Elisa
Hebu tusubiri kwa vile Gwajima yupo huenda nae akatueleza kwa upande wake. Huu ni upande mmoja tu wa habari
Fatma
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
-----Original Message-----
From: "'ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tue, 1 Sep 2015 14:09:47
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya
Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
Hii ndiyo hatari ya kukariri kapengele kamoja au mstari mmoja. ukitaka kuelewa unasoma paragraph . Swala la maaskofu alikuwa anaeleza alichoambiwa na Gwasma hivyo mashehe hawaingii
--------------------------------------------
On Wed, 9/2/15, Neatness Msemo <nmuzeh@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, September 2, 2015, 12:06 AM
Ameonyesha udini
kuchochea kuwa maaskofu wamehongwa anataka waislam wajione
kuwa lowasa ni wakristo hii ni mbaya ametumwa tunamsamehe
bure yaani hasira imezidi
On Sep 1, 2015 11:49
PM, "Neatness Msemo" <nmuzeh@gmail.com>
wrote:
Nadhani ni vema sana kuangalia kwa makini kwani
pamoja na ukweli au uongo wa anayezungumza je chanzo cha
haya yote source yake ni hasita au kukosa au nia yake ni
kumwaga mboga lakini watanzania wamechoka kwani hakuna
msafi
On Sep 1, 2015 11:01
PM, "'mpombe mtalika' via Wanabidii"
<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Slaa:
Watanzania wana kiu ya kujua kwanini amekuwa kimya kwa muda
mrefu sasa licha ya
harakati za kisiasa kuendelea.
Muda utakaotumika ni saa moja, hakuna muda mrefu sana.
Ameamua kufanya hayo kwa kuwa imefika mahali ukweli lazima
usemwe na
upotoshwaji ukomeshwa. Namna pekee ya kufanya hivyo ni
kutoka hadharani na
kuusema ukweli.
Sote
tunafahamu kuwa hana tabia ya kuchenga mambo, mengi
yamesemwa na watu tofauti,
kwenye mitandao, magazeti na viongozi wake! Hana ugomvi na
kiongozi yoyote, kwa
kuwa siasa sio ugomvi. Kama binadamu wa kawaida hana chuki
wala hasira na
binadamu mwingine yoyote!
Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna misingi ambayo inaongoza
taifa. Inapofika
mahali taifa linaongozwa kwa msingi ya propaganda na
upotoshwaji matokeo yake
ni vurugu kubwa katika taifa. Yeye amekataa hayo yote!
Anasema kuwa YEYE hakuwa likizo kama inavyosemwa na viongozi
wake! Atafafanua
kwa kifupi! Kilichotokea ni kuwa aliamua kuachana na siasa,
tarehe 28 Julai
2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona yanayofanyika
ndani ya chama
chake hayamridhishi.
Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa alishiriki tangu mwanzo kwenye
mchakato. Anasema
ni kweli alishirii kwenye majadiliano, akaweka msingi na
msimamo wako. Kuna
wakati wengi wanashinda kutokana na wingi wao, wewe
unayeamini katika misingi
inabidi uachie ngazi.
Baada ya Edward Lowassa kukatwa na CCM Dodoma, Mshenga wake
alimpigia simu na
kuuliza nini kifuate baada ya tukio la dodoma. Akamuambia
wawasiliane na
mwenyekiti Freeman Mbowe, Gwajima nae akafika kwenye kikao
hicho.
Msimamo wa Slaa ni kuwa ni lazima kumsikiliza mtu kabla ya
kuamua nini cha
kufanya. chadema ni cham cha siasa na hakiwezi kumkataa mtu
yeyote kujiunga na
chama.Wakaweka vijana kuchunguza nini wanataka hao wanaotaka
kujiunga na chama!
Slaa akataka kwanza Lowassa atangaze kutoka kwenye chama
chake alichopo, kisha
atangaze anakwenda kwenye chama gani. Atumie nafasi hiyo ya
mkutano huo
ajisafishe na tuhuma zote ambazo amekuwa akituhumiwa na
watu.
Chadema ni cham ambacho kwa muda mrefu kimejijenga kwa
msingi, na ni lazima
wapokee mtu ambaye hawezi kukichafua chama chao. Lowassa
hakutangaza kujitoa,
wala kujisafisha hadi kwenye mkutano ambao uliandaliwa na
chadema. Slaa
hakuhudhuria ule mkutano.
Kwenye kila jambo kuna jambo la kuzingatia. Mtu anayejiunga
popote anakuja kama
mtaji au kama mzigo? Lowassa anakuja chadema kama asset au
liability? Ijulikane,
suala sio urais! Mpaka siku hiyo Slaa hakuwa amechukua fomu
ya Urais kwenye
chama chake. Slaa hakuwa anamzuia Lowassa kugombea urais
chadema. Alitaka
mgombea mwenye sifa na uwezo wa kukitoa Chama cha
Mapinduzi.
Hakutamka popote kuwa anataka kugombea, hata 2010
hakugombea, aliombwa
kugombea! Urais wake binafsi hauwezi kuikomboa nchi bila
mchango wa jamii
nzima.
Mwafrika,
[01.09.15 15:45]
Suala la adha Lowaasa ni msizo au mtaji halikujibiwa hadi
siku ya mkutano
tajwa. Wakataka kujua anapokuja anakuja na akina nani, ni
wafuasi wa aina gani;
vijana wa bodaboda, vijana wasio na ajira au watu
waliosombwa tu, au wanakuja
kwenye mapambano?
Jibu lilikuwa ni kuwa tungepata wabunge 50 na wenyeviti wa
CCM mkoa wasiopungua
22, wenyeviti wa CCM wilaya 88. Slaa akakiri kuwa kama ni
hivyo kutakuwa na
tetemeko (la kisiasa).
Wakahitaji majina ya hao waliotajwa kwa kuwa walikuwa kwenye
mchakato wa
kupitisha majina kwenye chama. KAtibu mkuu makini huwezi
kuchukuwa watu usiowajua.
Hakuna jina nililopewa mpaka tarehe 25.
Tarehe 25 wakamfata na kumuambia aitishe Kamati Kuu ya
chama. Akakubali lakini
akatahadjharisha kuwa hajapata majina na hajapata jibu kuwa
Lowassa ni asset au
liability. Lakini akaitisha kikao kwa kuwa ni jukumu la
kikatiba la katiba.
Mwenyekiti akapiga simu, anasikia kuwa hajaridhika. Tangu
2004 Slaa hajawahi
kugombana na mwenyekiti wake, isingekuwa sawa kama
wangetofautiana kwenye kikao
rasmi.
Wakakutana na Mwenyekiti, Gwajima, Lissu na wakajadiliana
mpaka saa 9 mchana.
Maneno kuwa alikuwa anakubaliana na mpango huo tangu mwanzo
SI KWELI!
Mkutano ukashindikana. Wdau wakasema waende nyumbani kwa
Lowassa, Slaa akakataa
wakaenda Kamati kuu.
Kikao kikafanyika hadi saa 12 jioni. Ikaundwa kamati ndogo
ya kumshawishi Slaa.
Akakataa! Akaandika barua ya kujiuzulu kwa kamati, Prof.
Safari akaichana barua
yake. Akaandika barua nyingine kwa Makamu-Zanzibar, makamu
akamuambia kuwa haya
mambo yamepangwa, asijisumbue!
Wanasema siasa ni mchezo mchafu, yeye anaaamini kuwa siasa
ni sayansi! Asubuhi
ya kesho akaandika barua, wasichojua ni kuwa kujiuzulu
hakuhitaji barua. Maneno
yakazuka kuwa Slaa hajaandika barua! Upotoshwaji ukaendelea
kuwa Slaa
atazungumza na waandishi wa habari, wengine wakasema
amefungiwa, amefungiwa na
mkewe na kadhalika! Ukweli ni kuwa alikuwa na Lissu, Gwajima
na Mbowe tangu
asubuhi.
Maamuzi aliyoyafanya yanatokana nadhamiri yake! Josephine
nae ni mwanaharakati,
ana sababu ya kuwa na uchungu. Alipigwa mwaka 2011 wakati
wengine walijificha!
Propaganda hizo tumeshazisoea!
Kama kuna mwenye ushahidi wa propaganda hizi aje, audited
report zipo!
Josephine halipwi na chama! Watu wanasema kuwa Slaa analipwa
mil. 7, yeye
ameendelea kula mihogo na maharage kama walivyoahidi mwaka
2010. Wana uchungu
na harakati!
Kikubwa katika harakati ni credibilty, jina la chama
kilichojengwa kwa muda
mrefu kisichafuliwe kwa namna yoyote! Mwanasiasa yoyote
hataki kuchaguliwa, na
Slaa nae hataki kuchaguliwa! Wanasema kuna maslahi mapana ya
taifa, ni nani
anayapima? Lazima kuwe na kipimo cha kuapima hayo maslahi
badala ya kutegemea
mtazamo wa mtu!
Anafafanua suala la liability sasa!
Wamekuwa waongo kwa kuwa hakuna kipengele hata kimoja cha
madai ya Slaa
kimetekelezwa. Alisema wabunge waje kabla ya kura ya maoni
ya CCM, kuja baada
ya hapo ni kutafuta kichaka cha kujificha!
Watanzania wameijenga Chadema kwa damu yao, rasilimali zao!
Watu hawawezi
kukimbilia kirahisi wakati sio wasafi, akiwemo Sumaye na
wengine. Nani hajua
kama Sumaye ni fisadi? Kwa muda mrefu Slaa haongei na Sumaye
kwa kuwa
alimtuhumu kwa ufisaidi.
Sumaye ni mtu ambaye wanahabari walidai kuwa Sumaye alisema
kuwa atahama chama
endapo Lowassa atateuliwa, leo akageuka!
Leo anamsafisha Lowaasa, dhambi haisafishwa kwa
dhambi. Anakumbusha jina
la Mr. Zero (jina la utani la Sumaye). Chama
kimepokea makapi, na katibu alitahadharisha kuwa chama
hakipokei makapi! Hakuna
ambaye alijitoa kwa hiari, wengi walikuja baada ya kukatwa.
Wenyeviti wengi ni
mzigo, akiwemo Msindai.
Anangoja ajibu amlipue hadharani kwa kuwa alikuwa mwenyekiti
wa kamati ya bunge
hesabu za serikali z mitaa. Siku aliyoambiwa aitishe kamati
kuu aliuliza
majina, akaambiwa anakuja chizi! Chizi ni nani, hata nyie
hamumjui! Anaitwa
chizi kwa kuwa ni mwizi wa kura ndani ya CCM.
Kuna haja gani ya kushindana kama tunampango wa kuiba kura
pia. Wakamtaja
Guninita, nani asiyemjua udhaifu wake? Hawezi kuandika hata
ukurasa mmoja wa
ripoti, amehama vyama mara kadhaa!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Viongozi wa Chadema wamepata kigugumizi, waseme nani
ameongeza thamani kwenye
chama? Najua maneno ya kuwa ni lazima kuiondoa CCM kwanza
hata ikibidi tuweke
mkataba na shetani, mimi ni padre wa Kanisa Katoliki!
Kuwaondoa CCM kwa namna
yoyote hakuleti maendeleo. CCM itaondolewa kwa program
siriaz, sio kutumia watu
wale wale!
Lazima tujue nini kilifanya Watanzania waamini chadema, kwa
kuwa waliamini wana
misingi isiyoyumba na uadilifu. Leo tunasimamia uadilifu?
Wanasema mwenye
ushahidi aende mahakamani. Kama tusingewatuhumu Mramba na
Yona wasingefikishwa
kizimbani. Chadema imefungwa mdomo kwa kisingizio cha
ushahidi!
Ni bora kukaa kimya kuliko kupotosha. Anasema nukuu ya
biblia kuhusu
wapotoshaji! Inapofika mahali unapoambiwa hakuna mwenye
dhambi ni makosa,
dhambi haisahihishwi kwa dhambi nyingine! CCM wamekuwa
waoga, wamewalea watu
hawa kwa muda mrefu!
Kwa Wafrika choo ni neno baya, kwa wazungu choo ni rest
room! Choo cha
Kitanzania huwezi kukihamisha ndani ya chumba cha kulala na
ukakiita choo,
huwezi kulala kwa kuwa kitanuka, tena zaidi! Ufisadi ilikuwa
ajenda iliyowapa
umaarufu CHADEMA, leo wamewachukua. Waanweza kuwa na ujasiri
wa kukemea
ufisadi?
Mwaka 2008 Slaa alikuwa bungeni wakati wa sakata la
Richmond, anafahamu kwa
uzuri anachokimaanisha. Bahati mbaya waandishi hawasomi
makaratasi, na wabunge
wa CCM pia.
Lowassa hatuhumiwi kwa habari ya Richmond pekee! Lowassa
aliambiwa na Slaa
aache kulalamika, atangaze uhalali au uharamu wa Richmond,
anamtaka aseme hao
'wakubwa' ni akina nani? Ni afadhali sifa yake
iharibike kuliko kusema uongo.
Ni aheri kupotea kwenye siasa za dunia kuliko kusimamia
uongo! Msingi wa kwanza
wa Richmond: Ili uelewe ni lazima urudi kwenye taarifa ya
Kamati ya Mwakyembe,
Slaa alifuatwa asubuhi ya siku ile kupewa rushwa, anashuru
Sitta na Mwakyembe
wajitokeze!
Akamuuliza mtoa rushwa kama anatoa m.500 kwa mbunge, atakuwa
nazo ngapi?
Aliwaambia Sumaye na Lowassa kuwa rushwa ni jambo
linaloanzia kifuani kwanza.
Mwanzo wa jambo hili ni taarifa ya Baraza la Mawaziri la
10.2.2006. Kamati ya
mwakyembe iliangalia faili la kikao kile kisha kuandika
ripoti!
Suala hili lilianzia wakati wa utawala wa mkapa kutokana na
dharura ya umeme
nchini, wakawasiliana na kampuni moja ya Amerika Kaskazini
kwa suluhu ya muda
mfupi ya umeme. Serikali ya Kikwete ikapokea lile suala.
Wakaruhusu mpango uendelee,
ila kwa kufuata sheria. Hiyo ilikuwa kauli ya Baraza la
Mawaziri!
Wakati auala lile linaamuliwa, Lowassa alikuwa Waziri Mkuu!
Na ndie mwenye
mandate ya maamuzi ya Serikali, iweje leo akane kuhusika?
Taarifa ya Mwakyembe
inapotoshwa! Taarifa ilitaka Waziri Mkuu ajipime, au bunge
limjadili na
kumchukulia hatua. Lowassa akakimbia kwa kuwa alijua Bunge
lingemfukuza kazi!
Waliioomba tenda walikuwa 26, waliorudisha walikuwa 8.
Kamati ya Tathmini
ikaona hakuna anayefaa hata mmoja! Waziri Msabaha akaagiza
taarifa ile ifutwe
na tathmini ifanyike upya, mara ya kwanza, ya pili, ya tatu
na ya nne. Jeuri wa
Msabaha ilitoka wapi? Baraza likaamua baadaye tenda
iliyopewa kwa kampuni ya
kwanza ifutwe! Lowassa alishiriki!
TANESCO wakatoa ushauriwa wao, Mamlaka husika ikatafute
internatonal tender ya
kununua turbine! Lowassa akaingilia mchakato dakika za
mwisho, akamuagiza
katibu muhtasi wake!
Kwanini Lowassa, kwa kuwa anagombea urais, rais asiyeaminika
hawezi
kuchaguliwa!
Lowassa alishawahi kumuita Slaa kuhusu habari ya Meremeta,
na kumuambia kuwa
taarifa yake inaiaibisha Serikali! Kampuni ya jeshi imewahi
kutengeneza gari,
imehujumiwa na wahuni. Akamtaka Lowassa amuambie ni nani
aliyehusika?
Akamuita mwingine kwnye Speaker lounge. Slaa akamuambia kuwa
yeye ni fisadi
kichwani, rohoni mpaka...!
Tunamsifia Lowassa kuwa an=taleta maji wakti jimbo la
Lowassa halina maji na
ufisadi mkubwa umefanyika kwneye jimbo hilo. Mnazungumzia
shule za kata wakati
wakati hamjua zimeanza wapi? Slaa anataja nafasi alizowahi
kushika Afrika.
Uamuzi wa kujenga shule za kata ulifikiwa mwaka 90 huko
Thailand, mpango huo
ukaitwa Education for All, sio MMES kama unavyoitwa leo!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Anasoma barua ya Ibrahim Msabaha kwa Flugence Kazaura,
mkurugenzi wa bodi wa
TANESCO!
Mpango ulikuwa kuondoa suala la umeme mikononi mwa tanesko
kwa kuwa imeshindwa
kutekeleza. Ugomvi wake na Masha ni kwa kuwa Lowassa
alimlaumu Masha kuingilia
mchakato wa serikali, akawekewa kinasa sauti chumbani.
Waziri Mkuu haruhusiwi
na sheria kuingilia mchakato wowote wa tenda.
Kwenye kampuni nane zilizowasilisha maombi ya zabuni,
Richmond ni kampuni
iliyokuwa mbovu. Ilikuwa ni kampuni ya steshenari, sio
umeme!Wakadai wana
ushirikiano na kampuni nyingine ya umeme, kampuni hiyo
ikakataa kujihusisha na
Richmond, wala kuzalisha na majenereta!
Bill Clinton aliwai kukutwa na kashfa, walitaka kumchukulia
hatua si kwa sababu
ya zinaa, bali kwa kuwa alifanya uongo! Kwa kuwa alidanganya
umma! Hata sheria
za Tanzania zinakataza kuongopa, hata kesi za uchaguzi za
Slaa zimethibitisha
hilo.
Lowassa anadai yeye alisimamisha tenda, Slaa anaonesha
uthibitisho wa hilo kwa
barua za Lowassa kwenda kwa Msabaha zinazokanusha hilo,
'Anaisoma'! Waziri Mkuu
aliharakisha mchakato wa tenda, tofauti na sheria ya PPRA.
Barua imeandikwa
miezi mitatu baada ya mkataba kusainiwa, kwa maagizo ya
Waziri Mkuu.
Tanesko ikaagizwa kusaini mkataba ambao haikuhusika kwenye
kuujadili! Anaona
aishie hapo... Anaupigia chapuo mdahalo wa Sitta na
Mwakyembe, anasema Lowaasa
nae afike kuondoa utata na kusema ukweli!
Chadema ni chama kilichotoa matumaini kwa vijana wengi!
Isifike mahali tukawa
washabiki kama 2005 ambapo watu waliahidiwa maisha bora,
wakajikaanga kutokana
na ushabiki! Anatoa ushahidi wa kitakwimu wa mfumuko wa
bei...
Slaa ana uchungu kuona chama alichokijenga, kikifikia hatua
ya kusomba watu kwa
mabasi na malori kisha mkasema mafuriko hayazuiliki! Hayuko
tayari,... Anakataa
kuwa ZEZETA! Ajenda ya Chadema ni nini, ilikuwa ni rushwa!
Wananchi waliamini
kwa kuwa msingi huo ndio unakijenga chama!
Sehemu kubwa ya kilichosemwa Jangwani ni ilani ambayo
ilishaandaliwa tayari,
hakuna kipya kilichosemwa. Kinachomuuma ni chama makini kuwa
kibovu zaidi ya
Chama cha Mapinduzi! Hatuwezi kujenga maadili tukiwa na watu
wachafu, anaishi
na mwanamke bila kufunga ndoa kwa kuwa Serikali ya CCM
haitaki afunge ndoa.
Kesi yake ililetwa na mawaziri, waandishi wa habari na mtu
kutoka IKULU. Ndoa
inafungwa na Mungu!
Scotland Yard iliamrisha Lowassa achunguzwe, inakuwaje leo
tunamtetea? Huu ni
ushabiki usio na vielelezo, Slaa ana ushahidi! Hakuna
ulazima wa kwenda
mahakamani kwa kuwa kesi ya rushwa ni jinai, ni kesi ya
serikali! Slaa au
mwingine hana locus ya kwenda mahakamani kwa kesi ya jinai!
Mwakyembe alisema
kesi ya jinai haina mwisho (kama zilizyo za madai). chadema
iliahidi kusafisha
nchi kwanza endapo itashika dola, huku maendeleo
yakiendelea!
Anasoma barua ya mchakato wa Richmond kuwa DOWANS. Kampuni
imesajiliwa Costa
Rica, na mwenyekiti asiye na anuani, simu wala jengo! Siku
iliyosajiliwa,
mmiliki alisajili makampuni mengine 99! Zaidi ya hayo ana
makampuni mengine
zaidi ya 50, DOWANS ni jina tu. Kampuni haipo! Dowans sio
kampuni halisi huko
Kosta Rika, nchi nzima hakuna kampuni yenye uwezo wa
kuzalisha umeme kwa
kiwango hicho!
Leo Lowaassa anatuambia tufunge mdomo, huu ni udikteta!
Anakumbusha sakata lake
na Waziri Marmo... Mabilioni ya fedha yanalipwa kwa kampuni
ambayo haipo!
Tunapenda ushabiki... Acha sifa iharibike!
Anasema hataki kuingia kwenye mambo ya Babu Seya! Vyuo vikuu
vinatumia kesi ya
Babu Seya kama case study. Mtoto mdogo hawezi kutoa ushahidi
mahakamani, haki
inapuuzwa kwa kuwa mtoto hawezi kutoa ushahidi!
Kesi ya Ulawiti rais hana mamlaka nayo, anatoa wapi kiburi
cha kusema kuwa
atamtoa? Aliyeagiza polisi kuingia na polisi kuingia na mbwa
msikiti wa
mwembechai ni Sumaye, akiwa waziri mkubwa. Leo hii ni mpiga
kampeni wa Lowassa!
Leo tunataka kura kwa namna yoyote! Ni afadhali kutokuwa na
rais wa aina ya mtu
huyu! anayesaka kura kwa kusaka huruma za watu. Slaa hayuko
tayari kuona hilo
linatokea... Anahitimisha kwa kusema hajagusa chochote
kuhusu ilani wala
mkakati!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Kama taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua vitu nje ya
shamrashamra, maneno
matamu! Tumeshaumwa na nyoka, tusilaghaiwe na maneno ya watu
hawa tena! Utendaji
uliotukuka unapimwa kwa utafiti, sio kwa ukasuku na kunukuu
maneno ya
wanasiasa!
Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu, matatizo ya wakulima na
wafugaji yalikuwepo,
alifanya nini? Lowassa aliwahi kubadili mpaka wa Monduli na
Karatu na
kusababisha mgogoro! Mkampenia wake, Sumaye alisababisha
matatizo ya ardhi
Mvomero, akipora ardhi ambayo ilitakiwa yajengwe makao makuu
ya Mvomero!
Mengine ya Sumaye ameyaweka kiporo, hisa zake za kampuni
aziweke wazi kama
Sekretarieti ya Maadili inavyotaka!
Kutotangaza mali kunatosha kumtoa mtu ubunge! Sembuse
Urais?
============================== =========================
Ukweli huwa una tabia ya kuegemea upande, anasemea
speculation kuwa ameisema
chadema peke yake. Anasema amestaafu siasa, hana chama
lakini bado anabaki kuwa
mtanzania, mtetezi wa wanyonge na atabaki hivyo! Ataendelea
kuwatumikia
watanzania kadiri ya Mungu alivyomjalia vipawa! Kama
alivyoombwa kugombea urais
2010!
Anaweza kuwatumikia Watanzania bila kuwa na chama!
Anasema kuwa hajapata vitisho kama alivyopata kipindi hiki,
inazidi hata wakati
alipotangaza List of Shame. Rostam ndiye anafadhili kampeni
za urais wa
Lowassa! Anamnukuu vitisho vyake! anakiri kuwa maaskofu
wamehongwa, Rostam
akiwa anaona, m60-m300! Anasema hatenda chama chochote,
anasisitiza! Amejitoa
rasmi siasa za vyama vya siasa... Ataendelea kuwa msimamiaji
wa anachokiamini!
Anawataka watu aliowataja watoke hadharani, anatoa baraka za
KIMUNGU kwa nchi
na watu wake!
MASWALI!
Swali: Unawammbia nini Watanzania kuelekea uchaguzi, ni rais
yupi anafaa?
Amesema hana chama, hampigii kampeni mtu yoyote! Amesema
anafanya uchambuzi wa
madhara ambayo taifa litapata endapo watamchagua Lowassa, na
kwa kuwa na uzoefu
nao kwa muda mrefu!
Hataki kufanya kampeni yoyote. Anawaelimisha Watanzania
kuacha ushabiki
utakaowagharimu! Ni watu wachache wanoweza kumtaja mtu kwa
majina, kuna tofauti
ya wanaotaja ajenda tu na wanaotaja majina.
Rostam alimuambia kuwa ana dakika 5 za kuishi, apige magoti
na kusali! Aliweka
roho yake rehani kwa ustawi wa taifa hili...Anakumbusha ya
Mwembeyanga na namna
Usalama wa Taifa walivyokuwa na tension. Magazeti mengi
yaliogopa hata kuandika
habari, isipokuwa MWanaHalisi!
Swali: Siasa ingekuwa asset kama angekuja na wabunge kadhaa.
Angekuja kama asset,
mengine yangesafishika? Kulikuwa na vigezo viwili, ama asset
na liability,
yaani hayo madhambi yote aliyoyasema. Baada ya hayo
wangefanya tathmini kama
anapokelewa au hapokelewi. Anatoa mfano wa Shirikisho la
Afrika Mashariki na
nchi zinazotaka kujiunga!
Swali: Waliopokelewa ni makapi. Je wewe ulikuwa kapi 95?
Anauliza kama watu wanaamini yeye alikuwa kapi? Tupime
vigezo... Makapi ni watu
waliokataliwa na watu wao baada ya kuwa wabunge kwa muda
mrefu. CCM wakasema
kuwa hakuwa mwenzao: hakuwa anahonga, hakuwa anapokea rushwa
na kadhalika! Kuingia
kwa tiketi ya Chadema ulikuwa ukombozi kwake!
Swali: Umetangaza kustaafu siasa, una kadi za vyama viwili.
Unazirudisha au
unakaa nazo?
Watanzania tuelimika, kadi sio uanachama. Kadi ni mali ya
mwanachama, unaweza
kuichoma, kuweka kumbukumbu au vyovyote, sawa na kadi ya
ndoa ambayo
hairudishwi hata kama ndoa itavunjika. Tuulize maswali ya
kujenga.
Swali: Anaoneka baada ya kukosa urais anamshambulia
Lowassa!
Wapi Slaa alichukua fomu ya Urais, hakuwa na nia na urais
wala hawezi
kukasirika. Tuache ushabiki, tuwe na mtiririko na kuzingatia
hoja! Mwandishi
awe msikivu sana... Ameeleza tangu mwanzo, hana chuki wala
ugomvi na mtu
yoyote!
Chama cha Mapinduzi kilishakuja kumpa ofa kadhaa kuachia
jimbo la Karatu, akaweka
sharti la mkataba wenye sahihi za watu watatu; Rais, Slaa na
Yesu Kristo.
Swali: Kama wewe uliweza kuhama, wengine nao hawawezi?
Dr. Slaa hakuwa na uchafu wowote, tatizo halikuwa kuhama
chama, tatizo ni watu
wa aina gani wanahama chama?
Swali: Unahamasisha uwazi, mbona wewe umemficha muovu mmoja?
Silaha haziwekwi zote mezani, amewaomba anaowatuhumu
wajitokeze!
CHANZO kwa hisani
ya jf
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment