Tuesday 28 August 2012

Re: [wanabidii] Neno La Usiku: CCM Na Sifa Ya Mchawi!

Asante sana Gaston!

2012/8/29 Gaston Mbilinyi <mbilinyi.gaston49@gmail.com>
Pamoja na mazuri tunayoweza kuyaona na kusikia juu yao, nawachukia
wachawi na hakika naichukia ccm. Hapa nusura nikuchukie na wewe
uliyeleta hoja hii.

Kilichosaidia nisikuchukie mtoa hoja ni kwamba wewe ni mtu wangu tangu
unaabdikia gazeti la Rai mpaka humu Jamvini ingawa wewe hulijui hili!

Hivyo naamini kuwa ujumbe wako utakuwa una kitu ambacho sijakibaini,
kwanini nikuchukie kama ninavyowachukia wachawi na ccm?

On 8/29/12, maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu,
>
> Usiku wa saa sita  umeingia tena hapa Iringa. Kabla sijaondoka kwenye meza
> ya kibarua changu nina neno fupi la usiku.
>
>  Naam, inasemwa, kuwa mchawi mchukie, lakini, sifa yake mpe, anajua kuroga!
>
>  Majuzi hapa nilipokuwa kwenye shughuli za kijamii kijijini Mahango,
> Madibira, kuna kitu kilichonifanya nishangae, lakini, baada ya tafakuri
> nikauona ubunifu kwa aliyekitenda.
>
>  Nikiri, kuwa huko nyuma  nimefanya vikao kadhaa na Kamati ya Shule ya
> Mahango chini ya Uenyekiti wa Bw. Victor Kadama ( Pichani).  Sikupata kujua
> kuwa Victor Kadama, mbali ya kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Shule, pia ni
> Katibu Mwenezi wa CCM, Kata ya Madibira. Ndio, Victor Kadama ndiye Nape
> Nnauye wa Madibira.
>
>  Maana, kwenye vikao vyetu hakuwahi hata siku moja kuvaa nguo za rangi ya
> chama chake wala kofia. Lakini, majuzi hapa tulipokuwa na mkusanyiko mkubwa
> wa wanakijiji kuwapokea wageni kutoka Norwich, Uingereza  waliokuja
> kuzindua mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Kijamii kijijini hapo, basi, kwa
> siku mbili mfululizo, nilimwona Bw. Victor Kadama akiwa ametinga kofia ya
> chama chake, CCM.
>
>  Bw. Kadama  kwa siku zote mbili hakuongea hata neno moja kuhusu chama
> chake, lakini, kofia yake ilikuwa inaongea.  Kulikuwa na uwepo wa CCM
> kupitia kwa kofia ya Kadama. Na hata  wageni waipopangiwa ziara ya miguu
> kuona mazingira ya kijiji, Victor Kadama na kofia yake haraka alichukua
> jukumu la kuongoza msafara.  Aliendelea kufanya ' kazi ya uenezi' wa Chama
> chake.
>
>  Kwa vyama vingine vya siasa kuna ya kujifunza kutoka kwa CCM. Pamoja na
> dhambi zao zote, CCM bado wana oganaizesheni inayoeleweka na  yenye kufikia
> hadi ngazi za vitongoji. Ni mtaji wao mkubwa kisiasa. Tofauti na vyama
> vingine, makada wa CCM wanajipenyeza kila mahali, iwe kwenye kamati za
> shule au za kuchimba visima. Ndio, hata, uwe na harusi ya mwanao, bado kuna
> makada wa  CCM watakaojipenyeza kwenye Kamati za harusi.
> Naam, mchawi mchukie, lakini sifa yake mpe, anajua kuroga, hakyamungu!
>
>  Maggid,
> Iringa.
> 0788 111 765
> http://mjengwablog.com
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment