Wednesday, 28 November 2012

Re: [wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM

Sasa hapa Dr kafumu kaongea kama Gaddafi aliposema kuwa waandamanaji walikuwa panya na Mende na walileshwa na bangi za marekani
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: Peter Kafumu <kafumu@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wed, 28 Nov 2012 21:44:23 +0300
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM

Ri hard hayo ndiyo madhara ya kushupalia m4c inayohamasishwa na mabeberu, bila kuona mbele, kila aina ya sababu fitinishi hutolewa juu ya utawala uliopo kumbe ni ukoloni mamboleo unaolenga kupata nafasi ya kuchuma mali za mataifa machanga. Tujiangalie watanzania na demokrasia hii fitishi ya kimagharibi.

Wasalaam...

Ngw'izukulushilinde

On 28 Nov 2012, at 15:51, RICHARD MGAMBA <rmgamba2000@yahoo.com> wrote:

Mike,
Nadhani wamisri ni vichaa fulani. Hivi Muslim brotherhood waliwahi kuipima wapi kwamba ikinyakua madaraka haita kuwa corrupted na power? Leo Rais ameingia tu amefuata yale yale ya aliyekuwepo kawa stooge wa marekani sasa kelele yote ya mwaka jana ilikuwa nini?
 
Tunisia mpaka leo mkate bado ni taabu mitaani, lakini angalalu kumetulia. Libya ni shida tupu hakuna mwelekeo sahihi, na sasa Misri iko njia panda, Syria iko kitanzini, hatari tupu.

From: Mike Zunzu <mikezunzu@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, November 28, 2012 10:21 AM
Subject: Re: [wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM

Tusiwaone Wamisri ni wenda wazimu, hapana, inawezekana njia wanayotumia siyo sahihi, maana matokeo yake kuna watu wanapoteza maisha yao.
Lakini kisa hasa ni viongozi kumiliki sheria na kuwa ni mali yao, swala lamagari ya umma kutumika kwa manufaa ya chama tawala si jambo geni, vyama vya upinzani vimepiga kelele weee! "Inakuwa sawa na methali ya kelele za kuku hazimdhuru mwewe." Hata kulikuwa na tukio huko Mbeya vijana kumsahambulia kwa mawe msafara wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani siku Mh Vuai, kisa ni vijana kuchukizwa na kitendo cha kutumia magari ya umma kwa manufaa ya chama, kisingizio eti wana kofia mbili.
Ukweli ni kwamba wenzetu wako juu ya sheria na sheria inaweza ikapindishwa kwa namna yoyote ile ili kukidhi matakwa ya viongozi wetu.
Swala lakutumia muda wa umma ni kina Fredrick na wengine ndiyo wanaodhani muda unatumiwa visivyo, kwa wenzetu ndiyo muda mwafaka wa kuboresha shughuli za chama, muda ya kutafuta maendeleo ya wananchi inabidsi utafutwe kama kutakuwa na ulazima. 

From: Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: mabadiliko Tanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 28 November 2012, 6:45
Subject: RE: [wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM

Hata mimi nakubaliana na Fredrick. Wanapokuwa katika ziara hizo ni kazi ngapi ambazo zinalala Wizarani? mafail na mambo mengi yanakuwa yanasubiri baraka za Waziri, hivyo wanachelewesha mambo kwa kiasi kikubwa. Hili ni tatizo la mifumo yetu, sheria zetu na taratibu zetu. Tumeshindwa kabisa kuwa na mfumo ambao unatenganisha shughuli za chama kilichopo madarakani na shughuli za Serikali. Nionavyo mimi, Waziri, Rais, waziri mkuu etc wanatakiwa kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama. Sasa wanapopanda katika majukwaa na kufanya kazi ya chama, je wananchi ambao ni wanachama wa vyama vingine wanakuwa na nafasi gani? Je hawabaguliwi hapa? na jee gharama zao zinalipiwa na nani? Na CCM? magari yao? na madereva ni wa CCM? Nadhani zinalipiwa na walipa kodi wote ambao wana itikadi tofauti, iweje sasa yeye atumie kodi zetu kukijenga chama cha mapinduzi? ambacho wengine hakubaliani na sera zao za chukua chako mapema na tumeona kimeshindwa kazi? kikae pembeni?
 
 Hapa lipo tatizo. Tumeshindwa kuwa na mpaka ulio wazi kati ya shughuli za chama na serikali. Na hili ni hata kwa watumishi wa umma. Tumeshindwa kuwa na watumishi wa umma ambao hawafungamani na chama tawala. Mtumishi wa Umma yupo pale kuwatumikia wananchi, wanatakiwa kubaki kuwa hivyo hata chama gani kikija kutawala wao wanabaki vilevile. Na hata taasisi zetu nyingi sio huru. Tatizo hili ni vizuri tukajaribu kuli-address katika zoezi linaloendelea hivi sasa la mabadiliko ya katiba.
 
Moja ya ndoto yangu kubwa katika zoezi hili ni kuweza kutupatia taasisi huru, watumishi wa serikali huru, kutenganisha shughuli za chama na serikali, tuweze kuwa na mgawanyo wa madaraka mazuri kati ya yale mafiga matatu; Bunge, Mahakama na Dola. Pia tuweze kuongeza utamaduni wa vyombo hivi kuchungana na kudhibitiana, yaani checks and balances. Unaweza kufakinisha mambo haya iwapo tu tutapunguza madaraka makubwa ya Rais na kuangalia muundo wa taasisi na vyombo vyetu kadhaa kama vile Bunge. Sijasikia mjadala katika zoezi la marekebisho ya katiba kuhusu Bunge letu. Ninaamini katika taasisi ambayo ina muundo mbaya, muundo wa kiimla na kidikteta ni Bunge letu. Kwani nionavyo mimi, Spika ana madaraka makubwa ndani ya Bunge. Yeye ni Alfa na Omega. Inabidi tubadilishe muundo huu. Na jee Spika na Naibu Spika wanapokuwa wametoka katika chama cha siasa, tena ni wajumbe wa NEC na kamati kuu, je wanaweza kuendesha shughuli za Bunge bila upendeleo? Je Spika ambaye pia ni mjumbe wa NEC na kamati kuu ni wakati gani anakuwa Spika na ni wakati gani anaacha kuwa mjumbe wa NEC na Kamati kuu? Anawezaje kuvaa kofia hizi mbili bila kuathiri demokrasia na haki ndani ya Bunge?? Haya ni mambo ya kuyajadili kipindi hiki.
 
Vyombo vingine ni kama vileTAKUKURU, TBC1, Magazetui ya Serikali, Jeshi la Polisi, Mahakama na hasa uteusi wa majaji. Katika hili la uteuzi wa majaji, ningependa kuuliza swali moja: Katika siku za hivi karibuni, utasikia mara nyingi sana, Serikali kupitia Mawaziri ikisema kuwa kama mnaona mmeonewa, nendeni mahakamani, ni wepesi sana kuwaambia watu waende mahakamani. Swali langu ni je, kwa nini wakimbilia kuwaambia watu kwenda mahakamani? Je wana uhakika wa kushinda kesi siku zote? iwapo unatambua kuwa Mahkamani kuna kushinda na kushindwa, kwa nini ukimbilie kumwambia mtu kwenda mahakamani?!! kwa nini usishauri njia za mashauriano? Lingine la kuangalia, kwa nini mambo mengi yanapelekwa mahakamani halafu serikali inasema haliwezie kujadiliwa kwa sababu lipo mahakamani? kwa nini zinafunguliwa kesi haraka haraka katika matukioa ambayo yana utata ili kuzuia mijadala? Kwa nini mamlaka zinazohusika zinakubali kufungua haraka haraka ambazo hazina kichwa wala miguu? yule kichaa aliyetangazwa na Kova na aliyekamatwa eti kuhusika na kumtesa Ulimboka ameishia wapi?? 2015 ukisikia Kova anawania Ubunge kupitia chama cha CCM jimbo la Kinondoni, utashangaa?? Je mambo haya yananahitaji akili sana kujua kuwa hatuna taasisi huru?? Ukisema kuwa taasisi zote zinatumikia chama tawala umekosea??? 
 
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na hasa uteuzi wake, nadhani huyu ni vyema akathibitishwa na Bunge, na jee kuna haja ya yeye kuwa Mbunge?
 
Je kuna mantiki gani, kwa mfano, Rais kuteua watendaji wakuu wa mifuko ya jamii?? kama vile NSSF n.k.??!! Kwa nini nafasi hii isiwe ya ushindani wa wazi?? Kwa Rais kumteua Mtendaji mkuu wa NSSF naona ni sawa kabisa na Rais kwa mfano, kumteua Mtendaji Mkuu wa NMB au NBC! Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Tawala anapomteua Mtendaji mkuu wa NSSF, halafu NSSF wakitumia pesa za michango yetu kuikopesha serikali iliyopo madarakani ili ijenge machinga complex na chuo kiuu cha Dodoma, halafu CCM ijitape kuwa imefanya makubwa kwa kujenga chuo kikubwa, je huoni kuwa hapa kuna mfumo mchafu ambao umehalalishwa, umesafishwa na unatumika kuwahadaa wananchi na kuhakikisha kuwa chama kilichopo madarakani kinapata upendeleo wa kuendelea kukaa madarakani. Na hii sio haki kwa vyama vingine na kwa Watanzania wote hasa wale wanaochangia mifuko hiyo. Kwani hawawezi kukopa hata shilingi elfu kumi kutoka katika michango yao!!!!
 
 Je kuna mantiki gani kwa Rais kuteua Wenyekiviti wa bodi mbalimbali?? kama vile TANAPA, Korosho Pamba? Kahawa n.k??!! Kwa nini asichaguliwe na wadau wenyewe miongoni mwao?
 
Je ni kwa kiasi gani Jeshi la polisi ni neutral? tumewahi kushuhudia Makamanda waandamizi baada ya kustaafu wanagombea nafasi za kisiasa kupitia chama tawala!! Je ni lini walichukua kadi za chama tawala? au walikuwa wakifanya kazi za polisi huku wakiwa ni wananchama wa chama tawala? na hivi ni kinyume na sheria!! Tumewahi kuona msajili wa vyama vya siasa baada ya kustaafu akigombea nafasi ya kisiasa kupitia chama tawala!! si hao tu pia wapo Makatibu wakuu, mabalozi, watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali na mashirika ya umma!! Lakini hatujawahi kuona watu wa aina hii wakigombea kupitia chama chochote cha upinzani!!! je ni kwa nini???
 
Njia pekee ya kuleta uwajibikaji ni kupuguza madaraka ya Rais na hasa huu utitiri wa uteuzi ambao hauna kikomo na wala hauwezi kuchungwa wala kudhibitiwa. Matokeo ya uteuzi huu wa utitiri unaleta hulka na tabia mbaya sana ya kila mtu kujipendekeza, kufanya unafiki na fitna kwa minajili ya kusubiri uteuzi. Matokeo yake ni kulindana kukosekana kwa uwajibikaji.
 
Selemani 
 
From: emmbaga@hotmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM
Date: Tue, 27 Nov 2012 18:54:57 +0000

Fredrcik

Umeandika  Ukweli mtupu  ni  juu  ya  Wahusika  kusikia  na  kuufuta  ushauri  huo

Ernest

Date: Tue, 27 Nov 2012 10:24:21 -0800
From: fredrick197958@yahoo.com
Subject: [wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM
To: wanabidii@googlegroups.com

Hivi karibuni baada ya kumalizika mkutano mkuu wa CCM Kanali (mstaafu) Kinana amekuwa akizunguka huku na kule akiambatana na mawaziri kufanya siasa yenye nia ya kuijenga CCM. 
Binafsi sina tatizo na Waziri kama yuko likizo akatumia muda wake wa mapumziko kutumikia chama. Ninashawishika ni kinyume cha taratibu za kazi kutumia rasilimali za umma kama magari, posho za safari kutoka serikalini kwa lengo la kutumikia chama.
Nadhani ni vema kazi ya kujenga chama wakaachiwa waajiriwa wa chama watennde kazi hizo.

Nidhamu na kuheshimu kazi na uweledi ni muhimu sana kwa sasa katika jamii yetu sisi Watanzania. 
Hizo kazi za wizarani nani atafanya kama kila waziri akiwa barabarani kujenga chama?
Napendekeza CCM iweke mfumo wa kuigwa na vyama vingine. Hivi mfanyakazi wa umma wa kada ya chini akiacha kazi zake na akitumia gari ya ofisi na rasilimali zingine kufanya kazi za NGO binafsi kwa mfano, na jambo hilo likafanyika bila makubaliano rasmi na bosi wake ataangaliwa tu aendelee au atawajibishwa?Jibu liko wazi atawajibishwa.
Ifikie mahali mawaziri wawajibike kwa umma kwa kuwa wanalipwa kwa kodi zetu na hawalipwi na CCM

Rai yangu ni kuwataka mawaziri na watumishi wengine wa umma tuwatumikie Watanzania kwa nidhamu na unyenyekevu kwa kuwa si wote wanafurahishwa na porojo za majukwaani. watu wanataka kuona kazi zinafanyika zinazoleta tija katika jamii.

Nawasilisha.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment