Monday, 30 September 2013

Re: [wanabidii] Neno Fupi La Usiku; Shaaban Robert Na Wasadikika...

Mjengwa,
Busara ya Babu yetu Shaaban Robert uliyonukuu inajidhihirisha kwa vitendo sasa. Eti baada ya shambulio la Alshabaab Nairobi, sasa askari wanafanya ukaguzi unaodaiwa kuwa kina katika viwanja vya mpira, tena katika geti lenye washaabiki wengi tu. wengine wakiwemo na wenye magari wanaachwa tu! Kwa mtazamo wangu hii ni hatua muhimu, lakini ni sawa na kutafuta bakora (wala siyo fimbo) kumtishia nyoka asiyekuwepo eneo la tukio kabisa.
 
jmakongo
 
----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, September 30, 2013 10:22 PM
Subject: [wanabidii] Neno Fupi La Usiku; Shaaban Robert Na Wasadikika...



Shaaban Robert anaandika; " Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka. Ni kwa matendo yetu mabaya ya zamani.

Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.

Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote."- Shaaban Bin Robert.

Maggid.
Iringa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment