Wednesday, 2 July 2014

[wanabidii] RAIS KIKWETE ASIFIA UHUSIANO MZURI KATI YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesifia uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini akisema kuwa uhusiano huo haujapata kuwa mzuri zaidi ya ulivyo sasa.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Afrika Kusini kuendelea kuonyesha uongozi katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa sababu kwa kufanya hivyo Afrika Kusini itakuwa inatimiza jukumu lake la kihistoria.

Rais Kikwete alikuwa akizungumza mwishoni mwa wiki mjini Dar es Salaam wakati anaagana na Balozi wa Afrika Kusini katika Tanzania Mheshimiwa Thanduyise Henry Chiliza ambaye amemaliza muda wake wa utumishi nchini.

Rais Kikwete alimwambia Balozi huyo kuwa ni nchi chache dunia kwa sasa ambazo zina uhusiano wa karibu zaidi na Tanzania kuliko Afrika Kusini. "Tumekuwa washirika wa karibu sana katika uhusiano wa kikanda na uhusiano wa kimataifa. Uhusiano wetu haujapata kuwa wa karibu zaidi ya sasa katika historia. Tunakushukuru Mheshimiwa Balozi kwa mchango wako katika kuimarisha uhusiano wetu kiasi hicho."

Rais Kikwete pia amesifia mchango wa Afrika Kusini katika utulivu ulioko katika eneo la Kusini kwa Afrika akisema kuwa anatambua mchango na uongozi wa nchi hiyo katika hali hiyo.

"Tunatambua uongozi wa Afrika Kusini katika eneo letu la Afrika. Ni jukumu la kihistoria la nchi hiyo ambalo Afrika Kusini lazima iendelee kulitimiza kwa kiwango kinachotarajiwa na sisi wote."

Naye Balozi Chiliza amemshukuru Rais Kikwete kwa kumuunga mkono wakati wa uwakilishai wake na hivyo kumsaidia kutimiza majukumu yake ya kibalozi. "Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais kwa ushauri na maelekezo yako ya kiuongozi wakati wa utumishi wangu katika Tanzania. Bila kunisaidia pengine kazi yangu ingekuwa ngumu zaidi."

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
2 Julai, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment