Saturday 11 August 2012

[wanabidii] Tamko Juu ya Wezi wa Kazi za Wasanii Nchini Tanzania

SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za
wasanii 'zimeapa' kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda
maslahi ya wasanii.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es
salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la
wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya
yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.

Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia
aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa
kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii
huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.

"Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka
mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa
masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi
zao"

"Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza
kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii
kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache
ndiyo wananufaika nayo" alisema Mwakifwamba.

Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven 'JB' alisema sanaa inaweza
kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato
linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.

Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika
wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa
nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.

Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema
Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari
Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubalina kuweka
mikakati ya kupamba na suala hilo.

Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili
ya kuhakikisha kazi zao zinakwebnda kwa haki ili wasanii wapate na wao
wawe ni watu wa kusaidi wasanii kusambaza kazi zao

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment