Thursday 31 March 2016

[wanabidii] PONGEZI KWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

PONGEZI KWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Wahenga wasema "asiye mpongeza mtenda mema ni mnafiki". Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa mambo mengi mazuri uliyoyafanya kwa muda mfupi uliopo madarakani.Japo sitaweza kueleza yote nitaelewa machache sana. Yakiwemo yafuatayo-:

Kutokomeza Rushwa na Ufisadi, Katika kampeni zako alipenda kutumia usemi usemao "mafisadi mtaisoma namba", wengi hawakujua dhana ya usemi huu kwani wengine walisema "CCM ni walewale, rushwa na ufisadi ndio zao" Sasa naona rais unatimiza dhamira yako na ahadi yako ya kutomeza rushwa na ufisadi kwa kuwatumbua waharifu hata kama ni wanaccm wazawa.Jambo hili limewaacha wapinzani midomo wazi na watanzania kuwa na imani na wewe katika ujenzi wanchi hii. kiukweli Hajawai tokea katika nchi hii rais aliye na kasi na nguvu ya ajabu ya kupambana na ufisadi na rushwa kama wewe baada ya Mwalimu. Jambo hili linafanya vyama vya upinzani kutokuwa na nguvu tena katika mawanda ya kisiasa nchini kwani imani ya watanzania wa ari ya chini juu ya utawala wako inakua kila siku ukilinganisha na utawala uliopita ambapo imani ya watanzania ilikufa juu ya utawala huo. Pongezi hizi pia zimuendee Waziri Mkuu Mhe: Kassim Majaliwa, kwa kweli kajaliwa kuwa mstari wa mbele kuijenga Tanzania mpya yenye heshima kwa watu wote bila kujali vyeo, chama cha kisiasa au udugu.

Kuleta heshima kazini, Kauli mbiu yako ya "HAPA KAZI TU" imekuwa chachu ya uwajibikaji makazini ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo watumishi wa umma walikuwa wanafanya kazi kimazoea bila kufuata taaratibu za kazi zao jambo ambalo lilipelekea kuongezeka kwa wimbi la rushwa na ufisadi katika sekta za serikali.Sasa heshima imerudi makazini kwani watumishi wa umma wanawajali na kuwanyenyekea wananchi na kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata taratibu za kazi zao. Kitendo cha mtumishi wa umma kwenda kinyume na taratibu za kazi yake na kuharibu kazi "kutumbuliwa" kimeleta umakini na ufanisi makazini. Kwa hilo nakupongeza sana Rais kwa kasi na nguvu uliyonayo ya kufanya kazi kizalendo bila upendeleo wakichama au wakisiasa.

Hakika wewe ni MZALENDO wa kweli kama mwalimu. Halmashauri na sekta nyingi za serikali zilioza kwani watumishi walijiona wao ni waungu watu kwa raia, hawakuwajali wala kuwathamini juu ya matatizo yao.Piga kazi baba na sisi tuishi kama ulaya kwani mali tunayo, nguvu kazi tunazo na nia tunayo tupo pamoja nawe kuijenga nchi yetu. Kilicho nifurahisha zaidi mawaziri uliowateua wana profession ya kazi za wizara zao na uzoefu mkubwa, hapo heshima imerudi.


Lililo gusa mioyo ya wazalendo wengi wanchi hii ni hili sakata la kuwasaka watumishi hewa ambao wanapokea mishahara bila kazi yoyote jambo ambalo linawanyima watumishi walio harari kulipwa madeni yao ya muda mrefu na kuongezewa mishahara yako au posho.watumishi hao wachukuliwe hatua kama waujumu uchumi pamoja na wale waliowaingiza kwenye mfumo wa malipo ya mishahara hiyo. Kwani wameliingizia taifa hasara kubwa sana.
Pia napenda kutoa ushauri kuwa watumishi kama vile walimu, manesi na madaktari muwafikirie kwa fikra pevu juu ya masrahi yao.

Kwa haya machache sana kati ya mengi sana uliyo yafanya nakupongeza sasa wewe Rais JPM, makamu SSH na waziri mkuu KM. Mungu hawape amani na nguvu nyingi zaidi muwashinde mafisadi na walarushwa wanaonufaika kupitia mgongo wa watanzania maskini,murudishe heshima ya nchi na wananchi iliyopotoe kwa muda mrefu na Mungu awajalie afya na uzima mpate kuiongoza nchi hii kwa misingi ya HAKI NA USAWA, AMANI NA UPENDO kwa watu wote kama ilivyo sasa.Na tunazidi kuwaombea.



AMINAAAA


MWALIMU: MOHAMED NINDI HAMIS.

KILINDI -TANGA -TANZANIA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment