Thursday 31 March 2016

[wanabidii]

Rais George Bush alipofanya ziara ya kwanza enzi za awamu ya nne, kulikuwa na kundi kubwa la wanaharakati wakiwemo maprofesa maarufu wa vyuo vikuu, ambao walijitokeza hadharani na kupinga lengo zima la ziara ile.

Vyombo vya habari vikawaonyesha wakiwa kwenye maandamano hayo. Kama kawaida katika ile mida ya jioni kwenye vipindi vya runinga vya mahojiano, maprofesa maarufu wakajenga hoja nyingi na nzito za kuipinga ziara ya George Bush.

Leo Rais JPM ni kama vile anakifanya kile kilichokuwa ndani ya mioyo yao kwa wakati ule, anasisitizia katika kujenga nchi mpaka iwe na uwezo wa kuwa "donor country", na wote tunatambua kuwa nchi inayofadhili nchi nyingine inakuwa na kiburi kikubwa. Inawezekana awamu hii inaongozwa na dhana za kutaka kujitawala, kwa maana ya kutotaka kuwa bendera hufuata upepo.

Nadhani huu ni wakati muafaka kwa maprofesa wale walioipinga ziara ya George Bush kuingia kazini katika kutumia kuelimika kwao katika kutoa mawazo mbadala kwa uongozi wa awamu ya tano ili wazo lao la kujitegemea, ambalo msingi wake na unaanzia awamu ya kwanza, liweze kuwekwa katika uhalisia wa maisha yetu.

Siasa za harakati zilizofanywa na maprofesa wakati wa ziara ya Bush, kwa sasa zimepata kiongozi anayeziunga mkono kivitendo. Ni jukumu la maprofesa wetu kuja na fikra ambazo zitajenga ushawishi wa sisi wenyewe kuweza kujitegemea.

Maprofesa walitumia nguvu nyingi katika kupinga udhalimu wa George Bush, wanayo nafasi na kila sababu ya kuonyesha ni kwanini walikuwa sahihi kufanya vile, kupitia constructive ideas zitakazoelekezwa kwa rais wa sasa na wasaidizi wake, katika mfumo wa ushauri au katika mtindo wa zile hoja zao wakati wanahojiwa na watangazaji wa vituo vya runinga.

Huu ni wasaa muafaka kwa wananchi hii kwa wananchi wengi wa nchi kuyasikia mawazo mapya na ya kimaendeleo kutoka kwa maprofesa wetu.

0 comments:

Post a Comment