Sunday, 1 September 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Nashauri, Media Yetu Iache Kupiga Ngoma Ya Vita...!

Ndg Majid hakuna atakayemsikiliza JK kwa sababu yeye hataui migogoro yake ya ndani kwa mfumo wa masikilizano. Hii ina maana anatoa ushauri asiouamini

CHARITY BEGIN AT HOME


______________________________________________
Real Change for Real Development,  

Lemburis Kivuyo
+255654650100Website: www.kivuyo.com,  
Unlimited Webhosting at TZS. 10,000/-/Month - www.webstar5.net


2013/9/1 Augustine Rukoma <rukomapekee@gmail.com>
Maggid, acha mambo ya wakoloni weupe walisha ondoka, hawa weusi
wanaotaka kuchukua nafasi yao hatukubali ni kuwadunda tu hakuna
mazungumzo nao. Ujanja utamalizwa kwa mtutu si maongezi ya kihuni.
Subiri wa kusema hongera urudi, tumechoka na utemi wa kagame na m7
sasa ni mmoja baada ya mwingine mpaka waishe na vibarakawao

On 9/1/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ona hapa moto wa Wahutu na Watusi ulivyoanza kwa jambo dogo sana...
>
> Fires on the Hills;
> -Good morning Sub-chief, how are you?
> - Thank you! The mass was beautiful and the sermon digestible,
> don't you think so?
> - You are becoming very important sub-chief?
> People talk a lot about you these days.
> - Are you reproaching me something? ( Antoine Lema, Africa Divided, page
> 37.)
>
> Ndugu zangu,
>
> Goma ya DRC imekuwa Kosovo ya Ukanda Wa Maziwa Makuu. Naziona ishara za
> janga kubwa linalonyemelea nchi zetu hizi.
>
> Naam, Congo imekuwa Balkan yetu, na Goma ni kama Kosovo. Moto wa vita vya
> Balkan kule Ulaya ulianzia Kosovo.
>
> Na Afrika moto ukiwaka nyumba ya jirani wahi kushiriki kuuzima, maana, moto
> unaowaka kwenye nyumba moja unaweza kusambaa ukazifikia nyumba za jirani.
> Na ukiendelea kupuuziwa, basi, kijiji kizima chaweza kuteketea.
>
> Lililo la muhimu ni kutanguliza hekima na busara. Nimefuatilia kwa karibu
> kuona jinsi media yetu inavyoripoti kinachotokea DRC Congo. Mathalan,
> magazeti kadhaa ya siku ya leo yamefanya kazi ya kupiga ' ngoma ya vita'.
> Imefika mahali hata kuonyesha kuwa ni ' Vita Vyetu'. Na kwamba tunaelekea
> kupata ushindi mkubwa.
>
> Nimependa analysis za Jarida la ' The East African' ( Agosti 31- Septemba
> 6)  Na mtu makini akizisoma analysis zile akazimaliza, basi, kamwe hawezi
> akachukua ngoma ya vita kuanza kuipiga. Kuna hatari kubwa inakuja mbele
> yetu.
>
> Nalo Jarida la ' The Guardian' la hapa limefanya analysis ya kina na ya
> kurasa nyingi kuhusiana na chimbuko la mgogoro wa DRC- Congo. Bahati mbaya,
> nalo pia limeshindwa ku-link tatizo lililopo na wakoloni walioasisi
> mgawanyiko na chuki miongoni mwa watu wa DRC Congo. Kimsingi  M23 ni sehemu
> ndogo tu ya tatizo kubwa la Congo.
>
> Bahati mbaya DRC Congo inaangaliwa zaidi kwa kuanzia na alipoondolewa
> Mobutu.  Tunasahau, kuwa Wakoloni wa Kibelgiji walifanikiwa sana kuwagawa
> WaCongo. Ikafika mahali Jimbo la Katanga likajitenga na kuunda Taifa lao.
>
> Baada ya Wabelgiji kuwapa Wacongo Uhuru wao 1960, wakafanya hila kuwapa
> nguvu Waalunda na Wabayeke wa Katanga waunde taifa lao. Na huko ndiko
> kwenye utajiri mkubwa wa madini ya Congo.
>
> Moise Tshombe akajitangaza kuwa Rais wa Taifa la Katanga, Makao Makuu yake
> ni Lubumbashi. Na katika kufanya hivyo, Wabelgiji wakawatenga tena Wabaluba
> wasiwe sehemu ya mamlaka ya Katanga. Wabaluba wako kaskazini ya Katanga
> kuelekea majimbo ya Kasai na Kivu ambapo Gomba ndipo Makao Makuu ya majimbo
> hayo.
>
> Ikafika mahali, Moise Tshombe alipiga marufuku ndege ya Rais wa Congo Huru,
> Joseph Kasavubu na Waziri Mkuu wake Patrick Lumumba isitue kwenye uwanja wa
> ndege wa Lubumbashi. Tshombe alijazwa kiburi na Wabelgiji. Na uhasama wa
> Wabaluba wa Kaskazini na Waalunda wa kusini ukaendelea. Hata hii leo, bado
> kuna mabaki ya mgogoro huu wa tangu mwaka 1960!
>
> Na hakika, DRC Congo ni mtihani kwa viongozi wa mataifa yetu haya
> yanayozunguka Maziwa Makuu.
>
> Siamini kuwa suluhisho la mgogoro wa DRC Congo litapatikana kwa njia ya
> VITA. Naamini katika njia ya siasa, hivyo basi MAZUNGUMZO.
>
> Na Rais wetu, Jakaya Kikwete  aendelee kusimamia kauli yake, kuwa wahusika
> kwenye mgogoro huu wafanye mazungumzo ya kutafuta suluhu.
>
> Kama nchi, tufanye yote yanayowezekana kuiepusha nchi yetu kuingia kwenye '
> Vita vya kiwendawazimu' na majirani zetu. Na media hapa ina mchango mkubwa.
> Iache kupiga ngoma za vita.
>
> Vita si ngoma ya Lelemama. Vita  ni kitu kibaya sana hususan kwa nchi zetu
> hizi masikini.
>
> Leo tunaona picha za magazetini za wanajeshi wenye kutembea na silaha.
> Tujiandae pia kuona picha za raia wasio na hatia kwa maelfu wakiyahama
> makazi yao. Wengi wao ni akina mama na watoto migongoni.
>
> Mbali ya raia kuawa, vita huzaa wakimbizi pia. Vita hupelekea akina mama
> kubakwa mchana wa jua kali. Hivyo, vita huendana na uvunjwaji wa haki za
> kibinadamu. Vita husimamisha shughuli za kiuchumi. Ni mambo mabaya sana.
>
> Na Chifu  kwenye mazungumzo ya hapo juu kabisa alijibu nini baada ya
> kukasirishwa?
>
> Chifu alikuwa Mtutsi. Alirusha konde kwa Mboyumutwa ( Mhutu). Naye
> akalikwepa konde lile. Akakimbia. Tukio hili tunasoma kwenye vitabu, kuwa
> ndilo liliashiria mwanzo wa mgogoro wa kitabaka kati ya Watutsi na Wahutu.
>
> Maana, wakati akikimbia, Mboyumutwa njiani alikutana na watu wa kabila
> lake. Nao walijawa na wasiwasi. Walishaarifiwa kilichotokea. Siku
> iliyofuatia, Wahutu wakaandama katika kitongoji cha Gitarama.
>
> Inaandikwa, kuwa shambulizi lile alilofanyiwa Mboyumutwa, kiongozi
> mashuhuri wa Wahutu, ndilo likawa cheche iliyowasha moto mkubwa wa uhasama,
> kati ya Watutsi na Wahutu. ( Antoine Lema, Africa Divided)
> Mchango mdogo kwa kidogo nilichojitahidi kukifahamu..
>
> Maggid,
> Iringa
> http://mjengwablog.com
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
>  http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
> Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.

TEMBELEA Facebook yetu:
 http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl

For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment