Sunday 23 September 2012

Re: [wanabidii] Ramani mpya ya Tanzania: mpaka katika ya ziwa Nyasa.

Alex,

Ramani inayoonyesha mpaka katikati imekuwepo miaka mingi haswa ramani kabla ya 1970. Baada ya malawi kubadilisha jina from Nyasaland walibadilisha jina la ziwa kwa upande wao lakini sisi tuliendelea na jina la zamani la ziwa Nyasa.

Uzembe wa wizara ya Ardhi miaka ya 1980 ndipo ikaachia ramani zisizo rasmi kuuzwa barabarani na machinga ambazo zilichapishwa ikionyesha mpaka upo mashariki mwa ziwa! Ni uzembe wa wizara kitengo cha ramani walioachia hili kwa kisingizio cha biashara huria! Zamani ramani zote zilizochapishwa na McMillan na Oxford publishers ndizo pekee zilizokuwa na kibali cha wizara.

Haijulikani Malawi walituzidi maarifa kwa kujua complacency yetu na hivyo kuingiza ramani za upotoshwaji. Kutoa ramani mpya leo bila kutangaza kuzitoa au kukusanya ramani zote zilizokosewa sioni kama itasaidia kuziondosha ramani hizo! Kupiga marufuku na pia kutoa refund kidogo kwa walio nazo (maana walizinunua), itasaidia!

Kesi ya malawi haina uzito sana hata wakienda huko mataifani, waingereza walifanya uhuni kwani mkutano wa berlin wa kwanza 1890 ndio ulizingatia mipaka ambayo ziwa malawi lilikuwa mali ya nchi tatu (Tanganyika, Nyasaland na Mozambique. Re-alignment ya mipaka tena hapakuwa na provision inayoruhusu hilo kwenye makubaliano ya 1890 (nisahihishe mwaka!). Ndicho hadi sasa kwa miongo karibu 4 Malawi wameshindwa kwenda Den Hague!

Sidhani kwa Malawi kuchapisha ramani zao zenye kupotosha ndiyo ifanye sisi tujali hilo! Wanaweza kufurahishana wenyewe tu.
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

-----Original Message-----
From: "Alex Manonga" <manonga2003@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 23 Sep 2012 10:38:24
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Ramani mpya ya Tanzania: mpaka katika ya ziwa Nyasa.

Imeripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba serikali imetangaza ramani mpya ya Tanzania ikionesha mipaka ya wilaya, mikoa na Tanzania na majirani zake. Ramani inaonesha mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya ziwa.

Maswali,

Mosi, nini itakuwa hatma ya mazungumzo yanayoendelea kati ya nchi hizi mbili juu ya mpaka baada ya upande moja kutangaza mipaka yake?

Pili, kwa wale wataalamu wa sheria za kimataifa, msingi wa uhalali wa ramani yetu itatokana na nini?

Tatu, iwapo Malawi kwa upande wao wataweka mpaka upande wa mashariki mwa ziwa, sisi tutakuwa na option ipi?
Alex
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment