Friday 30 May 2014

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] SOMA HOTUBA YA SUGU - LINAGANISHA NA MAJIBU YA ZITTO KISHA TOA HUKUMU

Duu,

Pole Mh Zitto kwa Kuuguliwa na mama, twamuomba Mola ampe nafuu kwa haraka,

ila nimeshangaa kidogo uliposema CHAMA CHAO!! kweli wewe haumo!!?

kama maneno haya ni ya Mh Zitto basi tumpe nafasi kwanza amuuguze mama then atatangaza rasmi kuwa hayupo Chadema ili umma ujue rasmi.

Simon.
--------------------------------------------
On Fri, 30/5/14, 'Jovi kamuntu' via Mabadiliko Forum <mabadilikotanzania@googlegroups.com> wrote:

Subject: [Mabadiliko] SOMA HOTUBA YA SUGU - LINAGANISHA NA MAJIBU YA ZITTO KISHA TOA HUKUMU
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, 30 May, 2014, 11:59

Hapa
nawawekea sehemu ya hotuba ya Sugu, na majibu
ya Zitto ndipo sasa uweze kuhukumu:-
 

Sehemu ya Hotuba ya Waziri Kivuli Joseph
Osmundi Mbilinyi aka
Sugu

Mheshimiwa Spika,
Tarehe 13 Agosti,
2012, Msajili Msaidizi wa Makampuni katika Wakala wa Usajili
wa Makampuni na
Leseni (BRELA) alitoa Hati ya Usajili (Certificate iof
Incorporation) kwa
kampuni inayoitwa Leka Dutigite Limited. Kwa mujibu wa
nyaraka za BRELA, Leka
Dutigite Ltd. ina ofisi zake katika ghorofa ya kwanza ya
jengo la City House
lililoko katika Mtaa wa Mkwepu, Dar es SalaaM. Mheshimiwa
Spika, 



Katiba, yaani Memorandum and Articles of Association,
ya kampuni ya Leka Dutigite Ltd. iliyosajiliwa BRELA tarehe
13 Agosti, 2012
inaonyesha kwamba mwenye hisa nyingi katika kampuni hiyo ni
kampuni nyingine
inayoitwa Gombe Advisors Ltd. ya Dar es
Salaam. 

Kwa mujibu wa taarifa
za kibenki ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako
tukufu imezipata, mnamo
tarehe 10 Desemba, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani
ilihamisha jumla ya
shilingi 12,200,000 kwenda kwenye akaunti na. 0150357447800
iliyoko CRDB Bank
tawi la Pugu Road, Dar es Salaam, inayomilikiwa na Leka
Dutigite Ltd. Hifadhi
ya Taifa ya Saadani inamilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa (TANAPA), ambayo
ni shirika la umma. Siku moja baadae, fedha hizo zilitolewa
kwa pesa taslimu
kutoka kwenye akaunti hiyo. 



Baada ya hapo, kati ya tarehe 14 Januari na 7
Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa
jumla ya shilingi
28,600,000. Fedha hizi zote ziliingizwa kama fedha taslimu
na mtu aitwaye
Mchange (shilingi 3,600,000 tarehe 14 Januari, 2013) na Leka
Dutigite (shilingi
25,000,000 tarehe 23 Januari na 7 Februari, 2013). Kufikia
tarehe 7 Februari,
2013, fedha hizo zote zilikwishatolewa
benki.

 Mheshimiwa Spika,
Tarehe 28 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd.
iliingiziwa shilingi
32,367,000 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kwa
mujibu wa taarifa
za kibenki, siku hiyo hiyo, fedha hizo zilitolewa kwenye
akaunti hiyo. Siku nne
baadae, yaani tarehe 4 Machi, 2013, NSSF ilifanya malipo
mengine kwenye akaunti
ya Leka Dutigite Ltd., kwa mikupuo miwili, ya jumla ya
shilingi 46,663,000.
Siku hiyo hiyo, fedha hizo nazo zilitolewa kutoka kwenye
akaunti hiyo kwa
mikupuo miwili. Kwa hiyo, katika kipindi cha miezi mitatu
katika ya tarehe 10
Desemba, 2012 na 4 Machi, 2013, Leka Dutigite Ltd. ililipwa
shilingi
119,930,000 kwa utaratibu huo huo wa ingiza na toa fasta.
Kati ya fedha hizo,
shilingi 12,200,000 zililipwa na TANAPA na shilingi
79,027,000 zililipwa na
NSSF.

Mheshimiwa Spika,
Katika mazingira ya kawaida, sio kitu cha ajabu kwa
mashirika ya umma kama NSSF
na TANAPA kufanya biashara na watu au taasisi mbali mbali
kama makampuni
binafsi. Ukweli ni kwamba, kwa upande wa malipo yaliyofanywa
na TANAPA, Kambi
Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imeweza kupata nakala
ya mkataba
unaohusu Maandalizi ya Filamu (Documentary) kwa Ajili ya
Kuhamasisha Shughuli
za Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa Kutumia
Wasanii Kutoka Kigoma.
Mkataba huo umesainiwa tarehe 5 Desemba, 2012, kati ya
Hifadhi ya Taifa ya
Saadani na Leka Dutigite Ltd. na una thamani ya shilingi
12,200,000, kiasi kile
kile kilicholipwa na Hifadhi
hiyo.

Hata hivyo, Mheshimiwa
Spika, mazingira ya malipo haya sio ya kawaida. Hii ni kwa
sababu ya uwepo wa
kampuni ya Gombe Advisors Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka za
BRELA, kampuni hii
ilisajiliwa tarehe 24 Novemba, 2011. Kwa mujibu wa nyaraka
hizo, ofisi za Gombe
Advisors Ltd. ziko kwenye jengo la City House, Mtaa wa
Mkwepu, Dar es Salaam,
ziliko ofisi za Leka Dutigite Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka
hizo, wakurugenzi wa
Gombe Advisors Ltd. ni Zitto Zuberi Kabwe ambaye kazi yake
inatajwa kuwa
'mchumi', na Raphael Ongangi ambaye anatajwa kuwa
'mchambuzi wa fedha na vitega
uchumi' (Financial and Investment Analyst). Bwana Ongangi
aliwahi kutajwa na
gazeti la kila wiki la ----- la tarehe 26 Desemba 2013 kuwa
ni mmoja wa
washauri wa Zitto Zuberi Kabwe na anasemekana kuwa msaidizi
wake. 

Mheshimiwa Spika, Zitto
Zuberi Kabwe sio 'mchumi' anayetajwa katika nyaraka za
BRELA zinazoihusu
kampuni ya Gombe Advisors Ltd. pekee, bali pia ni Mbunge,
tangu mwaka 2005, wa
Bunge lako tukufu. Kama Mbunge, Mheshimiwa Zitto Kabwe ni
'kiongozi wa umma'
kwa mujibu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, 1995.
Sheria hii inawalazimu
viongozi wa umma, wanapokuwa madarakani, kuwa "waadilifu,
wenye huruma,
utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya
maadili ili kujenga na
kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa
Serikali."

Aidha, viongozi wa umma
"... watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na
kuendesha shughuli zao
binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni
wazi kwa umma na
haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria
tu." Vile vile,
kuhusiana na maslahi binafsi, Sheria hii inaelekeza kwamba
"... viongozi wa
umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza
kuathiriwa na maamuzi ya
serikali wanayoshiriki katika
kuyafanya." 

Mwisho, kuhusiana na
maslahi ya umma, viongozi wa umma wanatakiwa, pale
wanapochaguliwa au
kuteuliwa, kupanga masuala yao "kwa namna itakayozuia
migongano ya maslahi ya
wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo
migongano hiyo
inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi
itatatuliwa kwa
kuangalia zaidi maslahi ya umma." Kwa kadri ya ufahamu wa
Kambi Rasmi ya
Upinzani ya Bunge lako tukufu, Mheshimiwa Zitto Kabwe
hajawahi kutangaza maslahi
aliyonayo kwenye mikataba ya Gombe Advisors Ltd. na Leka
Dutigite Ltd. na NSSF
na TANAPA.

Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe sio tu ni Mbunge anayebanwa na
masharti ya Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bali pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Fedha za Serikali (PAC). Kwa mujibu wa kipengele
cha 12 cha Nyongeza
ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, mojawapo
ya majukumu ya PAC
ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi
mabaya ya fedha za umma
katika Wizara na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika
taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. NSSF na TANAPA ni baadhi
tu ya Mashirika ya
Umma yaliyo chini ya usimamizi wa kibunge wa
PAC. 

Kwa maana hiyo,
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwa kutumia
makampuni yake ya Leka
Dutigite Ltd. na Gombe Advisors Ltd., amefanya biashara na
TANAPA, shirika la
umma analolisimamia kama Mbunge na Mwenyekiti wa PAC.
Mheshimiwa Zitto Kabwe na
wanamuziki washirika wake, kwa kutumia makampuni ya Gombe
Advisors Ltd. na Leka
Dutigite Ltd., wamelipwa fedha za umma za TANAPA na
NSSF. 



Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa
maelezo juu ya madai ya ukiukwaji wa Sheria uliofanywa na
viongozi wa umma na
mashirika ya umma katika kashfa hii. Pamoja na maelezo
yatayotolewa , Kambi
Rasmi ya Upinzani inataka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) kufanya
ukaguzi maalum juu ya matumizi ya fedha zilizotolewa na
TANAPA na NSSF; msukumo
uliofanya fedha hizo zitolewe na matumizi ya fedha hizo kwa
kuzingatia masharti
yanayosimamia fedha za umma na utawala bora katika usimamizi
wa fedha za umma.
Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
ifanye uchunguzi juu
ya malipo na matumizi husika kwa kurejea masharti ya Sheria
ya Maadili ya
Viongozi wa Umma na Sheria nyingine zinazohusika. Kwa upande
mwingine, kwa kuwa
suala hili linahusu mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
inayohusika na
usimamizi wa fedha za umma, Kamati ya Kinga, Haki na
Madaraka ya Bunge nayo
ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya
Nchi, Sheria ya
Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya
maadili ya kiongozi
wa umma ikiwemo yahusuyo utangazaji wa maslahi.



Mheshimiwa Spika; Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani ya
Bunge lako tukufu inatoa rai kwa wanamuziki na wasanii
wengine wote nchini kuwa
waangalifu na watu wanaotaka kutumia umaarufu wao kama
wanamuziki na wasanii
kwa lengo la kufanikisha dili za kifisadi. Bila kuchukua
tahadhari ya kutosha,
wasanii hao wanaweza kujikuta wakipoteza sifa na umaarufu
wao ambao wameujenga
kwa jitihada zao wenyewe



YANAYODAIWA KUWA MAJIBU YA
ZITTO

Nasikitika
kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu
naingizwa kwenye siasa za
majitaka.

Kampuni
ya Leka Dutigite inamilikiwa na wasanii. Gombe Advisors ni
kampuni isiyofanya
faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote
ya kibiashara. Wasanii
wa Kigoma wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo
zinajulikana na zipo.
Leo mpigie simu mfanyakazi yeyote wa NSSF utasikia kazi ya
wasanii hao.



Kwa namna yeyote ile hii ni ishara ya kukosa ubinaadam maana
waliyoyasema
wanajua sina faida yeyote ya kifedha Leo wala kesho kwa Leka
Dutigite na Gombe
Advisors.



Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa
kamati kuu ya chama
chao, pole ninayopewa ndio hiyo. Hakuna namna ya kukosa
ubinaadamu zaidi ya
hivi.


Hata
hivyo, ni vema CAG afanye ukaguzi haraka sana na Mimi
binafsi nitawajibika
iwapo itaonekana kwa namna yeyote ile nina maslahi ya
kifedha katika LekaDutigite
na gombe advisors.

Ni ushetani. Ni roho
mbaya. There are limits to political attacks.--

Chanzo: Zimenukuliwa toka uzi za
wanabidii na Mabadiliko

Jovin Bifabusha



DIRECTOR

KWFF LTD

P. O. Box 313

Skype: jovin.bifabusha

Karagwe, Tanzania

+255 784 709200



--

Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la
'Mabadiliko'.

Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
mabadilikotanzania@googlegroups.com

 

 

For more options, visit this group at:

http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Mabadiliko Forum" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.

To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.

Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.

To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1401440397.67207.YahooMailNeo%40web140505.mail.bf1.yahoo.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment