Mi najua kwa nini tume ya Warioba iliamua kuja na serikali tatu...na hilo haliepukiki kwani haiwezekani hata kidogo kuendelea na wazo la serikali mbili kwa nchi mbili kinyume na malengo ya serikali mbili kwa nchi moja ya waaasisi wake. Na wao lengo lao kuu lilikuwa ni kuelekea kwenye nchi moja na serikali moja. Cha msingi wana CCM wangeachana na wazo la kuwa na serikali mbili ambalo litaimega na kuigawa nchi, bali mipango ingeelekezwa katika kuwa na nchi mbili na serikali tatu,lakini mambo ya muungano yaongezeke na nyufa zote zinazozaniwa zaweza ama kuleta magaidi visiwani zizibwe iwe kwa democrasia au udicteta. Wakuu wa nchi husika wasiwe na madaraka makubwa na pia madaraka makubwa ipewe serikali ya muungano ambayo ndio itakuwa na mustakabali wa nguvu.kwa watu wa mataifa haya mawili.
NOTE: Huwezi ukasikiliza kila inayoitwa kero kwa mzanzibar na ukaendelea kuwa na Tanzania. Hata katika vitabu vya dini hakunaga kitu kinaitwa democrasia ya wajinga. Sometimes songa mbele kimtindomtindo,others will understand you later. Kufumbiwa macho kwa wanzanzibar walipokuwa wanachakachua katiba ya muungano ndiko kunakoleta shida hizi za leo na taifa linaingia gharama kubwa.NGupula
--------------------------------------------
On Fri, 1/8/14, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA UKAWA KUHUSU WITO WA VIONGOZI WA DINI WA KURUDI BUNGENI.
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 1 August, 2014, 13:07
Kumbe watu, including
wengi wa wajumbe wa bunge maalum la katiba, hawajui bunge
hilo linapaswa lifanye nini! Lengo ni kuboresha na siyo
kuendelea kukosoa kama kuna mapungufu. Mijadala ya bunge
maalum la katiba lina lengo hilo. Mfano, kwenye serikali 3
wajumbe wangejikita kutafuta ni njia zipi zingeweza
kuboresha muungano ndani ya serikali 3. Pili kuwa na
serikali tatu hakuna maana ya kuwa na marais watatu. Je, ni
kweli kwamba nchi zenye serikali ya shirikisho kama US wana
marais wengi pia kama anavyodhani Ndaki? Shida yetu kubwa ni
kama mtu anayeonyesha mwezi kwa kidole - akimaanisha kuwa
ukifuatisha kidole chake utaona mwezi na badala ya kufanya
hivyo anayeonyeshwa mwezi anadhani uko kwenye kidole na
anabaki kuangalia hicho kidole akidhani ndiyo mwezi!
2014-08-01 12:57
GMT+03:00 Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>:
Sa haya unayosema Ndaki, ndiyo yanapaswa
kujadiliwa kwa hoja bila matusi au kejeli ili wananchi
watakaokuja kupiga kura ya maoni baadaye, wawe wamefuatilia
hoja. Sasa haya hayakujadiliwa. Yametupwa na kubaki zomea
zomea, matusi na taarabu! Mimi naona ndiyo shida hii.
> Date: Fri, 1 Aug 2014 09:47:41 +0000
> Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA UKAWA KUHUSU WITO WA
VIONGOZI WA DINI WA KURUDI BUNGENI.
> From: hosea.ndaki@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Edgar, ukisoma randama ya warioba ndo utaona mapungufu
ya tume, alicheleta ni muswada na sio maoni ya wananchi,
tusifanye haraka tujiridhishe kwanza na tufikie mwafaka,
huwezi kuwa na marais watatu katika nchi moja mkabaki
salama, amezungumzia mashirikisho kama brazil na marekani
lakini hakusema hizo nji zina marais wangapi? Randama haina
takwimu hata moja japo kila aya anasema kutokana na maoni ya
wananchi, wangapi? Wapi? Hajasema.
>
> Kwa katiba ya zanzibar rais wa zanzibar ni rais mwenye
mamlaka kamili japo hana jeshi na hana mpango wa kubadili
nia, je huyu wa tanganyika nae atakuwa kama wa zanzibar au?
>
> Tuweke kando uccm na ukawa tuangalie uhalisia.
> ----------
> Sent from my Nokia phone
>
> ------Original message------
> From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
> To: "Wanabidii Mawazo" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Friday, August 1, 2014 8:50:14 AM GMT+0000
> Subject: RE: [wanabidii] TAMKO LA UKAWA KUHUSU WITO WA
VIONGOZI WA DINI WA KURUDI BUNGENI.
>
> "Yeyote anayedharau hitaji la Katiba Mpya, ama
anayejaribu kupuuza na kuweka kando Rasimu II, huyo sio
mwakilishi wa utashi wa watu. Mwisho wake historia
itamhukumu vikali mtu huyo". (Maaskofu Katoliki
Tanzania, 27.06.2014)
>
> Date: Thu, 31 Jul 2014 22:40:14 -0700
> From: hamisznz@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: [wanabidii] TAMKO LA UKAWA KUHUSU WITO WA
VIONGOZI WA DINI WA KURUDI BUNGENI.
>
> TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI,DAR ES SALAAM, ALHAMISI,
31 JULAI 2014 SAA 5.00 ASUBUHI.Ndugu waandishi wa
habari,Kama mnavyofahamu Wajumbe wa Bunge
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment