........"Kabuli alipopelekwa mbele ya Jeta limkuta amekaa kitako midomo wazi. Mto mrefu na mpana ulikuwa ukimimika katika kinywa chake kikubwa sana. Tone la maji hata moja halikupata nafasi ya kukiepa kinywa hicho. Tani milioni moja za mwamba, milioni moja za chuma, milioni moja za magogo, na milioni nyingi za samaki zilimiminika pamoja na mkondo wa maji humo kinywani pia kila dakika tano. Lakini kila dakika moja Jeta alilia: Kiu, njaa, kiu, njaa!" (Kusadikika, 1991 ukurasa wa 23....., Mkuki na Nyota Publishers).
Tusiwe kama Majuju au Jeta wa KUADIKIKA; tutumie KIASI katika kufanya MAAMUZI yanayozingatia UHURU, HAKI na USAWA. Binadamu hupimwa kwa AKILI ya kibinadamu na si hawaa za kihayawani! Binadamu ni mtu si mangondi katu; binadamu anatakiwa atumie utu wake, aamue kwa dhati yake!
 
NAWASILISHA.
Bakari M Mohamed, BBA [PLM], CPSP [T], MSc (PSCM), Reg. PSP (AU 0005)
  1. Lecturer in Procurement and Supply Chain Management
  2. Procurement and Supply Chain Auditor
  3. Procurement and Supply Chain Specialist, Consultant, Researcher and Trainer in Procurement Contracts Management
  4. Doctor of Alternative Medicines [DAM] & Natural Healing Therapist
Department of Procurement and Logistics Management
Mzumbe University
Box 6
Tel (Office): + 255 23 2604381/3/4
Mobile      : + 255 713 593347

MZUMBE, Tanzania.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, September 27, 2012 8:50 PM
Subject: RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!

Ngupula,
Hakuna kuuvunja Muungano. Tutasumbuka zaidi. Tuujadili na kisha tuurekebishe. Huu ulalamishi usitupe shida.
Matinyi.
 
> Date: Thu, 27 Sep 2012 16:55:58 +0100
> From: ngupula@yahoo.co.uk
> Subject: Re: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
> yap.wabara hatukotayari tena kutoa even a single dot in the name ya kulinda muungano..hatutaki tena.Let the zanzibar go if they may want.
>
>
>
> ------------------------------
> On Thu, Sep 27, 2012 6:20 PM EEST Emmanuel Muganda wrote:
>
> >Dr. Mohamed,
> >Naamini wewe ni msomi wa historia. Unaweza kuniambia ni wapi, circa 1964
> >ambapo nchi ziliunganishwa kwa kura ya maoni? Wamarekani leo wanasifia
> >umoja wao lakini umezaliwa kwa ncha ya upanga. Wamarekani wahamiaji,
> >waliwasweka
> >kwenye maeneo ya reservation Wamarekani wa asili na kuchukua ardhi yao.
> >Isitoshe, California na Texas zilichukuliwa kwa mabavu kutoka Mexico. Kule
> >Hawaii, kisiwa kilivamiwa, mfalme akauawa na kisiwa kuchukuliwa chini ya
> >himaya ya Marekani. Lousiana na Alaska zilinunuliwa kwa fedha. Kwa hakika
> >Nyerere alikuwa muungwana sana. Baada ya kumsaidia Karume kumwondoa Sultani
> >na kumpa jeshi la ulinzi angeweza kukimeza kile kisiwa na historia
> >isingemhukumu. Lakini hakufanya hivyo. Leo tunasikia upupu huu wa muungano
> >wa mikataba na kura za maoni. Upuuzi mtupu. Tumechoshwa na malalamiko ya
> >Wazanzibari, wakati umefika, kama alivyosema ndugu Makundi, tuachane kwa
> >amani. Hata Malaysia na Singapore waliachana kwa amani tu.
> >em
> >
> >2012/9/27 Bakari Maligwa Mohamed <maligwa1968@yahoo.com>
> >
> >> Mobhare,
> >> Nadhani wewe ni muamini wa dini ya Kikiristo (samahani kwa kuanza hivi);
> >> na nadhani wewe ni muumini wa "ukweli" kwa kuwa kuamini KWELI ni UHURU
> >> (vilevile, nakuomba radhi kwa hili); na pia, nadhani wewe ni muumini wa
> >> sayansi ya UTAFITI inayotokana na MAARIFA, UJUZI na MAADILI ya kisomi
> >> (weled)i; kama NDIYO, naomba upime hoja hizi juu ya MUUNGANO WA TANGANYIKA
> >> na ZANZIBAR.
> >>
> >> MOJA, "muungano" huu ulizaliwa kwa SHINIKIZO lisilokuwa na shaka tangu
> >> awali (yaani, 1964) na ndio maana uliingiwa na watu WAWILI (Nyerere na
> >> Karume) na wawili hao walihakikisha kwamba HAWAPINGWI na wale
> >> waliowapinga aidha walipotezwa kisiasa na au WALIUAWA (rejea KIFO CHA
> >> ABDULLAH KASSIM HANGA na wengino wasiyetajika sana).
> >>
> >> PILI, Nyerere alimfunika Karume (kwenye siasa) kwa kutumia ujanja wa
> >> kuitumia Katiba ya Tanganyika kama "katiba ya mpito" ilikuwa mbinu mahsusi
> >> katika kuiweka rehani Zanzaibar kwenye "Mwavuli wa Tanganyika" na hivi
> >> ndivyo ilivyokuwa na baadaye kuchukua sura ya Zanzibar (kama nchi) ndani ya
> >> Tanganyika (inayoitwa Tanzania).
> >>
> >> TATU, katika kufanikisha mpango wa kuimeza kabisa Zanzibar ndani ya tumbo
> >> la Tanganyika (wengi wanaita Tanzania Bara) nchi iliingizwa kwenye mfumo wa
> >> "nchi ya chama kimoja" Julai, 1965 na miaka 12 baadaye TANU iliimeza ASP na
> >> kuanzisha Chama Cha Mapinduzi [CCM] ambayo kwa ujumla iliyameza "Mamlaka ya
> >> Zanzibar" kutoka "Kisiwandui" hadi Dodoma (Tanganyika) ambapo maamuzi yote
> >> ya Zanzibar yanafanywa Dodoma kwa utashi wa CCM-Tanganyika (Tanzania Bara).
> >>
> >> NNE, Mwalimu Nyerere (1965 hadi 1985) alijipa "nguvu" zote za "dola" na
> >> mamlaka ya kuwaamulia Wazanzibari nini kifanyike pasipokuwa na "domo la
> >> kusema" sio demokrasia; tazama, mifano ya kumuwajibisha Mzee Aboud Jumbe
> >> Mwinyi na hatimaye kuwafukuza wananchama 17 wa CCM kulikofanywa na Mwalimu
> >> Nyerere akiwafukuza akina Maalim Seif Sharif Hamad, Shaaban Mloo, Juma Duni
> >> Haji, Hamad Rashid Mohamed na wengineo.
> >>
> >> TANO, kama ni kweli (kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyotaka nchi iendeshwe);
> >> basi, uhakika ni kwamba Mwalimu Nyerere alitumia "udikteta" kuulazimisha
> >> "muungano" huku akiwatumia baadhi ya Wazanzibara (sio Wazanzibari)
> >> waliotengenezwa katika kufanikisha mpango mahsusi (specific) juu ya
> >> kuufanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika kuzuia "vuguvugu" la
> >> UKOMUNISTI (sio USOSHALISTI wa Nyerere) na ukiitazama historia ya
> >> kuanzishwa kwake utaona kwamba wakati mfumo wa muungano unafanywa ulifanywa
> >> katika mazingira ya USIRI mkubwa na hata inadaiwa kwamba "wasomi" wa
> >> ki-Zanzibari kama Profesa (marehemu) Muhammad Abdul'Rahman Babu hakuwapo
> >> Zanzibar. Inasemekana (na ushahidi unaonyesha kwamba hati za Muungano wa
> >> Tanganyika na Zanzibar ziliandaliwa Tanganyika na mwanasheria (Muingereza)
> >> wa Tanganyika na mwanasheria wa Zanzibar (Mhindi) Wolfgang Dourado hakuwahi
> >> kuiona hati hiyo [!!!!] hadi ilipofanywa sheria na Bunge la Tanganyika).
> >>
> >> SITA, kama wote tunakubali kwamba MUUNGANO ni watu (na si nchi, kwa vile
> >> nchi zinaundwa na watu); wananchi wa pande zote mbili hawakushirikishwa
> >> kwenye UAMUZI wa hatma ya nchi zao kwenye "muungano" kwa nini iwe nongwa
> >> leo wananchi wa pande mbili (nchi mbili) kuamua hatma yao kwa kuulizwa
> >> wanataka nini [?]. Kwa nini muungano ulaimishwe kwa "Nguvu za Dola" kama ni
> >> kweli hoja ya muungano ni kuwaunganisha watu (wa pande mbili) wanaotokana
> >> na nchi mbili zinazosemekana zilikuwa HURU [???]. Kwa nini Mwalimu Nyerere
> >> alikuwa "championi" wa kushinikiza kile alichotaka kiwe na akakifanya
> >> "kiwe" vile yeye (Mwalimu Nyerere) alivyotaka?
> >>
> >> SABA, na mwisho; nadhani umefika wakati sasa waanchi wapewe haki yao kwa
> >> UHURU, USAWA na UADILIFU wa hali ya juu kama tunataka AMANI na USTAWI wa
> >> wat na wenye manufaa ya UMOJA na UHURU wa "kila mtu kuwa na maoni ya ujenzi
> >> ya jamii ya watu waliyo sawa na huru." Kama Mwalimu Nyerere na Shikh Karume
> >> waliweza kuwalazimisha wananchi takriban milioni 12 (pungufu au ziada
> >> kidogo [+ or -]) haiwezekani leo baada ya miaka takriban 49 kuwalazimisha
> >> wananchi wanaokadiriwa milioni 43 [!] kuamini kwamba sababu za muungano
> >> miongo mitano iliyopita ni sawa na sababu za muungano leo (2012!); sidhani!
> >>
> >> Nionavyo mimi; ni wajibu wa kisheria na ni haki kwa wananchi wa nchi mbili
> >> kuulizwa juu ya aina ya muungano wanaoutaka! Kwa kuwa Zanzibar ni "nchi
> >> iliyojitambulisha kwenye Katiba ya Zanzibar ya 1984 [Toleo la 2010], na kwa
> >> kuwa Wazanzibari wameshaanza "kujitambua" na "kujitambulisha" na UTAIFA wao
> >> (yaani, WAZANZIBARI) kuna kila sabau ya kuwauliza Wazanzibari wanatakaje
> >> juu ya muungano wetu; na vilevile, ni HAKI kuwauliza WATANGANYIKA juu ya
> >> hatma ya nchi yao (Tanganyika). Napenda ieleweke hapa kwamba; Tanganyika ni
> >> nchi (iliyopoteza utaifa wake kwa kutengeneza muungano) hata hivyo, ndio
> >> nchi iliyopata UHURU tarehe 9 Desemba, 1961 na kuendelea hivyo hadi
> >> ilipoungana na Zanzibar na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na
> >> Zanzibar na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (baada ya kubuniwa jina
> >> la TANZANIA).
> >>
> >> Sidhani kama ni muafaka kudhani kwamba nchi zilizoungana haziwezi
> >> kutengana! Na si muhali kushadidia utengano kama watu wa upande mmoja
> >> wanaona "muungano" ni dnoana kwao. Kuna mifano michache ndani ya Afrika
> >> nchi zimetengana kutoka nchi moja - rejea, SUDAN MOJA (2011) = SUDAN KUSINI
> >> + SUDAN (YA WAARABU) na ETHIOPIA MOJA (1990s) = ETHIOPIA (YA ZENAWI) +
> >> ELITREA. Na hivi ndivyo historia ilivyo; tumekuwa tukishuhudia vurumai za
> >> nchi kutaka kujitenga Afrika, Ulaya, Asia na Latino Amerika...nadhani mambo
> >> haya yanahitaji AKILI, BUSARA, HEKIMA na UJUZI wa kuamua kwa UHURU na HAKI
> >> kwa watu na si matumizi ya nguvu za kijeshi au kipolisi. Kama tutalazimisha
> >> sababu za muungao kama zilivyokuwa 1964 tunaweza (narudia, tunaweza)
> >> kusababisha songombingo zitakazowavutia "wapenda vita" kuchukua nafasi ya
> >> ombwe la demokrasia ya watu na kuingiza demokrasia ya kijeshi (militarised
> >> democracy) kama iliyotumiwa na Sheikh Karume (ASP) na Mwalimu Nyerere
> >> (TANU) na baadaye CCM (chama kushika hatamu na kulifanya jeshi [JWTZ] kuwa
> >> taasisi ya chama).
> >>
> >> Nawasilisha,
> >>
> >> *Bakari M Mohamed*, BBA [PLM], CPSP [T], MSc (PSCM), Reg. PSP (AU 0005)
> >>
> >> 1. *Lecturer in Procurement and Supply Chain Management*
> >> 2. *Procurement and Supply Chain Auditor*
> >> 3. *Procurement and Supply Chain Specialist, Consultant, Researcher
> >> and Trainer in Procurement Contracts Management*
> >> 4. *Doctor of Alternative Medicines* [DAM] & *Natural Healing Therapist
> >> *
> >>
> >> Department of Procurement and Logistics Management
> >> Mzumbe University
> >> Box 6
> >> *Tel (Office): + 255 23 2604381/3/4
> >> Mobile : + 255 713 593347*
> >> *MZUMBE, Tanzania*.
> >>
> >> *From:* Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> >> *To:* Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
> >> *Sent:* Tuesday, September 25, 2012 9:15 PM
> >>
> >> *Subject:* RE: [wanabidii] SEIF SHARRIF HAMAD APASUWA BOMU!!!
> >>
> >> Jabir,
> >>
> >> Nil
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment