Sunday 12 August 2012

RE: [wanabidii] Tamko la Maaskofu kuhusu Urais na mengineyo

Ni Maaskofu gani?
 
> Date: Sun, 12 Aug 2012 01:26:47 -0700
> Subject: [wanabidii] Tamko la Maaskofu kuhusu Urais na mengineyo
> From: oldmoshi@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Ndugu zangu
>
> Hivi karibuni maaskofu wametoa tamko ambalo haliwezi kupita hivi hivi
> bila kujadiliwa haswa baada ya kugusia suala la urais wa jamhuri ya
> muungano wa Tanzania .
>
> Katika kipengele hicho wamesema hawaoni haja ya urais kupokezana kati
> ya bara na visiwani , kipengele hiki kinaihusu CCM moja kwa moja kwa
> sababu ndio imekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 35 sasa na ndio
> kumekuwa na fununu za baadhi ya wanachama kutaka zamu hii urais kwenda
> Zanzibar kwa sababu muungano .
>
> Nakubaliana na tamko hili la maaskofu haswa kipengele cha urais na
> wangeenda mbali zaidi kwa kuhimiza suala hili kujadiliwa na kuwekwa
> kwenye katiba yetu mpya ambayo wananchi mbalimbali wa Tanzania
> wameanza kutoa maoni yao ili kila mtanzania anayetimiza vigezo awe na
> uwezo wa kugombea nafasi hiyo bila kujali ametoka wapi .
>
> Pia suala la urais na ubunge liwekwe wazi kwa vyama vyote vya siasa
> ili kila mwananchi haswa wapiga kura wajue mchakato wa kupata wagombea
> wa kila chama maana kumekuwa na malalamiko ya rushwa , watu kutishwa
> kunakosababisha baadhi yao kukosa nafasi za kuwakilisha wananchi .
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

0 comments:

Post a Comment