Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuuelezea na kuwajulisha wananchi na Jumuiya ya Kimataifa kuwa hakiitambui na hakina mnasaba na Kamati ya Maridhiano inayodai kuwa ina uwakilishi wa wajumbe toka vyama vya CCM na CUF hapa Zanzibar.
Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Zanzibar Idara ya Itikadi na Uenezi Waride Bakari Jabu (MB) amesema CCM ina utaratibu na kanuni zake za kuunda kamati na si kuundiwa au kusemewa na kundi lolote.
Inapotokea haja ya kuunda kamati kama yeyote , wajumbe wake hutokana na maazimio ya vikao halali vya kikatiba na si kukurupuka kama ifanyavyo Kamati inayojiita ya Maridhiano chini ya Mwenyekiti wake Hassan Nassor Moyo.
Chama Cha Mapinduzi kinaitambua Kamati ya Moyo kuwa ni Kamati ya mvurugano yenye malengo na

madhumuni binafsi kwa tamaa na kukamilisha haja na matakwa yao.
Kamati ya Maridhiano ya inayoongozwa na Moyo haitambuliwi na Kamati Malum ya NEC Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM na wala Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).
Kitendo chochote cha Kamati hiyo kulihusisha jina la Chama Cha Mapinduzi kihesabiwe na wananchi kuwa ni utapitapi, chokochoko na ukorofi wa kisiasa.
Ni vyema toka sasa wajumbe wanaojiita ni wawakilishi wa CCM katika kamati hiyo wakaeleza wamepata wapi ruhusa au wametumwa na kiongozi gani wa juu wa CCM ili kushiriki kwenye kamati hiyo.
CCM haijamtuma mjumbe yeyote kushiriki kwenye kamati hiyo na kwamba wajumbe hao wamejipeleka wenyewe ili kuwapotosha na kuwaisha wananchi kwa manufaa yao.
Mwisho CCM inawajuulisha Wazanzibari na Watanzania kwa jumla kuwa haihusiki kabisa na Kamati ya maridhiano inayovishirikisha vyama vya CCM na CUF hapa Zanzibar.
"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Waride Bakari Jabu (MB)
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Chama Cha Mapinduzi,
ZANZIBAR.

Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment