Thursday 9 August 2012

[wanabidii] KUHUSU VITAMBULISHO VYA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR

09/08/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Idara ya Habari(MAELEZO) tunawakumbusha tena waandishi wa habari juu
ya ulazima wa kuwa na kitambulisho cha kufanyia kazi ya uandishi wa
habari Zanzibar kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo(Press Card)
kwa mujibu wa sheria Zanzibar.

Aidha, waandishi wa habari kutoka nje ya Zanzibar hawataruhusiwa
kufanyakazi ya uandishi wa habari mpaka pale amepata ruhusa ya Idara
ya Habari Maelezo kwa mujibu wa sheria ya usajili magazeti N0 5 ya
mwaka 1988 ya Zanzibar.

Kutokana na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo
vya habari ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri,
Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na
wasemaji katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo
vya habari kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara
ya Habari Maelezo Zanzibar.

Hivyo, kuanzia tarehe 1/09/2012 waandishi wa habari wote wakiwa kazini
ni muhimu kuonyesha kitambulisho kilichotolewa na Idara ya Habari
Maelezo.

Aidha,, tunasisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria ya usajili wa
magazeti sheria N0 5 ya mwaka 1988,kifungu cha 13 kinasisitiza kwamba
mtu yeyote atakayechapisha Kitabu, Magazeti, Vipeperushi,
Vijarida,Ramani na Chati lazima awasilishe nakala tatu si zaidi ya
siku 14 baada ya kuchapishwa kwa Mrajis Idara ya Habari Maelezo
Zanzibar.

Kutofanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria ya Usajili Magazeti na
Vitabu N0 5 ya mwaka 1988 hatua za kisheria zitachukuwa kwa
atakayekiuka.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment