Saturday 4 August 2012

Re: [wanabidii] TAARIFA YA MABADILIKO YA SHERIA YA MAFAO???

Clement naungana na wewe, mbona wazee wa jumuia ya africa mashariki pamoja na kuwa na miaka 80 mbona hawajalipwa? hivi police aliyeachiswa kazi akiwa na umri wa miaka 46 ambaye hana taaluma nyingine zaidi ya upolice ambao ajira zao ni serikalini tu atasubiri hadi afikie miaka 55 kweli? kwani kikomo cha umri wa kuajiriwa serikalini ni miaka 45.
 
Kijana anaendesha lori la kichina wakati wa ujenzi wa barabara akiwa na miaka 20 atasubiri hadi miaka 55! kwani hana ujuzi mwingine zaidi ya kuendesha greda la kichina na halipo popote tanzania. Wapo watumishi waliopunguzwa kazi community airlines na zara airlines wakiwa na miaka 19 hadi leo wajapata ajira nao watasubiri hadi wafikie miaka 55 kweli?

2012/7/23 Clement Marcel <kitogwa@yahoo.com>
Sheria kandamizi isiyoangalia faida kwa aliyechangia, bali kwa mamlaka za serikali na watu wake
sasa nauliza, hivi ushawahi kuona tangazo la kazi halafu halitoi mipaka ya umri (jeshini, polisi, magereza, wizara za serikali wote naona huwa wanaweka kikomo cha umri (tena maximum watakuambia mwenye Masters asizidi miaka 35), hivi wewe ushaachishwa kazi (lets say kampuni imefilisika) una miaka 40, nani atakuajili wewe, utakaa miaka 15 usubiri mafao yako!? LAZIMA TUFE NA KIHORO na pesa zetu ndo zitaliwa hovyo..
mmmh, hatari, SIZITAKI MBICHI HIZI.
CKMK.
 

From: robert kisanga <kisangarmf@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, July 23, 2012 10:03 AM
Subject: Re: [wanabidii] TAARIFA YA MABADILIKO YA SHERIA YA MAFAO???

kumekucha

2012/7/23 Constantino Kudoja <c.kudoja@zantel.co.tz>
Security ya kazi haipo kwenye mashirika yetu katika nchi yetu halafu wanaleta sheria kama hii?///
 
SOMA HII 
Hebu tuchungulie kwenye hio link hapo chini kidogo
 
 
TANZANIA MINES, ENERGY, CONSTRUCTION AND ALLIED WORKERS UNION (TAMICO)
 
Comrades viongozi wa matawi ya Tamico,wanachama wa Tamico,wafanyakazi wote na wadau mbalimbali,
 
MSHIKAMANO DAIMA.
 
 
 
Kwa takribani wiki mbili zilizopita kumekuwepo na Taharuki kubwa miongoni mwa wafanyakazi wa sekta binafsi na hasa wafanyakazi walioko katika sekta ya migodi juu ya taarifa kuhusu kuwepo kwa MAREKEBISHO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA 2012.Taarifa hizo zilidai kwamba sheria hiyo imelenga kuwazuia wafanyakazi kuchukua mafao yao pindi wanapoacha kazi mpaka pale watakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari miaka 55 au kwa lazima miaka 60.
 
 
 
Bahati nzuri nimekuwa nikilifuatilia suala hili tangu lilipojitokeza kwa maana kwamba lilianzia Geita baada ya semina ya PPF na NSSF iliofanyika Mgodini Geita tarehe 26 Juni 2012.Napenda nitumie fursa hii kuwafahamisha kwamba Jana tarehe 18 Julai 2012, nikiwa nimeambatana na mwenyekiti wa tawi la Tamico ndani ya Tamico bwana Joseph Mugomba tulikwenda makao makuu ya mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya Jamii (SSRA) yaliyoko ALFA house mjini Dar es salaam.
 
 
 
Tukiwa ofisini hapo tulifanikiwa kukaa kikao na watendaji wakuu wa mamlaka hiyo ambao ni Bi Irene Isaka(Mkurugenzi wa Mkuu),Bwana Ngabo Ibrahim(Director of Legal services),Bi Lightness Mauka(Director of compliance and Registration).Katika kikao chetu masuala yafuatayo yalijadiliwa:-
 
  
 
1. Tuliomba kujua kuhusu SSRA,madhumuni yakuanzishwa kwake na uhusiano uliopo kati yake na uwepo wa MAREKEBISHO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA MWAKA 2012.
 
 
 
JIBU LA MKURUGENZi MKUU NA LA MKURUGENZI WA HUDUMA  ZA SHERIA.
 
 
 
SSRAni Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mifuko ya Jamii(social security regulatory authority) ambayo imeanzisha kwa madhumuni ya kudhibiti na kusimamia mifuko yote ya hifadhi ya jamii ikiwemo NSSF,PPF,LAPF,PSPF,GEPF na NHIF.Uhusiano uliopo na MAREKEBISHO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA 2012 ni kwamba mamlaka hiyo kupitia kwa waziri wa kazi na Ajira ndo walitengeneza marekebisho hayo na kuyapeleka Bungeni kama muswada wa Sheria mnamo mwezi Januari 2012.
 
 
 
Kwamba Mnamo mwezi April 2012 Bunge lilijadili muswada huo na kuupitisha kuwa sheria na hadi sasa hivi sheria hiyo iko mikononi mwa rais kwa ajili ya utiwaji sahihi na baadaye kutungiwa kanuni ili ianze kutumika rasmi.Mchakato wa kutengeneza kanuni utawashirikisha wadau wote ikiwemo wafanyakazi kutoa maoni,mapendekezo na ushauri juu ya kuboresha sheria hiyo.
 
 
 
2. Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mkurugenzi wa mamlaka,nilitoa maelezo yafuatayo kwa niaba ya wafanyakazi ikiwa ndio baadhi ya sababu za kupinga uwepo wa sheria hiyo:-
 
 
 
. Kwanza wafanyakazi wa sekta zinazosimamiwa na chama chetu cha TAMICO na hasa wafanyakazi wa sekta ya MIGODI wanataka kujua juu ya uwepo wa marekebisho ya sheria hii,na kama yapo kwa nini mamlaka haikuwashirikisha katika kupata maoni yao wakati wa mchakato mzima wa utungwaji wa sheria hii?
 
 
 
.Kwa kuwa mumekiri kuwepo kwa sheria hii,wafanyakazi wa MIGODI na sekta nyingine wamenituma niwaambie kuwa wanaipinga vikali sheria hii na hawako tayari kuona inatumika kwao kwa sababu zifuatazokwa uchache:-
 
 
 
(i) Kwanza Ajira zao hazijalindwa kisheria(NO SECURITY OF EMPLOYMENT),waajiri wamekuwa wakiwafukuza kazi bila kufuata misingi ya sheria na kwa makosa ya kuhisiwa na kusingiziwa tu.Na pale mfanyakazi anapofukuzwa kazi kwa kosa lolote hata la kuangusha gari makampuni yameunda mtandao  ambao mfanyakazi huyo hawezi kuajiriwa katika kampuni yoyote ile.Kila atakapoenda ataambiwa uko kwenye BLACKLIST hatuwezi kukuajiri.
 
 
 
Kwa sababu hiyo mfanyakazi akiachishwa kazi akiwa ametumikia kampuni mfano kwa miaka 5 na akiwa na umri wa miaka 30 hawezi kupata kazi kampuni yoyote ile.Kama ndivyo hivyo kwa nini azuiliwe kuchukua mafao yake ambayo yangemsaidia kuanzisha mradi wowote ule hivyo kujiajiri mwenyewe.
 
 
 
(ii) Pili Mazingira ya kazi za migodini yana athari kubwa kwa afya za wafanyakazi.Leo hii baada ya miaka karibia 10 tangu kuanza kwa shughuli za migodi nchini,tumeshuhudia wafanyakazi wengi wakiugua magonjwa yatokanayo na kazi zao.Mojawapo ya magonjwa hayo yakiwa ni kuugua migongo,magoti, mapafu ambayo yanapelekea watu kupata ulemavu wa maisha kwani mfanyakazi huyu hawezi tena kufanya kazi yoyote ya kutumia nguvu.
 
 
 
Mbaya zaidi mwajiri akiona hali hiyo mfanyakazi anaachishwa kazi wakati bado anakuwa anaendelea na matibabu.Sasa kwa mazingira hayo unategemea mfanyakazi huyu asubiri miaka 55 kuchukua mafao yake,ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kumsaidia kutibiwa baada ya kutelekeza na mwajiri? Au unataka kumsababisha afe mapema kwa kukosa pesa ya kujitibia ilihali ana mafao yake ambayo yamezuiliwa mpaka afikishe miaka 55.Katika jambo hili ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo tunao,mkihitaji tutawapatia.
 
 
 
(iii) Baadhi ya makampuni yanawaajiri wafanyakazi kwa mikataba ya miezi mitatu mitatu au sita ilihali kazi za kampuni hizo zipo kwa muda mrefu.utakuta mfanyakazi ana miaka mitatu na kampuni moja lakini kwa kuajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu mitatu.
 
 
 
kitendo hicho kinawanyima wafanyakazi fursa ya kulipwa ujira halali kulingana na kazi zao hivyo kujikuta anafanya kazi ili kuganga njaa tu.ikitokea akaacha au kuachishwa kazi mtaji pekee anaokuwa anategemea ni mafao yake.Kwa sheria hii hamuoni kama mnataka kuwageuza wafanyakazi hawa kuwa manamba wa mafao yao licha ya umanamba wa kazi zao?
 
Mwisho tuliwaeleza kwamba kama suala hili halishughulikiwa ipasavyo,wafanyakazi wako tayari kupiga kura ya maoni kupinga sheria hii ambayo inakandamiza haki yao ya msingi kuhusu mafao yao.
 
 
 
3. BAADA YA SISI KUTOA MAELEZO HAYO KWA UFUPI NA BAADA YA MAJADILIANO YA MUDA MREFU HATIMAYE MKURUGENZI MKUU AKAKUBALI YAFANYIKE MAMBO MAWILI YAFUATAYO:-
 
 
 
(i) Kwa kuwa mchakato wa kutengeneza kanuni za sheria hiyo unatarajiwa kuanza,basi wafanyakazi wapewe fursa ya kutoa maoni,mapendekezo,ushauri na maswali kwa mamlaka hii juu ya kile wanachokitaka kuhusiana na kanuni za sheria hii.
 
 
 
Maoni na mapendekezo hayo yafanyike kwenye sehemu ya kampuni husika kupitia kwa  viongozi wa matawi,kisha viongozi wa matawi wayatume maoni hayo kupitia kwa KATIBU WA TAMICO WILAYA YA GEITA ambaye yeye atayatuma moja kwa MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA KAMA YALIVYO.
 
 
 
Ukusanyaji maoni uanze mara moja kuanzia leo na wafanyakazi wapewe taarifa sahihi juu ya suala hili ili waweze kutoa maoni na mapendekezo yao juu ya sheria hii na kanuni zinazotarajiwa kutengenezwa ili ziweze kuwa suluhisho la kutatua na hatimaye kuondoa taharuki iliopo miongoni mwa wafanyakazi.
 
  
 
(ii) TUMEKUBALIANA KWAMBA,wiki ya kwanza ya mwezi wa nane 2012,Mamlaka itakuja kufanya semina Mkoani Geita ambapo semina hiyo itafanyika mjini Geita.Lengo la semina hiyo ni kuleta majibu kwa wafanyakazi juu ya maoni na mapendekezo watakayokuwa wameyatoa.Pili watakuja kutoa ufafanuzi wa sheria hiyo kwa undani zaidi.
 
 
 
Tatu watakuja kupata maoni na mapendekezo ya pamoja juu ya utengenezwaji wa kanuni kabla ya kanuni hizo hazijakamilishwa na mwisho ni kuwapa nafasi ya kutosha wafanyakazi kueleza na kutoa msimamo wao juu ya suala hili.
 
  
 
Tumekubaliana semina hiyo ifanyike Geita kwa sababu ya kuwapa fursa wafanyakaziwamigodijirani ya Bulyanhulu,Tulawaka,Buzwagi,Northmara,Mwadui,Resolute na kwingineko waweze kuwakilishwa na viongozi wao wa matawi.Lakini vilevile kuwapa fursa wafanyakazi watakaokuwa off,rotation au likizo waweze kuhudhuria semina hiyo.
 
 
 
Kilichozingatiwa zaidi ni kwamba Geita ndiko limeanzia vuguvugu hili la Taharuki na sehemu pekee ambapo baadhi ya wafanyakazi wameonja machungu na sheria hii.Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba Geita inafikika kwa urahisi kwa wafanyakazi wa kutoka migodi husika ya jirani.
 
 
 
BAADA YA KUSEMA HAYO naomba niwatakie ukusanyaji mwema wa maoni na mapendekezo.
 
 
 
Tarehe rasmi ya semina na utaratibu mwingine mtajulishwa mapema iwezekanavyo na Ofisi ya Katibu Mkuu wa TAMICO.Taarifa hizi ziwafikie wafanyakazi mapema iwezekanavyo.Tumieni Mbao za matangazo za waajiri,barua pepe na hata kuitisha mikutano ya dharula ya wafanyakazi kupitia uongozi wa matawi palipo na matawi.
 
 
 
SOLIDARITY FOREVER
 
 
 
Tuwasiliane kupitia,
 
 
 
Benjamin Daudi Dotto
 
Katibu wa Tamico wilaya ya Geita,
 
SLP 335,
 
Geita – Tanzania.
 

This email is Virus free! Has been Scanned.
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/

Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma


Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.






--
..Blaming fate instead of oneself is always the way cowards sleep better at night!
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment