Mpango wa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha mikoa ya Arusha na Mara utaendelea kama ilivyotangazwa na Serikali isipokuwa katika eneo la kilometa 53 lililoko katika Hifadhi ya Serengeti.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Deusdedit Kakoko alipokuwa akizungumzia hukumu ya Mahakama ya Afrika ya Mashariki iliyozuia ujenzi wa barabara hiyo. "Serikali imekwishatangaza kuwa kipande cha barabara ambacho kinapita Hifadhi ya Serengeti chenye urefu ya kilomita 53 hakitajengwa kwa lami, hivyo naamini ujenzi wa maeneo mengine hautakuwa umeingilia uamuzi wa mahakama hiyo," alisema Kakoko.
Alisema kama Serikali ilivyoahidi, barabara hiyo itajengwa kwa Mkoa wa Arusha, kutoka Kigongoni wilayani Monduli hadi Loliondo, Makao Makuu ya Wilaya ya Ngorongoro hadi geti la Crence na baada ya hapo kutakuwa na barabara ya changarawe katika eneo la hifadhi hadi lami itakapoanza tena eneo la Mugumu, Serengeti.
Hivi karibuni, Mahakama ya Afrika Mashariki ilitoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Mtandao wa Kutetea Haki za Wanyama (ANAW), ukipinga ujenzi huo kwa madai kuwa utakuwa na athari za kimazingira, hivyo kuzua sintofahamu.
Hukumu hiyo ilitolewa na majaji watatu wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki, Jean-Bosco Butasi, Isaac Lenaola na John Mkwawa katika kesi namba 9/2010.
Hatua hiyo iliisukuma jumuiya ya wasomi wa Wilaya ya Ngorongoro kuipinga hukumu hiyo na kuweka wazi msimamo wake wa kuungana na Serikali kutaka kujengwa kwa barabara hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Onesmo Ole Ngurumwa alisema barabara hiyo ina umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Loliondo ambao wamekuwa na shida ya usafiri na kulazimika kusafiri zaidi ya kilomita 400 katika barabara ya vumbi kwenda makao makuu ya Mkoa wa Arusha.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mhandisi-asisitiza-barabara-ya-Arusha--Mara-itajengwa/-/1597296/2369122/-/571eyo/-/index.html
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment