Sunday 5 August 2012

Re: [wanabidii] Tanzania Malawi ziunde Shirika la Maendeleo la Ziwa Nyasa

Yona
Pendekezo lako ni zuri sana na lingeweza kuutatua mgogoro huu.
Lakini sijaelewa (labda) mimi na naona tofauti kubwa kati ya mgogoro huu na mifano uliyotoa.
Ziwa Victoria na Tanganyika nchi majirani wanakubaliana juu ya mipaka ya nchi zao kwanza na huu ni mtaji mkubwa ndipo wanaunda hizo mamlaka. mfano inajulikana Tanzania inamiliki eneo kubwa la ziwa Victoria.
Kwa mto Nile vile vile. Unaanzia Rwanda unapita Tanzania Uganda Sudani etc.
 
Kwa upande wa Ziwa Nyasa: Malawi wanadai ni lao lote. Wana haja gani kuunda Mamlaka ya kuendeleza ziwa hilo na Tanzania wakati Tanzania haina umiliki wowote wa ziwa hilo?
 
Tanzania inadai nusu ni mali yake.
Ili kuunda mamlaka ya kuendeleza ziwa hilo lazima kwanza ubishi huu uishe ama kwa mazungumzo ama kwa kuchapana kidogo au kikubwa ndipo kuheshimiana kuje na tuweze kuamua ustawi wa ziwa hilo.
 
Mimi ningependa mgogoro huu ukaisha sasa kwa kutumia njia yoyote. Na yoyote ni kati ya hizi mbili zilizo mbele yetu.
 
Nakumbuka wakati tuko vitani na Uganda Afrika ya Kusini iliwahi kuisaidia Malawi kutaka kumaliza mgogoro huu kijeshi. Ni kama jeshi letu la ulinzi wa anga lilijibu bila 'adabu' wakanywea.
 
Africa ya Kusini walidhani Tanzania kuwa na vita sehemu mbili Uganda na Malawi tusingemudu (nilisikia hivyo). Na tanzania ikadhibitisha kuwa kuwa na vita uganda hakujadhoofisha ulinzi mipaka mingine.
 
Kama wakati wa Nyerere na Mkapa diplomasia ilishindwa tunahitaji kuamua kiume kwamba miaka ijayo diplomasia itashinda au tuwawekee watoto wetu mgogoro. Vinginevyo ni vinginevyo.
 
Binafisi sipendi vita. Na vita ni njia mojawapo ya kuzuia vita. Eneo hili la africa hakukuwa na bwege lolote ambalo lingeweza kuichokoza Tanzania baada ya vita ya Amini. Sasa yapo. Moja ni hilo.
 Lisaidieni na majirani watakumbuka.

--- On Sun, 8/5/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Tanzania Malawi ziunde Shirika la Maendeleo la Ziwa Nyasa
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 5, 2012, 12:11 AM

Ndugu zangu

Kufuatia kutokuelewana kati ya Tanzania na Malawi Juu ya ziwa nyasa na
maeneo mengine ya karibu na eneo hilo haswa yanayozunguka ziwa nyasa ,
ni vizuru tujifunze kutokana na baadhi ya nchi zilizofanya katika
kushiriki pamoja katika utumiaji wa rasilimali za mito , maziwa ,
bahari na rasilimali nyingine zilizoko mpakani au zinazounganisha nchi
hizo .

Kwa hapa Afrika haswa maeneo ya maziwa makuu kuna

Nile Basin Initiative  http://www.nilebasin.org kwa ajili ya maendeleo
ya mto nile na nchi husika ambapo mtu huo umepita ingawa kuna baadhi
ya nchi hazijasaini baadhi ya mikataba yake .

lake victoria basin commission www.lvbcom.org kwa ajili ya maendeleo
ya ziwa Victoria kwa nchi za jumuiya ya afrika mashariki haswa .

Lake Tanganyika Authority http://lta.iwlearn.org/ kwa ajili ya
maendeleo ya ziwa Tanganyika

Katika kamisheni zote za maendeleo tajwa hapo juu Tanzania ni mshiriki
na mtendaji katika shuguli za kila siku za maziwa hayo , kwa uzoefu
huu tulioupata katika maeneo mengine pia tunaweza kuupeleka kwenye
ziwa nyasa na maeneo mengine ya bahari ambayo yanaweza kuleta utata wa
kimipaka na kutoelewana kwingine kwa siku zijazo .

Tukumbuke watu wanataka maendeleo na sio porojo na vitisho , jamii
nyingi haswa za kiafrika zimekuwa zinaishi pamoja kwa kipindi kirefu
hata wakoloni walivyoweka mipaka yao bado jamii hizo ziliendelea kukaa
pamoja kwa kutumia jumuia kama za afrika mashariki , sadc , comesa na
ecowas  .

Mungu ibariki Afrika .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment