Monday, 2 December 2013

[wanabidii] Mwaliko kwenye Kongamano la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 8/12/2013


Kwa niaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, napenda kuwakaribisha watanzania wote wenye mapenzi mema kwenye kongamano  la kujadili mchango wa rasilimali zetu kwa maendeleo ya taifa letu. Kongamano hilo litafanyika tarehe 8 Desemba 2013  ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia saa 7.30 mchana hadi saa 12 jioni. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV na Radio one.
 
Mada kuu ya kongamano hilo ni, "Mchango wa Rasilimali zetu katika maendeleo ya Taifa na Nafasi ya Mtanzania Kumiliki Rasilimali hizo".
 
Tunapenda kuchukua fursa hii kwa heshima kubwa kuwaomba wote wenye uchungu na rasilimali zetu na wadau wote wenye uelewa mpana kuhusiana na masuala ya usimamizi wa rasilimali mfike ukumbini siku hiyo ili muwe miongoni mwa watanzania wenye nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika kutoa elimu kwa watanzania juu ya nafasi yao katika kumiliki rasilimali zetu na mchango wake kwa maendeleo ya taifa letu.  
 
Miongoni mwa wazungumzaji siku hiyo ni pamoja na maprofesa waliobobea katika usimamizi wa rasilimali, wazungumzaji wengine waalikwa ni pamoja na Mheshimiwa John Mnyika (Waziri kivuli wa Nishati na Madini), Dkt Reginald Mengi (Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania), na wadau katika sekta ya madini. Na Mgeni Rasmi atakayefunga kongamano hilo ni Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini.
                                                    
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki  wenu kwenye kongamano hili.
 
Karibuni nyote:
 
Mr. Faraja Kristomus
(Katibu – UDASA)
0787525396 / 0717086135
Kwa maoni kuhusu mada husika tuandikie: kongamanoudasa@gmail.com
 

0 comments:

Post a Comment