Mngonge,
Naomba kutofautiana na wewe. Mwalimu aliamua uwepo wa vyama vya upinzani baada ya kuona CCM inakwenda mrama bila kuwepo chombo chochote cha marekebisho
au kuikemea. Ukifuatilia hotuba zake tangu alipostaafu, ukianza na ile ya Singida 1986 alipokuwa anatembelea matawi ya CCM utatambua hayo. Katika ule mkutano wa Februari 1992 Mwinyi alitaka utawala wa chama kimoja uendelee, na Nyerere akasema mkiamua kuwa na utawala wa chama kimoja mtaganda nao hata kama chama hicho kimegeuka kuwa kibovu. Huo ndio ulikuwa msukumo wa Nyerere na wala si shinikizo ya "wanaume tunaowaomba."
em
2014-07-29 8:17 GMT-04:00 mngonge franco <mngonge@gmail.com>:
Hosea Nyuma ya mambo kama haya ya ujio wa vyama vingi na uundwaji wa katiba kwa nchi kama ya kwetu yenye budget tegemezi huwa yana shinikizo la wanaume tunawaomba. Na si raisi kuwa wawazi katika hili huwa tuanjitahidi kutoa sababu za hapa na pale huku tukizikwepa sababu au mashinikizo yenyewe.Binafsi huwa nauliza swali moja kubwa kuhusu muundo wa serikali, hivi ni kweli muundo wa serikali mbili una gharama kidogo kuliko hizo tatu zinazopendekezwa? Utamsikia mtu akisema muundo wa serikali tatu una gharama kubwa bila kutufafanulia ni kwa namna gani? Nijuavyo mimi ukiondoa mambo ya muungano ukayapeleka kwenye muungano, serikali mbili za Zanzibar na Tanganyika zitabaki na mambo mache ya kushughulikia hivyo gharama zitakuwa zimegawanywa tu.
Kimsingi serikali yetu ya CCm kupitia waziri wake pamoja na wabunge wa CCM tangu nyuma walikataa kuundwa katiba mpya kulingana na wakati wa sasa walisema iliyopo inatosha. Hivi mbona hawakutwambia sababu za kurejea tena na kukubali kuifanyia marekebisho katiba yetu? Hapa unagundua kuna shinikizo fulani la chini kwa chini lililowafanya na kugeuka kukubali kwa shingo upande kuifanyia marekebisho katiba yetu.
Kwa sababu bado tuna nafasi ya kurekebisha muundo na uendeshajiwa serikali za Tanganyika na ile ya Zanzibar. Ni swala la kupitia rasimu na tukaja na muundo mpya utakao wapunzia madaraka na matumizi ya fedha hawa viongozi wawili wa Tanganyika na Zanzibar. Watuletee proposal inayoonyesha mipaka na matumizi ya huo muundo wa serikali tatu huku tukifananisha na haya matumizi ya muundo uliopo tuweze kuwa na informed decision. Siyo kutuhubiria uzushi na kutukaririsha maneno ya uwongo kwa maslahi binafsi. Dunia ingekuwa na watu wenye mawazo mgando tusingekuwa na ndege, gari, neno demokrasia, meli, computer na vingine vingi tu. Tuepuke kuwa dogmatised na wanasiasa wenye nia ya kujilimbikizia mali na madaraka
2014-07-29 6:30 GMT+03:00 <hosea.ndaki@gmail.com>:Hamis, tusilete siasa za pilato za wengi wape, ikumbukwe mwaka 1990 wakati wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi maoni ya wananchi wengi yaliukataa lakini busara ikatumika. Hata hapa busara zinaweza tumika pia.
Hamis, unasema shein ni amiri jeshi mkuu wa jeshi lipi? Ni command base gani iliyoko zanzibar? Na kama ni wimbo wa taifa hata tff wanao, kama ni mizinga hata kwenye mazishi ya koplo tunapiga tatizo liko wapi, kama unadhani ni nchi huru dodoma wanatafuta nini? Siwakae hukohuko.
Huyo mpemba wa uamsho aliuliza swali chokonozi wasira akaliona akalikwepa kwa kujifanya hajalisikia. Kwanza ukumbi ulijaa wahuni huo mdahalo kwanini hawa kuupeleka nkurumah hall? Wakamwalika na nape?
Kama ni mapato 90% ya mapato yanatoka dar es salaam mbona mnyika hajadai 90% yatumike dar es salaam? Kimara msewe hakuna maji, kawe barabara mbovu sijui hata mkapa anaishi kawe au alishahama. Kuna mikoa ina barabara nzuri umeme hadi migombani na ndio maarufu kwa ukwepaji kodi.
70% ya exports ni dhahabu na inatoka geita na kahama, kaone vituko huko barabara zinajengwa kwa beleshi, lami inamwangwa kwa vikopo, bodaboda zikipita inabanduka, barabara ya geita kahama haiwekewi lami na ndiyo yenye maroli makubwa yaliyobeba sumu za migodini, badala yake inawekewa ya geita nyanhwale yenye costa moja tu!
Kaone lami inayozunguka stendi ya kahama ukikanyaga inabonyea kama umekanyaga godoro la banco. Hayo hatuyaoni tunaona muungano tu.
----------
Sent from my Nokia phone
------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, July 28, 2014 8:13:31 AM GMT-0700
Subject: [wanabidii] MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA STEVEN WASSIRA UBUNGO PLAZA
MASWALI MAGUMU YALIYOMSHINDA
STEVEN WASSIRA UBUNGO PLAZA HAYA HAPA:
Swali la Kwanza;
Kama unaukataa muundo wa muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa na
wananchi kupitia Tume ya Jaji Warioba kwa uchache wa Takwimu, wewe
unapendekeza uwepo wa Serikali mbili kwa Takwimu zipi?.
Swali la Pili;
Je, gharama za kuuendesha muungano huu wa Serikali mbili za sasa ni
Shilingi ngapi, wananchi wa pande zote mbili tunataka ufafanuzi wa Serikali
maana ni haki yetu ya kikatiba kufahamishwa gharama tunazotumia katika
kuiendeshea Serikali yetu kama walipa kodi, ili tufahamu na tulinganishe na
gharama zilizoainishwa na Tume ya Jaji Warioba kwenye muundo wa Serikali
mbili kwa lengo la kupata ukweli wa hoja hii ya gharama.
Swali la Tatu;
Awadhi alimuuliza Wassira kwamba, kama mgao wa mapato ndio kikwazo cha
muundo wa Serikali tatu kwamba Zanzibar watadai 50% ya mapato ya muungano
kama CCM wanavyotoa hoja, Kwani ni lini Zanzibar ilipewa 50% ya mapato yote?
Mbona miaka yote Zanzibar inapewa 4% (asilimia nne) ya mapato yote ya
muungano?.
Swali la Nne;
Kama muungano huu ni wa Nchi moja yenye Serikali mbili, ni kwa nini Rais wa
Zanzibar ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar na ni kwa nini apigiwe mizinga ishirini na moja kama Rais wa
muungano?
Na kama hayo ni ya kweli, ni kwa nini hamtaki kukubali kwamba Tanganyika
ndiyo iliyovaa koti la muungano baada ya Zanzibar kutambuliwa na Katiba yao
kama Nchi yenye mamlaka kamili?
Pia ni kwa nini mnakuwa ving'ang'anizi hata kwenye hoja za kweli na zenye
ushahidi wa wazi hata inafikia hatua hamtaki kukubali kwamba muungano huu
ni wa Nchi mbili zenye Serikali mbili badala ya muungano wa Nchi moja yenye
Serikali mbili?
Hapa hakuna muungano bali hiki ni kiini macho, tunaitaka Tanganyika yetu
sasa, na wazanzibar wanaitaka Zanzibar yao huru, maana nusu karne ya
unafiki na uongo wa CCM umefika mwisho sasa.
Swali la Tano;
Kama mnaukataa muundo wa Serikali tatu, ni kwa nini Katiba hii iliyopo hivi
sasa ya mwaka 1977 inatambua uwepo wa muundo huo wa Serikali tatu na hata
kufikia hatua ya kuwataja mawaziri watatu kwa kila Wizara, ikiwa na maana
kwamba, Waziri anayeshughulikia mambo ya muungano kwenye Wizara husika
ndani ya Bunge la muungano, Waziri wa Wizara husika na Waziri anayehudumu
kwenye Bunge la wawakilishi Zanzibar?
Swali la Sita;
Tume zote zilizowahi kuundwa ili kukusanya maoni ya wananchi tangu uhuru
mpaka leo, nikiwa na maana ya Tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Jaji Nyalali,
kundi la G55 na hii ya sasa chini ya Jaji Warioba, zote zimeleta maoni na
mapendekezo ya wananchi yenye muundo wa Serikali tatu.
Licha ya kwamba michakato yote hii ya Katiba mpya tangu enzi hizo mpaka leo
imekuwa ikiwagharimu walipa kodi wa Taifa hili mabillioni ya Shilingi, ni
kwa nini kwa miaka yote hiyo mpaka leo Serikali hii ya CCM mmekuwa
mkiikwepa hoja hii ya msingi inayopaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya Taifa
zima.
Lakini pia, mbona tunazo timu tatu za Taifa za mpira wa miguu?
Kwani Zanzibar Hilloes ni ya wapi kama sio ya Zanzibar?
Kwani Kilimanjaro Stars ni ya wapi kama sio ya Tanganyika?
Kwani Taifa Stars ni ya wapi kama sio Timu ya muungano?
Kuna hoja gani nyuma ya pazia, inayowafanya muendelee kuifanya Zanzibar
kama koloni la Tanganyika?
Nusu karne ya uongo ubabe na unafiki wa CCM na vibaraka wao, imefika mwisho
sasa kwa sababu hiki sio kizazi cha analogia tena bali ni kizazi cha
digital.
Tunautaka ukweli na uwazi katika masuala nyeti na ya msingi kama hili la
kuivua Tanganyika Joho la muungano.
Mwisho!
Imeandaliwa na;
Francis Boniface Garatwa,
Mwanaharakati wa CHADEMA,
Kanda ya Ziwa Mashariki,
Mkoa wa Mara,
Wilaya ya Serengeti.
28/07/2014.
Email:francisboniface50@gmail.com
0785881009/0767881009.
*********************
Naomba kuwasilisha!
Ahsanteni sana!!!
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:
Post a Comment