Thursday 9 August 2012

[wanabidii] YAHUSU WAISLAMU WA ZANZIBAR KUGOMEA ZOEZI LA SENSA

Sensa ni zoezi la kuhesabu pamoja na mali zao na mambo mengine ya
msingi ili kuweza kuipa nafasi Serikali ipange mipango na mikakati
mbambali ya maendeleo kwa jamii kama vile ya uchumi, afya, kielimu nk.
Ni hatua moja muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa lolote lile duniani.

Narudi tena kwa mara nyengine ili basi niweze kwa uchache
kuwakumbusha Wazanzibar wenzangu juu ya suala la sensa ambalo kwa
namna moja au nyengine limeonekana kuwa na ajenda nyingi za siri
zilizofichwa ndani yake kwa lengo zima la kutaka kuipa tena nafasi
jamii fulani ya Imani fulani nchini hapa iweze kutekeleza malengo yake
kwa ufanisi zaidi maana katika hali isio ya kawaida inaonekana
mwelekeo wa Imani hio sasa iko MASHAKANI NA KITANZI KINAZIDI KUIKAZA
SHINGO YA IMANI YAO KIMASLAHI.

Kwa upande mwengine, Waislamu, nao waomeonekana wazi kutumia zoezi
hili Sensa kuitunishia Serikali misuli kwani bila ya utafiti wa kina
utaona jinsi ilivyojiegemeza kwenye upande dini ambayo ndio inayo-
iongoza UISLAM katika kila Wizara na Idara Seerikalini, kutokana hali
hii na ikiwa ni katika kuwaridhisa zaid UPANDE HUO PENDWA, Serikali
imeamua kukiondosha kipengele cha kuwahesabu watu kwa mujibu wa DINI
zao ili kisiwe ni sehemu ya Zoezi la Sensa lakini huo huo kiwekwe
kipengele cha kuhesabu NYUMBA za ibada kwani kwa kupitia nyumba za
Ibada wana UHAKIKA wanazo nyingi kuliko MISIKITI kwani jamii yote ya
Waislamu haichagui msikiti wa kufanyia Ibada zao eti kwa sababu ya
Madhehebu yao, tofauti na upande wa pili ambao wao lazima ufanye ibada
kulingana na imani ya kanisa lako kama ni kakobe au kanani basi iwe
humo. Hapo ajenda yao baada ya Sensa kwisha ni kusema kwa vile nyumba
zao ni nyingi kuliko Waislam basi ni wazi na idadi yao ni kubwa kuliko
Waislam. Kwa hili Waislam Amkeni..! Msilale..!!

Ndugu zangu Wazanzibar sisi kwa asilimia 99.9 ni Waislamu ni jambo la
wazi wala halihitaji utafiti kwani Mizengo alikiri hivo Bungeni majuzi
tu kama mnakumbuka alipomjibu yule "MHARIBIFU, MCHAFU WA MAADILI". Kwa
sababu hii sisi hatuna haja ya kuwa woga na wasiwasi na hizi MBINU
CHAFU za wenzetu, ni laziwe tuwe macho MARA MBILI HATA ZAIDI tusije
tukaingizwa katika mtego wa Waislamu wanafiki wa Tanzania Bara, hawa
hawana umoja wa mshikamano katika kudai haki zao huku na wao ni rahisi
sana KUGAWANYWA na kupigwa MAPANDE ndani ya misikiti, katika Taasisi
Zao Kiislam na kweningineko. Hebu Wazanzibar angalieni hivi sasa kuna
makundi mangapi tayari yameshajitokeza juu ya Suala hili la Sensa
ndani ya Waislamu wa T,Bara? Kuna kundi la Bakwata,
kundi la Ally Baseleh nk hali hii yote inaonyesha UDHAIFU wa Waislamu
T,Bara pale wanapodai haki zao kwani bila ya kuficha wa hawa wanaweka
mbele MASLAHI yao kuliko Uislamu. Lengo la kusema hivi ni kutaka
kuwaambia kinagaubaga eti Waislamu wa T,Bara wanataka wapate kuugwa
mkono na Waislamu wa Zanzibar katika suala hili la Sensa ili tuigomee
kwa kuwasaidia wao mpaka pale serikali itakapo rejesha Kipengele cha
Dini kwenye Sensa 2012. Hizi ni njama zisizo chembe ya UKWELI ndani
yake na Sisi Wazanzibar tusijiuze kwa bei rahisi kwa UNAFIKI wao
huu.Sisi tuna madai yetu maalum na ya msingi kweli kweli kipindi hiki
na tuwaepuke waislamu wa aina hii kwani NGUO YAO KUBWA NI UNAFIKI.
hawa ni watu hatari sana katika jamii ya kiislam na hata Uislam
hushindwa kusonga mbele kwa kuweka mbele Maslahi yao.

Sisi wazanzibar tusiiamuliwe mambo yetu na WATU WAISLAMU HAWA
HATARISHI, sisi tuna hiari yetu kama tunahisi tuna sababu zetu za
msingi basi tutaigomea SENSA na kama hatuoni sababu ya msingi basi
tutashiki kama kwani haya ni maamuzi yetu kama Waislamu wa Wazanzibar.

Kuna sababu za msingi za Wazanzibar kutowaunga mkono Waislamu wa
T,Bara, na hizi zifautazo ni baadhi hizo kwa UCHACHE tu:-

Kama wanataka waungwe mkono na Wazanzibar basi kwanza wangeungana
mkono wao kwao kwanza

Hakuna dhamira ya DHATI walio-ionesha Waislamu T'Bara katika
kugomea sensa 2012.

Hata Waislamu wa Zanzibar wakiunga mkono, basi lengo halitofikiwa
kwa vile waislam wengi T'Bara hawaonyeshi kuigemea Sensa. Jee waislamu
karibu milioni 1 na nusu Zanzibar watafua dafu mbele ya Watu karibu
milioni 50 na wengi wao wanashiriki Sensa?

Bado hatujawahi kuona juhudi za Waislam T'Bara kuisadia Zanzibar
kisiasa ijikwamue na makucha ya Mkoloni mweusi kwani hivi juzi tu
Waislamu wa BAra walishirikiana na Kanisa kulaani vikundi vya
kiislamkutokana na machafuko yalitokea hapa wakati msingi wa kutokea
kwake sio Waislam wahusika wanajulikana?

Sensa ya Zanzibar ni kwa ajili Wazanzibar na sio T'Bara na idadi
ya watu wake itakua ni kwa ajili ya Zanzibar kila upande una watu wake
wa kuhesabiwa, msichanganye vitu ambavyo ni "UNPAIRED"

ZANZIBAR DOWN! DOWN! WITH TANGANYIKA!!!

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment