Friday, 1 August 2014

Re: [wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?

Wanaosema wakurya wengi jeshini mtupatie idadi yao, binafsi kikosi nilichokuwepo wakurya walikuwa wawili meja chacha na mp koplo marwa, pia kutopewa nafasi za juu inawezekana kutokuwa na elimu, jeshini hupandi cheo kwa kulenga shabaha tu ni pamoja na kuhudhuria mafunzo mbalimbali.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, July 31, 2014 11:05:20 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?



NA MOBHARE MATINYI

Naomba niwapatie ukweli ninaoujua kwa kutafiti na kufuatilia kuhusu uwepo
wa Wakurya wengi jeshini na madai kwamba Nyerere aliwapeleka jeshini - si
kwa kuwa mimi ni mkurya! La hasha!
Kwanza niseme hivi, ni kweli kwamba Wakurya ni wengi sana jeshini
kulinganisha na makabila mengine ya Tanzania ingawa katika miaka ya
karibuni wamekuwawakipungua kutokana na sababu nyingi ambazo hapa si
mjadala wake.

NANI ALIWAINGIZA JESHINI
1. Wakurya waliingizwa jeshini kwa mara ya kwanza na Waingereza wakati wa
kuandaa jeshi la kikoloni ambapo ilipotokea vita ya pili ya dunia,
Waingereza walikwenda vijijini kwa Wakurya na kuwakamata amakuwahamasisha
vijana wao waingie jeshini ili kwenda kupigana. Baadhi yao waliporejea,
akiwemo Marehemu babu yangu mzaa mama na baba yangu mkubwa, walikataa
kuingia jeshini wakisema wana mali nyingi na wakaenda kuangalia ng'ombe
zao. Hawawalipigania nchini Burma huko Asia. Utamaduni huu wakuingia
jeshini ukaanzia hapo na kuendelea.

2. Kwa nini Waingereza waliwachukua Wakurya wengi kwenda jeshini? Ni kwa
sababu ya dhana kwamba makabila ya Waafrika yana vipaji tofauti na kwamba
ili kuwatawala Waafrika kwa urahisi, inabidi kuvitumia vipaji hivyo.
Mfano,Waingereza walisema kwamba ukitaka madaktari wengi watiifu na wapole
wachukue Wasukuma kwa sababu ya upole wao na utiifu na kweli tunao wengi
sana. Waingereza wakasema tena, wafanyakazi wazuri wa ndani ni Wanyasa -
kweli, wafanyakazi wa ndani wa balozi na maofisa ubalozi wa Uingereza hata
sasa hivi ni Wanyasa kwa sababu ya uaminifu wao. Walisema pia kwenye elimu
weka Wachaga na Wahaya na ni kweli hadi leo waliobobea shuleni zaidi nchini
na nani? Tunajua wote! Wakasema, kule Kenya, ukitaka wasomi chukua Wajaluo
na Uganda wakasema ukitaka wasomi chukua Waganda. Kwenye uaskari walisema
kwamba kwa Uganda chukua Walango, Waacholi na ikibidi sana Wakakwa (kabila
la Idi Amin). Nchini Kenya walisemakwamba kwa askari bora uchukue Wakamba.
Kwa Tanganyika wakasema chukua Wakurya na ongeza Wangoni na Wahehe.
Wakaongeza zaidi na zaidi kwenye mpangilio wao. Ipo orodha ndefu.
Waingereza walifanya utafiti mzuri na walipoondoka walimwachia kila
kiongozi wa Afrika (makolonini) matokeo ya utafiti wao ingawa akina Nyerere
hawakuzifuata.

MATOKEO YA SERA YA WAINGEREZA
3. Nini matokeo ya mpangilio huu wa Waingereza? Kule Uganda karibu
wanajeshi wote wakati Amin anaichukua nchi (walikuwa 8,000 hivi), walikuwa
Walango, Waacholi na Wakakwa lakini kwa kuhofia kupinduliwa akaanza
kuwauaWaacholi na Walango na kuwajaza Wakakwa na baadaye akawaweka mpaka
Wazaire na Wanubi wa Sudankusini na kaskazini mwa Uganda. Kule Kenya hadi
kesho, majeshi ya Kenya yamejaa Wakamba na kwa mnaofuatilia mtamkumbuka
Jenerali Muringe. Kwa kuwa Wakikuyu wamekuwa wakishika dola, Wakamba
waliminywa kwenye vyeo vya chini lakini wamejaa majeshini Kenya kupita
kiasi, hasa kutokana na umaskini wa nchi yao ya Ukambani ambayo ni kame pia.

NYERERE KUUNDA JWTZ 1964
4. Kwa Tanganyika Wakurya walijaa jeshini mno wakati tunapata uhuru kiasi
kwambaNyerere akasema hili ni tatizo.Alipovunja Kings African Rifles na
kuunda JWTZ baada ya maasi ya 1964, Nyerere aliamua kuweka sera kimya kimya
kwamba jeshi hili litakuwa na watu wa makabila yote. Ilikuwa kazi ngumu
kwake kwa kuwa waliokuwa wanakuja kujiandikisha kwa wingi walikuwa ni
Wakurya zaidi kutokana na utamaduni wa kawaida wa Wakurya wa kupenda
kupigana, vita, ukakamavu, umwamba, n.k. Wakurya, kama Wakamba, Waacholi,
Walango, na Wakakwa waliitwa na Waingereza "Marshal Tribes" -yaani makabila
ya wapiganaji. Hata hivyo, Nyerere alifanikiwa kuwapunguza mno lakini bado
alibakia nao wengi kutokana na utamaduni, historia na ukweli wa
mambo,kwamba ukitaka askari mzuri chukua anayependa vita, siyo mtu mwoga.
Kama si Nyerere, jeshi lingekuwa wakurya watupu, siyo wakurya wengi, bali
wao wenyewe kwa hata 90%.

WAKURYA NA NYERERE
5. Wakurya hawakuwa na urafiki wowote na Nyerere kama watu wanavyodhani
kutokana na fikra za Kiafrika kwamba kila kitu kina nguvu za siri nyuma
yake, iwe baraka za Mungu, rushwa, udini, mapenzi, ukabila, uchawi, fitna,
mkosi, n.k. Mwafrika haamini kwamba kitu kinaweza kutokea kwa sababu zake
chenyewe bali mpaka kuwe na mtu mwingine anayekifanya kitokee. Kati ya watu
waliotaka kumpindua Nyererekwenye miaka ya 1960 mwishoni, kwa mnaofuatilia,
walikuwepo akina Chacha (nahifadhi jina lake kamili), na kutokana na tabia
ya Wakurya kumtukana Nyerere alipokwenda ziarani Tarime, aliamua kuacha
kufanya ziara huko. Si hivyo tu, Nyerere alikwepa hata kuwapa nafasi za juu
Wakurya na mkurya pekee aliyewahi kushika uwaziri katika miaka 25 ya
Nyerere ni Bhoke Munanka ambaye walikorofishana hata hivyo (waziri pekee
aliyemwambia kwamba huu ujamaa wako utaumiza watu na hakuna anayeutaka).
Kamamjuavyo, Munanka alikuwa mfanyabiashara mkubwa katikati ya ujamaa.

6. Aidha, Rais Nyerere hakuwahi kumteua mkurya kuwa mkuu wa majeshi wala
msaidizi wala chochote cha juu ingawa ukiongea na watuwanakwambia mambo
mengine kabisa. Mkuu wa kwanza wa JWTZ alikuwa Sarakikya kutoka Meru; akaja
Twalipo kutoka Songea; akajaMusuguli kutoka Bunda (si mkurya). Rais Mwinyi
ndiye aliyekuwa wa kwanza kumteua mkurya kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali
Kyaro, na baadaye Mkapa akamteua Jenerali Waitara. Hata kwenyeVita ya
Uganda, Nyerere hakumpa mkurya kuongoza vita ile ingawa kwenye makamanda wa
chini Wakurya walijazana kama utitiri, achilia mbali askari wa kawaida. Ni
Mwita Marwa pekee ndiye aliyekuwa kwenye makamanda wa kuongoza brigedia,
lakini wengine wote walibanwa pembeni........Nyerere hakutaka taabu baadaye.

WAKURYA KUPENDA VITA/JESHI
7. Kwa wenye kumbukumbu na wanaofuatilia, tulipovamiwa na Amin Oktoba 31,
1978, na baadaye Nyerere kutangaza vita, serikali ilitoa mwito kwa wananchi
kujiunga na mgambo/jeshi kwa hiari. Nafasi zilikuwa 2,000 kwa kilamkoa.
Wakurya walilaani kitendo hicho cha kuweka ukomo wa idadi na wakatuma
wajumbe kwenda kulalamika kwa Nyerere kwamba idadi ya 2,000 ni ndogo mno
kwa mkoa wa mashujaa. Nyerere akasema hawezi kuondoa ukomo huo. Wakatuma
tena ujumbe wa pili, na Nyerere akashauriwa na makamanda wake kwamba kwa
kuwa mikoa mingine imeshindwa hata kufikisha 500 tu, basi ni heri Wakurya
waachiwe waje tu. Nyerere akasema kwamba basi anaruhusu nafasi 4,000 kwa
mkoa wa Mara. Hii imeandikwa kwenye vitabu na waandishi wasiokuwa
Watanzania.

8. Wazee wa mkoa wa Mara walikerwa mno na uamuzi waNyerere wa kuweka ukomo
mwingine wa 4,000 na wakaamua kwamba dawa ni rahisi sana, kwamba vijana wao
waende kwenye mikoa ambayo ilikuwa imeshindwa kufikisha idadi ya 2,000 ya
awali. Huu si utani. Kaka yangu alikwenda Morogoro. Baba yangu mkubwa
alikwenda Moshi na ndugu yangu mwingine alikwenda Usukumani na wote
wakaenda vitani na wakarejea kwa ushindi na furaha. Wote wapo hai hadi leo
na kaka yangu huyu aliingia Magereza baadaye. Kwa kifupi, Nyerere aliwabana
Wakurya wasiendevitani kwa wingi kama walivyotaka. Mjomba wangu Nyaronyo
Kicheere alipata medani ya vita pia kwa kujitolea kwenda vitani akitokea
JKT - yumo humu ukumbini muulizeni.

KWA NINI WAKIMBILIE JESHINI
9. Mimi binafsi, wakati ninamaliza kidato cha sita na huku nikiwa
nimefaulu, uamuzi wangu ulikuwa kwenda JWTZ kwanza na mambo mengine yafuate
baadaye. Kama si wazee wangu kunikatalia, leo hii ningekuwa kwenye
magwanda. Naomba Kivuyo na LKK mniambie, mimi niliyezaliwa mjini, nikakulia
Dar es Salaam, simjui Nyerere wala hanijui, ninahusika vipi na Nyerere
wakati aliacha urais nikiwa sijafika miaka 18? Nyerere ametoka kwenye urais
mwaka 1985 lakini miaka 27 baadaye bado Wakurya wamejaa jeshini ingawa
wananyanyaswa kutokana na maneno ya kipuuzi kama haya, je, Nyerere
anahusika vipi na kuwepo kwao? Mkurya wa miaka 20 leo, aliyeko jeshini,
anahusika vipi na Nyerere? Kwa ufupi ni hivi ........... Wakurya
tunalipenda jeshi, basi! Nenda hata Kenya utawakuta jeshini, mpaka hapa
Marekani wamo jeshini. Je, Nyerere aliitawala Kenya na Marekani?

10. Pili, kutokana na maendeleo kuwa nyuma sana mkoani Mara, sehemu pekee
ya ajira ilikuwa jeshini kwa miaka mingi hadi walipoanza kuchimba dhahabu
kwa wingi kule Nyamongo, na kuuza ng'ombe kwa magendo nchini Kenya. Wilaya
ya Tarime, wakati ule wa Nyerere, ilikuwa kama sehemu ya Kenya kwani
magharibi ilizibwa na Ziwa Viktoria, kusini na mbuga ya Serengeti, na kuja
Mwanza kulikuwa na mto usiokuwa nadaraja (Mwinyi alilijenga baadaye), kule
mashariki na kaskazini ilikuwa nchi ya Kenya. Nyerere hakutaka hatakufanya
ziara tu, achilia mbalikujenga walau shule moja. Hivyo, jeshi likawa kama
kimbilio la ajira lakini hii ikiwa ni baada ya kuangalia kwanza hulka na
silka ya Wakurya kwenye masuala ya kupigana/jeshi/ushujaa, n.k.

Ndugu zanguni Kivuyo na LKK, siwalaumu kwa kudhani hivyo kwa kuwa haya
maneno yako hivyo lakini kama nilivyosema, ndivyo Waafrika tulivyo.
Ushahidi uliopo ni kwamba Nyerere hakuelewana na Wakurya hata mara moja na
aliwabana wasiingie jeshini lakini akafika mahali akashindwa. Ushahidi ni
wa kutosha na mkitaka nitawapa kwenye barua pepe zenu binafsi kwa kuwa hapa
si vema kuyataja majina ya watu bila vibali vyao.

Wakurya tuna vitu vitano tunavyovipenda sana: Kupigana, familia, ng'ombe,
ukweli na utaifa. Ni fahari kubwa kwa mkurya kuingia jeshini, fahari kubwa
mno; wanangu madume wote wawili, mmoja miaka 9 na mwingine 6, wako hapa
Marekani lakini wanapenda kuvaa nguo za jeshi na kucheza na matoi ya
vifaru, ndege za jeshi, n.k.
Jeshi liko damuni kwa Wakurya!

CHANZO: MOBHARE MATINYI, na MHADHIRI MWANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES
SALAAM

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment