Minja, Tatizo kubwa la Tanzania sio kwamba haiwezi kuzalisha chakula cha kutosha kulisha watu wake. Shida kubwa ni kuwa na mipango/miradi rukuki inayotekelezwa kwa ubabaishaji na isiyozingatia hali halisi na mahitaji ya wakulima. Angalia mfano mfumo wa ruzuku ya vicha za pembejeo. Tangu unapoundwa ulikuwa umekaa vibaya (kiulaji). Ushauri unaolewa, hauzingatiwi. Hata KILIMO KWANZA yenyewe ambayo imeanza kutekelezwa na wewe huna habari, imeishafeli kuanzia mwanzoni. Kama tunashindwa kusimamia mambo madogo, tunawezaje kujiingiza kwenye complicated, sophisticated and too expensive technologies kama GMO? Tatizo jingine ni uoga na kutojiamini! Hatuwezi kufanya maamuzi yetu wenyewe na kuyasimamia kwa dhati na uthabiti. Ndo maana Rwanda inaendelea mbele nasi tunashangaa na kisingizio cha wale tuliowachagua kutuongoza ni pamoja na kusema Rwanda ni nchi ndogo!! Kama ni hivyo Zanzibar si ingekuwa mbali sana. Ukubwa wa Tanzania ndo wingi wa rasilimali pia!!! GMO sio tu kuwa si salama kiafya na mazingira! Itaongeza umasikini wa kutupwa kwa watanzania na mwisho itaifanya nchi yetu kuwa tegemezi zaidikuliko jana. Siku wakigoma kuleta mbegu tutakuwa na njaa kali na ili tupate chakulaitabidi tuwagawie sehemu ya ukubwa wetu (Kama ni mkristo kumbuka kisa cha Esau na Yakobo!) Ogopa njaa!! Kwa heri Martin Pius P. O. Box 561, BABATI Manyara Tanzania Mob: +255 78 447 4940 / +255 71 3474940 Email:malagila01@yahoo.co.uk --- On Thu, 6/9/12, achengula@gmail.com <achengula@gmail.com> wrote:
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment