Thursday 2 August 2012

Re: [wanabidii] Re: IJUE SHERIA - SHERIA YA HAKI MILIKI NA SHIRIKI TANZANIA

Nakubaliana na Uchambuzi wa Neville na maelezo ya Felix Mwakyembe kuwa haya mambo tusiyaongee kishabiki, ni vema tukaangalia mzingira yanayokaribia uhalisia  kama ambavyo Neville ameeleza katika namba tano kuwa 'Ni kitu gani kinachomsukuma Zitto kutoa maelezo mengi kuhusu tuhuma ambazo kimsingi hazijajadiliwa wala kufikishwa na kusikilizwa katika chombo chochote rasmi?'

Nikweli Mh. ZZK anaweza kumtafuta Mh.Profesa Sospeter Muhongo na katibu wake Eliakimu Maswi
asionane nao hapo bungeni au nini anataka kusema. Hebu tusubiri kamati iliyotangazwa na Mh Spika leo asubuhi ili tuone Pumba na Mchele ni kipi.
Tusije shangaa wanaojitoa wakaonekana wamepewa rushwa na wasiosema wakaonekana hawano.
Tuwe makini na tunachotetea hapa mtandaoni ili ukweli ukijulikana tusije onekana ni washabiki au watetezi wa wala rushwa. ZEM


--- On Sun, 29/7/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Re: IJUE SHERIA - SHERIA YA HAKI MILIKI NA SHIRIKI TANZANIA
To: "Yona F Maro" <oldmoshi@gmail.com>
Cc: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 29 July, 2012, 10:08

KATIKA mambo yanayowasumbua watu wengi duniani (Tanzania ikiwemo) ni
suala la hakimiliki na hakishiriki kwa wasanii na wabunifu wa
sanaa.Hapa nchini, baada ya sheria ya hakimiliki ya mwaka 1966
kuthibitika kwamba ina mapungufu mengi, ndipo mwaka 1999 Bunge la
Jamhuri ya Muungano lilipotunga sheria mpya ya hakimiliki na
hakishiriki, namba 7 ya mwaka 1999, yenye sura ya 218 ya sheria za
Tanzania (kama zilivyorekebishwa mwaka 2002).

Kwa mujibu wa utangulizi wa sheria hii, imeletwa kutengeneza na kutoa
manufaa zaidi na ulinzi zaidi wa kazi za wasanii wa kazi zinazolindwa
na haki miliki na hakishiriki na zingine zote zinazoendana na
hizo.Chini ya kifungu cha 2(c) cha sheria hii, ambacho kimsingi
kinazungumzia madhumuni ya kutungwa kwa sheria hii ya muhimu kwa
maendeleo ya wasanii na watunzi na wabunifu wote katika nyanja za
nyimbo, maigizo na tasnia nyingine zinazoendana na hizo.Sheria hii ina
madhumuni ya kuinua kazi za fasihi na za kisanii pamoja na nyinginezo
zinazofanana na hizo.

Kwa mujibu wa sheria hii, kuna makundi makubwa mawili ya haki za
wasanii zinazolindwa na sheria hii, ambazo ni haki ya kiuchumi na haki
za kitamaduni ambazo mtunzi wa kazi zinazolindwa na sheria hii ana
haki nazo.

Haki hizi zina msingi katika mkataba wa kimataifa wa Benne wa mwaka
1883 ulioridhiwa na Tanzania Julai 25, 1994; na hivyo kwa mujibu wa
kanuni za kisheria za kimataifa, Tanzania ina wajibu wa kutimiza
yaliyomo katika mkataba huu iliyouridhia.Kwa mujibu wa sheria hii,
chini ya kifungu cha 3(i) cha sheria hii, kazi zinazolindwa na sheria
hii ni zile ambazo zimetengenezwa na mtunzi wa Kitanzania au zile
ambazo mtunzi wake si Mtanzania lakini ana makazi yake ya kudumu hapa
nchini au kazi hiyo iliyotengenezwa kwa mara ya kwanza hapa Tanzania,
au kazi ambazo ni za kusikika na kuona (audio-visual) ambazo
mtayarishaji wake ni Mtanzania au makao makuu yake yakutengeneza kazi
hizo zipo nchini.

Na kwa mujibu wa kifungu cha 3(3) cha Sheria hii wasanii wanaomiliki
kazi za kisanii na wana hakishiriki pia watapewa ulinzi na sheria
hii.Katika kifungu cha 4, msanii ametafsiriwa kama mwigizaji,
mwimbaji, mwanamuziki, mchezaji (dancer) au mtu anayeigiza, kuchonga
au kufanya maonesho jukwaani.
Hata hivyo, sheria hii kama sheria nyingine nyingi za hakimiliki,
imetoa sharti kwa kazi za kisanii kulindwa na sheria hii na kigezo
hiki ni kwamba kazi hiyo iwe katika hali ya kushikika, na kwa maana
nyingine ni kwamba wazo/mawazo hayatalindwa na sheria hii hata kidogo.

Kwa mfano, kama A na B walio katika sehemu tofauti lakini wana wazo
linalofanana la kutengeneza wimbo unaohusu foleni za magari, na A
akawa wa kwanza kuingiza wimbo huo katika hali ya kushikika (katika
minajili hii akawa ameurekodi studio), basi B hawezi kuja kumshitaki A
kwa kuiba wimbo wake kwani yeye alikuwa na wazo tu na wakati mwenzake
aliliweka katika hali ya kushikika.

Hii ina maana kwamba, kazi ya kisanii haitalindwa na sheria hii kwa
njia ya kusajili kazi hiyo, bali kwa njia ya kuiweka kazi yenyewe
kuwekwa katika hali ya kushikika.
Kifungu cha 5 cha sheria hii kinaorodhesha baadhi ya kazi zinazolindwa
ikiwa ni pamoja na kazi za sinema na michezo ya sinema, mihadhara,
vitabu, majarida, kazi za muziki,upigaji wa picha za kawaida, ramani
na picha za kuchonga na kadhalika.

Kifungu hiki kinaendana na maamuzi ya Mahakama ya Uingereza katika
shauri la University of London Press Ltd dhidi ya University Tutorial
Press, (1916) 2 Ch.601 ambapo nayo ilitafsiri nini ni kazi ya kisanii
kumaanisha yaliyomo katika kifungu cha 5 cha sheria ya hakimiliki na
hakishiriki ya Tanzania.Kwa upande mwingine, sheria hii imetaja baadhi
ya kazi ambazo haziwezi kulindwa na sheria hii ikiwa ni pamoja na
habari zinazochapishwa/tangazwa katika vyombo vya habari, sheria na
maamuzi ya vyombo vya kutoa maamuzi kama mahakama na mabaraza, na pia
wazo la aina yeyote ambalo halijawekwa katika hali ya kushikika na
kudumu, kama ambavyo wenzetu wa Uingereza walivyolipatia ufumbuzi
katiak shauri la Springfield dhidi ya Temp, (1903) 19 TLR 650, ambapo
mahakama iliamua kwamba wazo la aina yeyote haliko katika ulinzi wa
sheria ya haki miliki wala hakishiriki.

Haki ya kiuchumi kama tulivyoona hapo awali, katika sheria ya
Tanzania, inapatikana chini ya kifungu cha 9, na haki hii ni ile haki
ambayo mtunzi wa kazi inayolindwa na sheria hii amepewa kuwa na haki
zote juu ya kazi yake, katika masuala yote yanayohusiana na kutafsiri
kazi yake, kuikodisha, kuionesha katika umma, kuionesha katika vyombo
vya habari, kuisambaza, kuitumia hadharani na kadhalika.

Hizi ndizo zinazoitwa haki za kiuchumi, ambayo mtu yeyote hawezi
kuzifanya isipokuwa kama ana kibali cha mtunzi wa kazi hiyo. Chanzo
Tanzania Daima.

On Dec 18 2011, 1:10 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
> Mashitaka ya Jinai na utetezi
>
> Utangulizi
>
> TAALUMA yasheriaimegawanyika katika matawi mawili makubwa: Madai na
> Jinai.Sheriaza mikataba, ndoa, kazi na kadhalika ni mfano wa tawi la
> kwanza ambaposheriazote ambazo zikikiukwa kosa hufanyika na adhabu
> hutolewa ni mfano wa lile tawi la pili. Aidha liko tawi jingine muhimu
> mno linaloelezea mwenendo yaani uendeshaji wa mashauri yote katika
> mahakama pamoja na kanuni za ushahidi. Kitabu hiki kinahusiana na tawi
> hili la mwisho.
>
> Mwenendo wa mashitaka ya jinai ni utaratibu mzima wa upelelezi wa
> kosa, kushukiwa na kutiwa nguvuni kwa mtuhumiwa, kupekuliwa,
> kuandikisha maelezo, kufunguliwa mashitaka, kuwekwa mahabusu,
> kusikilizwa kwa shauri lenyewe, kuita mashahidi na kadhalika. Utetezi
> ni hatua inayofuatia mashitaka. Upande wa mashitaka unapomaliza kuita
> mashahidi wake mahakama huamua iwapo mshitakiwa, kwa ushahidi uliopo
> dhidi yake, anawajibika kujitetea.
>
> Hivyo basi kujitetea, kama ilivyo kuendesha mashitaka, ni sehemu
> muhimu ya utekelezaji wa haki katika mashauri ya jinai. Muhimu vile
> vile ni uamuzi wa mahakama baada ya kuupokea na kuupembua ushahidi wa
> pande zote mbili.
>
> Kwani huo ndio upeo wa shauri na sio siku zote mahakama huwa sahihi
> katika hukumu na adhabu inayotoa. Ndiyo maana kuna utaratibu wa rufani
> na masahihisho mahususi kwa kuangalia uhalali wa uamuzi wa mahakama ya
> daraja mbalimbali.
>
> Kila mwanasheria, na hakika yeyote yule aliye na uzoefu wa mahakama,
> anaelewa kuwa mwenendo wa mashitaka ya jinai ni mithili ya mtambo
> unaoendesha chombo cha haki katika mashauri haya ya jinai
> yanayojadiliwa hapa. Kabla, na hata baada ya kukamatwa na kushtakiwa
> rasmi, kuna utaratibu ambao daima lazima ufuatwe kuhakikisha kuwa haki
> inatendeka hasa kutokana na dhana kwamba kila mtu hana hatia mpaka
> pale inapothibitishwa hivyo bila ya shaka yoyote ya maana.
>
> Pamoja na mwenendo wa mashitaka ya jinai, kanuni za ushahidi ni muhimu
> kwa kiwango kile kile katika hatua mbili: Kabla ya wakati wa
> mashitaka. Kabla ya mashitaka kanuni za ushahidi ni zana muhimu ya
> kuamua iwapo kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa kuweza
> kumfikisha mahakamani na wala sio kumshitaki tu na kumtesa. Wakati wa
> kusikiliza shauri lenyewe kanuni za ushahidi zinabainisha iwapo
> mshitakiwa ana hatia au la. Kwa bahati mbayaSheriaya Ushahidi ni
> ngumu na inawatatiza hata baadhi ya wanasheria wa siku nyingi.
>
> Hivyo basi azma ya kitabu hiki ni kumpa mwongozo kila mmoja mintaarafu
> ya utekelezaji haki katika mashitaka ya jinai. Kimekusudiwa kwa
> wanasheria na wasiokuwa wanasheria. Jitihada imefanywa kukiandika kwa
> wepesi bila ya kuzama katika tata za kitaaluma ambazo huweza
> kuwakanganya wasomaji wa kawaida. Lakini taratibu zote muhimu za
> kuandika kazi za kitaaluma, pamoja na tanbihi na istilahi za kutosha
> ziemzingatiwa hasa kwa faida ya watendaji katika mahakama na
> wanasheria.
>
> Natumaini kuwa kitabu hiki kitaondoa dhana ya wale wenye taasubi ya
> Kiingereza kwambasheriani taaluma ambayo haieleweki wala
> kufundishika kwa Kiswahili ila Kiingereza pekee.
>
> Upelelezi
>
> MARA tu kunapotokea malalamiko ya kutendeka kwa kosa hatua ya kwanza
> muhimu ni kufanya upelelezi ili kupata ushahidi unaomhusisha mtu
> anayeshukiwa na kosa linalohusika. Upelelezi sio lazima uanze baada ya
> kupokea malalamiko ingawa hiyo ndiyo njia kuu ya kuanzisha upelelezi:
> yaani mtu anatendewa kosa na mtu anayemfahamu au asiyemfahamu na
> kwenda kituo cha usalama kutoa taarifa ya tukio hilo. Lakini, mathalan
> hata polisi wenyewe wanaweza kukuta mtoto mchanga ametupwa ndaniya
> pipa au mtu ameuawa na kutupwa kando ya barabara. Hiyo huwa namna ya
> pili ambayo husababisha upelelezi kufanyika.
>
> Katika nchi nyingine upelelezi huweza kufanywa na mtu binafsi ambaye
> analalamika kutendwa kosa linalohusika au anaweza kumwajiri mtaalamu
> wa shughuli hiyo. Hali hiyo hufanyika zaidi kwa kuwa na imani kubwa
> juu ya uwezo wa mtaalam fulani kuliko kuliacha suala lote la upelelezi
> mikononi mwa polisi. Kinadharia, hapa Tanzania, mlalamikaji dhidi ya
> kosa la jinai hakatazwi kufanya upelelezi wake binafsi kumpata
> mhalifu. Lakini kwa kawaida kazi hiyo iko mikononi mwa Mkurugenzi wa
> Upelelezi wa Jinai kwenye Jeshi la Polisi.(Sheriaya Jeshi la Polisi,
> Sura ya 322)
>
> Haikusudiwi kuingia katika mjadala wa mbinu zenyewe za upelelezi wa
> makosa ya jinai ambazo hutegemeana sana na aina ya makosa na mazingira
> yenyewe. Badala yake masuala muhimu kuambatana na hatua hii ya
> upelelezi yatajadiliwa. Nayo ni mtuhumiwa na mshitakiwa, hati ya kutia
> nguvuni, hati ya kupekuwa, hati ya kuita shaurini, maelezo ya
> mshitakiwa na mashahidi, pia dhamana.
>
> Mtuhumiwa na Mshitakiwa
>
> Mara nyingi upelelezi unapoanza huwa kuna mtu anayetuhumiwa kwamba
> ndiye aliyetenda kitendo kilichosababisha kosa linalohusika. Kunaweza
> kuwa na ushahidi wa mazingira au hata wa moja kwa moja kwamba mtu
> fulani ametenda kosa hilo. Mpelelezi anayehusika na kesi yenyewe
> hukusanya ushahidi wote huo na kutoa maoni yake kwa kiwango gani
> mshukiwa anahusika na ushahidi huo.
>
> Iwapo ushahidi unaonekana kumwelemea na kumhusisha mtuhumiwa na kosa
> linalohusika basi hufunguliwa mashitaka naye huitwa mshitakiwa.
> Mashitaka huanza pale hati ya mashitaka dhidi ya mshitakiwa
> inapowasilishwa mahakamani.
>
> Uamuzi sahihi wa kumfungulia mashitaka mtuhumiwa hutegemea sana
> kiwango cha uwezo wa anayechukua uamuzi huo katika kuupima ushahidi
> uliopatikana katika upelelezi dhidi ya mtuhumiwa. Kinadharia mtuhumiwa
> hufunguliwa mashitaka pale ambapo ushahidi wa kutosha umepatikana
> kiasi cha kuweza kufungua na kuendesha mashitaka dhidi yake
> kikamilifu. Lakini kwa bahati mbaya, kiutendaji, hivyo sivyo kama
> ambavyo itaonekana sura inayofuatia.
>
> Hati ya kupekua
>
> Ili kupata ushahidi dhidi ya mtuhumiwa mara nyingi inabidi apekuliwe
> mwenyewe au sehemu anamoishi. Kitendo cha kumpekua mtu huingilia uhuru
> na hata hadhi yake hivyo ni lazima kifanywe kwa mujibu wa masharti yasheria.
>
> Kuna namna mbili za kufanya upekuzi kwa njia ya halali. Kwanza ni
> kupata hati ya kupekua kutoka mahakama yoyote iliyo karibu na tukio
> lenyewe (F. 40,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, Na. 1, 1985).
>
> Pili kupata hati ya kupekua kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi. Kwa
> kawaida hati hizi za njia ya pili hutolewa kwa Polisi. (F. 38,Sheria
> ya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Hati ya kupekua inaweza ikatolewa na kutekelezwa siku yoyote ile hata
> Jumapili. (F. 40,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Kwa kawaida
> upekuzi hufanyika asubuhi hadi jioni lakini mahakama huweza kuamuru
> upekuzi ufanywe saa yoyote ile kama yanaona sawa kufanya hivyo.
>
> Inatokea kuwa wakati wa kutaka kufanya upekuzi jengo au sehemu ya
> kupekuliwa imefungwa na mtuhumiwa hayupo. Ikiwa atakuwepo mtu mwingine
> yeyote anayeishi ndani ya jengo au sehemu hiyo au ana milki yake, mtu
> huyo atatakiwa kumpa polisi au yeyote mwenye hati hiyo, (baadaya
> kuonyeshwa), ruhusa na msaada wa kufanya upekuzi. (F. 43,Sheriaya
> Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Polisi au mtu mwenye hati ya upekuzi anaweza kutumia nguvu za kutosha
> kama vile kuvunja na kuingia au kutoka ndani ya jengo linalohusika
> kutekeleza amri hiyo. (F. 43 (2),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Licha ya majengo, mtuhumiwa mwenyewe anaweza kupekuliwa. (F.42,Sheria
> ya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Iwapo mtuhumiwa ni mwanamke atapekuliwa
> na mwanamke mwenzake. Mwisho wa upekuzi hati itarejeshwa mahakamani
> ikionyesha kitu au vitu ambavyo vimepatikana. (F. 45(2),Sheriaya
> Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Vitu hivyo vilivyopatikana vitahifadhiwa hadi mwisho wa upelelezi au
> shauri lenyewe. Kama mtuhumiwa atashitakiwa na kupatikana na hatia
> kitu hicho (ambacho kitakuwa kielelezo) kitashughulikiwa kwa mujibu washeria. Na kama mshitakiwa amekata rufaa basi kitahifadhiwa hadi
> wakati wa kusikiliza rufani hiyo. Iwapo mshitakiwa amepelekwa Mahakama
> Kuu hicho kitahifadhiwa hadi wakati wa kusikilizwa shauri lake. (Hapa
> inahusiana na mashitaka ambayo husikilizwa na mahakama Kuu tu, kama
> vile kuzinga na maharimu, mauaji, uhaini na kadhalika).
>
> Maelezo ya Mtuhumiwa, Mshitakiwa na Mashahidi
>
> Mtuhumiwa, mshitakiwa na mashahidi wanaweza kutakiwa kutoa maelezo
> polisi ili kusaidia upelelezi na uendeshaji wa mashitaka. Utaratibu wa
> kuandika maelezo ya watu hao unatofautiana kama ambavyo itaelezwa hapa
> chini.
>
> Tukianza na mashahidi ni kuwa polisi wana uwezo wa kumwita na kumhoji
> mtu yeyote ambaye wanaamini anaweza kutoa taarifa kusaidia upelelezi
> wa kesi inayohusika. (F.32.Sheriaya Jeshi la Polisi, i.h.j. Pia F.46
> (1)Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Kama ni lazima maelezo ya mtu huyu yatanakiliwa na polisi. Maelezo
> hayo yanaweza baadaye kutumika katika kuendesha na kuthibitisha
> shitaka dhidi ya mshitakiwa. Kwa kawaida polisi huandika maelezo hayo
> wenyewe kadiri shahidi anavyoeleza. Mwisho humsomea Shahidi maelezo
> hayo na kumtaka afanye masahihisho yoyote kama yapo. Shahidi hutakiwa
> kuweka saini katika maelezo yake pamoja na saini ya mwandishi wa
> maelezo hayo. (F.48,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Itabidi amfungulie mashitaka rasmi mtuhumiwa huyo halafu amhiarishe
> kama bado anapenda kutoa maelezo yake au la. (F.52(1),Sheriaya
> Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Katika kufanya hivyo ni lazima mahakamani.
> (F.32(4),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Pia amueleze kuwa iwapo
> atakataa kumpa maelezo yoyote yanayoweza kuwa ushahidi kuhusiana na
> shitaka lenyewe atafikiriwa kuwa amefanya hivyo kwa nia ya kujiepusha
> na shitaka hilo. (F.52(4),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Maana ya mashauri hayo dhidi ya mshitakiwa ni kujaribu kupata ushahidi
> muhimu kutoka kwake bila ya vipingamizi, lakini kwa hiari. Kwa kawaida
> polisi hawamuachii mshitakiwa atoe na kuandika maelezo yake mwenyewe
> bali humhoji na kuyaandika maelezo hayo. Askari wengine wanadai kuwa
> bila ya kumhoji mshitakiwa huwezi kupata ushahidi muhimu na wala
> huwezi kujua kama anasema kweli au anadanganya.
>
> Utaratibu huu una tatizo moja kubwa katika utoaji haki kwa mujibu washeria. Ni hivi: polisi na upande wa mashitaka wanapoamua kuendesha
> kesi mahakamani huwa wanao ushahidi muhimu (kama mshitakiwa hakutoa
> maelezo ya uwongo) dhidi ya mshitakiwa. Lakini mshitakiwa huwa haelewi
> hali na uzito wa ushahidi wa upande wa mashitaka. Jambo hili lastahili
> kurekebishwa ili kumwezesha mshitakiwa aandae utetezi wake vizuri.
> Hivi sasa utaratibu huo unafanyika katika mashauri ambayo
> yanatanguliwa na Uchunguzi wa Awali kabla hayajasikilizwa na Mahakama
> Kuu.
>
> Aidha, huweza kutumika katika mashauri ya madai. Pengine inasahauliwa
> kwamba baadhi ya mashauri katika mahakama ya wilaya ni magumu kisheria
> na kiushahidi kuliko hata yale yanayosikilizwa na Mahakama Kuu kwa
> mara ya kwanza. Na kwamba mashauri ya jinai huadhibiwa kwa kifungo au
> faini au vyote pamoja, hivyo kuna haja kubwa ya kumpa mshitakiwa kila
> nafasi ya kuandaa utetezi wake vizuri.
>
> Mashahidi wa nyongeza kabla ya hukumu
> Na Dkt. Abdallah J. Saffari
>
> KATIKA haja ya kuhakikisha kuwa ushahidi wote muhimu unapatikana kabla
> ya hukumu kutolewa mahakama yana mamlaka ya kuita mashahidi wa
> nyongeza (F. 195,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Kwanza
> tutaangalia jinsi uamuzi huo unavyoweza kuchukuliwa katika uendeshaji
> wa shauri kwa mara ya kwanza. Katika hatua hiyo mahakama yanaweza
> kuwaita mashahidi wa nyongeza kwa namna moja kubwa. Inawezekana wakati
> shahidi wa upande wowote ule anapotoa ushahidi akawa anamtaja mtu
> mwingine ambaye hakuitwa kabisa kutoa ushahidi. Mahakama yanaweza
> kuona kwamba mtu huyo ambaye hakuitwa na upande unaohusika labda
> anaweza kutoa ushahidi muhimu kufikia uamuzi sahihi wa shauri hilo.
> Hata hivyo, mara nyingine sio lazima shahidi huyo awe amemtaja mtu
> fulani katika ushahidi wake pale mahakamani. Kumbukumbu za maelezo
> yake mbele ya askari au afisa yoyote yule mathalan Mlinzi wa Amani
> kabla ya kusikilizwa kwa shauri hilo zinaweza kuonyesha kwamba kuna
> mtu ambaye ametajwa, ambaye kama akiitwa mahakamani, anaweza kutoa
> ushahidi kugundua mtu gani anaweza kuitwa kama shahidi wa nyongeza
> mbali na njia hizo mbili. Hata hivyo, kinadharia, mahakama bado yana
> mamlaka na uwezo wa kumwita mtu yeyote yule kama shahidi ilimradi kuna
> imani kwamba anaweza kutoa ushahidi wa maana katika uamuzi wa shauri
> linalohusika (F. 142,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> Mashahidi muhimu katika shauri wanaweza wasiitwe na pande zinazohusika
> bila ya kukusudia au pengne kwa makusudi kabisa. Aghalabu kila upande
> unakuwa na haja ya kushinda kesi kwa kila hali. Wakati mwingine, kwa
> nia njema kabisa, upande mmoja unaweza ukaacha kumwita shahidi wa
> maana pengine kwa imani tu kuwa ushahidi wake sio muhimu hata kidogo,
> au labda kwa dhana kuwa tayari umeshatolewa na kutomwita shahidi
> muhimu ikawa ni kuficha kweli. Ya kwamba iwapo shahidi huyo ataitwa
> mahakamani basi atasema kweli ambayo itaukandamiza upande unaohusika.
>
> Bila ya kujali makusudi hayo mawili matokeo ya kutoitwa mashahidi hao
> muhimu ni mmoja: Kuathiri utoaji hukumu ya haki.
>
> Katika shauri la R.V. Lawrent Kihwele (Shauri Maalum la Jinai Na. 50,
> 1977, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mbeya (Haijachapishwa) mshitakiwa,
> Mmasi, alishitakiwa kwa kumwua kwa makusudi kijana mdogo aliyekuwa
> akichunga ng'ombe wa baba yake katika shamba la mshitakiwa. Wakati wa
> tukio hilo mshitakiwa alikuwa na kaka yake. Jamhuri ilichelea kumwita
> kaka yake huyo kwa hofu kuwa asingetoa ushahidi wa kweli. Mshitakiwa
> alipokuwa anatoa ushahidi alikiri kuwa wakati wa tukio alikuwa na kaka
> yake, lakini hata hivyo hakupenda kumwita kama shahidi. Mahakama
> yalitumia uwezo wake kumwita shahidi huyo. Shahidi huyo alikuwa
> hakutoa maelezo marefu kuhusiana na mauaji yenyewe mbele ya polisi
> miaka kadhaa kabla ya shauri lenyewe kusikilizwa. Ushahidi wake, hata
> baada ya kuitwa na mahakama, ukawa hauna uzito wowote ule. Hapana
> shaka, hata hivyo, kuwa hatua hiyo ya mahakama ilikuwa katika kutafuta
> kweli - ushahidi sahihi ili kufikia uamuzi wa haki katika shauri.
> Hatimaye mshitakiwa alipatikana na hatia ya mauaji ya kutokusudia
> kutokana na ushahidi wa mazingira ingawa yeye alikana kosa kabisa kuwa
> hakumpiga na kumwua marehemu.
>
> Katika shauri la Joseph Mwinuka v R. (Shauri la Jinai la Rufani Na.
> 159, 1979, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mbeya (haijachapishwa) ambapo
> mshitakiwa alikabiliwa na shitaka la wizi wa shilingi 16,483.20 upande
> wa mashitaka uliacha kumwita shahidi muhiju Edward Mapunda. Lakini
> mahakama yalimwita shahidi huyo na kumtia hatiani mshitakiwa sio kwa
> wizi wa shilingi 16,483.20 kama ambavyo ilidaiwa bali shilingi
> 9,340.15.
>
> Wakati wa kusikiliza shauri kwa mara ya kwanza kwa kawaida mahakama
> huwaita mashahidi wa nyongeza mwisho kabisa wakati pande zote mbili
> wamemaliza kuita mashahidi wao. Lakini mahakama yanaweza kumwita
> shahidi wa nyongeza wakati wowote katika hatua ya kusikilizwa shauri
> hilo iwapo kufanya hivyo kutasababisha ufanisi. Sababu kuchelewa
> kumwita shahidi huyo kunaweza kuathiri mfululizo wa ushahidi, ambapo
> kung'ang'ania kufanya hivyo kunaweza kuchelewesha shauri hasa pale
> ambapo shahidi huyo hayupo mahakamani na anahitaji muda mrefu
> kupatikana. Kumwita shahidi huyo katikati ya shauri kunaweza kuwa na
> athari ya kuingilia mpango au utaratibu wa kuendesha shauri kwa upande
> ambao wakati huo unafanya hivyo. Shahidi wa mahakama au wa ziada
> huhojiwa na mahakama yenyewe. Pande zinazohusika katika shauri huweza
> kumhoji kwa ruhusa ya mahakama. Vinginevyo utaratibu wote wa kuhoji ni
> kama ule mintaarafu ya shahidi mwingine yeyote yule.
>
> Kuita mashahidi wa ziada hakuishii tu katika hatua ya kwanza ya
> kusikiliza shauri. Mahakama yana mamlaka ya kufanya hivyo hata wakati
> wa kusikiliza rufani. Yanaporidhika kwamba ushahidi huo wa nyongeza ni
> lazima yataandika kuelezea sababu zake kisha yanaweza kuchukua
> ushahidi huo yenyewe au kuyaamuru mahakama ya chini kuchukua ushahidi
> huo kwa niaba yake (F. 360 (1),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
> Iwapo yatafuata hatua ya pili mahakama ya chini yatachukua ushahidi wa
> shahidi anayehusika na kupeleka kumbukumbu ya ushahidi huo katika
> mahakama ya juu ambayo yatautilia maanani wakati wa kuandika hukumu.
>
> Jambo hili linadhihirisha umuhimu wakuwa na ushahidi sahihi ili
> kufikia uamuzi wa haki. Masuala ya ushahidi yanaweza kubishaniwa
> katika rufani ya kwanza isipokuwa ya pili mpaka kwa ruhusa maalum ya
> mahakama ya rufani yanayohusika (K. 65, Kanuni za Mahakama ya Rufani
> Na. 15, 1979).
>
> Kwa bahati mbaya mahakimu wengi na baadhi ya majaji hawatumii uwezo
> waliopewa chini ya mafungu haya yasheriainavyopasa. Mfano mzuri ni
> shauri la R.v. Wilbert Mushi (Shauri la Jinai la Rufani Na. 31,
> Mahakama Kuu ya Tanzania, Mbeya (Haijachapishwa) ambapo ilidaiwa
> kwamba mrufani alipokea rushwa ya shilingi 1,000 kutoka kwa mtu
> aliyeitwa Idd Bakari ili mrufaniwa achomoe vielelezo vya ushahidi
> kwenye jalada la kesi dhidi ya mtu aliyeitwa Erick Nyonyona. Wakati
> kesi hiyo inasikilizwa mara kwa mara jina la Erick Nyonyona lilitajwa
> na baadhi ya mashahidi. Hata hivyo mwisho wa kesi Erick Nyonyona
> mwenyewe hakuitwa na upande wa mashtaka. Mahakama hayakutumia uwezo
> wake kumwita shahidi huyo wa maana sana kuthibitisha kama kweli
> mrufani aliomba na kupokea rushwa ili amsaidie huyo Erick Nyonyona.
> Kwa kushindwa kufanya hivyo ushahidi huo muhimu mno ulikosekana.
> Badala yake mara tu baada ya mshitakiwa kumaliza kujitetea Hakimu
> aliyesikiliza kesi hiyo aliandika hukumu kumtia hatiani mshitakiwa
> kama alivyoshitakiwa.
>
> Wilbert Mushi alikata rufani katika Mahakama Kuu dhidi ya hukumu hiyo
> ya mahakama ya Wilaya. Katika hukumu yake ndefu kiasi Jaji Mwakibete
> alisema: "Hakuna shaka ushahidi unathibitisha kwamba mrufani alipokea
> noti zilizowekwa alama kutoka kwa Idrisa Bakari zenye thamani ya
> shilingi 1000. Lakini sio kitendo cha kupokea fedha pekee kinachozua
> kosa ambalo kwalo mrufani ameshitakiwa". Mheshimiwa Jaji huyo
> aliendelea kusema: "Upande wa mashitaka ulidai kuwa mrufani alimfuata
> Erick Nyonyona kumwomba shilingi 1000 kwa kubadilishana na vielelezo
> vya ushahidi wa kesi dhidi ya Erick Nyonyona. Mrufani alikana dai
> hilo. Inadaiwa kwamba mrufani aliomba rushwa hiyo wakati akiwa yeye na
> Erick Nyonyona tu. "Kwa maoni yangu inaonekana ni Erick Nyonyona pekee
> anayeweza kuthibitisha kweli au uongo wa madai hayo pamoja na
> kuyaeleza mahakama mazingira ya maombi hayo ya rushwa iwapo kweli
> yalifanyika". (Msisitizo ni wangu).
>
> Kwa sababu hizo rufani ya Wilbert Mushi iliruhusiwa.
>
> Ni kweli kwamba kama upande wowote unashindwa kumwita shahidi
> anayeonekana ni wa maana katika shauri linalohusika dhana ni kuwa
> laiti shahidi huyo angeitwa na upande huo angetoa ushahidi dhidi yake.
> Hivyo pengine ni sawa kusema au kufikiri kuwa upande wa mashitaka
> uliogopa kumwita Erick Nyonyona kwa vile angetoa ushahidi dhidi yao.
> Bali pamoja na hayo yote haki katika shauri hili ilihitaji Erick
> Nyonyona aitwe hata katika hatua hii ya rufani. Kwamba kufanya hivyo
> kungekuwa sawa na kuusaidia upande wa mashitaka, kwa sasa , sio lazima
> amwite shahidi huyo hata kama aina ya ushahidi atakaoutoa unasaidia
> upande wa mashitaka (Kolukuna Otim v R. (1963) E.A. 253, na kufuatiwa
> baadaye katika Faustin Manoni v. R (1969) H.C.D. n.29). Izingatiwe
> kwamba shahidi wa aina hiyo ataitwa inapolazimu tu.
>
> Katika kesi maarufu ya hivi karibuni ya Abel Mwanga v Elisaph Lima
> (Shauri la Madai la Rufani Na. 4 1982, Mahakama ya Rufani Tanzania,
> Mwanza (Haijachapishwa) Mahakama ya Rufani ya Tanzania yalipinga hoja
> ya wakili wa mrufani kwamba Mahakama Kuu yaliyosikiliza shauri hilo
> mara ya kwanza yalistahli kumwita shahidi mmoja kwa vile mahakama hayo
> yaliona hakuna haja ya kufanya hivyo pale ambapo kweli
> imeshadhihirika.
>
> On Nov 12, 4:01 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:> Na. Dkt. Abdallah Saffari
>
> > Mshitakiwa anaweza kukata rufani dhidi ya amri ya kulipa fidia
> > iliyotolewa na mahakama katika shauri la jinai (F. 348(3),Sheriaya
> > Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Mbali ya mlalamikaji, fidia inaweza
> > kutolewa hata kwa mshitakiwa ambaye hakuonekana na hatia iwapo
> > mahakama yanaona mashitaka dhidi yake yalikuwa hayana msingi (F. 347,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Fidia hiyo ni kwa usumbufu na
> > hasara iliyopatikana.
>
> > Hata hivyo ni nadra sana mshitakiwa kulipwa fidia kwa mujibu wa fungu
> > hili lasheria.
>
> > Amri nyingine
>
> > Mbali na adhabu mbalimbali zilizoelezwa kwa kifupi juu ya mahakama pia
> > yanaweza kutoa amri nyingine nyingi dhidi ya mhalifu kufuatana na
> > mazingira ya kosa lenyewe. Mathalan yanaweza kuamuru mali inayohusika
> > na kosa lenyewe irejeshwe kwa mwenyewe kama yupo (F. 357(a),Sheriaya
> > Mwenendo wa Jinai, i.h..j). au ishughulikiwe kama mali isiyo na
> > mwenyewe.
>
> > Katika makosa mengine kama ya usalama barabarani, mahakama yanaweza
> > kumnyang'anya mshitakiwa leseni ya udereva (Sheriaya Usalama
> > Barabarani, Na. 30, 1973)
>
> > Amri nyingine muhimu sana ni kuachiwa kwa masharti au bila ya masharti
> > (F. 38, Kanuni ya Adhabu, i.h.j) . Amri hii ni maarufu kwa jina la
> > kifungo baridi. Yaani iwapo kutokana na mazingira ya shauri lenyewe
> > kama vile uzito wa kosa au tabia ya mhalifu, mahakama yataona sio
> > vyema kutoa adhabu, basi yanaweza kumwachia mhalifu bila ya masharti.
> > Au yanaweza kumwachia kwa masharti kama vile asitende kosa jingine
> > katika kipindi fulani. Mahakama yanawajibika kumwelewesha mshitakiwa
> > kuwa iwapo atavunja masharti hayo yaliyowekwa ataadhibiwa kwa kosa
> > alilolitenda awali.
>
> > Namna ya kutoa adhabu
>
> > Mahakama yanatakiwa kutoa adhabu au amri yoyote ile inayofaa (na
> > kuonyesha wazi katika mwenendo wa shauri) kwa kila kosa ambalo
> > mshitakiwa ametiwa hatiani (Meyerowitz (1947) 14 E.A.C.A. 130). Kama
> > makosa ni matano basi kila kosa litakuwa na adhabu yake. Mahakama
> > yataamua jinsi ya kutumikia adhabu hizo. Mshitakiwa anaweza akatakiwa
> > kutumikia kila adhabu pekee (F. 168(2),Sheriaya Mwenendo wa Jinai,
> > i.h.j). Kwa mfano ikiwa amepatikana na hatia ya makosa mawili
> > mbalimbali na kuhukumiwa kifungo, basi ataanza kutumikia kifungo cha
> > kosa la kwanza, halafu ndipo ataendelea kutumikia kifungo cha kosa la
> > pili. Lakini kwa vyovyote vile idadi ya miaka ya kutumikia kifungo
> > haitazidi kumi (F. 168(3),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> > Njia ya pili, ambayo ndiyo hutumika zaidi, ni kuzitumikia adhabu za
> > makosa yote kwa pamoja (F. 168(2),Sheriaya Mwenendo wa Jinai,
> > i.h.j).Mshitakiwa atatumikia ile adhabu kubwa kupita nyingine (F.
> > 168(5),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Hivyo hata kama makosa ni
> > arobaini, pengine yote ya wizi na yametolewa adhabu ya kifungo,
> > mshitakiwa atatumikia kifungo kile kikubwa kupita vifungo vingine
> > katika makosa hayo. Mahakama hutumia njia hii zaidi wakati makosa
> > yanayohusika yametendeka wakati mmoja (Sawedi Mukasa v. R. (1946) 1
> > E.A.C.A. 97). Kwa mfano makosa kama vile wizi (F.265, Kanuni ya
> > Adhabu, i.h.j) na kughushi maandishi (F.337, Kanuni ya Adhabu i.h.j)
> > yanaweza kutendeka kwa kutumia hundi moja, wakati na siku moja tu.
>
> > Mahakama yanao uwezo wa kuchanganya aina za adhabu, kama vile kifungo
> > na viboko au na faini. Lakini Hakimu wa Wilaya ambaye siye Mwandamizi
> > hawezi kuchanganya adhabu ya viboko na aina nyingine mpaka
> > ithibitishwe na Mahakama Kuu (F.167,Sheriaya Mwenendo wa Jinai,
> > i.h.j).
>
> > Pamoja na yote hayo ikumbukwe kuwa kila shauri linaamuliwa kulingana
> > na mazingira yake. Adhabu, halikadhalika, hutolewa kufuatana na
> > mazingira ya shauri lenyewe.
>
> > Kuitumikia adhabu
>
> > Kwa kawaida adhabu ya kifungo huanza kutumikiwa mara baada ya kutolewa
> > (F. 327,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j) isipokuwa ikiwa
> > mshitakiwa ataomba na kupewa dhamana kabla ya kusikilizwa rufani yake
> > (F. 368,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Adhabu pia inaweza
> > isitumike kwa masharti kuwa mshitakiwa hatatenda makosa katika kipindi
> > kisichozidi miaka mitatu (F. 326(1),Sheriaya Mwenendo wa Jinai,
> > i.h.j). Iwapo ni adhabu ya faini pekee italipwa katika kipindi ambacho
> > mfungwa anaweza kukata rufani kupinga adhabu hiyo. Na iwapo adhabu
> > mbili, kifungo au faini zimetolewa, mahakama yanaweza kumpa dhamana
> > mshitakiwa, kwa masharti au bila masharti, alipe faini hiyo katika
> > muda wa siku kumi na tano (F.330(1),Sheriaya Mwenendo wa Jinai,
> > i.h.j). Mwisho wa muda huo mahakama yataamua mshitakiwa aanze
> > kukitumikia kifungo kama atashindwa kuilipa (K.h.j). Lakini bado muda
> > wa kulipa faini hiyo unaweza kuongezwa tena kwa sababu za kutosha
> > (K.h.j).
>
> > Utaratibu ulioelezwa hapo juu unahusiana, kwa kiwango kikubwa, na
> > jinsi ya kuzitumikia adhabu nyingine isipokuwa kifo.
>
> > Kwa vile adhabu ya kifo ni nzito mno utaratibu wake ni mrefu vile
> > vile. Kwanza, kwa kawaida mashauri yote ambayo kwayo mshitakiwa
> > amehukumiwa kifo, hupelekwa Mahakama ya Rufani kubishaniwa tena, na
> > pili hata pale rufani ya mshitakiwa inapokataliwa, bado adhabu ya kifo
> > haiwezi kutekelezwa mpaka Rais wa Jamhuri ameidhinisha adhabu hiyo (F.
> > 325,Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).
>
> > Mambo ya kutiliwa maanani katika utoaji wa adhabu
>
> > Baadhi ya waandishi wa vitabu (Brown, D. Criminal Procedure in Uganda
> > and Kenya, Toleo la Pili, London, 1970, uk. 126-130) wameorodhesha
> > mambo ambayo hutiliwa maanani wakati wa utoaji adhabu. Baadhi yake ni
> > chanzo cha kosa lenyewe, uzito wake, tabia ya mkosaji kabla ya kosa na
> > wakati wa mashitaka, makosa ya zamani, wingi wa kosa lenyewe, usalama
> > wa jamii, hali ya familia ya mkosaji na kadhalika.
>
> > Hakika yote hayo ni mambo yanayostahili kuzingatiwa wakati wa utoaji
> > adhabu lakini pengine chanzo cha kosa lenyewe ndiyo suala kubwa kupita
> > yote. Kwa nini magereza yamejaa zaidi watu wa kipato cha chini?
> > Wafungwa wengi hutenda makosa kinyume na ridhaa yao bali kwa msukumo
> > wa mazingira magumu. Suala hili ni la maana sana kutiliwa maanani
> > katika makosa ya wizi, ambayo ndiyo mengi sana kuliko yoyote. Kwa
> > maana hii basiSheriaya Viwango vya Chini vya Adhabu (SheriaNa. 1,
> > 1972) hailiangalii suala la adhabu katika mtazamo sahihi hususan kwa
> > sababu kadhaa. Mosi inalirahisisha tatizo la uhalifu, hasa wa mali ya
> > umma, kuweza kutatuliwa kwa njia ya vifungo virefu. Hii sio sahihi.
> > Pili inaweka ubaguzi mkubwa wa utoaji adhabu kwa vile karani wa
> > serikali au shirika la umma atafungwa miaka mitano na kuendelea kwa
> > wizi wa shilingi mia na hamsini tu wakati ambapo wa laki moja, mali ya
> > raia, anaweza kufungwa miezi miezi michache tu. Tatu, basisheriahii
> > inaelekea kudharau usalama wa raia binafsi na mali yao, jambo ambalo
> > ni muhimu mno kwa vile taifa ni watu.Sheriaimeingilia mno kauli
> > adhimu ya uendeshaji wa mashauri kwamba kila shauri liamuliwe kutokana
> > na mazingira yake. Mahakama yanaweza kubainisha kosa zito na mazingira
> > ambayo adhabu kali inastahili bila ya kuyalazimisha kupitisha adhabu
> > kubwa kwa makosa ambayo kwa kweli, mengine, hayastahili adhabu hizo.
> > Isitoshe siku zote serikali inaweza kukata rufani kupinga uamuzi wa
> > mahakama ambayo yanaona yametoa adhabu ndogo kupita kiasi.
>
> > On Nov 12, 3:58 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>
> > > Dk. Abdallah J. Saffar
>
> > > Mamlaka
>
> > > MAHAKAMA ya Wilaya na Mahakama Kuu yana mamlaka ya kuangalia usahihi
> > > na uhalali wa hukumu na uamuzi wa mahakama yaliyo chini yake na kuweza
> > > kusahihisha makosa yaliyopo. Kwa hali hiyo basi mahakama ya Wilaya
> > > yanaweza kutumia mamlaka yake hayo juu ya Mahakama ya Mwanzo (F.22
> > > (a),Sheriaya Mahakama ya Mahakimu, Na. 2, 1984) ambapo Mahakama Kuu
> > > yanaweza kutumia mamlaka hayo juu ya Mahakama ya Wilaya (F. 373,
> > >Sheriaya Mwenendo wa Jinai, Na. 9, 1985).
>
> > > Utaratibu
>
> > > Kwa kawaida mahakama yanayohusika yatafanya masahihisho hata bila ya
> > > kupata maombi ya kufanya hivyo kutoka kwa mlalamikaji. Mara nyingine
> > > Mahakimu Wakaguzi (F. 22(1),Sheriaya Mahakama ya Mahakimu, i.h.j)
> > > huorodhesha mashauri yote ambapo pengine yatahitaji kusahihishwa na
> > > Mahakama ya Wilaya au Mahakama Kuu kadiri ilivyo.
>
> > > Mtu ambaye hakuridhika na hukumu au uamuzi wowote ule wa Mahakama ya
> > > Mwanzo au Wilaya anaweza kuyaomba Mahakama ya Juu kufanya masahihisho.
> > > Hivyo iwapo shauri lenyewe lilishughulikiwa na Mahakama ya Mwanzo
> > > maombi yatapelekwa Mahakama ya Wilaya; iwapo awali shauri hilo
> > > lilishughulikiwa na Mahakama ya Wilaya, maombi yatapelekwa mahakama
> > > Kuu (F. 373,Sheriaya Mwenendo wa Jinai , i.h.j).
>
> > > Jamhuri, halikadhalika, inaweza kuwa mlalamikaji na kuwasilisha maombi
> > > yake ya kufanya masahihisho mbele ya mahakama yanayostahili.
>
> > > Uwezo
>
> > > Katika kutumia uwezo wa masahihisho Mahakama Kuu (K.h.j) na Mahakam ya
> > > Wilaya (F.22(2),Sheriaya Mahakama ya Mahakimu, i.h.j) yana uwezo
> > > kama ule yaliyopewa katika mashauri ya rufani. Isipokuwa mahakama hayo
> > > hayawezi kumtia hatiani mshitakiwa ambaye aliachiwa huru na mahakama
> > > ya awali (F.373(4),Sheriaya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Vile vile
> > > hayawezi kutoa amri yoyote dhidi ya mlakamikaji bila ya kumpa fursa ya
> > > kujitetea binafsi au kupitia wakili wake.
>
> > > Sababu za kufanya masahihisho zinatofautiana na ni nyingi. Baadhi yake
> > > ni kama hizi zifuatazo:
>
> > > Kutiwa hatiani kinyume chasheria
>
> > > (a) Kutokuwepo kwasheriainayodaiwa
>
> > > Katika Lawrence Mwanga v. R (Shauri la Jinai la Masahihisho Na. 12
> > > 1981, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam (Haijachapishwa)
> > > mshitakia alipatikana na hatia ya kutumia vibaya kibali cha Jumapili
> > > kinyume cha Tangazo la Serikari Na. 264 la 1/11/1974 pamoja na kifungu
> > > cha 61 chaSheriaya Usalama wa Barabara Na. 30/75. Mnamo tarehe
> > > 31/11/1981 Jaji Ruhumbika alibatilisha hukumu ya awali na kumwachia
> > > huru mshitakiwa kwa vile alishitakiwa na kutiwa hatiani kutokana na
> > >sheriaisiyokuwepo nchini Tanzania.
>
> > > Uamuzi kama huo pia ulipitishwa na Jaji Kiongozi Nassoro Mnzavas
> > > katika shauri la Benedicto Edward v. R (Shauri la Jinai la
> > > Masahishisho Na. 12, 1981, Mahakama Kuu ya Tanzania,
>
> > ...
>
> > read more »

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment