Sijachangia mjadala huu wa Katiba Mpya unavyojadiliwa humu ila husomasoma. Mchango wangu mdogo kuhusu Matakwa ya Wananchi kuhusu Katiba Mpya na suala ya Rasimu ya Katiba Mpya.
Nielewavyo rasimu kwa Kiingereza ni Draft. Katika Consultancies mtu unapewa kazi ya kufanya tafiti kwa mfano uandike ulichokiona kwa mbinu unazotakiwa kutumia kisha kutoa mapendekezo. Ukimaliza hiyo kazi unaiwakilisha kimaandishi bila au pamoja na kutoa presentation-inavyotakiwa na client. unaweza ukaitwa kurudia kitu au kumalizia kazi kwa kuzingatia comments baada ya kuwakilisha draft yako iwe final report.
Kama Jaji Warioba na heshina zote na kundi lake walipewa kazi, wamewakilisha, wamemaliza-ni kazi ya Client aliyewatuma kuendelea na alichotaka. Wao yao imekwisha labda waitwe tena kwa hili na lile. Unapowakilisha draft na final report ya kazi yako kwa aliyekutuma sio wewe tena uwe unapita kila kona kuwakilisha kazi ya watu na kupiga kelele zinazoweza kuleta mtafaruku. Unavunja TOR.
Katika tafiti zote shirikishi unaweza kukuta target group zikatoa maoni kinyume na sheria, sera na mikakati na misingi ya nchi. Mfano-mahusiano na Zanzibar. Hakuna Mtanzania wa umri wa 60+years ambae hakusoma huko nyuma (sio elimu ya sasa) kuhusu ujio wa watu Tanzania kuanzia Sultani wa Oman na Persians na Utawala Kilwa Kisiwani na Mafia na Ule wa Unguja na Pemba; ujio wa Maa Groups kutoka North Africa; ujio wa Wareno na utawala wao na makabila mengi na uhamiaji wa watu kutoka South na West or central Africa kiasi kwamba leo Makabila Makuu nchi hii Wasukuma from Chad, Wangoni from South Africa, tuna wala matunda from Botswana na other Groups-Datoga etc Kila mtu nchi hii ni mhamiaji (kama USA) kasoro vikabila vyenye watu kiduchu.
vichache. Sasa wapo wa ZNZ wanaotaka Wajitenge watakuwa wamesema yao ndani ya katiba uonevu wanaouona wao kwa tafsiri yao. Ila hawaangalii wanavyofaidi ardhi ya TZ, wapo kila kona ya TZ mpaka Kilombero wanalima mipunga na biashara za maduka; Mafia wanapambana na Marine Park kuvua ndani ya mbuga ya hifadhi ya samaki; kuvusha magendo bandari bubu bagamoyo, Tanga Rufiji; umeme kutoka Kidatu; biashara za Taxi DSM na maduka ya biashara kariakoo, mbagara, mkuranga walianzisha wao. Maduka ya Bagamoyo ya kuuza baiskeli, TV za kwanza bongoiland ni wao-Hawa wanataka kujitenga-wanaonewa! Utaiweka hii ktk Katiba na Kuikubali? (rasimu haijali matakwa ya wanaichi-unataka ikubali ubaguzi tukubali wajitenge kwa manufaa ya kisiasa ya wachach?). Tusahau udugu wa kuwa Muunguja na Mpemba ni mbongo mwingine ana chale za kimakonde, mwingine alitoka congo au Tabora etc?
Kuna wanaotaka Mbuga ya Hifadhi ya Serengeti ipewe Wamaasai serikali iondoke inawatesa. Hivyo Loilondo, Serengeti NP na game reserves na conservation areas kuzunguka Serengeti NP zifutwe ili wafuge na kuishi kwa raha-Warioba akiandika mawazo yao haya (na kuna NGO za Nje na ndani ya nchi zinaunga mkono hili na mihela inatumika) serikali ya Kikwete na CCM ikubali iache kubaki njia kuu ya maamuzi yao ya kulinda mazingira na mali asili. Wahamie makundi ya wafugaji na jamaa zao toka nchi jirani, kuwe degraded, usalama mdogo (kama 1990 wasomali majambazi waligeuza kwao kwa kuvuna)-wananchi wametaka! Basi iwe hivyo kwa mbuga zote (Mikumi, Udungwa, Selous etc) si tutakuwa vichaa na misitu hifadhi maji, wetland areas UHURU-wanachotaka waannchi. Hivyo misitu wakate mbao, Mito mikuu ikauke, nchi iwe jangwa kama Somalia na Ethiopia kulikokuwa na misitu kama yetu zamani. uhuru bila sheria sawasawa na kuwa KICHAA au Mwendawazimu. Mtu anatoa maoni ya kutaka wasifukuzwe
barabarani kufanya biashara, wasiondolewe kutoka catchment forest, kujenga mabondeni na kato ya mito, bahari-wanaonewa! Lakini hata enzi za mababu kulikuwa na sheria za kimila za hata mazingira na upokeaji wageni na kuwapa ardhi ya muda au kudumu-Tribal chief, tribal customary land systems zimeandikwa zipo na hata kuchangia mito kwa irrigation; kuwinda wanyama wa aina gari na wakati gani na ukiwa mfugaji huwindi wanyama wakubwa bali digidigi tu. Ukiwinga ng'ombe mwitu, nyumbu unaua ng'ombe; swalapala-unaua mbuzi unabaki masikini. Hivyo mfugaji si muwindaji. Waachie wakulima waluguru, wavidunda, ndamba, benamanga na wapogoro wapate kichaa kama hawajala nyama ya mbogo, ngiri, nguruwe pori (wakristu) pori-unajipenda au hujipendi? Waachie wawinde na wale hizo nyama bila kukataza uone kana unakuta mnyama Mikumi National Park! hatulani bila kula nyama ya mbogo!! Serikali imewawekea miradi ya mbuzi wa kisasa na ya nguruwe wa kufugwa kukidhi uroho wao huo wa
nyama pori. Waruhusu wafanye watakavyo Ukose Maji ya Mito (Rufiji, Kilombero, Ruaha) ukose umeme wa Kidatu, Kihansi; waondoe wafugaji wanaotaka kuzurura nchi nzima na mifugo ili weltands zisaidie hydrological cycle na mto Rufiji ambao umepita chini ya bahari hadi Mafia ya Visiwa vya ZNZ. Kubali kila tutakacho uone kama utakuwa na nchi.
Hakuna mafanikio ya mabadiliko yoyote kama kila mwananchi, mtanzania me au ke, kijana au mzee kubadilika kiakini, kitabia, kimatendo. hata ukiangalia mashirika au kampuni binafsi ni fisadi badala ya kuwa efficient and effective kiutendaji. Wamepewa viwanda wamegeuza godown za kuhifadhi used items na kuuza; viwanja vya kujenga viwanda-wamejenga hall za arusi na hao ni waume na ndugu zetu. Wanaima tunawatetea na kuwawekea mawakili wanashinda kesi. Kesi ya akina Mramba ni wangapi walilia au kulipwa uwakili. Hiyo ya Richmond, Escrow mbona tunawatetea. Ni sisi ndugu, watanzania. Hata mbakaji anawekewa dhamana na mawakili. kwa nini PPP na liberalization of the economy imeshindwa na matajiri wapo? Tunawaona wakipiga kelele tu sio kuboresha uchumi zaidi ya kuwa na mabasi na malori ya kusafirisha bidhaa na kuleta mitumba na vitu ambavyo wangezalisha hapa na kupitisha mapaka njia za panya. Fisadi sote na kama hatutotoa siri za wezi ambao ni ndugu zetu tunabaki
kuendesha magari ya ufahari na kuwapokea kwa shangwe wanapotoka gerezani kurudi nyumbani-hatutobadilisha kitu ktk kudumisha haki nchini. Vibaka wapigwe tu nasisi wenyewe. Mali tunazipora sote-Udadali (hasa wanaume) wa mazao, ticket ya bus afanyae ni mumeo, nduguyo, mwanao bila ya aibu anamuibia mtanzania mwenzake masikini. Kwa nini hatumjali Mungu na kubadilika. Jibaba la kifua kikubwa lipo kijiweni kijijini au mjini kusubiri kuibia wengine. Zikiundwa Saccos, VICOBA ni wizi tu chache kudumu. Unataka serikali ikufanyie nini? Ni kuilaumu tu basi. Chama kinaahidi kutoa kila kitu bure huduma zote eti kuna mafuta na madini-Usitoze kodi, matajiri wa nchi wasiendeshe viwanda utegemee huduma za bure? Tuwe wakweli. Wavivu sio watendaji. Tunamsifu na kumpenda mtu asemaye-kila kitu Bure, wezi wafungwe wakati ni jamaa zetu tunawalinda!
Kuna visima nimeviona Mafia Island 2008 vya Shell BP 1954, 1956. Minara na maandishi. Mbona wapo akina Dangote hapa? kazi yao ni kulongalonga tu kuwa raslimali hazifaidishi wananchi. sasa Dangote anakwenda kujenga kiwanda cha cement India baada ya cha Kusini TZ-Wao wapowapo tu kuuza soda za rangi maembe yanaoza Mtwara, Lindi, Bagamoyo, Mkuranga-Aibu-ila Serikali ikubali kila asemalo mwananchi katiba ni yake!! Je mwananchi ni mtendaji, tunawajibika sawasawa maofisini? Ukiwa kiobgozi wa kijiji mkali kijijini unayetaka maendeleo-watakufanyizia unapowabana kikamilifu. Tupoje sisi? Lawama tu. Hata nje ya ofisi zetu za NGO za Afya hatuna muda wa kuhamasisha usafi wa mazingira mpaka tupate donor funds!! Ila tupo kupanda juu ya mawe kuvuka mafuriko ya kinyesi ili tufike maofisini mwetu. Tunataka vishuke vije.
Usawa 50 kwa 50 tunahitaji lakini wanawake wasiishie viti maalum tu. Wagombanie washinde na pia waache tabia ya kupenda vitenge, khanga na wakipewa vijisent wanakuwa corrupt wanapigia kura wanaume na kuwa na kampeni against wanawake wenzao-kujitambua ni suala kuu na ukipata nafasi ulinde heshima yako. Nawashangaa baadhi ya waheshimiwa nao wakisimama wamejichubua na lipstick nyekundu kama mando la nyani. mamikufu kifua kibao na panki juu!! Anyway hii ni private life ya mtu lakini tujitambue, kura zetu zinatosha kumuweka mgombea mwanamke mwenye sifa ila hatujipendi. Tukiwa viongozi-jee ni mfano majimbo yetu yanaongoza kimaendeleo? Tujifunze kutoka mama Malecela-Ni Jembe. Vijiji vyake nilivyovitambua 1993-97 na matatizo ya maji ya kemikali toka mashambani na kansa za koo na utumbo. Kufika huko 2003 niliyoyaona nilipiga saluti katika miradi ya maji na kuuna WUAs. Tunahitaji kuona haya Monduli ambako mifugo ni mali na ni pesa; tuone haya Morogoro rural ambako
DAWASA sasa inahaha kipa maji DSM, Kibaha na Bagamoyo mifugo kutoka Mwanza, Manyara na Monduli ipo juu milimani Mgeta. Huu ni ufisadi-mwananchi anahonga hela afanye atakavyo. Yupo tayari kuhonga milioni 1 aachiwe na atahonga kila anakokwenda na kuvunja sheria lakini sio kuchangia Madawati, madarasa, mradi wa maji ya kisima cha milioni 5 ila watalipia matibabu ya gharama kwa kunywa maji ya kinyesi na uchafu wao. halafu-Serikali ya CCM haijali afya zetu, huduma ziwe za bure!! Hii ipitishwe. Umwage uchafu wako, wa mifugo yako, kampuni yako, genge lako plastiki kila kona, uzibe mitaro halafu unataka kila huduma bure-hii ikubaliwe. Kuharibu mabomba au miundo mbini ya gharama-unataka bure. Hata ulaya muuza mchicha barabarani ana mashine ya kodi ambayo hela zao ndio zinatoa misaad kwenu. Bado hatujitambui. Tusikubali ujinga kuwa kila kisemwach na wananchi kiewe hivyo kwa kisingizio cha ESCROW, Richmond. Sote tu mafisadi. Na ndio maana kesi ya hata mtu kubaka
mwanae, kubaka katoto, kuua mke, kulawiti, ujambazi na kuiba mali, kuua-zinachukua miaka kutokana na ndugu kuhonga na kuifanya kesi isiende ipasavyo. Hata mke anahonga kwa njia mbali mbali eti analinda ndoa. Mume kabaka housegirl; kijana wake kalawiti kadogo kake-hawatokei kutoa ushahidi au wanahonga- mifano ni mingi. Na tukifika bungeni tunafanya yapaswayo au tunalinda tu nafasi zetu. silaumu lakini utata na ufisadi mpaka kwetu na kwa raia. Ndugu watamtetea sifasi na kumuwekea mawakili serikali ikashindwa. Ni akina mama wanaoajiri watoto wadogo, kuwatumikisha kazi na kuwaonea. Pamoja na kuwahusisha katika elimu ya haki mpaka miliki ardhi-bado wanadhulumiwa na koo zao (utu wetu) na ndugu kuzalisha watoto wa mtaani. Serikali haitoweza kuzuia rushwa, kuleta haki sawa kama sisi wenyewe tunaficha wakosaji, kuwawekea mawakili na kuhakikisha wanashinda hata kesi kwa makosa yanayoonekana.
Wanawake wabunge walisimama na kulalamika kuwa pesa milioni 200 za mafao zipunguzwe ile ziingie hospitali kuboresha labour wards? Ubinafsi mpaka kwa wanawake.
Samahani.
--------------------------------------------
On Tue, 1/9/15, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] RE: [Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]
To: Wanazuoni@yahoogroups.com, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, wanabidii@googlegroups.com
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Tuesday, 1 September, 2015, 21:36
Ndugu Saru
Neno mabadiliko katika muktadha wa uchaguzi
Tanzania mwaka huu 2015 linatumika kumaanisha wananchi
kuchagua serikali mpya tofauti na serikali ya
CCM iliyoko madarakani ambayo ilikataa kuandika Katiba Mpya
inayotokana na maoni ya wananchi. Serikali Kitiba Mpya
inayotokana na maoni ya wananchi. Katiba hiyo pamoja na
mambo mengine itaweka misingi mizuri ya kuwepo usawa
wa kijinsia katika uongozi hasa 50 kwa 50 wabunge wanawake
na wanaume majimboni. Pia itaweka
misingi ya kuzuia serikali kuwa chanzo ufisadi
wa fedha za umma. Mfano ufisadi
wa mwaka jana 2014 wa Tegeta escrow bilioni
306, ufisadi wa Richmond bilioni 172 mwaka 2008
na ufisadi wa EPA bilioni 133 mwaka 2005 na hakuna
aliyefikishwa mahakamani.
Katiba Mpya pia itaweka misingi
itakayozuia watawala wachache
wakijitajirisha kwa kutumia fedha za wananchi kujilipa
mishahara mikubwa, mafao na marupurupu wakati
watumishi wengine wa umma madaktari, wauguzi, walimu, polisi
na wananchi wengi wakibaki maskikini. Mfano mbunge
kulipwa mshahara shilingi milioni 10 mkwa mwezi na
mafao zaidi ya shilingi milioni 200 baada ya kustaafu
miaka mitano tu ya utumishi. huku ni kutajirisha kikundi
kidogo cha watu katika nchi huku wengi wakibaki mafukara.
Nimeandika kwamba kwa vile vyama vinavyounda UKAWA
vina agenda ya kuandika Katiba Mpya inayotokana
na maoni ya wananchi, wapewe kura. Hayo ni maoni
yangu baada ya kusoma dondoo za ilani za vyama mbali
mbali vinavyotafuta ridhaa ya kuchaguliwa hapo Oktoba
25 mwaka huu 2015. Nimesema pia kuwa serikali ya
UKAWA wasipotimiza ahadi hiyo miaka 5 ijayo wananchi
watapiga kura watawaondoa madarakani. Bila
wananchi kufanya mabadiliko ya uongozi na kuweka
uongozi utakaoandika Katiba Mpya inayotokana na maoni
ya wananchi siasa za vyama vingi Tanzania
zitaendelea kuongeza umaskini wa wananchi na
nchi yenyewe huku mali zetu zikiwa zinaporwa na wawekezaji
kwa kwenda mbele.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Tue, 9/1/15, Surumedia majiydsuru@gmail.com
[Wanazuoni] <Wanazuoni@yahoogroups.com>
wrote:
Subject: RE: [Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE
UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]
To: Wanazuoni@yahoogroups.com,
"mabadilikotanzania@googlegroups.com"
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>,
wanabidii@googlegroups.com
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>,
"Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Tuesday, September 1, 2015, 5:39 PM
Mama yangu Nkya umetumia muda
wako mwingi kupiga kampeni kwenye jukwaa la wanazuoni.
Mambo
uliyoyazungumza ni mazuri sana kwenye uwanja wa siasa
lakini
siyo kwenye jukwaa ambako wengi wanajijua na wanafanya
upembuzi makini kuhusu hatima ya Taifa badala ya hatima ya
makundi ya wasakatonge. Naomba ujikite zaidi kwenye mambo
ya
msingi na hatima ya taifa. Kwa mfano Unazungumzia
mabadiliko
bila ku-define neno mabadiliko. Maswali yangu kwako ni:
Mabadiliko ni nini? Je! Mabadiliko maana yake ni kuwapa
UKAWA kuongoza nchi tu na si zaidi ya hapo? Je ikitokea
tetemeko la ardhi siyo mabadiliko? Je, nchi ikivamiwa na
maadui kupitia wasaliti wa uhuru wetu siyo mabadiliko?
Kama
UKAWA walitumia miaka nane kutudanganya kwamba Lowassa ni
fisadi, lakini wakatumia siku moja kumsafisha na
kutudanganya kwamba Lowassa si fisadi tutawaamini vipi
kwamba hawatabadili kauli zao kama walivyobadili kwa
maslahi
ya kundi hilo la UKAWA? Hivi unaposema mnataka katiba ya
wananchi, je wale wabunge walioshiriki kwenye Bunge la
Katiba hawakuchaguliwa na nchi wa Tanzania kutoka majimbo
yote? Je, wao (wabunge) walikuwa raia wa nchi gani? Hao
wananchi sura zao ni tofauti na hawa tunaowajua sisi raia
wa
Tanzania? Hivi mtu ambaye hayupo UKAWA siyo mwananchi wa
Tanzania? Wewe umesema haupo Chama chochote kwa sababu
huna
kazi ya Chama chochote au fikra zako na imani yako haipo
kwenye Chama chochote? Kama utadai UKAWA siyo Chama, je!
UKAWA wafuasi wake hawana Chama? Kama hawana Chama basi
pia
hawana haki ya kutafuta uongozi wa nchi hii kwa njia ya
sanduku la kura!
"Ni
bora kukaa kimya kuliko kuzungumza yasiyowafaa watu,
lakini
ni bora zaidi kusema yanayowafaa watu kuliko kukaa
kimya".
Baba
Nouman,
Bongonyika, East
AfricaFrom:
ananilea
nkya ananilea_nkya@yahoo.com
[Wanazuoni]
Sent:
01/09/2015
17:26
To:
Wanazuoni@yahoogroups.com;
mabadilikotanzania@googlegroups.com;
wanabidii@googlegroups.com
Cc:
WANA
BIDII; Paschally
Mayega
Subject:
[Wanazuoni] WANANCHI WAFANYE
NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15 [1Attachment]
WANANCHI WAFANYE NINI
WASHINDE UCHAGUZI 2015?
Na Ananilea Nkya
Mmoja wa watu waliosoma makala yangu Raymond
Mauki, makala
niliyoandika kwamba CCM ilimtoa Edward
Lowassa kafara
kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond ili chama
hicho
kidanganye wananchi kwamba fisadi ni Lowassa na CCM
ni
chama safi, amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa
kupitia ile makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu
maswali mawili.
Kwenye malaka hiyo iiliandika kwa serikali ya CCM
ndiyo
fisadi wa fedha za umma na hivyo chanzo cha wananchi
wengi
hapa nchini kuwa maskini. Nilitoa mfano wa serikali
ya CCM
kuwa fisadi kusimamia wizi wa fedha
za umma kwenye
akaunti ya Tegeta Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana
2014. Nilitoa pia mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni
serikali ya CCM yenyewe ilihusika lakini walidanganya
umma
kwamba muhusika ni Edward Lowassa.
Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye alikuwa
fisadi wa
Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama Mramba na Yona.
Nilisema pia kwamba hivi sasa nchi imejaa
ufisadi
unaofanywa na watawala wa serikali ya CCM kwa hiyo
hata
mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli
wanayejidai ni
mtu msafi akichaguliwa yerikali yake italazimika
kufanya
ufisadi penda asipende. Na yeye
mwenyewe Magufuli
amekaririwa akisema kwamba ataika mfano marais
waliomtangulia.
Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura wakiwepo wanaCCM
kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane na ufisadi wa
fedha
za umma na jeuri ya watawala wa CCM kujitajirisha huku
wananchi wengi wakiwa ni maskini wa kutupa, na tena
watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi masikini kwamba
ni
malofa na wapumbavu ni lazima wananchi wafanye
mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka huu 2025
kwa
kutumia sanduku huru la kura hapo tarehe 25 Oktoba .
Maswali mawili ambayo msomaji wangu alitaka
niyajibu ni
haya ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa wanawake kwenye harakati
hizi za leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?
Mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha
yao kupitia uchaguzi wa mwaka huu
2015 ni mkubwa na
muhimu sana. Wanawake kwa wingi wao wakijitokeza
kusikiliza
kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga kura
na
wakaipigia kura UKAWA wataleta mabadiliko.
Hivyo kila
mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze
kitambulisho chake cha kupiga
kura(kichinjio).
Afanye hivyo kwa kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote
kitambulisho chake. Kitambulisho chako ni siri yako
(ni
silaha yako) ya itunze kama mboni ya jicho hakuna mtu
mwingine yeyote hata kama ni kiongozi, hata kama ni polisi
au mgambo hapaswi kukiona kitambulisho (kichinjio)n
chako.
Zaidi hata kama huyo mtu atakuwa amekuletea zawadi ya
kanga,
kitende, fulana, sukari, fedha au chochote kile mwanamke
USIDANGANYIKE.
Mimi sina chama chochote cha siasa nimefungamana nacho
lakini nasisitiza wanawake waipigie kura UKAWA
kwa sababu
ilani ya UKAWA ina agenda kuu mbili muhimu
zinazogusa
maisha ya wanawake moja kwa moja.
Kwanza UKAWA wana agenda ya kutoa elimu bure hadi
Chuo
Kikuu. Hili ni muhimu kwa sababu elimu ndiyo msingi
wa
maendeleo yote kwa mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike,
familia na taifa zima.
Pili UKAWA wana agenda ya kuandika Katiba
Mpya
inayotokana na maoni ya wananchi. Moja ya jambo
muhimu
katika Katiba ya wananchi ni kuweka uhusiano
mpya kati ya
viongozi na wananchi. Katiba Mpya itazuia viongozi
kujitajirisha kwa mali za umma huku mamilioni ya
wananchi
wakiwepo wanawake wakitaabika kwa umaskini.
Fedha za nchi zinazotafunwa na watawala
wachache
zitatumika kwa mfano kuboresha elimu,
huduma za
afya,maji, umeme, kujenga viwanda kuwapatia maelefu
ya watu
ajira. Pili Katiba mpya itaweka
misingi imara ya
kuhakikisha uwakilishi wa wanawake kwenye
vyombo vya
maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.
Kashalika Katiba Mpya italeta usawa wa kweli wa
kijinsia
nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri
uchaguzi wa
2020 kwa kutoa idadi sawa
wanawake na wanaume madiwani
kwenye kata na idadi sawa ya wabunge wanawake
na wanaume
majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na mitaa mwanamke akiwa
mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu mwenyekiti.
Utaratibu wa viti maaluma utatumika kwa
watu wenye
ulemavu peke yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa
mbunge
mwanamke na mwanaume. Hayo ndiyo mabadiliko kamili
nay a
kweli kuhusu usawa wa kijinsia unaotakiwa Tanania ili
nchi
yetu na watu wake waondokane na umaskini.
Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama vinajinasibu
eti
vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka mwanamke mgombea
mwenza au mgombea wa Urais. Ni sawa lakini hiyo ni
geresha
ya danganya toto kwa sababu kwa mfumo wa sasa
ambapo usawa
wa 50 kwa 50 haujawekewa misingi kwenye Katiba
wanawake
wanatumika tu kama wanaume kupitisha sheria na
sera za
maendeleo za kunufaisha kikundi kidogo cha watawala
wananchi
wanaume na wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.
Usawa wa jinsia wa kweli na wa kudumu
hauwezi kufikiwa
hapa nchini bila Katiba Mpya ya wananchi
kuandikwa na
kuweka misingi ya kutekeleza usawa wa jinsia kwa
vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo vya
kugombea na kushinda sawa na wanaume majimboni na
kwenye
kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50 baada ya
nchi kupa uhuru.
Kwa hiyo ushuri wangu kwa wanawake na wale wote
wanaofanya
kampeni UKAWA ni kuwaeleza wanawake na wananchi
ukweli
kwamba wakitaka mabadiliko ya kweli katika maisha
yao
wachague UKAWA ndio waliobeba ajenga ya
ukombozi—agenda
ya kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa
kwenye misingi imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni
ya
wananchi.
Swali la Pili: Watanzania tufanye nini kuzuia
CCM kuiba
kura uchaguzi wa mwaka huu 2015? Mimi
napendekeza
yafuatayo:
Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume wakiwepo wana CCM
mnaouchukia kuona watu wengi
wanateseka kwa umaskini na
watawala wachache wana utajiri wa kupindukia,
kinachotakiwa
kama mnanataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni mwamzo
wa
kubadilisha maisha ya kimaskini wanayoishi mamilioni
ya
Watanzania, ni kutunza kitambulisho chako
(kichinjio) na
siku ya kupiga kura tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015
kwenda
kupiga kura kuchagua UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja
unaojumuisha vyama vya CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA
kwa sababu wana agenda ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA wana ajenda ya kuandika Katiba
Mpya inayotokana na
maoni ya wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya
kuongoza nchi kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini
unaotengenezwa kwa serikali ya CCM kukwapua fedha za
wananchi na jeuri ya kupora madaraka ya
wananchi—yaani
CCM kujifanya chama dola.
Hata kama itakulazimu kusubiri siku mbili au hata wiki
nzima
hata mwezi mmoja kuweza kupiga kura fanya hivyo usikate
tamaa. Kakikisha hukosi kupiga kura maana hakuna
ukombozi
wenye kuleta mabadiliko katika maisha ya wananchi
wengi
ambao hupatikana katika demokrasia ya vyama vingi vya
siasa
bila wananchi wenyewe kushiriki kuleta
mabadiliko hayo
kupitia sanduku huru la kura.
Umaskini wa wananchi ninaouzungumza ni pamoja na
ukosefu wa
ajira ya kuwapatia walio wengi wasio watumishi wa
umma
fedha za kujikimu. Watumishi wengi wa
umma mfano walimu,
madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa
mshahara isiyokidhi mahitaji ya msingi kama vile
chakula,
mavazi na malazi.
Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa kwa muda
mrefu. Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa maji,
watu
kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache
wakiugua
wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda kutibiwa
nchi
za nje.
Elimu duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina
chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo
mbinu mingine muhimu. Shule hazina hazina
walimu wenye
ubora na wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile
wanaheshimiwa, kuthaminiwa na kulipwa vizuri.
Vilevile umaskini na kuporw amadaraka wananchi
kunakojidhihirisha kwa vyombo vya dola hasa
polisi
kutumika kibabe kunyanyasa wananchi kama vile nchi
yetu
bado iko kwenye ukoloni.
Pili: Kila kila Mtanzania aliyejiandikisha kupiga
kura
anayeumwa na hali ya umaskini wa wananchi
wengi anapaswa
kutunza kitambulisho chake cha kupiga kura (kichinjio) na
asikubali kumuonyesha au kumpa mtu yeyote hata awe
mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji, kijiji,
mtaa , polisi , mgambo au mtu yeyote yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi sasa wanapita
nyumba kwa
nyumba wakijidai wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba
kumbe ni mbinu za kuwanunua au kuwadanganya na
kuwaogopesha
wananchi wanaotaka mabadiliko ambao Rais Mstaafu
Benjami
Mkapa amewaita ''MALOFA NA WAPUMBAVU''.
Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi ni ili
wasipige kura ya kuwaletea mabadiliko kwa
kuikataa
CCMambayo utawala wake umewafanya wananchi wengi
kuwa
malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali ya CCM
wakijilipa fdha za wananchi na kupata utajiri
wa kukufuru.
Nawashauri wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula
watakuwa wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni
walizosema watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni
maana
pengine hizo ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa
mwaka
jana 2014 kwenye akaunti ya Tegeta escrow Benki kuu
ambazo
nyingine zilibebwa kwa tandarusi. Ni fedha za
wananchi
kuleni na kama ni nguo vaeni ni mali yenu lakini
usimpe
tena kura yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine
na hakuna kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini
wataifanya miaka 5 ijayo.
Aidha kila anayepiga kampeni UKAWA awaeleze wananchi
ukweli
huu. Wananchi wakiujua ukweli kuhusu chimbuko la
matatizo
yanayowakabili kuwa ni serikali ya CCM kama
taasisi
kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka,
wananchi wataelewa na watapiga kura kikamilifu
kuleta
mabadiliko—kuchagua UKAWA kuendesha serikali
tuone miaka
mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi umaskini.
Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi chuo kikuu
na
Katiba Mpya uchaguzi wa 2020 watapigwa chini kupitia
sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama kwa
kuzingatia sera za maendeleo umaskini unaowasumbua
Watanzania wengi hautaondoka nchini.
Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na
maisha ya
mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao hawahongeki,
hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa wawe ni watu
wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha hadi kazi ya
kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi ikamilike.
Maana
kwenye uchaguzi wakala ukipepesa ukipepesa
macho kidogo tu
wajanja wanachakachua.
Nne: UKAWA kuweka mawakala makini ambao siyo
mamluki wa
CCM-- watu jasiri (siyo watu waoga) na wanaojua
kusoma,
kuandika na kuhesabu na wenye moyo wa kujitolea kwa faida
ya
walio wengi wanaoteseka na maisha duni. Kura ni
hesabu kwa
mtu asiyejua kusoma, kuandika na kuhesabu ni
rahisi sana
KUDANGANYIKA maana hataweza kusoma na kuelewa
kilichoandikwa.
Tano: UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye
anaweza kuvumilia njaa ikibidi kukaa bila
kula na kunywa
kwa zaidi ya saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita
kwa
kuendekeza ulaji na unywaji wakiwa kazini kwenye
vituo vya
kupiga kura, waliagiza vinywaji na vyakula na
vinywaji.
Lakini wajanja waliweka kwenye vyakula na vinywaji
hivyo
dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na
walikuja
kuamka uchaguzi ulikuwa umewisha na
kura za mgombea wao
ambaye alikuwa anapendwa na watu amekwishaibiwa kura
zake
wakiwa usingizini.
Ninachosema hapa ni kwamba uchaguzi ni wa mwaka huu
ni
mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini (wakiwepo
wanaCCM wengi tu) na kikundi cha watawala wa CCM
wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.
Hivyo mamilioni ya wananchi wanaoteseka na umaskini
wakiamua
kuvishinda vishawishi na ulaghai unaofanywa na watawala wa
CCM uchaguzi wa mwaka huu utaleta mabadiliko kwa mara
ya
kwanza kuwezesha mfumo wa vyama vingi kufanya kazi
Tanzania.
Zaidi fursa ya mamilioni ya wananchi wanaoishi maisha
ya
kimaskini kushinda uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni
kubwa
kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama
vingi
nchini kwetu.
Sita: UKAWA wahakikishe inawaelekeza
mawakala wake mambo
muhimu ya kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura.
Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha
wanachukua kwa usahihi
matokeo kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye
halmashauri
kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.
Umuhimu wa kufuatilia hadi matokeo yatangazwe ni
kuhakikisha
waliopewa mamlaka kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na
Rais hawachakachui matokeo. Umma ukiwa unafuatilia
matokeo-wenye kutaka kufanya mchezo mchafu watauogopa
umma.
Hakuna kinachoshinda nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Ninaruhusu Makala hii ichapishwe na yeyote anayetaka.
Lengo
ni kuelimishana ili kuleta mabadiliko . Ukiwa na
swali:
niandikie: ananilea_nkya@yahoo.com
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>,
"mabadilikotanzania@googlegroups.com"
<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "WANA BIDII"
<wanabidii@googlegroups.com>,
"Paschally
Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM
Mama Nkya nimekuelewa sana
sana na sana, siku zote nimekuwa nikifuatilia
harakati
zako
ila sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa
kuwaambia
watanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni
yake
haijalishi yupo wapi, ana nafasi gani kwa jamii au
yupo
upande gani kisiasa. Ulichokiandika ni very simple
and
very
true hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha
ajabu
kuna
wasomi watakuja kupinga na wanaendeta kupinga
ulichokiandika
tena wakitumia data za uongo kabisa. Ni ukweli
uliowazi
kuwa
watanzania wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na
nashukuru
yeye mwenyewe amekiri hilo juzi kupitia kituo kimoja
cha
redio(clouds fm), watanzania wa leo wanahitaji
mabadiliko
chanya na wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia
nyingine yoyote japo hatupendi ifike huko.Mama
Nkya, naomba ukipata muda unijibu haya mawili,
Je, tufanye nini watanzania lei hii ili kuzuia
kabisa
mchezo wa ccm kutuibia kura zetu kwenye uchaguzi
mkuu?
Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za
leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?
Asante
na ubarikiwe sana,
RAYMOND
MAUKIKIGAMBONI,
DAR ES SALAAM.
From:"ananilea nkya
ananilea_nkya@yahoo.com
[Wanazuoni]"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
[Attachment(s) from
ananilea nkya
included below]
LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU
KUZUIA MABADILIKO
Na Ananilea Nkya
Nimeandika hoja hii baada ya kusoma na
kusikia hoja
zinazotolewa na baadhi ya Watanzania
kwamba eti CHADEMA
,
CUF, NCCR-Mageuzi na NLD -vyama
vinavyounda UKAWA kwa
kumsimamisha Edward Lowassa kugombea
Urais vimepoteza
usafi wa kuongoza mapambano dhidi ya
ufisadi.
Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA
kumsimamisha
Lowassa kuwa mgombea urais wamecheza kama Pele. Tena
wanastahili pongeze kubwa maana walitumia akili kali
na
saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM ilikuwa
ilicheza
mchezo mchafu kisiasa kuwatumia wapinzania
kumpakazia
Lowassa ufisadi na hatimaye CCM kupata nguvu ya
kumtoa
Lowassa kafara ili eti CCM ionekane inajisafisha
ufisadi.
Wanaodhani CHADEMA na UKAWA wamekosea pengine
hawajaelewa
kuwa tangu upepo wa mabadiliko
wa kukataliwa mfumo
chama
kimoja kuwa madarakani kwa muda mrefu ulipoanza
kuvuma
duniani kote mwishoni mwa miaka ya 1980, baadhi
ya
wanaCCM
hawajakubali kwa dhati kabisa ukweli huo na
kuamini kwamba
CCM inaweza kupunzishwa kuongoza nchi angalao
kwa miaka
mitano.
Hasa baada ya Mwalimu Nyerere CCM kuondoka duniani,
CCM
imebaki na viongozi ambao hawako tayari kutumia
ujasiri
kuongoza mabadiliko kwa amani. Baadhi ya
vongozi
wanaojali
zaidi maslahi ya wana CCM wachache wanaotumia kauli
kama
hirizi kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere kuwa
bila
CCM
imara—Tanzania itayumba kujidanganya wenyewe na
kudanganya
wananchi.
Wanasahau kwamba Mwalimu Nyerere kama mwanafalsafa
na
mwanasiasa makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri
kwa
faida ya taifa na wananchi kulingana na hali halisi
ya
wakati husika kwa kusoma upepo wa wananchi. Kwa
mfano
Nyerere aliwahi kusema CCM si mama yake akimaanisha
Tanzania
na Watanzania ni muhimu zaidi kuliko umuhimu wa CCM
kuwa
madarakani.
Mfano Mwalimu Nyerere mwaka 1992 alionyesha mfano
kwamba
maslahi ya nchi na wananchi ndiyo muhimu kuliko
maslahi
ya
CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi wa wanaCCM
wengi
waliokuwa wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama
vingi
nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa nchi
--kuharakisha
maendeleo ya wananchi.
Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila
mwanaCCM
anayechaguliwa kuwa Rais, kwa kuogopa kulaumiwa
kwamba
eti
kama CCM haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura
atabeba
lawama za kufanya CCM iondoke madarakani, serikali
zote
za
CCM baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka duaniani
zimekuwa
zinajihusisha na ufisadi.
Serikali ya CCM imekuwa ikikwapua kwa wizi wa wazi
mabilioni
ya fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi
kuhakikisha
CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi zinafanyika
kama
geresha tu—kudanganya wafadhili na mataifa kuwa
Tanzania
ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi.
Mfano uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya CCM chini
ya
Rais
Mkapa ilikwapua fedha za wananchi kutoka Benki Kuu
Akaunti
ya EPA shilling bilioni 133 ambazo ziliiwezesha CCM
kumweka
madarakani Rais Ki
[The
entire original message is not included.]
__._,_.___
Posted by: Surumedia
<majiydsuru@gmail.com>
Reply
via web post
•
Reply to sender
•
Reply to group
•
Start a
New
Topic
•
Messages in this
topic
(2)
Visit Your Group
New Members
7
• Privacy • Unsubscribe • Terms of Use
.
__,_._,___
#yiv8322858708 #yiv8322858708 --
#yiv8322858708ygrp-mkp {
border:1px solid #d8d8d8;font-family:Arial;margin:10px
0;padding:0 10px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mkp hr {
border:1px solid #d8d8d8;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mkp #yiv8322858708hd {
color:#628c2a;font-size:85%;font-weight:700;line-height:122%;margin:10px
0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mkp #yiv8322858708ads {
margin-bottom:10px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mkp .yiv8322858708ad {
padding:0 0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mkp .yiv8322858708ad p {
margin:0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mkp .yiv8322858708ad a {
color:#0000ff;text-decoration:none;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-sponsor
#yiv8322858708ygrp-lc {
font-family:Arial;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-sponsor
#yiv8322858708ygrp-lc #yiv8322858708hd {
margin:10px
0px;font-weight:700;font-size:78%;line-height:122%;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-sponsor
#yiv8322858708ygrp-lc .yiv8322858708ad {
margin-bottom:10px;padding:0 0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708actions {
font-family:Verdana;font-size:11px;padding:10px 0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708activity {
background-color:#e0ecee;float:left;font-family:Verdana;font-size:10px;padding:10px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708activity span {
font-weight:700;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708activity span:first-child {
text-transform:uppercase;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708activity span a {
color:#5085b6;text-decoration:none;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708activity span span {
color:#ff7900;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708activity span
.yiv8322858708underline {
text-decoration:underline;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708attach {
clear:both;display:table;font-family:Arial;font-size:12px;padding:10px
0;width:400px;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708attach div a {
text-decoration:none;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708attach img {
border:none;padding-right:5px;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708attach label {
display:block;margin-bottom:5px;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708attach label a {
text-decoration:none;}
#yiv8322858708 blockquote {
margin:0 0 0 4px;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708bold {
font-family:Arial;font-size:13px;font-weight:700;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708bold a {
text-decoration:none;}
#yiv8322858708 dd.yiv8322858708last p a {
font-family:Verdana;font-weight:700;}
#yiv8322858708 dd.yiv8322858708last p span {
margin-right:10px;font-family:Verdana;font-weight:700;}
#yiv8322858708 dd.yiv8322858708last p
span.yiv8322858708yshortcuts {
margin-right:0;}
#yiv8322858708 div.yiv8322858708attach-table div div a {
text-decoration:none;}
#yiv8322858708 div.yiv8322858708attach-table {
width:400px;}
#yiv8322858708 div.yiv8322858708file-title a,
#yiv8322858708
div.yiv8322858708file-title a:active, #yiv8322858708
div.yiv8322858708file-title a:hover, #yiv8322858708
div.yiv8322858708file-title a:visited {
text-decoration:none;}
#yiv8322858708 div.yiv8322858708photo-title a,
#yiv8322858708 div.yiv8322858708photo-title a:active,
#yiv8322858708 div.yiv8322858708photo-title a:hover,
#yiv8322858708 div.yiv8322858708photo-title a:visited {
text-decoration:none;}
#yiv8322858708 div#yiv8322858708ygrp-mlmsg
#yiv8322858708ygrp-msg p a span.yiv8322858708yshortcuts {
font-family:Verdana;font-size:10px;font-weight:normal;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708green {
color:#628c2a;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708MsoNormal {
margin:0 0 0 0;}
#yiv8322858708 o {
font-size:0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708photos div {
float:left;width:72px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708photos div div {
border:1px solid
#666666;height:62px;overflow:hidden;width:62px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708photos div label {
color:#666666;font-size:10px;overflow:hidden;text-align:center;white-space:nowrap;width:64px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708reco-category {
font-size:77%;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708reco-desc {
font-size:77%;}
#yiv8322858708 .yiv8322858708replbq {
margin:4px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-actbar div a:first-child
{
margin-right:2px;padding-right:5px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mlmsg {
font-size:13px;font-family:Arial, helvetica, clean,
sans-serif;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mlmsg table {
font-size:inherit;font:100%;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mlmsg select,
#yiv8322858708 input, #yiv8322858708 textarea {
font:99% Arial, Helvetica, clean, sans-serif;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mlmsg pre,
#yiv8322858708
code {
font:115% monospace;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mlmsg * {
line-height:1.22em;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-mlmsg #yiv8322858708logo
{
padding-bottom:10px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-msg p a {
font-family:Verdana;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-msg
p#yiv8322858708attach-count span {
color:#1E66AE;font-weight:700;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-reco
#yiv8322858708reco-head {
color:#ff7900;font-weight:700;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-reco {
margin-bottom:20px;padding:0px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-sponsor #yiv8322858708ov
li a {
font-size:130%;text-decoration:none;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-sponsor #yiv8322858708ov
li {
font-size:77%;list-style-type:square;padding:6px 0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-sponsor #yiv8322858708ov
ul {
margin:0;padding:0 0 0 8px;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-text {
font-family:Georgia;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-text p {
margin:0 0 1em 0;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-text tt {
font-size:120%;}
#yiv8322858708 #yiv8322858708ygrp-vital ul li:last-child {
border-right:none !important;
}
#yiv8322858708
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment