Ndugu zangu,
Cris Lukosi ameandika haya kwenye Jamii Forums jana...
"Nndugu zanguni
Naona kila kukicha makamanda wa chadema wamekuwa wakiendeleza ile singo yao ya rambi rambi dhidi yangu.
Huu wimbo umenikera sana na nadhani sasa ni wakati muafaka kwa Mchungaji Msigwa kujitokeza hapa na kutoa ufafanuzi ziliko hizo hela ambazo mimi nilizifikisha kwake kupitia Maggid Mjengwa
Sio vyema kwa kiongozi wa dini tena mbunge kukaa kimya kwenye suala kama hili.
Watu walitoa kwa moyo, hivyo ni vyema wajue hela zao kama zilifika au zilitumika kwenye mikutano ya pale mwembetogwa
JITAMBUE!"-
Mwingine amechangia...
"JF Senior Expert Member Array
Default Re: Namuomba Mchungaji Msigwa aje hapa kutueleza ziliko rambirambi za Mwangosi nilizompa.
Hapa kuna watu watatu wanaoujua ukweli wa nani ametafuna pesa za rambi rambi. Chris Lukosi, Maggid Mjengwa, au Mchungaji Msigwa. Lukosi anasema amekabidhi pesa kwa Mjengwa, sasa kama Msigwa anakanusha hakupewa pesa, basi pesa aidha zimeliwa na Lukosi au Mjengwa. Tunataka Maggid Mjengwa aje hapa athibitishe kama ni kweli alikabidhiwa pesa na Lukosi? Na yeye jee alizikabidhi kwa Msigwa?
Embu mwenye namba ya simu ya Mjengwa aiweke hapa tafadhali. " ( Chanzo JF)
Ukweli wangu:
Kwa kufuatilia mjadala kwenye mada hii mtandaoni nimeona dhahiri, kuwa wasionitakia mema wameanza hila za kuliingiza na kulichafua jina langu na rekodi yangu ya kujitahidi kuishi na kutenda yalo mema na kwa uadilifu. Na mengine si ya kuyapuuzia, maana kuna wenye kuamini upuuzi pia. Ndio sababu nimeamua kuweka ukweli wangu hapa...
Baada ya kuawa kinyama kwa rafiki na mwanafamilia mwenzetu katika tasnia ya habari, Daud Mwangosi, niliitisha harambee kupitia Mjengwablog ili kumsaidia mjane wa marehemu na watoto wake.
Yafuatayo yawe wazi;
1. Ni kweli kuwa Cris Lukosi kupitia nduguye Augustino Lukosi aliniingizia shilingi milioni moja kwenye akaunti yangu ya MPESA kama mchango wa rambirambi uliokusanywa UK kutoka kwa wanachadema Lukosi akiwa mwenyekiti wao.( Angalia siku, tarehe na muda kwenye kiambatanishi)
2. Kwenye orodha ya wachangiaji niliorodhesha mchango huo kama kutoka kwa Jumuiya ya Watanzania UK. Ni kwa vile kama mratibu, niliweka wazi kuwa suala hili la msiba na rambirambi halihusiani na itikadi za vyama.
3. Cris Lukosi hakukubaliana na utaratibu huo na kunitaka niwakilishe mchango wao kwa Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na uwakilishwe kwa mjane wa marehemu Mwangosi kama mchango kutoka kwa WanaChadema UK. Nilifanya kama alivyotaka Lukosi ( Ushahidi ni kiambatanisho hapo chini).
Hitimisho: Ukweli wangu ndio huo. Hakuna hata senti moja ya rambirambi kwa mjane wa marehemu Mwangosi iliyopotea mikononi mwangu. Na chini hapo ni risiti ya CRDB ikionyesha fedha zote zilizochangwa na nilizoziingiza kwenye akaunti ya Itika Mwangosi, mjane wa marehemu Mwangosi. Ushahidi wa majina ya waliochangia na kiasi walichochanga pia upo.
Nimeyaweka haya hadharani kwa nia njema ili kuzuia upotoshaji na hali ya kuchafuana majina kama ningeamua kubaki kimya.
Nawashukuru nyote mnaoendelea kuniamini hata mnaposikia yenye kuzushwa juu yangu.
Wenu Katika Ujenzi wa Nchi Yetu.
Maggid Mjengwa.
Iringa.
0754 678 252
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment