Thursday 29 November 2012

[wanabidii] Re: SEREKALI YA CCM INATAKA KUWAFUNGA MIDOMO WATANZANIA

Serekali ya Tanzania pamoja na kutaka kuingia kwenye mtandao wa DIGITAL na kutoka kwenye ANALOG lakini nimekuja kugundua kuwa wanafanya njama na TCRA ili kuwafunge midomo Watanzania ili wasione haya matangazo ya Television kwa aijili ya uchaguzi 2015. CCM na Serekali yake inatia aibu sana. Baada ya kuboronga kwenye utawala wake sasa inajaribu kila njia Watanzania wasione matangazo ya Kampeni za vyama vya Siasa (CCM wanaviita vya upinzani) Tanzania vinavyotaka kumkomboa Mtanzania.

 

CCM imeshaona kuwa vyama vya upinzani vinapata nguvu kwa kupita kila mahali kuwaelezea Watanzania mambo wanayofanyiwa, hivyo huo ndio ujanja waliouona wautumie kwa kuwa wanajua Watanzania wengi hawataweza kununua vingamuzi na pengine kushindwa kulipia malipo ya kila mwezi. Huu ni ufisadi wa hali ya juu na Watanzania mnatakiwa mlijue hilo na kuhakikisha mnalipinga kwa hali na mali labda wakubali na channel zingine nazo ziwe bure kama Star TV, ITV Channel 10, nk. Kwa nini Channel ya bure kwenye matangazo haya iwe ni TBC peke yake. Hii inatia mashaka kwani TBC imekuwa ikitoa matangazo yake kwa kulenga zaidi chama tawala cha CCM. Janja yenu nyie CCM na TCRA tumeigundua. Hatukatai Watanzania kwenda na wakati lakini kama hamna nia mbaya basi hata channel za watu binafsi ziwe bure. Alafu wacha nichomekee swala la pesa. Ondoone mapesa yenu ya kifisadi kwenye mzunguko wa pesa. Tunataka kutumia fedha zetu za zamani. Hizi sio fedha ni kero.

Mkereketwa,

Lengai Ole Letipipi

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment