Sunday 12 August 2012

[wanabidii] Poleni ndugu zangu wa Kenya

Nachukua nafasi hii kuwapa pole ndugu zangu wa Kenya kwa msiba wa wanakwaya 11 waliofariki kwa ajali ya basi nchini Tanzania.
 
Namshukuru Raisi Mwai Kibaki kwa moyo wa kuwajali raia wake na kuamuru miili ya marehemu na majeruhi wote warudishwe Kenya kwa gharama ya serikali ya Kenya.
 
Namshukuru Balozi wa Kenya nchini Tanzania kwa kuwa karibu na wananchi wake kwa kipindi chote toka wapate ajali mpaka kurudishwa kwao.
 
Kwa Polisi  wetu wa Tanzania naomba kuwakumbusha kuwa ajali za magari zinaua watu wengi zaidi kuliko majambazi. Wapunguze ngojera na wafanye kazi ili kudhibiti ajali hizi.
 
Nawaomba ndugu zangu wa Kenya muendelee na mshikamano mliokuwa nao na Mwenyezi Mungu awabariki sana. Amen.

0 comments:

Post a Comment