Monday, 2 December 2013

Re: [wanabidii] Tusimuhukumu Zitto kwa Ukigoma

Sidhani kama Zitto amewajibishwa kwa sababu ya ukigoma je akina Mkumbo, Shonza na wengineo ndani ya kundi hilo ni wa Kigoma? Sijaona au kusikia popote ambapo CDM wametoa hoja ya ukigoma. Unataka kila anachotaka au kusema mtu toka Kigoma kikubaliwe kwa sababu tu katoka kigoma mkoa wenye historia? Kila mkoa una historia bwana, tuwaze kitaifa zaidi kuliko kikanda au kikabila. Ebu tafuteni hoja nyingine hii ya ukabila tumekwishaikataa. CDM ipo maeneo yote ya nchi hivyo sidhani kama makabila yote yamekubali kuburuzwa na kabila moja. CDM imeisha kuwa na sura ya kitaifa mwenye mawazo ya ukabila haoni mbali. Hatushangai kwamba mti wenye matunda mazuri ndo upigwa mawe. Mbona hamtwambii yanayojili TLP, CCM na kwingineko?

2013/12/3 <haha12@poczta.fm>
Watu wa Kigoma wamekuwa wakionewa kuanzia enzi za utawala wa hayati Mwl. Nyerere ambaye alionekana kuwaogopa watu wa kule kutokana na ujasiri wao wa ukweli. Watu wengi huwachukulia watu wa Kigoma ni wabishi, wajeuri n.k....... Ukweli ni kwamba, ni watu ambao walikuwa upeo mkubwa kimawazo kwani ni moja ya sehemu ya zamani sana kihistoria ukilinganisha na miji mingine nchini Tanzania ambayo hii leo ni maarufu. Mkusanyiko wa kutoka sehemu mbali mbali kabla na wakati wa biashari ulikuwa kiini cha civilization ya sehemu. Kiswahili kimeongelewa na watu wa Kigoma kwa zaidi ya karne. Pamoja na kwamba serikali za awamu hazikupeleka Kigoma changamoto za kimaendeleo kama shule za sekondari na hata viwanda vidogo dogo, watu wa Kigoma wamekuwa waki struggle kuendesha maisha . Mazingira ya mkoa wa Kigoma ni mazuri sana ukilinganisha na mkoa kama wa Mwanza ambao hauna historia yoyote, lakini leo angalia maendeleo ya mikoa hii miwili, utaona tofauti kubwa sana. Maendeleo ya baadhi ya mikoa haikujileta yenyewe, bali kwa misaada ya serikali. Projects nyingi zilikuwa zinapelekwa kwenye baadhi ya mikowa ambayo walikuwa na mawaziri. Hiyo kasumba bado ipo kwa baadhi ya watu, kwamba wasikiapo au waonavyo mtu anayetoka katika maeneo yanoyo kandamizwa wanajisikia vibaya kwani mtoto wa mbuzi anapaswa wakati wote afungwe kamba shingoni. Iwapo wafuasi na viongozi wa Chadema wanataka mabadiliko nchini ni lazima kasumba zote wazitupilie mbali. Kinachotakiwa ni uwezo ilkufanyikisha malengo mnayoyaweka na sio kuangalia huyu MWACHAMA ni mtu wa wapi. Watu wa Kigoma wamukuwa na imani sana na Chadema wakiamini kutakuwa na mabadliko ambayo kwa muda mrefu yanatakiwa nchini, leo mnawaona sio muhimu, kwani hawapasi kutawala kama ilivyokuwa enzi awali. Eliofo, waziri wa elimu wa baraza la kwanza la Tanganyika aliwezesha KiliMANJARO kuwa na shule za sekondari nyingi sana  mkoani huko, kitu ambacho kiliwezesha watoto wengi wa mkoa hou kupata elimu ya sekondari na baadae kuendelea na elimu za juu na kuwa watawala katika nafasi mbalimbali. Pesa zilitumika zilikuwa za umma na mashirika mengine ya kidini yalipelekwa huko badala sehemu zingine ambako pia watoto walihitaji kupata elimu. Hayo yote yanafahamika. Leo kinachotakiwa ni kujenga nchi ya kisasa bila kutafuta tofauti tofauti za kijinga na kutupa mbali superiority complex. Hakuna CHASAKA kwenye chama ambacho wafuasi wake ni wananchi wanaotoka katika kila kona ya nchi.

Mtanganyika

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment