Saturday 11 August 2012

[wanabidii] No Tax Revenue, No Mining Licence on Uranium – Zitto Kabwe

Leseni (Special Mining Licence) ya kuchimba Uranium (Mkuju River Project) isitolewe mpaka Kodi (capital gains tax) Tshs 290 bilioni ilipwe na Waustralia/Warusi.

(taarifa ya mbunge Zitto Kabwe Bungeni kama ilivyorekodiwa na Hansard)

=========

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa taarifa kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (8). Sikupenda kusimama wakati maswali yanaendelea ili kutokuondoa flow ya maswali, Wakati swali Na. 353 linajibiwa la Mheshimiwa Ali Khamis Seif la Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na swali la nyongeza kuhusiana na mradi wa Uranium wa Mkuju River Project, ambapo alitaka kufahamu kwamba Serikali imefaidika namna gani na mabadiliko ya umiliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika kwamba swali hilo halikujibiwa inavyopaswa, kwa sababu mwaka jana kampuni ya Mantra Resources ya Australia iliuza mradi huu, kampuni nzima asilimia 100, kwenda kwa kampuni ya Russia ya (ARZM) kwa thamani ya dola za kimarekani milioni mia tisa na themanini (USD980m). Baada ya mauzo hayo, mamlaka ya mapato Tanzania TRA walihitaji walipwe Capital Gains Tax ya asilimia 20, ambayo ni sawa sawa na shilingi milioni mia moja themanini na sita (USD 186m).

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa pesa hizi hazijalipwa, na Serikali inafanya mazungumzo na kampuni hii, na si kweli kwamba kampuni ya UraniumOne, ni tofauti na hiyo kampuni ya Urusi. Kampuni ya UraniumOne ni sehemu ya Subsidiary ya hiyo kampuni ya Urusi, inamilikiwa na hiyo kampuni ya Urusi. Kwa hiyo palitokea mabadiliko ya ownership katika mradi huu, Serikali inapaswa kuhakikisha kabla Special Mining License haijatolewa kwa ajili ya mradi wa Mkuju River Project wa Uranium, Serikali ipate dola milioni 186 za capital gains ambazo TRA mpaka sasa wanazidai. Tutasikitika sana iwapo Special Mining License itatolewa kabla ya tax compliance. Kwa sababu Tax Compliance ni lazima iwe ni sharti muhimu sana kwa miradi ambayo inaendelea.

[MHE. KABWE Z. ZITTO]

Mheshimiwa Naibu Spika, tusiridhike na mafanikio tutakayokuja kuyapata, kwa sababu kwenye dhahabu tuliambiwa hivyo hivyo kwamba tutapata ajira, tutapata mrahaba, tutapata FDI lakini matokeo yake ni kwamba mpaka leo wananchi bado wanalalamika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe rai kwamba special mining licence Waziri wa Nishati na Madini, asiitoe mpaka fedha zetu dola milioni mia moja themanini na sita za capital gains tax ambazo TRA wanawadai hawa watu wa Uranium zimelipwa, vinginevyo Serikali itakuwa imeshindwa kutetea na kulinda rasilimali za nchi yetu inavyotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba kutoa taarifa hiyo na Waziri aweze kuifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment