Sunday 1 December 2013

RE: [wanabidii] Taarifa ya kusainiwa kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki

Selly,
Hawajaliona hili lakini sio vibaya kuendelea kuwakumbusha kwa kuwa kiswahili sahihi cheo cha Premi kilitakiwa kiandikwe kama ifuatavyo:  "Mwandishi Msaidizi wa habari wa Rais" na Sio " Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi". Kujisahihisha hakuna maana hujui kwani kiswahili ni lugha nayo sio rahisi sana kwa wengine.  Kama sisi tunakosea basi tunaomba tusahihishwe ili tuelewe.

Ahsante

Herment A. Mrema

Date: Sun, 1 Dec 2013 19:40:25 +0800
Subject: Re: [wanabidii] Taarifa ya kusainiwa kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki
From: sellyserera@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Hivi huyu Premi bado tu hajashauriwa namna anavyoandika Cheo chake? Mbona anatia aibu kwa taaluma yake, walio karibu na "taasisi" walione hili la "Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi"!

On Dec 1, 2013 6:55 PM, "Abdalah Hamis" <hamisznz@gmail.com> wrote:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo kwa pamoja wametia  saini itifaki ya Umoja wa Fedha  wa Afrika Mashariki, (The East African Monetary Union) katika hoteli ya Speke, Munyonyo  mjini Kampala.

Marais waliotia saini itifaki kwa niaba ya wananchi wao ni Jakaya  Mrisho Kikwete wa Tanzania, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda .

Mara baada ya utiwaji wa saini, itifaki ya Umoja wa Fedha itapelekwa Kwenye mabunge ya nchi wanachama kwa ajili ya 
kuridhia ifikapo Mwezi Julai mwaka 2014.

Utiaji wa saini huu unaanzisha mchakato wa kuelekea kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kikao cha viongozi pia kilishuhudia Rais Kenyatta akichukua Uenyekiti wa Jumuiya kutoka kwa Rais Museveni na kuelezea matarajio yake ya Jumuiya kukua zaidi na kuzitaka nchi wanachama kuelimisha zaidi wananchi wa Afrika Mashariki kuhusu faida za Ushirikiano huu.

Itifaki ya Umoja wa Fedha ni ya tatu baada ya itifaki ya Umoja wa Ushuru wa Forodha na itifaki ya soko la pamoja na hatimaye kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.

Katika mkutano wa Leo, mbele ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwanafunzi Peter Robert kutoka shule ya sekondari Tushikamane, Morogoro amepokea cheti na zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka mshindi wa shindano la kuandika Insha inayohusu EAC.

Mara baada ya kikao,,Rais Kikwete amerejea jijini Mwanza kuendeleza na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu ambapo kesho tarehe 1, ataendelea na ziara katika Wilaya ya Busega.

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Kampala, Uganda
30 Nov 2013

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment