Monday 6 August 2012

[wanabidii] MSIMAMO WA TANZANIA KUHUSU ZIWA NYASA

Waziri Benard Membe ameweka wazi kuhusu mpaka wa Tanzania na
kubainisha kuwa mpaka unapita katikati ya ziwa Nyasa!

Na amebainisha kuwa mipaka hiyo iliwekwa kwakipindi hicho nyasa
ikiitwa Nyasaland nahivyo wamalawi wamekuwa wakijua Nyasa ni yao na
Tanzania inaishia pwani ya ziwa Nyasa!

Na amesema tatizo ni la mda mrefu tangu miaka ya 1960... Na hili
tatizo lilishindikana kutatuliwa kwakuwa Kiongozi wa Malawi Kamuzu
Banda Kuwa na urafiki na makaburu.. Hivyo Tanzania kwakuwa ilikuwa
inaendesha harakati za ukombozi mwa afrika kusini hivyo haikuwa rahisi
kwa Tanzania kukaa kitikimoja na Malawi kwakuwa Malawi iliwakumbatia
Makaburu.

Amewataka Malawi kushehimu mazungumzo ya tarehe 27/12 na katika
kipindi hiki, wasiruhusu mtu au kampuni au kikundi kufanya shughuli
zozote kama za kutafuta mafuta na gesi.

Hapa tunazungumzia mustakabali wa watu takribani 600 wanaotegemea ziwa
kwa maisha yao

Serikali imeyaonya makumpuni yote yanayofanya utafiti kwen ziwa nyasa
eneo linalobishaniwa kuacha MARA MOJA. Serikali haitaruhusu utafiti
kuendelea hadi makubaliano kuhusu mpaka yatakapopatikana

Wananchi waendelee na shughuli zaoziwani na nchi kavu. Serikali ipo
tayari kulinda mipaka ya nchi yetu kwa gharama yoyote .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment