Saturday 18 August 2012

Re: [wanabidii] TANZIA - ALFRED MBOGORA AFARIKI DUNIA

Inalillah waina illahi rajiun

Neville Meena <nevilletz@gmail.com> wrote:

>Wakuu,
>
>Habari za leo, habari za Jumamosi,
>
>Tumepata taarifa kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwamba mmoja wa
>maofisa wake na Mwanahabari na Mhariri wa siku nyingi, Alfred Mbogora
>amefariki Dunia leo saa 11.00 alfajiri katika hosipitali ya Taifa ya
>Muhimbili.
>
>
>
>Katibu Mtendaji wa MCT, Kajumbi Mukajanga amesema kwamba Mbogora alilazwa
>Muhimbili tangu Jumanne baada ya kuwa ameanguka katika eneo la Tegeta, mara
>baada ya kupata chakula wakiwa njiani kwenda Bagamoyo kwa shughuli za
>kikazi.
>
>
>
>Kabla ya kuanguka, Mbogora alikuwa akilalamika kwamba anasikia kuishiwa
>nguvu kwenye mguu na mkono na alipojaribu kusimama ili kutembea kutokana na
>hali aliyokuwa akiisikia mwilini alianguka.
>
>
>
>Tangu wakati huo (baada ya kuanguka) alikata kauli na hakuwa kusema
>chochote hadi hapo alipokata roho leo alfajiri. Ni pigo kwa sekta ya habari
>nchini, kumpoteza mwanahabari mwenzetu ambaye ametoa mchango mkubwa katika
>sekta yetu ya habari.
>
>
>
>Inasadikiwa kwamba msiba wa Mbogora uko nyumbani kwake Segerea, lakini
>taarifa zaidi tutazipata kadri tutakavyoendelea kuwasiliana na MCT pamoja
>na familia ya marehemu.
>
>
>
>Tunachukua fursa hii kuwapa pole wafiwa wote, kwanza ni familia ya
>marehemu, MCT na wanahabari wote nchini. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina
>lake luhimidiwe, Amen.
>
>--
>
>
>--
>*Neville C. Meena,*
>*Secretary General,*
>*Tanzania Editors Forum - TEF,*
>*Dar es Salaam - Tanzania.*
>*Cell: +255 - 787 - 675555*
> * +255 - 753 - 555556*
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment