Jambo la Kwanza ndugu zanguni, ni lazima tufungue macho tuone WaAfrica
wametoka wapi na wanaelekea wapi. Lapili ni, Historia ni somo la kwanza
katika kipimo cha kupanua fikira, ili kila mtu aweze kupanua akili na maarifa
vile ataweza kuhudumia ujira za mbeleni kwa hali ya mafanikio. Ujira katika
Historia ni la kisomi kwa kipimo, kwamba, ikiwa vilitendeka hivyo, inabidi hivi
sasa, iwe je ili WaAfrica wa songe mbele. Jambo la muhimu ni kwamba, ili
watu wa weze kufanikiwa, ni nini kinaleta mafanikio; na ni nini inalefa maafa
kwa kukosa mali na mazingira mazuri za kimaendeleo.........
Wa Belgiji au wapora mali kutoka nchi za nje ni
vigumu kuingia inchi ya watu na kupora kama si wenye inchi wa Kisiasa
waliwa karibisha kwenye Corruption. Na Corruption ina saidika kwa kuwa
na Democrasia inayo zingatiwa na wanainchi wenyewe kwenye Referendum.
Hapa ndipo mipango ya uongozi bora ina anza. Wanainchi wa Ki-Africa
wana hitaji kisomi na kuimarisha Civil Society iwe kama msingi wa kujitetia
kwa mambo ya Community Welfare ambacho kuna Baraza la Wazee na vijana
kutoka mashule za vijiji waki tetea huduma na mali za Uma. Itakuwa vigumu
kwa wa poraji mali wa Kisiasa kuwa dhulumu wanapo fanya dira za corruption
na wenzao wa inchi za inje.........
Kama hivi sasa, Museveni na Kagame wamepaga ku bomoa Congo na kuuza
mali ya Wa Congo kwa njia isiyo ya halali na kuji faidika na mali ya Wa Congo,
ni vipi utalaumu wazungu hali huku wenye kuwapatia akili ya kuwaibia ni wa
Kagame na Museveni kwa kiroho chao na kwa mpango wa kutumia M23. Kwani
Wazungu walijua M23 wapi.........Na kiroho cha Kagame na Museveni ndio sababu
wanatumia wazungu kuwapa mali kwa kuwatishia na kuterorize wa Congo kwa
fujo na vifo.
Watu wakichunguza pale penye shida, ni hilo shida ndilo lazima iweze kutatuliwa
kwa njia ya usawa na siyo kuota ndoto na kudhania kungoja mafanikio kwa kukaa
chini la mti itasaidia. Ndio vile Kikwete amamua kutenda jambo la busara, kwa
kukataa uwizi wa mali ya uma, kuiba mashamba na kuunganisha EAC ikiwa hakuna
makubaliano ya Ki-Democrasia ya kisawa iliyo kabidhiwa na wanainchi wenyewe..
Fungueni macho...........alie zubaa ndie aliwae na mali yake iki poromoshwa......
Basi, Museveni na Kagame wanaona watu wa East Africa kama wamezubaa wana
lala..........wanajiona kama kwamba wao ndio walio amka............Lakini, jambo
la umuhimu ni kwamba, WaAfrica wakizidi kulala, mali ya Uma na mashamba yao
yote itaporwa, watabaki hoye-haye bila pakukamatia, watazidiwa na kufanywa
WATUMWA kwenyi nchi yao wenyewe, na wengi watabaki maskini waliokosa mbele
wala nyuma.......na watabaki na maisha ya dhiki bila mafanikio wakati dunia ina
songa mbele........
Mwana mme goigoi hata bibiyake aki nyanganywa na mume mwingine na kulazwa
kwenye kitanda kimoja, hataona haja wala kosa lolote.........Ndiyo sinema ya
Ki-Africa inayo fanyika sasa hivi kwenye trailer ya mambo yanazo endeshwa na Kagame na Museveni na wenzio wezi wa kinyama..........
Judy Miriga
Diaspora Spokesperson
Executive Director
Confederation Council Foundation for Africa Inc.,
USA
http://socioeconomicforum50.blogspot.com
Diaspora Spokesperson
Executive Director
Confederation Council Foundation for Africa Inc.,
USA
http://socioeconomicforum50.blogspot.com
From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, September 1, 2013 2:23 PM
Subject: [Mabadiliko] Nashauri, Media Yetu Iache Kupiga Ngoma Ya Vita...!
To: mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Sunday, September 1, 2013 2:23 PM
Subject: [Mabadiliko] Nashauri, Media Yetu Iache Kupiga Ngoma Ya Vita...!
Ona hapa moto wa Wahutu na Watusi ulivyoanza kwa jambo dogo sana...
Fires on the Hills;
-Good morning Sub-chief, how are you?
- Thank you! The mass was beautiful and the sermon digestible,
don't you think so?
- You are becoming very important sub-chief?
People talk a lot about you these days.
- Are you reproaching me something? ( Antoine Lema, Africa Divided, page 37.)
Ndugu zangu,
Goma ya DRC imekuwa Kosovo ya Ukanda Wa Maziwa Makuu. Naziona ishara za janga kubwa linalonyemelea nchi zetu hizi.
Naam, Congo imekuwa Balkan yetu, na Goma ni kama Kosovo. Moto wa vita vya Balkan kule Ulaya ulianzia Kosovo.
Na Afrika moto ukiwaka nyumba ya jirani wahi kushiriki kuuzima, maana, moto unaowaka kwenye nyumba moja unaweza kusambaa ukazifikia nyumba za jirani. Na ukiendelea kupuuziwa, basi, kijiji kizima chaweza kuteketea.
Lililo la muhimu ni kutanguliza hekima na busara. Nimefuatilia kwa karibu kuona jinsi media yetu inavyoripoti kinachotokea DRC Congo. Mathalan, magazeti kadhaa ya siku ya leo yamefanya kazi ya kupiga ' ngoma ya vita'. Imefika mahali hata kuonyesha kuwa ni ' Vita Vyetu'. Na kwamba tunaelekea kupata ushindi mkubwa.
Nimependa analysis za Jarida la ' The East African' ( Agosti 31- Septemba 6) Na mtu makini akizisoma analysis zile akazimaliza, basi, kamwe hawezi akachukua ngoma ya vita kuanza kuipiga. Kuna hatari kubwa inakuja mbele yetu.
Nalo Jarida la ' The Guardian' la hapa limefanya analysis ya kina na ya kurasa nyingi kuhusiana na chimbuko la mgogoro wa DRC- Congo. Bahati mbaya, nalo pia limeshindwa ku-link tatizo lililopo na wakoloni walioasisi mgawanyiko na chuki miongoni mwa watu wa DRC Congo. Kimsingi M23 ni sehemu ndogo tu ya tatizo kubwa la Congo.
Bahati mbaya DRC Congo inaangaliwa zaidi kwa kuanzia na alipoondolewa Mobutu. Tunasahau, kuwa Wakoloni wa Kibelgiji walifanikiwa sana kuwagawa WaCongo. Ikafika mahali Jimbo la Katanga likajitenga na kuunda Taifa lao.
Baada ya Wabelgiji kuwapa Wacongo Uhuru wao 1960, wakafanya hila kuwapa nguvu Waalunda na Wabayeke wa Katanga waunde taifa lao. Na huko ndiko kwenye utajiri mkubwa wa madini ya Congo.
Moise Tshombe akajitangaza kuwa Rais wa Taifa la Katanga, Makao Makuu yake ni Lubumbashi. Na katika kufanya hivyo, Wabelgiji wakawatenga tena Wabaluba wasiwe sehemu ya mamlaka ya Katanga. Wabaluba wako kaskazini ya Katanga kuelekea majimbo ya Kasai na Kivu ambapo Gomba ndipo Makao Makuu ya majimbo hayo.
Ikafika mahali, Moise Tshombe alipiga marufuku ndege ya Rais wa Congo Huru, Joseph Kasavubu na Waziri Mkuu wake Patrick Lumumba isitue kwenye uwanja wa ndege wa Lubumbashi. Tshombe alijazwa kiburi na Wabelgiji. Na uhasama wa Wabaluba wa Kaskazini na Waalunda wa kusini ukaendelea. Hata hii leo, bado kuna mabaki ya mgogoro huu wa tangu mwaka 1960!
Na hakika, DRC Congo ni mtihani kwa viongozi wa mataifa yetu haya yanayozunguka Maziwa Makuu.
Siamini kuwa suluhisho la mgogoro wa DRC Congo litapatikana kwa njia ya VITA. Naamini katika njia ya siasa, hivyo basi MAZUNGUMZO.
Na Rais wetu, Jakaya Kikwete aendelee kusimamia kauli yake, kuwa wahusika kwenye mgogoro huu wafanye mazungumzo ya kutafuta suluhu.
Kama nchi, tufanye yote yanayowezekana kuiepusha nchi yetu kuingia kwenye ' Vita vya kiwendawazimu' na majirani zetu. Na media hapa ina mchango mkubwa. Iache kupiga ngoma za vita.
Vita si ngoma ya Lelemama. Vita ni kitu kibaya sana hususan kwa nchi zetu hizi masikini.
Leo tunaona picha za magazetini za wanajeshi wenye kutembea na silaha. Tujiandae pia kuona picha za raia wasio na hatia kwa maelfu wakiyahama makazi yao. Wengi wao ni akina mama na watoto migongoni.
Mbali ya raia kuawa, vita huzaa wakimbizi pia. Vita hupelekea akina mama kubakwa mchana wa jua kali. Hivyo, vita huendana na uvunjwaji wa haki za kibinadamu. Vita husimamisha shughuli za kiuchumi. Ni mambo mabaya sana.
Na Chifu kwenye mazungumzo ya hapo juu kabisa alijibu nini baada ya kukasirishwa?
Chifu alikuwa Mtutsi. Alirusha konde kwa Mboyumutwa ( Mhutu). Naye akalikwepa konde lile. Akakimbia. Tukio hili tunasoma kwenye vitabu, kuwa ndilo liliashiria mwanzo wa mgogoro wa kitabaka kati ya Watutsi na Wahutu.
Maana, wakati akikimbia, Mboyumutwa njiani alikutana na watu wa kabila lake. Nao walijawa na wasiwasi. Walishaarifiwa kilichotokea. Siku iliyofuatia, Wahutu wakaandama katika kitongoji cha Gitarama.
Inaandikwa, kuwa shambulizi lile alilofanyiwa Mboyumutwa, kiongozi mashuhuri wa Wahutu, ndilo likawa cheche iliyowasha moto mkubwa wa uhasama, kati ya Watutsi na Wahutu. ( Antoine Lema, Africa Divided)
Mchango mdogo kwa kidogo nilichojitahidi kukifahamu..
Maggid,
Iringa
0 comments:
Post a Comment