Saturday 31 May 2014

Re: [wanabidii] Profesa Muhongo anapata wapi jeuri hii?

Sijaelewa Othiambo anataka kuongelea nini! Mohongo hakutaja wasifu kwani alizuiliwa wewe umetaja shule hadi mwaka aliomaliza shule sasa nani anamakosa kati ya mohongo na wewe?

Umesema ni wajibu wa kamati kuufanyia kazi ushahidi sasa mohongo unamtaka ajibu hoja ipi? Si kamati ichunguze na ikihitaji msaada takukuru wapo, na jinai ikipatikana dpp yupo sasa tatizo ni nini?

Mohongo kaumaliza mgogoro wa iptl sasa tatizo ni nini? Au mlitaka wale mawakili waendelee kupiga hela za tanesco?

Hili la kujitapa, watanzania tukijenga tabia ya kujisifia mafanikio yetu tutaondokana na umasikini kwa haraka sana, kila mtu ajitape kwa mafanikio yake, mengi ajivunie utajiri wa vitalu vya madini, muhongo ajivunie u profesa wake.



----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: 'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>,"Mabadiliko" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Date: Saturday, May 31, 2014 1:22:45 PM GMT-0700
Subject: [wanabidii] Profesa Muhongo anapata wapi jeuri hii?

Ndugu Mhariri,
Wakati
anasoma bajeti ya Wizara yake, Profesa Muhongo akimchana Dr Ole Sendeka bungeni
kwa kumkejeli na kumdhalilisha hadharani huku akifikia hatua ya kutaka kuweka
hadharani matokeo yake (Ole Sendeka) ya mtihani wa kidato cha nne aliokaa mwaka
1984 katika Shule ya Sekondari Monduli.

Isingekuwa busara za Spika Makinda ni dhahiri kwamba Muhongo angeanika matokeo
ya Ole Sendeka hadharani.

Badala ya kujibu tuhuma za ufisadi wa fedha za umma unaomkabili yeye (Profesa
Muhongo) na mshirika wake (Maswi), Muhongo alitumia muda wa umma vibaya kwa
kumshambulia Ole Sendeka kama mtu binafsi na kumdhalilisha vya kutosha.

Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, ushahidi ukishatolewa bungeni, kama alivyofanya
Dr Kafulila na Dr Ole Sendeka, ni jukumu la tume ya maadili ya bunge
kuuchunguza na kuona kama unakidhi haja na kisha kuwapelekea TAKUKURU na
mahakama waufanyie kazi.

Sasa inakuwaje Madam Spika akamruhusu Prof Muhongo apoteze muda wa umma kwa
kumshambulia Ole Sendeka kama mtu binafsi huku akikwepa tuhuma za ufisadi
zinazomwandama yeye na Maswi? Hili suala sio sawawa hata kidogo.

Aidha, inaonekana kwamba Prof Muhongo ni mtu wa ajabu sana kwa jinsi
anavyojisifu kwa usomi wake bila kuzingatia kwamba sisi watanzania tumemtuma
akatuwashie umeme sio kututangazia usomi wake! Mh Mbowe aliomba muda uongezwe
ili kila mbunge apate nafasi ya kuhoji namna mambo yanavyokwenda ovyo kwenye
wizara hii lakini Prof Muhongo akambeza na kumdharau.

Majisifu ya kila siku ya profesa Muhongo na kuringia usomi wake sio tija kwa
watanzania. Watanzania tunataka umeme na tunataka mafisadi wanaokula fedha za
umma washughulikiwe.

Sisi hatuna haja na usomi wa Muhongo. Hata kama Wizara hii ikiongozwa na mtu
aisiyekwenda shule kama vile Kapteni Komba au Prof Majimarefu, sisi hatuna
shida na hilo. Shida na taabu yetu ni kuona kila mtanzania anapata huduma ya
umeme wa uhakika.

Profesa Muhongo anatakiwa ajiandikishe kwenye chuo siasa cha CCM Kivukoni,
akajifunze taaluma ya siasa na namna ya kuheshimu watu na mawazo yao, tofauti
na jinsi anavyotenda mambo kwa sasa. Kutaja matokeo ya mtihani ya Ole Sendeka
bungeni haikuwa hoja ya msingi. Hoja ya msingi ilikuwa ajibu tuhuma
zinazomkabili yeye na msaidizi wake wa karibu (Maswi). Vitendo vya kifisadi
vinavyofanywa na watu wa chama na serikali haviwafurahishi wananchi hata
kidogo. Wananchi wanataka mawaziri wachapakazi watakaowaletea maendeleao
endelevu. Hawataki mawaziri domo kaya wanaoringia usomi wao wakati wanashindwa
kutumia usomi huo kuwaletea wananchi maendeleo. Kutamba kwamba amewahi kuwa
Rais wa wanajioljia Afrika hakutuongezei shibe na wala hakutupunguzii njaa.
Muhongo anapaswa kupima kila neno linalotoka kinywani mwake na kutathimini
madhara yake kabla ya kuropoka.

Kutaja hadharani matokeo ya mtihani ya mtu anayetetea wananchi, ni utovu wa
maadili ya uongozi na nidhamu kwa kiongozi mkubwa kama Muhongo ambaye
anategemewa kuwaletea watanzania maendeleo. Matokeo ya mtihani ya mtu ni SIRI,
hayatakiwi kutajwa hadharani—hii ni NYARA ya serikali. Muhongo na hao watumishi
kengeufu wa Baraza la Mitihani (NECTA) waliomchapia matokeo ya Ole Sendeka
yafaa wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka miiko ya utumishi wa umma.
 
Thobias Odhiambo,
Dar es Salaam,
Simu: 0719 786 226

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment