Thursday 29 May 2014

[wanabidii] Taarifa ya LAPF kuhusu kumkopesha Mbowe kuwasaidia Msigwa, Mbilinyi

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF NI MFUKO WA HIFADHI YA JAMII NCHINI TANZANIA WENYE MAKAO MAKUU YAKE MJINI DODOMA.

MFUKO WA LAPF UNAPENDA KUKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUWA LAPF ILITOA MSAADA KWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI NA MBUNGE WA IRINGA MJINI MH. PETER MSIGWA.

IELEWEKE KUWA INGAWA WAHESHIMIWA WABUNGE AU MTU AU TAASISI YEYOYE HAWAZUILIWI KUOMBA MSAADA WA KIJAMII, MH. MBILINYI NA MH. MSIGWA HAWAJAWAHI KUWASILISHA MAOMBI NA HAWAJAWAHI KUPEWA MSAADA WOWOTE NA LAPF.

AIDHA LAPF INAKANUSHA HABARI ZILIZOTOLEWA KATIKA GATEZI LA MTANZANIA LA TAREHE 26 MEI 2014 TOLEO NA. 7472 KUWA WAHESHIMIWA WABUNGE NI WASUMBUFU NA KUMFANYA MKURUGENZI MKUU 
ASIENDE BUNGENI.

LAPF INAKANUSHA PIA HABARI ILIYOTOLEWA KATIKA GAZETI LA THE GUARDIAN LA TAREHE 27 MEI 2014 TOLEO NA. 6031. IELEWEKE KUWA LAPF HAIJAWAHI KUMKOPESHA MH. FREEMAN MBOWE (kulia) KIASI CHA SHILINGI BILIONI MOJA. MFUKO WA LAPF HAUNA UTARATIBU WA KUKOPESHA MTU MMOJA MMOJA HIVYO HAKUNA MIKOPO YA AINA HIYO. LAPF HUTOA MIKOPO YA WANACHAMA WAKE KUPITIA VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA (SACCOS) NA MIKOPO YA NYUMBA KWA WANACHAMA WANAOKARIBIA KUSTAAFU.

AIDHA, SI KWELI PIA KWAMBA LAPF HAISHIRIKI KATIKA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWANI MFUKO HUU UKO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI NA INASHIRIKI KATIKA VIKAO HIVYO.

LAPF INAPENDA KUWAJULISHA UMMA WA WATANZANIA KUWA MFUKO HUTOA MISAADA YA KIJAMII KWA KUZINGATIA MPANGO NA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KWA KUZINGATIA SERA YA MISAADA YA KIJAMII NA MAOMBI YANAYOWASILISHWA. PIA HAKUNA TAASISI AU MTU BINAFSI INAYOPEWA FEDHA TASLIM ISIPOKUWA MFUKO HUNUNUA VIFAA NA KUWASILISHA MOJA KWA MOJA KWA WAHUSIKA. 

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAENDESHWA CHINI YA SHERIA YA LAPF (THE LOCAL AUTHORITIES PENSIONS FUND ACT NO. 9 OF 2006). SHERIA HII IMEFANYIWA MAREKEBISHO KUKIDHI MAHITAJI YA SHERIA YA USIMAMIZI WA HIFADHI YA JAMII YA MWAKA 2008 (SSRA) NA KWA SASA LAPF INAANDIKISHA WANACHAMA TOKA SEKTA ZOTE NCHINI NA JINA LA MFUKO LILIREKEBISHWA NA SASA LINAJULIKANA KAMA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF (LAPF PENSIONS FUND).

SHUGHULI KUU ZA MFUKO NI PAMOJA NA KUANDIKISHA WANACHAMA, KUKUSANYA MICHANGO, UWEKEZAJI NA KULIPA MAFAO. 

KWA SASA LAPF INATOA MAFAO MBALI MBALI AMBAYO NI MAFAO YA UZEENI, MAFAO YA MIRATHI, MAFAO YA KUUMIA KAZINI, MAFAO YA UZAZI, MAFAO YA KUJITOA, MSAADA WA MAZISHI, MIKOPO YA NYUMBA, MIKOPO YA WANACHAMA KUPITIA SACCOS NA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUTOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA.

PAMOJA NA MAJUKUMU MAKUU YA MFUKO YALIYOTAJWA HAPO JUU, MFUKO UNASHIRIKI PIA KATIKA KUISAIDIA JAMII NA HIVYO KUSAIDIA KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUCHOCHEA MAENDELEO ( CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY).

MISAADA HII INA LENGO LA KUSAIDIA JAMII YOTE YA WATANZANIA YENYE MAHITAJI MBALI MBALI NA KWA KUTAMBUA KUWA MISAADA HII ITAWANUFAISHA SI WANACHAMA WA LAPF TUU BALI PIA WANANCHI WOTE.

LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA KIJAMII KATIKA SEKTA MBALI MBALI KAMA VILE AFYA, ELIMU, VITUO VYA WATOTO YA YATIMA, TAASISI ZA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM, SEKTA YA MICHEZO NA KUSAIDIA MAAFA KWA KUTOA VIFAA MBALI MBALI KAMA MASHUKA, VYANDARUA NA MADAWA, KATIKA ELIMU KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA, UNUNUZI WA MADAWATI NA VIFAA VYA MAABARA. KATIKA VITUO VYA WATOTO YATIMA LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA VYAKULA, MAVAZI NA VIFAA VYA SHULE. KADHALIKA KATIKA MICHEZO LAPF IMEKUWA IKICHANGIA VIFAA VYA MICHEZO KAMA JEZI NA MIPIRA. 
KWA MIAKA MITATU MFULULIZO MFUKO WA LAPF NDIO UMEKUWA MDHAMINI MKUU WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA) AMBAO NI WANACHAMA WATARAJIWA WA MFUKO.

KATIKA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 MFUKO WA LAPF UMETOA MISAADA MBALI MBALI KAMA VILE VIFAA VYA UJENZI CHUO CHA MADAKTARI BUGANDO NA CHUO KIKUU HURIA (OUT).

KADHALIKA LAPF IMEOTA VIFAA MBALI MBALI VYA SHULE KAMA VILE MADAWATI, TAA ZA SOLA NA MASHINE ZA FOTOKOPI. 

KATIKA SEKTA YA AFYA LAPF IMETOA MSAADA KWA HOSPITALI NA ZAHANATI MBALI MBALI NCHINI KWA KUTOA VYANDARUA, MASHUKA, MADAWA, VIFAA VYA MAABARA, TAA ZA SOLA PAMOJA NA KUCHANGIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.

KATIKA MICHEZO LAPF IMEENDELA KUWA MDHAMINI WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA) NA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHIRIKISHO LA SERIKALI ZA MITAA (SHIMISEMITA).

HII NI BAADHI TU YA MISAADA AMBAYO LAPF IMETOA KWA MWAKA HUU KWA KUZINGATIA MAOMBI MBALI MBALI YALIYOWASILISHWA PAMOJA NA BAJETI NA MPANGO WA MFUKO ULIOIDHINISHWA. KWA MWAKA HUU WA FEDHA, MISAADA YOTE HADI SASA INA JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA MOJA NA ISHIRINI. AIDHA, KUTOKANA NA UFINYU WA BAJETI YA MFUKO, SEHEMU KUBWA YA MISAADA HII NI KATI YA SHILINGI LAKI TANO HADI MILIONI TATU. MISAADA HII HUTOLEWA MOJA KWA MOJA KWA WALENGWA NA PIA SI FEDHA TASLIMU, BALI VIFAA HUSIKA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment