Tuesday, 31 December 2013

[wanabidii] SALAAM ZA MWAKA MPYA KUTOKA MJENGWABLOG. COM

Mwaka 2014 Uwe Ni Wa Kusonga Mbele...

Ndugu zangu,

Tumeingia Mwaka Mpya wa 2014. Kwangu binafsi mwaka 2013 umekuwa wa bahati mbaya ya kukumbwa na balaa lililonirudisha nyuma kwa takribani miezi minne.

Tukio la mwezi Machi mwaka jana, la kushambuliwa na kuteswa kwa ndugu yangu na mwanafamilia mwenzangu kwenye tasnia ya habari, Absalom Kibanda, sio tu lilinigusa na kunitia hofu, bali, kukatokea pia ' kituko' cha mwaka cha mimi kuhusishwa na uovu ule.

Nilifahamu kuwa nchi yetu ina mambo mengine ya ovyo ovyo, lakini, kamwe sikufikiri ningeingizwa kwenye mambo ya ovyo ovyo ya staili iliyonitokea mimi.

Hakika, jambo lile halikunifedhehesha mimi tu, bali, umati wa watu walionifahamu kwa miaka mingi kupitia kalamu yangu nao walifedheheshwa pia. Waliponipigia simu kunipa pole ajabu mimi niliyejibu nilijikuta nikiwapa pole wao. Kwangu inabaki kuwa ni moja ya ' Kumbumbu ya aibu'- Memories of shame.

Nami, kama ilivyo kwa wengine, nina kiu ya kuujua ukweli wa kilichomtokea Kibanda. Hatuwezi kulala kwa amani bila kujua haswa ni akina nani waliomfanyia unyama ule Absalom Kibanda.

Kwa wale ndugu zangu waliohusika kwa namna moja au nyingine kwenye kazi ile ya kunifedhehesha na kunidhalilisha kwa lengo moja kuu la KUNICHAFUA mbele ya macho ya jamii. Ndugu zangu ambao wengine ni rafiki zangu na wanafamilia wenzangu kwenye tasnia ya habari na wenye kujiita wanasiasa wapenda demokrasia, ningependa niwahakikishie, kuwa mimi kama Maggid, nawahesabu bado ni ndugu na rafiki zangu. Sina kinyongo nao. Nitapenda kuendelea na udugu na ushirikiano wetu kama Watanzania, na wao wala wasisite kunishirikisha kwenye mambo ya msingi kwa ajili ya nchi yetu.

Ndugu zangu,
Kwangu mwaka 2014 nadhamiria uwe ni wa kusonga mbele. Na ningependa sote tuwe na dhamira hiyo ya kusonga mbele kama watu binafsi na kama taifa. Tutangulize zaidi maslahi mapana ya nchi yetu.

Kwa misukosuko niliyopata mwaka huu, kuna ambayo nimeshindwa kuyafanya kama nilivyodhamiria na kuweka bayana kwenye 'hotuba' yangu ya mwisho wa mwaka jana.

Mwaka 2014, mbali ya kazi zangu za kila siku kwenye Jumuiya ya Karibu Tanzania Association, nitapenda nitimize dhamira yangu ya kuupanda Mlima Kilimanjaro. Nitapenda pia nijikite kwenye kuhamasisha juhudi za maendeleo kwa Wanawake na Vijana wa Vijijini. Nitapenda pia niimarishe Jukwaa la ' Kwanza Jamii Dialogue' kwa maana ya mijadala ya wazi kuhusiana na masuala muhimu ya kitaifa.

Naam, nitapenda kujikita kwenye yale yenye pia kuibua mijadala endelevu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja na yote hayo, mwaka 2014 nitajitahidi, kama mzazi, kutenga muda zaidi wa kuwa na familia yangu; mke wangu mpenzi na wana wangu.

Nawatakia nyote HERI YA MWAKA MPYA!

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252

http://mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment