Friday 17 August 2012

[wanabidii] RE: KAULI ZA WAZIRI MKUU

Ndugu Watanzania mimi nilisikitishwa sana na Kauli za Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa Sera ya Serekali ya CCM ni kupita katika majimbo ya Wapinzani na hata majimbo yao kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi Mwaka 2015. Kauli hii inamaanisha kwamba:

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuruhusu kuboresha Katiba mpya inayoweza kusimamia masilahi ya wengi, bali kusimamia masilahi ya viongozi wa CCM.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kulipa Wafanyakazi wake malipo na mishahara sahihi inayolingana na kazi zao wanazofanya.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwataja watu walioficha fedha zetu nje ya nchi zaidi ya Bilioni 350.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwalipa Wazee waliokuwa wanatumikia Jumuiya ya Afrika Mashariki, wala mashirika mengine ya Serekali.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuweka mkazo katika sekta ya elimu nchini. Madarasa, madawati, vyoo, vyote hivyo ni vitu vya anasa kwa Serekali sikivu ya CCM.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuboresha huduma za tiba nchini. Wakiugua wao wanatibiwa nje ya nchi ila mwanakijiji akiugua anaachwa afe na ni mlipa kodi.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya juu. Ukiandamana kudai haki yako unamwagiwa maji ya pilipili uwashwe na ukamatwe uswekwe ndani.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kutoa huduma ya visima vya maji nchini. Lazima mwanakijiji utumie maji yanayotumiwa na mifugo yako.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini kuwazuia wawekezaji kuwakwapua Watanzania maeneo yao ya asili. Madini, na rasilimali za nchi ni za wawekezaji. Tanzania haifaidiki lolote na uwekezaji. Asilimia 3 haitoshi mtu kuchimba rasilimali za nchi. Kama tulisomeshwa kwa kilimo cha Katani, Pamba na Kahawa kwa nini madini na utalii visisomeshe watoto wa Kitanzania.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kufufua na kuendeleza viwanda watu wapate ajira. Matokeo yake thamani ya fedha imeshuka sana. Nchi inategemea wafadhili zaidi kuliko kuzalisha.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kumsaidia Mtanzania wa hali ya chini aweze kula milo mitatu kwa siku. Umasikini wetu umeletwa na wizi wa viongozi. Rasilimali za nchi zinanufaisha wageni. Madini, Wanyama, Misitu nk.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kusimamia mfumko wa bei za bidhaa nchini. Leo hii kuna Watanzania hawajui sukari ina ladha gani. Tusidanganyane. Lazima Serekali ya CCM inakula sahani moja na wafanya biashara wakubwa. Tuchukue tahadhari.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kusimamia uingizaji holela wa watu kutoka nchi za nje. Watu wanajijia hovyo na kujazana nchini na kuhamisha fedha za kigeni.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwataja na kuwashitaki watu walioiba mali za umma. Viongozi wamejiuzia mashirika ya umma, nyumba za umma nk.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuzuia uwindaji na uuzwaji wa wanyama ambao kila kukicha idadi yake inapungua. Wawekezaji kwenye sekta za uwindaji wa Kitalii na Picha wanahamisha wanyama.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kufufua na kuendeleza mashamba ya Serekali ili kuzalisha chakula kwa wingi. Sera zao ni kuuza ardhi na kumilikisha ardhi kwa wageni.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kutekeleza ahadi zake za kufufua mashirika ya umma yaliyofilisika mfano: Shirika la reli na ndege. Sera zao ni kuwekeza hata pale anakonufaika Mtanzania.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuingia kwenye ushindani wa kuboresha viwanja vya ndege. Kenya wanajenga kiwanja Taveta wao wanalalamika kwa nini wajenge karibu na kiwanja chetu nyie mnasubiri nini msikiboreshe.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kupunguza tofauti ya walionacho na wasio nacho. Watanzania wengi ni masikini. Tajiri ndiye anakopeshwa masikini anakimbizwa alipe kodi.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuboresha makazi ya wapiga kura wake. Watanzania mpaka leo wanaishi nyumba za tembe wakati Viongozi wanaficha fedha ulaya.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kumaliza migogoro ya wafanyakazi ambao kila kukicha wanagoma. Sio kumaliza migogoro ya Wakulima na Wafugaji.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kumaliza tatizo la deni la Taifa. Nchi inadaiwa Trilioni 22 Serekali inaona ni sawa tu, na inaendelea kukopa na kujininulia magari ya kifahari.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kurekebisha bajeti ya nchi. Nchi inaendeshwa kwa fedha za wahisani. Nchi imefulia. Hazina hakuna kitu.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kupunguza utitiri wa wabunge bungeni. Nchi masikini lakini wabunge 400 na vikao visivyo na tija zaidi 66.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio sikivu na ni Serekali yenye kulindana na kutetea watendaji wabovu. Watu ni wezi wa mali za umma wanapewa madaraka. Fisadi anakuwa Waziri. Mwizi anakuwa naibu Waziri.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuzuia viongozi wake wasile rushwa. Ndani ya CCM rushwa ni amri ya chama. Lazima ukiwa mwana CCM uwe unajua kula rushwa. Vinginevyo unatimuliwa chama.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio ya kuwalipa watumishi malipo mazuri bali kujilimbikizia mishahara minono na marupurupu kibao.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini na sio Serekali ya Watanzania bali ya Mafisadi. Ukidai haki yako lazima utekwe, upigwe, na kutupwa ufilie mbali.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuacha ushabiki wa Siasa za ukandamizaji. Masilahi ya CCM mbele ndio Kiongozi atizame shida za Watanzania hasa katika jimbo lake.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwakamata watendaji wabovu ila kuwakingia kifua. Mapato na matumizi ya Serekali hayawekwi wazi.

 

Mwisho nataka niwaambie Watanzania wakati umefika wa kuwataja kwa majina watu wote walioibia nchi hii na kuhakikisha hawabaki madarakani mwaka 2015. Hakikisheni tunaweka sura mpya kabisa kwenye Serekali ijayo. Tanzania ni ya kila mtu na sio nchi ya baadhi ya watu. Kauli ya Waziri Mkuu ndiyo kauli ya Rais na ndiyo kauli ya wana CCM wote nchi nzima. Sera zao ni za kujilimbikizia mali na sio sera za kujenga nchi. Tukiendelea kuwapa madaraka tutakuwa tumeweka watoto na wajukuu zetu rehani na watakuwa watumwa baadae. Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na tumenyonywa kiasi cha kutosha. Sasa tunataka mapinduzi. Lazima Watanzania tufanye maamuzi mazito.

Mkereketwa.

Lengai Ole Letipipi

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment