Saturday 4 August 2012

Re: [wanabidii] TAARIFA YA HALI YA UCHUMI NCHINI TANZANIA 03/08/2012

"If the theory does not fit the practice, change [ignore] the theory,"
alisema Albert Einstein. Hizi takwimu zisizoendana na hali halisi ya
Watanzania kwangu hazina maana. Uchumi ukue halafu serikali ishindwe
kuwalipa madaktari, walimu nk na bado uniaminishe na niamini kuwa
uchumi umekua si nitakuwa sina akili? Hivi ni kwa nini uchumi wa
Tanzania unakua tu kwenye takwimu na siyo kwenye uhalisia?

On 8/4/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
> OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA HALI YA UCHUMI , PATO LA
> TAIFA LA TANZANIA LAKUA.
>
> Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
>
> 3/8/2012. Dar es salaam.
>
> Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa ya hali ya uchumi
> nchini na kufafanua kuwa pato la taifa la Tanzania limekua kwa
> asilimia 7.1 katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ikilinganishwa na
> asilimia 6.1 za mwaka jana.
>
> Ukuaji huo wa asilimia 7.1 unatokana na ongezeko la uzalishaji katika
> shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo za kilimo, Uvuvi, Viwanda,
> Ujenzi na zile za utoaji wa huduma mbalimbali za jamii.
>
> Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za
> Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa
> lengo la utoaji wa taarifa hizo kwa vipindi vifupi vya vya robo
> mwaka unalenga kuwapatia wadau wa Takwimu za Pato la Taifa uwezo wa
> kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi nchini.
>
> Amesema kuwa jumla ya thamani ya pato la Taifa katika kipindi cha robo
> ya mwaka 2012 ni shilingi 4,220,535 milioni ikilinganishwa na kiasi
> cha shilingi milioni 3,940,261 za mwaka 2011.
>
> Amefafanua kuwa ukuaji wa shughuli uzalishaji katika shughuli za
> kilimo nchini ulifikia asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza
> ya mwaka 2012 zikilinganishwa na asilimia 1.2 katika kipindi hicho kwa
> mwaka 2011 kutokana na upatikanaji wa mvua za kutosha nchini katika
> mikoa inayozalisha mazao kwa wingi.
>
> Amesema ukuaji katika shughuli za uvuvi ulikua asilimia 2.6 katika
> robo ya kwanza ya mwaka 2012 huku shughuli za uchumi katika sekta ya
> viwanda na Ujenzi ambayo inahusisha uchimbaji wa madini na kokoto
> ikikua kwa asilimia 14.3 ikilinganishwa na 0.8% za mwaka 2011.
>
> Bw. Oyuke ameongeza kuwa ongezeko hilo la uzalishaji wa madini ya
> dhahabu linatokana na uzalishaji wa wa madini ya dhahabu kutoka kilo
> 8,140 kwa mwaka 2011 hadi kufikia kilo 16,736 kwa mwaka 2012.
>
> Pia amebainisha kuwa shughuli za utoaji wa huduma za biashara za
> jumla na rejareja, ukarabati wa magari na pikipiki na vifaa vingine
> vya majumbani katika kipindi hicho zilifikia asilimia 9.0 huku
> shughuli za upangishaji nyumba na biashara zikiwa 8.2 %, uchukuzi na
> mawasiliano 16.4%, hoteli na migahawa 3.8%, Benki asilimia 15 shughuli
> za uendeshaji serikali 6.4%, Elimu 6.1% na utoaji wa huduma za Afya
> nchini zikikua kwa kasi ya asilimia 5.1.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment