Thursday 31 March 2016

Re: [wanabidii] KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Mimi sina shida NA wamarekani wala hizo semi zisizokuwa na mashiko. Shida yangu kubwa watu kujikita kusema uongo wakati ukweli upo wazi na kutaka wote tuamini uongo. Marekani wote tunawajua na kwamba hawana rafiki wala adui wa kudumu na cha maana kwao ni maslahi yao tu. Pamoja na hayo wana misingi fulani wanayoisimamia. Siamimi pia kwenye kutegemea musaada kutoka nchi za nje kama kigezo cha maendeleo. Tumefika hapa tulipo kwa sababu tuna watu, ardhi lakini tumekosa siasa safi na uongozi bora ili tuweze kuelekea kwenye neema.

Tusifumbie macho matatizo lukuki tuliyo nayo kama ubadhirifu wa Mali ya umma na kutojituma katika kazi na kuendelea kuealaumu wamarekani Kama kwamba wao ndio wachawi wa maendeleo yetu. Tumepata Rais ambaye angalau ana uchungu na taifa hili. Tuungane naye tuwe na mwelekeo mzuri wa taifa letu.

Sent from Ezekiel's iPhone

> On 31 Mar 2016, at 09:56, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
>
> Hata Yuda alionekana wa maana aliposema 'mafuta yote kummwagia Yesu miguu si tungeuza na kuwagawia Maskini'.
> Ni kwa sababu Yesu alijua ni mwizi ndiyo maana akamkanusha. Unahitaji kuwaamini wamarekani na ili kuwaamini unahitaji kuwa umesahau matendo yao kuanzia walichowafanya wahindi wekundu.
> Lakini ni lazima kujua kuwa kuna muungano ambao sio wamarekani wala ushauri wao unaoulinda. Kama emokrasia haziulindi njia nyingine zitatumika, ikuwa ni pamoja na kufuta chaguzi. zilizoingiliwa
> --------------------------------------------
> On Thu, 3/31/16, Ezekiel J. Massanja <ezekielmassanja@gmail.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Thursday, March 31, 2016, 9:05 AM
>
>
>
> Mwandishi
> ameeleza vizuri kwa mtazamo wake anaoita wa kizalendo.
> Lakini naona uzalendo anaouuhubiri ni ubaguzi mkubwa NA
> kuwafanya wengine ni wajinga hawajui kitu. Uchaguzi wa
> Zanzibar CUF walishinda matokeo yakafutwa NA Jecha peke
> yake. Serikali ya Marekani NA wengine wote wanaopenda haki
> wamejiweka pembeni na kusema hawawezi kuhusika nao.
> Tuwaheshimu kwa hilo NA hawashurutishi kwa sababu hizo pesa
> ni za kwao.
> Kuliko
> kuendelea kutoa maandishi yenye ukakasi, ni afadhali turudi
> nyuma pale tulipojikwaa tuanze kutengeneza. Tusiwaendekeze
> sana wanaojaribu kutuonesha kitu ambacho hakipo.
>
> Sent from Ezekiel's iPhone
> On 30 Mar 2016, at 16:33, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>
> wrote:
>
> KUHUSU MCC
> KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA:
> MTIZAMO
>
>
>
> Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu
> Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.
>
>
>
> "Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can
> import. Democracy
> should develop according to that particular country". June
> 1991 in Rio
> De Janeiro, Brazil
>
>
>
> "Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza
> kuagiza. Demokrasia
> lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika".
> Juni 1991 Rio De
> Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)
>
>
>
> "No nation has the right to make decisions for another
> nation; no people
> for another people". From 'A Peaceful New Year'
> speech, Tanzania,
> January 1968
>
>
>
> "Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa
> lingine; wala
> watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka
> Mpya, Tanzania,
> Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)
>
>
>
> Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na
> haliwezi kuua
> mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani
> zinashirikiana kwa
> mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la
> ushirikiano.
> Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna
> nyingine ila
> kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa
> wale ambao
> wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na
> Ujerumani
> Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya
> Muungano wa
> Tanganyika na Zanzibar.
>
>
>
> Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka
> kuingilia
> Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda
> Nchi Mpya
> ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
> 1965 Tulivunja
> uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu
> wachache
> kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence)
> kule
> Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua
> hatua stahiki.
>
>
>
> Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru
> wa nchi za
> Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa
> kufahamu ni
> kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru
> wetu. Napenda
> ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa
> uhusiano
> wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada
> wao kwetu,
> lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si
> Marekani au
> Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.
>
>
>
> MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila
> masharti tena hela
> nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa
> moja na kupewa
> uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha
> maeneo kisha
> wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo
> hazikuwa
> zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na
> miradi ya
> maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata
> ufadhili. MCC 2
> sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi
> ya Marekani,
> hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.
>
>
>
> Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa
> kushirikiana na
> Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha
> kwa
> ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na
> fedha hizo?
> Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada
> ya kuweka
> fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.
>
>
>
>
> Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa
> Power
> Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la
> Nishati (si
> uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee
> wanaloweza
> kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko
> kuisaidia Afrika
> kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda.
> Wakaweka
> sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta
> Binafsi ya
> Marekani.
>
>
>
> Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama
> alitangazia dhamira
> ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio
> kwamba alipenda
> kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo
> kubwa sana
> na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post)
> kutaka
> kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.
> Zikaainishwa
> hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na
> kisera na
> hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi
> ikikutana
> wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela
> hizi zikawa
> zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na
> ule mchoro wa
> Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza
> mbele ya
> punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani
> atayafikia
> kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri
> uchaguzi mkuu
> jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya
> uchaguzi
> wakaibuka na suala la Zanzibar.
>
>
>
> Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni
> uamuzi wenye
> madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio
> ilikuwa itekeleze
> miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu.
> Ndio msingi
> wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa.
> Tumetofautiana na
> Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa
> maisha ya
> diplomasia.
>
>
>
> Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu
> kuituliza huko
> nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao
> kama ambavyo
> wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana.
> Marekani
> inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani.
> Marekani
> inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC
> 2.
>
>
>
> Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha
> na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.
>
>
>
> Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi
> Marekani
> isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa
> Egypt iliyo
> chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa
> Egypt na
> Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila
> mwaka kwa
> yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.
>
>
>
> Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake.
> Wazalendo wasimame
> na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au
> Imekosea" na Makuwadi
> watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko
> wapi?".
>
>
>
> Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu
> kama Taifa
> letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza
> kukusanya
> mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato
> yataongezeka
> maradufu kwa vyanzo vile vile.
>
>
>
> Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke
> aliyetoa tamko ni
> MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au
> Ikulu ya
> Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya
> Mitandao
> (Cyber crimes Act).
>
>
>
> Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka
> kitokee nini pale
> ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile
> ile ya
> Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na
> kisheria
> kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua
> nafasi yake.
> Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano
> mitandaoni badala
> ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana
> basi
> wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani
> wakashindwa,
> mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi
> ukaitishwa
> Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali
> na baraza la
> wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua
> Zanzibar lakini
> ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa
> za maendeleo.
> Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?
>
>
>
> Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende
> mahakamani,
> bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke
> hoja ya
> kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC)
> inapoweka
> shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na
> linaloweza
> kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule
> jamaa yao Trump
> alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa
> tena chini
> ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).
>
>
>
> INDHARI
>
>
>
> Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni
> ishara ya
> ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano
> yanayotweza
> Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za
> maendeleo
> (politics of development) na sio kujikita katika katika
> siasa za
> madaraka (Politics of Power).
>
>
>
> Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa
> watu wenye
> uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni
> mnufaikaji
> (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya
> Nje ya
> Marekani.
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment