Saturday 11 August 2012

[wanabidii] BOT YAKANA KUWEKA SHUGULI ZA BENKI YA NBC CHINI YAKE

Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe
10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye
maana kuwa "Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki
Kuu". Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo
kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa
benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka
operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe
kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki
na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama
zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa
kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA
BENKI KUU YA TANZANIA
11AUGUST 2012

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment