Sunday, 1 December 2013

RE: [wanabidii] Sera Ya Gesi

Mr. Maro

Samahani sana sio kuwa sikubalini na uliyosema lakini nilichotaka kuuliza ni JE SERA HII YA GESI INAWASHIRIKISHA WANANCHI WAZALENDO KUANZIA UTAFUTAJI, UCHIMBAJI, USAFIRISHAJI, UHIFADHI NA UUZAJI WA JUMLA?.

Nisingependa mtaji ukuwa ni tatizo kwani tuna uwezo wa kukusanya mitaji kutoka kwa watanzania hata kwa kuandikisha kampuni kwa ajili hiyo na tukauza hisa kwa Watanzania. Ninaamini kuna watanzania watakuwa tayari kununua hisa na wakasubiri miaka 5 kabla ya kupata gawio na wakaridhika. Tungependa kuwa wabia kwenye kampuni hizi za wageni

Kinachotakiwa ni Sera ambayo itawapa fursa sawa watanzania na wageni kama hatutaki ubaguzi.

Ahsante

Mrema

Date: Sat, 30 Nov 2013 07:37:53 -0800
Subject: Re: [wanabidii] Sera Ya Gesi
From: oldmoshi@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Ndugu Mrema ,

Nilikuwa maeneo ya kusini mwa Tanzania haswa maeneo ambayo bomba la gesi litapita au kutakapokuwa na shuguli haswa za mambo ya gesi .

Nimefurahishwa kuona jinsi wananchi wanavyoshirikishwa japo kwa kiwango kidogo ila tunazidi kusonga mbele tutafika kidogo kidogo , haya mambo tusiharakishe sana , twendeni taratibu ili mradi ni wananchi wanaofaidika zaidi maana kwenye biashara nzima ya mambo ya gesi unahitajika utaalamu ambao sisi hatuna tunatakiwa kwenda kusomesha watu wetu kitu kitakachochukuwa miaka kadhaa , tujenge miundo mbinu ambayo ndio inajengwa sasa kama mahoteli , mabarabara , shule , hospitali na huduma nyingine mbalimbali ambazo sasa hivi zinajengwa ingawa kidogo kidogo ile hali ya vurugu ilichangia kutisha watu .

Mimi ninachosema kila mtanzania anafursa ya kushiriki kwenye hili suala la gesi kama kuna madaktari wataweza kwenda kutoa huduma za kitabibu , kwa wakulima walime chakula kizuri na cha ubora watauza kwenye maviwanda na mahoteli yatakayojengwa , kwa watu wa IT kama sisi tufungue kampuni na kwenda kupata mafunzo zaidi yanayohusiana na gesi , kwa walimu vile vile watafundisha kila mtu atatumia utaalamu wake kulingana na kile alichojifunza au anachojua .

2013/11/29 Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
Ndugu Wanabidii,

Nimemsoma Reginald Mengi akisemea kupitia gazeti la Mwananchi la leo kuhusu sera ya Gesi. Mimi binafsi ninakiri kuwa anachosema kuhusu ushirikishwaji wa wananchi kina maana. Je Sera ya Gesi iliyozinduliwa hivi karibuni ina manufaa kwa Wazalendo kama ndio kwa vipi kama sivyo kwa vipi? Je tunahitaji Sera mbadala ambayo itaeleza bayana kwamba wananchi watashiriki kwenye shughuli za gesi kuanzia utafutaji, na uchimbaji, usafirishaji, uhifadhi na uuzaji jumla?

Naomba michango yenu ili tuweze kujenga hoja kwa Serikali yetu ambayo tunaamini ni sikivu.

Ahsante

Herment A. Mrema

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment