Friday, 1 August 2014

[wanabidii] ´La Constitutional Fatigue`- Je, Watanzania Wamechoshwa Na Mchakato Wa Katiba?



Ndugu zangu,

Mchakato wa Katiba ni mchakato wa kidemokrasia. Hivyo, ingesemwa pia ' La Democracy Fatigue' - Kuchoshwa kidemokrasia.

Ninavyoifuatilia mijadala ya kijamii, na ninayoyasikia mitaani kuhusiana na mchakato unaoendelea wa Katiba, naziona dalili za Watanzania kuonyesha, japo kwa wakati huu, kuwa wamechoshwa na mchakato wenyewe. 

Kwamba wanachotamani sasa ni mchakato wenyewe usitishwe, ili nao wapumzike na fedha za walipa kodi zisizidi kupotea. Labda ni mimi naona tofauti, ndio maana ya kuchokoza mjadala huu.

Ndio, kuna dalili kuwa Watanzania hawaoni mantiki ya Bunge hilo Maalum la Katiba liendelee katika mazingira ya sasa ya kulumbana na kushindana kwa wajumbe kupigania maslahi ya makundi yao. Watanzania wanaona ni heri jambo hilo la Katiba likasubiri baadae.

Watanzania hawataki shari pia, na wameshaziona dalili za wanasiasa kuwaingiza kwenye shari kwa kupitia migongo ya wananchi. Kuna dalili za wanasiasa kuanza kuwagawa Watanzania. Na wahenga walisema; Heri nusu shari. 

Huenda Awamu ya Kwanza ya Bunge la Katiba ilishakuwa nusu shari. Na kama sasa Wajumbe hao wa Bunge la Katiba hawayatamaliza kwanza kwa kuongea na kushikana mikono kama WaTanzania na wamoja katika kupigania Katiba yenye maslahi ya Watanzania, basi, ni heri wasikate tiketi za kwenda huko Dodoma.

Watuache na Katiba yetu ya sasa, isipokuwa ifanyiwe marekebisho muhimu yenye kuhitajika katika kutuvusha kwenye wimbi hili. Tufanye hivyo, ili kwa amani na utulivu, wananchi washiriki uchaguzi muhimu kwao. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Na mwakani ifikapo Oktoba twende kwenye Uchaguzi Mkuu.

Lakini kwa hali inavyoonekana sasa, yumkini Watanzania wanaonekana' Kuchoshwa Kikatiba'- Au?

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment