Sunday 5 August 2012

[wanabidii] Fw: Tuwe Tunawahi



--- On Sat, 4/8/12, PERPETUA KISAMBA <pepekiss2004@yahoo.co.uk> wrote:

From: PERPETUA KISAMBA <pepekiss2004@yahoo.co.uk>
Subject: Fw: Tuwe Tunawahi
To:
Date: Saturday, 4 August, 2012, 23:33




 











Padri mmoja mzee alistaafu na wanaparokia walimfanyia sherehe kubwa. Katika sherehe hiyo, mbunge wa eneo hilo alipangwa kutoa hotuba ya shukurani ya kumuaga padri huyo kwa niaba ya wanaparokia wote. Bahati mbaya, mbunge alichelewa kufika .   
 
 Mc akamwomba padri aseme machache wakati wanamsubiri mheshimiwa mbunge. Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi, aliongea.
 

"Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara ya kwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha. Mtu wa kwanza kabisa kumuungamisha alinishangaza sana. kwani alisema amemwibia bosi wake TV, amemwibia ndugu yake pesa za urithi, amezini na jirani yake, na pia katembea na house girl wake. Nikapata picha kuwa kumbe watu wa kanisa hili ndivyo walivyo, nikasikitika sana. Kumbe nilifikiria tofauti. Kwani baadaye nikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi mara kwa mara na ni wastaarabu sana".  
 
Mara mheshimiwa mbunge akawasili, padri akakatisha maongezi na mbunge akaanza kuhutubia. "Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kwani nilikuwa na majukumu makubwa ya kiserikali. Pia ninayo furaha kubwa kwa kunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu. Mimi nina bahati sana kwani padri huyu alipokuja hapa, mimi nilikuwa mtu wa kwanza kwenda na kuungama kwake...   

Fundisho-tuwe tunawahi








--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment