Friday 3 August 2012

Re: [wanabidii] Maji yashazidi unga Olimpiki

Nafikiri tunakuwa wepesi wa kulaumu na kulalamika bila kuangalia mchaakato mzima wa kushiriki mashindano. Ni rahisi kusema kuliko kutenda. Waulize Wachina, Wamarekani, Wazungu kwamba walianza maandalizi lini? Ungewauliza wachezaji maandalizi yao ungewapongeza sana hata kufikia viwango vya olimpiki na kushiriki maana hiyo tu ni shule. Wenzetu wanawaandaa tangu wakiwa shule ya msingi ila sisi tuliua michezo awamu ya 3 na Mungai. Imagine rekodi ya Bayi ya 1974 haijavunjwa na Mtanzania hadi leo. Na si ajabu akafa bila kuvunjwa!
 
Kwanza sisi tumepeleka wachezaji wachache. Hata wanaopata medali pia wanakosa siyo kwamba wanashinda kila mchezo. Tunahitaji kuwa na wigo mpana wakati ujao wa kuleta wachezaji wa michezo mingi siyo boxing, swimming na athletics!
 
Tunatakiwa kuwatia moyo hata hao maana ni mashujaa kwani ndio walioweza kupewa hadhi ya kutuwakilisha katika milioni 43 plus! Ni ajabu kwamba mtu ameenda vitani akiuawa tunamlaumu au akipata jeraha tunamlaumu badala kuangalia aina ya mafunzo na zana tulizompa. Mimi nilikuwa na timu ta taifa hapa Bradford wakati wa maandalizi yao. Nilijifunza mengi kwamba timu yetu ilikuwa na ari kubwa sana na uwezo ila walikuwa wanavunjwa moyo na kukosa support ya taifa. Hata vifaa walikuwa hawana vya kutosha na vingine wamekuja kununulia huko badala ya wafanyie mazoezi! Wacha hata suti ya ufunguzi walikuwa hawana na walikuwa wanangoja itumwe toka Dar maana walipimwa juu wakati wanakuja huko! So please kaani kimya badala ya kuhukumu! Mimi bado nawapongeza kwa hatua waliyofika ukilingalisha na nchi zingine!
 
NB: Halafu nijuavyo Tanzania haikuwa na wogeleaji wawili ili mmoja tu. Huyo mwingine  'Ammaar Ghadiyali' sijui alitokea wapi maana mimi sikumwona! Hata jina lenyewe ni kama siyo ya Tanzania?! Tulikuwa nao. Niwashukuru Watanzania waishio Bradford kwa umoja wao na kuwa wenyeji wazuri kwa mashujaa wetu tangu walipofika hadi wanaondoka kwenda London!
 
Ni kweli tuwaombea ila wanaohitaji zaidi ni viongozi wa nchi ili sera ya michezo iangaliwe upya. Ngoja wakati wa riadha tuone tutakavyopambana na Wakenya na Waethiopia. Naamini tutapata medali tu!

From: Kenneth Masuki <kennymasuki@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, 3 August 2012, 7:46
Subject: Re: [wanabidii] Maji yashazidi unga Olimpiki
Mzee Matinyi, hata tukiomba maombi ya kushusho moto kama maandalizi yalikuwa poor hakuna maana.
2012/8/2 Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Jamani, Tuzidisheni maombi ili walau tupate hata medali ya mbao - mambo magumu huko Landani. Hakuna njia nyingine ya kutuokoa isipokuwa sala tu kwa kuwa kujipanga kama taifa hatuwezi katika michezo, siasa, usafiri majini, n.k. Ni mwendo wa sala tu ndio umebaki.  
Tanzania hali mbaya Olimpiki  Send to a friend
Wednesday, 01 August 2012 21:31
Imani Makongoro
NDOTO za Tanzania kutwaa medali kwenye michezo ya Olimpiki zimeendelea kuyeyuka baada ya jana, mwogeleaji mwingine, Magdalena Moshi kushindwa kufurukuta.
Magdalena ameshindwa kupenya katika mchujo wa mita 100, free style hatua ya makundi baada ya kutumia muda wa dakika 1:05:80.
Magdalena anakuwa mchezaji wa tatu wa Tanzania kuondolewa katika hatua za awali za michezo hiyo inayofanyika London, England.
Wengine waliong'olewa mapema ni bondia Seleman Kidunda na mwogeleaji Ammaar Ghadiyali.
Tegemeo pekee la Tanzania kwenye Olimpiki sasa limebaki kwa wanariadha Mohamed Msenduki, Faustin Mussa na Samson Ramadhan
http://www.mwananchi.co.tz/michezo/18-michezo-mingine/25234-tanzania-hali-mbaya-olimpiki
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com   Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma   Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.    

0 comments:

Post a Comment