Tuesday, 1 September 2015

RE: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015

Ni kweli Elisa, lakini context inaelekea kuonyesha kuwa kile alichoambiwa na Gamanywa ndicho anachokiamini na ndicho anachokiwasilisha na kutaka watu waamini!
 
> Date: Tue, 1 Sep 2015 14:09:47 -0700
> From: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: Re: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Hii ndiyo hatari ya kukariri kapengele kamoja au mstari mmoja. ukitaka kuelewa unasoma paragraph . Swala la maaskofu alikuwa anaeleza alichoambiwa na Gwasma hivyo mashehe hawaingii
> --------------------------------------------
> On Wed, 9/2/15, Neatness Msemo <nmuzeh@gmail.com> wrote:
>
> Subject: Re: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Wednesday, September 2, 2015, 12:06 AM
>
> Ameonyesha udini
> kuchochea kuwa maaskofu wamehongwa anataka waislam wajione
> kuwa lowasa ni wakristo hii ni mbaya ametumwa tunamsamehe
> bure yaani hasira imezidi
> On Sep 1, 2015 11:49
> PM, "Neatness Msemo" <nmuzeh@gmail.com>
> wrote:
> Nadhani ni vema sana kuangalia kwa makini kwani
> pamoja na ukweli au uongo wa anayezungumza  je chanzo cha
> haya yote source yake ni hasita au kukosa au nia yake ni
> kumwaga mboga lakini watanzania wamechoka kwani hakuna
> msafi
> On Sep 1, 2015 11:01
> PM, "'mpombe mtalika' via Wanabidii"
> <wanabidii@googlegroups.com>
> wrote:
> Slaa:
> Watanzania wana kiu ya kujua kwanini amekuwa kimya kwa muda
> mrefu sasa licha ya
> harakati za kisiasa kuendelea.
>
>
>
> Muda utakaotumika ni saa moja, hakuna muda mrefu sana.
>
> Ameamua kufanya hayo kwa kuwa imefika mahali ukweli lazima
> usemwe na
> upotoshwaji ukomeshwa. Namna pekee ya kufanya hivyo ni
> kutoka hadharani na
> kuusema ukweli.
>
>
>
>
>
> Sote
> tunafahamu kuwa hana tabia ya kuchenga mambo, mengi
> yamesemwa na watu tofauti,
> kwenye mitandao, magazeti na viongozi wake! Hana ugomvi na
> kiongozi yoyote, kwa
> kuwa siasa sio ugomvi. Kama binadamu wa kawaida hana chuki
> wala hasira na
> binadamu mwingine yoyote!
>
>
>
> Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna misingi ambayo inaongoza
> taifa. Inapofika
> mahali taifa linaongozwa kwa msingi ya propaganda na
> upotoshwaji matokeo yake
> ni vurugu kubwa katika taifa. Yeye amekataa hayo yote!
>
>
>
> Anasema kuwa YEYE hakuwa likizo kama inavyosemwa na viongozi
> wake! Atafafanua
> kwa kifupi! Kilichotokea ni kuwa aliamua kuachana na siasa,
> tarehe 28 Julai
> 2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona yanayofanyika
> ndani ya chama
> chake hayamridhishi.
>
>
>
> Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa alishiriki tangu mwanzo kwenye
> mchakato. Anasema
> ni kweli alishirii kwenye majadiliano, akaweka msingi na
> msimamo wako. Kuna
> wakati wengi wanashinda kutokana na wingi wao, wewe
> unayeamini katika misingi
> inabidi uachie ngazi.
>
>
>
> Baada ya Edward Lowassa kukatwa na CCM Dodoma, Mshenga wake
> alimpigia simu na
> kuuliza nini kifuate baada ya tukio la dodoma. Akamuambia
> wawasiliane na
> mwenyekiti Freeman Mbowe, Gwajima nae akafika kwenye kikao
> hicho.
>
>
>
> Msimamo wa Slaa ni kuwa ni lazima kumsikiliza mtu kabla ya
> kuamua nini cha
> kufanya. chadema ni cham cha siasa na hakiwezi kumkataa mtu
> yeyote kujiunga na
> chama.Wakaweka vijana kuchunguza nini wanataka hao wanaotaka
> kujiunga na chama!
>
>
>
> Slaa akataka kwanza Lowassa atangaze kutoka kwenye chama
> chake alichopo, kisha
> atangaze anakwenda kwenye chama gani. Atumie nafasi hiyo ya
> mkutano huo
> ajisafishe na tuhuma zote ambazo amekuwa akituhumiwa na
> watu.
>
>
>
> Chadema ni cham ambacho kwa muda mrefu kimejijenga kwa
> msingi, na ni lazima
> wapokee mtu ambaye hawezi kukichafua chama chao. Lowassa
> hakutangaza kujitoa,
> wala kujisafisha hadi kwenye mkutano ambao uliandaliwa na
> chadema. Slaa
> hakuhudhuria ule mkutano.
>
>
>
> Kwenye kila jambo kuna jambo la kuzingatia. Mtu anayejiunga
> popote anakuja kama
> mtaji au kama mzigo? Lowassa anakuja chadema kama asset au
> liability? Ijulikane,
> suala sio urais! Mpaka siku hiyo Slaa hakuwa amechukua fomu
> ya Urais kwenye
> chama chake. Slaa hakuwa anamzuia Lowassa kugombea urais
> chadema. Alitaka
> mgombea mwenye sifa na uwezo wa kukitoa Chama cha
> Mapinduzi.
>
>
>
> Hakutamka popote kuwa anataka kugombea, hata 2010
> hakugombea, aliombwa
> kugombea! Urais wake binafsi hauwezi kuikomboa nchi bila
> mchango wa jamii
> nzima.
>
>
>
>
>
> Mwafrika,
> [01.09.15 15:45]
>
> Suala la adha Lowaasa ni msizo au mtaji halikujibiwa hadi
> siku ya mkutano
> tajwa. Wakataka kujua anapokuja anakuja na akina nani, ni
> wafuasi wa aina gani;
> vijana wa bodaboda, vijana wasio na ajira au watu
> waliosombwa tu, au wanakuja
> kwenye mapambano?
>
>
>
> Jibu lilikuwa ni kuwa tungepata wabunge 50 na wenyeviti wa
> CCM mkoa wasiopungua
> 22, wenyeviti wa CCM wilaya 88. Slaa akakiri kuwa kama ni
> hivyo kutakuwa na
> tetemeko (la kisiasa).
>
>
>
> Wakahitaji majina ya hao waliotajwa kwa kuwa walikuwa kwenye
> mchakato wa
> kupitisha majina kwenye chama. KAtibu mkuu makini huwezi
> kuchukuwa watu usiowajua.
> Hakuna jina nililopewa mpaka tarehe 25.
>
>
>
> Tarehe 25 wakamfata na kumuambia aitishe Kamati Kuu ya
> chama. Akakubali lakini
> akatahadjharisha kuwa hajapata majina na hajapata jibu kuwa
> Lowassa ni asset au
> liability. Lakini akaitisha kikao kwa kuwa ni jukumu la
> kikatiba la katiba.
>
> Mwenyekiti akapiga simu, anasikia kuwa hajaridhika. Tangu
> 2004 Slaa hajawahi
> kugombana na mwenyekiti wake, isingekuwa sawa kama
> wangetofautiana kwenye kikao
> rasmi.
>
>
>
> Wakakutana na Mwenyekiti, Gwajima, Lissu na wakajadiliana
> mpaka saa 9 mchana.
> Maneno kuwa alikuwa anakubaliana na mpango huo tangu mwanzo
> SI KWELI!
>
> Mkutano ukashindikana. Wdau wakasema waende nyumbani kwa
> Lowassa, Slaa akakataa
> wakaenda Kamati kuu.
>
>
>
> Kikao kikafanyika hadi saa 12 jioni. Ikaundwa kamati ndogo
> ya kumshawishi Slaa.
> Akakataa! Akaandika barua ya kujiuzulu kwa kamati, Prof.
> Safari akaichana barua
> yake. Akaandika barua nyingine kwa Makamu-Zanzibar, makamu
> akamuambia kuwa haya
> mambo yamepangwa, asijisumbue!
>
>
>
> Wanasema siasa ni mchezo mchafu, yeye anaaamini kuwa siasa
> ni sayansi! Asubuhi
> ya kesho akaandika barua, wasichojua ni kuwa kujiuzulu
> hakuhitaji barua. Maneno
> yakazuka kuwa Slaa hajaandika barua! Upotoshwaji ukaendelea
> kuwa Slaa
> atazungumza na waandishi wa habari, wengine wakasema
> amefungiwa, amefungiwa na
> mkewe na kadhalika! Ukweli ni kuwa alikuwa na Lissu, Gwajima
> na Mbowe tangu
> asubuhi.
>
>
>
> Maamuzi aliyoyafanya yanatokana nadhamiri yake! Josephine
> nae ni mwanaharakati,
> ana sababu ya kuwa na uchungu. Alipigwa mwaka 2011 wakati
> wengine walijificha!
> Propaganda hizo tumeshazisoea!
>
>
>
> Kama kuna mwenye ushahidi wa propaganda hizi aje, audited
> report zipo!
> Josephine halipwi na chama! Watu wanasema kuwa Slaa analipwa
> mil. 7, yeye
> ameendelea kula mihogo na maharage kama walivyoahidi mwaka
> 2010. Wana uchungu
> na harakati!
>
>
>
> Kikubwa katika harakati ni credibilty, jina la chama
> kilichojengwa kwa muda
> mrefu kisichafuliwe kwa namna yoyote! Mwanasiasa yoyote
> hataki kuchaguliwa, na
> Slaa nae hataki kuchaguliwa! Wanasema kuna maslahi mapana ya
> taifa, ni nani
> anayapima? Lazima kuwe na kipimo cha kuapima hayo maslahi
> badala ya kutegemea
> mtazamo wa mtu!
>
>
>
> Anafafanua suala la liability sasa!
>
>
>
> Wamekuwa waongo kwa kuwa hakuna kipengele hata kimoja cha
> madai ya Slaa
> kimetekelezwa. Alisema wabunge waje kabla ya kura ya maoni
> ya CCM, kuja baada
> ya hapo ni kutafuta kichaka cha kujificha!
>
>
>
> Watanzania wameijenga Chadema kwa damu yao, rasilimali zao!
> Watu hawawezi
> kukimbilia kirahisi wakati sio wasafi, akiwemo Sumaye na
> wengine. Nani hajua
> kama Sumaye ni fisadi? Kwa muda mrefu Slaa haongei na Sumaye
> kwa kuwa
> alimtuhumu kwa ufisaidi.
>
>
>
> Sumaye ni mtu ambaye wanahabari walidai kuwa Sumaye alisema
> kuwa atahama chama
> endapo Lowassa atateuliwa, leo akageuka! 
> Leo anamsafisha Lowaasa, dhambi haisafishwa kwa
> dhambi. Anakumbusha jina
> la Mr. Zero (jina la utani la Sumaye).  Chama
> kimepokea makapi, na katibu alitahadharisha kuwa chama
> hakipokei makapi! Hakuna
> ambaye alijitoa kwa hiari, wengi walikuja baada ya kukatwa.
> Wenyeviti wengi ni
> mzigo, akiwemo Msindai.
>
>
>
> Anangoja ajibu amlipue hadharani kwa kuwa alikuwa mwenyekiti
> wa kamati ya bunge
> hesabu za serikali z mitaa. Siku aliyoambiwa aitishe kamati
> kuu aliuliza
> majina, akaambiwa anakuja chizi! Chizi ni nani, hata nyie
> hamumjui! Anaitwa
> chizi kwa kuwa ni mwizi wa kura ndani ya CCM.
>
>
>
> Kuna haja gani ya kushindana kama tunampango wa kuiba kura
> pia. Wakamtaja
> Guninita, nani asiyemjua udhaifu wake? Hawezi kuandika hata
> ukurasa mmoja wa
> ripoti, amehama vyama mara kadhaa!
>
>
>
> Mwafrika, [01.09.15 15:45]
>
> Viongozi wa Chadema wamepata kigugumizi, waseme nani
> ameongeza thamani kwenye
> chama? Najua maneno ya kuwa ni lazima kuiondoa CCM kwanza
> hata ikibidi tuweke
> mkataba na shetani, mimi ni padre wa Kanisa Katoliki!
> Kuwaondoa CCM kwa namna
> yoyote hakuleti maendeleo. CCM itaondolewa kwa program
> siriaz, sio kutumia watu
> wale wale!
>
>
>
> Lazima tujue nini kilifanya Watanzania waamini chadema, kwa
> kuwa waliamini wana
> misingi isiyoyumba na uadilifu. Leo tunasimamia uadilifu?
> Wanasema mwenye
> ushahidi aende mahakamani. Kama tusingewatuhumu Mramba na
> Yona wasingefikishwa
> kizimbani. Chadema imefungwa mdomo kwa kisingizio cha
> ushahidi!
>
>
>
> Ni bora kukaa kimya kuliko kupotosha. Anasema nukuu ya
> biblia kuhusu
> wapotoshaji! Inapofika mahali unapoambiwa hakuna mwenye
> dhambi ni makosa,
> dhambi haisahihishwi kwa dhambi nyingine! CCM wamekuwa
> waoga, wamewalea watu
> hawa kwa muda mrefu!
>
>
>
> Kwa Wafrika choo ni neno baya, kwa wazungu choo ni rest
> room! Choo cha
> Kitanzania huwezi kukihamisha ndani ya chumba cha kulala na
> ukakiita choo,
> huwezi kulala kwa kuwa kitanuka, tena zaidi! Ufisadi ilikuwa
> ajenda iliyowapa
> umaarufu CHADEMA, leo wamewachukua. Waanweza kuwa na ujasiri
> wa kukemea
> ufisadi?
>
>
>
> Mwaka 2008 Slaa alikuwa bungeni wakati wa sakata la
> Richmond, anafahamu kwa
> uzuri anachokimaanisha. Bahati mbaya waandishi hawasomi
> makaratasi, na wabunge
> wa CCM pia.
>
>
>
> Lowassa hatuhumiwi kwa habari ya Richmond pekee! Lowassa
> aliambiwa na Slaa
> aache kulalamika, atangaze uhalali au uharamu wa Richmond,
> anamtaka aseme hao
> 'wakubwa' ni akina nani? Ni afadhali sifa yake
> iharibike kuliko kusema uongo.
>
>
>
> Ni aheri kupotea kwenye siasa za dunia kuliko kusimamia
> uongo! Msingi wa kwanza
> wa Richmond: Ili uelewe ni lazima urudi kwenye taarifa ya
> Kamati ya Mwakyembe,
> Slaa alifuatwa asubuhi ya siku ile kupewa rushwa, anashuru
> Sitta na Mwakyembe
> wajitokeze!
>
>
>
> Akamuuliza mtoa rushwa kama anatoa m.500 kwa mbunge, atakuwa
> nazo ngapi?
> Aliwaambia Sumaye na Lowassa kuwa rushwa ni jambo
> linaloanzia kifuani kwanza.
> Mwanzo wa jambo hili ni taarifa ya Baraza la Mawaziri la
> 10.2.2006. Kamati ya
> mwakyembe iliangalia faili la kikao kile kisha kuandika
> ripoti!
>
>
>
> Suala hili lilianzia wakati wa utawala wa mkapa kutokana na
> dharura ya umeme
> nchini, wakawasiliana na kampuni moja ya Amerika Kaskazini
> kwa suluhu ya muda
> mfupi ya umeme. Serikali ya Kikwete ikapokea lile suala.
> Wakaruhusu mpango uendelee,
> ila kwa kufuata sheria. Hiyo ilikuwa kauli ya Baraza la
> Mawaziri!
>
>
>
> Wakati auala lile linaamuliwa, Lowassa alikuwa Waziri Mkuu!
> Na ndie mwenye
> mandate ya maamuzi ya Serikali, iweje leo akane kuhusika?
> Taarifa ya Mwakyembe
> inapotoshwa! Taarifa ilitaka Waziri Mkuu ajipime, au bunge
> limjadili na
> kumchukulia hatua. Lowassa akakimbia kwa kuwa alijua Bunge
> lingemfukuza kazi!
>
>
>
> Waliioomba tenda walikuwa 26, waliorudisha walikuwa 8.
> Kamati ya Tathmini
> ikaona hakuna anayefaa hata mmoja! Waziri Msabaha akaagiza
> taarifa ile ifutwe
> na tathmini ifanyike upya, mara ya kwanza, ya pili, ya tatu
> na ya nne. Jeuri wa
> Msabaha ilitoka wapi? Baraza likaamua baadaye tenda
> iliyopewa kwa kampuni ya
> kwanza ifutwe! Lowassa alishiriki!
>
>
>
> TANESCO wakatoa ushauriwa wao, Mamlaka husika ikatafute
> internatonal tender ya
> kununua turbine! Lowassa akaingilia mchakato dakika za
> mwisho, akamuagiza
> katibu muhtasi wake!
>
>
>
> Kwanini Lowassa, kwa kuwa anagombea urais, rais asiyeaminika
> hawezi
> kuchaguliwa!
>
> Lowassa alishawahi kumuita Slaa kuhusu habari ya Meremeta,
> na kumuambia kuwa
> taarifa yake inaiaibisha Serikali! Kampuni ya jeshi imewahi
> kutengeneza gari,
> imehujumiwa na wahuni. Akamtaka Lowassa amuambie ni nani
> aliyehusika?
>
>
>
> Akamuita mwingine kwnye Speaker lounge. Slaa akamuambia kuwa
> yeye ni fisadi
> kichwani, rohoni mpaka...!
>
>
>
> Tunamsifia Lowassa kuwa an=taleta maji wakti jimbo la
> Lowassa halina maji na
> ufisadi mkubwa umefanyika kwneye jimbo hilo. Mnazungumzia
> shule za kata wakati
> wakati hamjua zimeanza wapi? Slaa anataja nafasi alizowahi
> kushika Afrika.
> Uamuzi wa kujenga shule za kata ulifikiwa mwaka 90 huko
> Thailand, mpango huo
> ukaitwa Education for All, sio MMES kama unavyoitwa leo!
>
>
>
> Mwafrika, [01.09.15 15:45]
>
> Anasoma barua ya Ibrahim Msabaha kwa Flugence Kazaura,
> mkurugenzi wa bodi wa
> TANESCO!
>
>
>
> Mpango ulikuwa kuondoa suala la umeme mikononi mwa tanesko
> kwa kuwa imeshindwa
> kutekeleza. Ugomvi wake na Masha ni kwa kuwa Lowassa
> alimlaumu Masha kuingilia
> mchakato wa serikali, akawekewa kinasa sauti chumbani.
> Waziri Mkuu haruhusiwi
> na sheria kuingilia mchakato wowote wa tenda.
>
>
>
> Kwenye kampuni nane zilizowasilisha maombi ya zabuni,
> Richmond ni kampuni
> iliyokuwa mbovu. Ilikuwa ni kampuni ya steshenari, sio
> umeme!Wakadai wana
> ushirikiano na kampuni nyingine ya umeme, kampuni hiyo
> ikakataa kujihusisha na
> Richmond, wala kuzalisha na majenereta!
>
>
>
> Bill Clinton aliwai kukutwa na kashfa, walitaka kumchukulia
> hatua si kwa sababu
> ya zinaa, bali kwa kuwa alifanya uongo! Kwa kuwa alidanganya
> umma! Hata sheria
> za Tanzania zinakataza kuongopa, hata kesi za uchaguzi za
> Slaa zimethibitisha
> hilo.
>
>
>
> Lowassa anadai yeye alisimamisha tenda, Slaa anaonesha
> uthibitisho wa hilo kwa
> barua za Lowassa kwenda kwa Msabaha zinazokanusha hilo,
> 'Anaisoma'! Waziri Mkuu
> aliharakisha mchakato wa tenda, tofauti na sheria ya PPRA.
> Barua imeandikwa
> miezi mitatu baada ya mkataba kusainiwa, kwa maagizo ya
> Waziri Mkuu.
>
>
>
> Tanesko ikaagizwa kusaini mkataba ambao haikuhusika kwenye
> kuujadili! Anaona
> aishie hapo... Anaupigia chapuo mdahalo wa Sitta na
> Mwakyembe, anasema Lowaasa
> nae afike kuondoa utata na kusema ukweli!
>
>
>
> Chadema ni chama kilichotoa matumaini kwa vijana wengi!
> Isifike mahali tukawa
> washabiki kama 2005 ambapo watu waliahidiwa maisha bora,
> wakajikaanga kutokana
> na ushabiki! Anatoa ushahidi wa kitakwimu wa mfumuko wa
> bei...
>
>
>
> Slaa ana uchungu kuona chama alichokijenga, kikifikia hatua
> ya kusomba watu kwa
> mabasi na malori kisha mkasema mafuriko hayazuiliki! Hayuko
> tayari,... Anakataa
> kuwa ZEZETA! Ajenda ya Chadema ni nini, ilikuwa ni rushwa!
> Wananchi waliamini
> kwa kuwa msingi huo ndio unakijenga chama!
>
>
>
> Sehemu kubwa ya kilichosemwa Jangwani ni ilani ambayo
> ilishaandaliwa tayari,
> hakuna kipya kilichosemwa. Kinachomuuma ni chama makini kuwa
> kibovu zaidi ya
> Chama cha Mapinduzi! Hatuwezi kujenga maadili tukiwa na watu
> wachafu, anaishi
> na mwanamke bila kufunga ndoa kwa kuwa Serikali ya CCM
> haitaki afunge ndoa.
> Kesi yake ililetwa na mawaziri, waandishi wa habari na mtu
> kutoka IKULU. Ndoa
> inafungwa na Mungu!
>
>
>
> Scotland Yard iliamrisha Lowassa achunguzwe, inakuwaje leo
> tunamtetea? Huu ni
> ushabiki usio na vielelezo, Slaa ana ushahidi! Hakuna
> ulazima wa kwenda
> mahakamani kwa kuwa kesi ya rushwa ni jinai, ni kesi ya
> serikali! Slaa au
> mwingine hana locus ya kwenda mahakamani kwa kesi ya jinai!
> Mwakyembe alisema
> kesi ya jinai haina mwisho (kama zilizyo za madai). chadema
> iliahidi kusafisha
> nchi kwanza endapo itashika dola, huku maendeleo
> yakiendelea!
>
>
>
> Anasoma barua ya mchakato wa Richmond kuwa DOWANS. Kampuni
> imesajiliwa Costa
> Rica, na mwenyekiti asiye na anuani, simu wala jengo! Siku
> iliyosajiliwa,
> mmiliki alisajili makampuni mengine 99! Zaidi ya hayo ana
> makampuni mengine
> zaidi ya 50, DOWANS ni jina tu. Kampuni haipo! Dowans sio
> kampuni halisi huko
> Kosta Rika, nchi nzima hakuna kampuni yenye uwezo wa
> kuzalisha umeme kwa
> kiwango hicho!
>
>
>
> Leo Lowaassa anatuambia tufunge mdomo, huu ni udikteta!
> Anakumbusha sakata lake
> na Waziri Marmo... Mabilioni ya fedha yanalipwa kwa kampuni
> ambayo haipo!
> Tunapenda ushabiki... Acha sifa iharibike!
>
>
>
> Anasema hataki kuingia kwenye mambo ya Babu Seya! Vyuo vikuu
> vinatumia kesi ya
> Babu Seya kama case study. Mtoto mdogo hawezi kutoa ushahidi
> mahakamani, haki
> inapuuzwa kwa kuwa mtoto hawezi kutoa ushahidi!
>
>
>
> Kesi ya Ulawiti rais hana mamlaka nayo, anatoa wapi kiburi
> cha kusema kuwa
> atamtoa? Aliyeagiza polisi kuingia na polisi kuingia na mbwa
> msikiti wa
> mwembechai ni Sumaye, akiwa waziri mkubwa. Leo hii ni mpiga
> kampeni wa Lowassa!
> Leo tunataka kura kwa namna yoyote! Ni afadhali kutokuwa na
> rais wa aina ya mtu
> huyu! anayesaka kura kwa kusaka huruma za watu. Slaa hayuko
> tayari kuona hilo
> linatokea... Anahitimisha kwa kusema hajagusa chochote
> kuhusu ilani wala
> mkakati!
>
>
>
> Mwafrika, [01.09.15 15:45]
>
> Kama taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua vitu nje ya
> shamrashamra, maneno
> matamu! Tumeshaumwa na nyoka, tusilaghaiwe na maneno ya watu
> hawa tena! Utendaji
> uliotukuka unapimwa kwa utafiti, sio kwa ukasuku na kunukuu
> maneno ya
> wanasiasa!
>
>
>
> Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu, matatizo ya wakulima na
> wafugaji yalikuwepo,
> alifanya nini? Lowassa aliwahi kubadili mpaka wa Monduli na
> Karatu na
> kusababisha mgogoro! Mkampenia wake, Sumaye alisababisha
> matatizo ya ardhi
> Mvomero, akipora ardhi ambayo ilitakiwa yajengwe makao makuu
> ya Mvomero!
> Mengine ya Sumaye ameyaweka kiporo, hisa zake za kampuni
> aziweke wazi kama
> Sekretarieti ya Maadili inavyotaka!
>
>
>
> Kutotangaza mali kunatosha kumtoa mtu ubunge! Sembuse
> Urais?
>
>
>
> ============================== =========================
>
>
>
> Ukweli huwa una tabia ya kuegemea upande, anasemea
> speculation kuwa ameisema
> chadema peke yake. Anasema amestaafu siasa, hana chama
> lakini bado anabaki kuwa
> mtanzania, mtetezi wa wanyonge na atabaki hivyo! Ataendelea
> kuwatumikia
> watanzania kadiri ya Mungu alivyomjalia vipawa! Kama
> alivyoombwa kugombea urais
> 2010!
>
>
>
> Anaweza kuwatumikia Watanzania bila kuwa na chama!
>
>
>
> Anasema kuwa hajapata vitisho kama alivyopata kipindi hiki,
> inazidi hata wakati
> alipotangaza List of Shame. Rostam ndiye anafadhili kampeni
> za urais wa
> Lowassa! Anamnukuu vitisho vyake! anakiri kuwa maaskofu
> wamehongwa, Rostam
> akiwa anaona, m60-m300! Anasema hatenda chama chochote,
> anasisitiza! Amejitoa
> rasmi siasa za vyama vya siasa... Ataendelea kuwa msimamiaji
> wa anachokiamini!
>
>
>
> Anawataka watu aliowataja watoke hadharani, anatoa baraka za
> KIMUNGU kwa nchi
> na watu wake!
>
>
>
> MASWALI!
>
>
>
> Swali: Unawammbia nini Watanzania kuelekea uchaguzi, ni rais
> yupi anafaa?
>
> Amesema hana chama, hampigii kampeni mtu yoyote! Amesema
> anafanya uchambuzi wa
> madhara ambayo taifa litapata endapo watamchagua Lowassa, na
> kwa kuwa na uzoefu
> nao kwa muda mrefu!
>
>
>
> Hataki kufanya kampeni yoyote. Anawaelimisha Watanzania
> kuacha ushabiki
> utakaowagharimu! Ni watu wachache wanoweza kumtaja mtu kwa
> majina, kuna tofauti
> ya wanaotaja ajenda tu na wanaotaja majina.
>
>
>
> Rostam alimuambia kuwa ana dakika 5 za kuishi, apige magoti
> na kusali! Aliweka
> roho yake rehani kwa ustawi wa taifa hili...Anakumbusha ya
> Mwembeyanga na namna
> Usalama wa Taifa walivyokuwa na tension. Magazeti mengi
> yaliogopa hata kuandika
> habari, isipokuwa MWanaHalisi!
>
>
>
> Swali: Siasa ingekuwa asset kama angekuja na wabunge kadhaa.
> Angekuja kama asset,
> mengine yangesafishika? Kulikuwa na vigezo viwili, ama asset
> na liability,
> yaani hayo madhambi yote aliyoyasema. Baada ya hayo
> wangefanya tathmini kama
> anapokelewa au hapokelewi. Anatoa mfano wa Shirikisho la
> Afrika Mashariki na
> nchi zinazotaka kujiunga!
>
>
>
> Swali: Waliopokelewa ni makapi. Je wewe ulikuwa kapi 95?
>
>
>
> Anauliza kama watu wanaamini yeye alikuwa kapi? Tupime
> vigezo... Makapi ni watu
> waliokataliwa na watu wao baada ya kuwa wabunge kwa muda
> mrefu. CCM wakasema
> kuwa hakuwa mwenzao: hakuwa anahonga, hakuwa anapokea rushwa
> na kadhalika! Kuingia
> kwa tiketi ya Chadema ulikuwa ukombozi kwake!
>
>
>
> Swali: Umetangaza kustaafu siasa, una kadi za vyama viwili.
> Unazirudisha au
> unakaa nazo?
>
>
>
> Watanzania tuelimika, kadi sio uanachama. Kadi ni mali ya
> mwanachama, unaweza
> kuichoma, kuweka kumbukumbu au vyovyote, sawa na kadi ya
> ndoa ambayo
> hairudishwi hata kama ndoa itavunjika. Tuulize maswali ya
> kujenga.
>
>
>
> Swali: Anaoneka baada ya kukosa urais anamshambulia
> Lowassa!
>
>
>
> Wapi Slaa alichukua fomu ya Urais, hakuwa na nia na urais
> wala hawezi
> kukasirika. Tuache ushabiki, tuwe na mtiririko na kuzingatia
> hoja! Mwandishi
> awe msikivu sana... Ameeleza tangu mwanzo, hana chuki wala
> ugomvi na mtu
> yoyote!
>
>
>
> Chama cha Mapinduzi kilishakuja kumpa ofa kadhaa kuachia
> jimbo la Karatu, akaweka
> sharti la mkataba wenye sahihi za watu watatu; Rais, Slaa na
> Yesu Kristo.
>
>
>
> Swali: Kama wewe uliweza kuhama, wengine nao hawawezi?
>
>
>
> Dr. Slaa hakuwa na uchafu wowote, tatizo halikuwa kuhama
> chama, tatizo ni watu
> wa aina gani wanahama chama?
>
>
>
> Swali: Unahamasisha uwazi, mbona wewe umemficha muovu mmoja?
>
>
> Silaha haziwekwi zote mezani, amewaomba anaowatuhumu
> wajitokeze!
> CHANZO kwa hisani
> ya jf
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment