TAARIFA KWA UMMA
ZABUNI YA 4 YA KUNADI VITALU VYA
UTAFITI WA GESI ASILIA
Utangulizi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), tarehe 25/10/2013 ilizindua rasmi zabuni ya nne ya vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi asilia vilivyoko bahari kuu na Ziwa Tanganyika kaskazini. Uzinduzi wa zabuni hii ulihusisha vitalu 7 vilivyoko bahari kuu (deep offshore blocks) pamoja na kitalu cha Ziwa Tanganyika kaskazini (Lake Tanganyika North). Vitalu vya bahari kuu vipo katika kina cha maji kati ya mita 2000 na 3000 wakati kitalu cha Ziwa Tanganyika kinafikia kina cha mita 1500. Mchakato wa zabuni utafungwa rasmi baada ya miezi sita na Zabuni zitakazowasilishwa kabla ya saa nne asubuhi ya Alhamisi ya tarehe 15 mwezi Mei mwaka 2014. Zabuni zitafunguliwa kwa uwazi mbele ya washiriki wa mnada watakaopenda kuwepo ama kuwakilishwa siku ya ufunguzi.
Majina ya vitalu vinavyonadiwa ni kama inavyooneka katika jedwali hapa chini.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment