Thursday, 29 November 2012

RE: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] MJADALA SASA UMENOGA: Ushahidi mwingine

Tatizo letu huwa nasema kila siku kuwa, ELIMU YETU IMEKUFA - NA HAKUNA DALILI WALA MPANGO WA KWELI WA KUIFUFUA.
 
Mimi niliposoma shahada yangu ya kwanza, pale chuoni tulikuwa na wanafunzi wa lugha tatu tofauti ndani ya shahada hiyo hiyo moja na ukienda maktaba au duka la vitabu unakumbana na hali halisi ya mgawanyo wa vitabu vyote katika makundi matatu kwa mujibu wa lugha.
 
Sisi Tanzania hivi leo hatuna hata wahariri wanaokijua Kiswahili na hata walimu wa Kiswahili ni wa kubahatisha; utamsikia mtu anapondea kuchukua shahada ya Kiswahili wakati Waingereza na Wamarekani wanajazana kwenye shahada za Kiingereza. Ni ulimbukeni na matokeo yake Kenya ina wahitimu wengi zaidi wa Kiswahili kuliko Tanzania, pia sababu moja ikiwa sera zetu za kijinga za kuzuia watu wengi kwenda chuo kikuu wakati wa Nyerere.
 
Ni kweli kabisa kwamba nchi zinazotumia lugha zao zina faida kubwa kwenye uchotaji wa elimu na kuiingiza vichwani lakini pia zina kitu ambacho sisi hatuna; nacho ni elimu bora. Tukishalikamilisha hilo ndipo tutakapoweza kulimudu zoezi la kuhamishia maarifa yote yaliyomo kwenye Kiingereza hivi leo na kuyaweka katika Kiswahili. Lakini kama bado tuna watu wanaoandika "mpango mkakati" au "kikosi kazi" au "katika Tanzania" wakidhani kwamba kuiga muundo wa Kiingereza ni ujanja, basi siku tutakapoamua kukivamia Kiswahili kwa kila ngazi ya elimu hatutakuwa hata na walimu wa kufundisha, achilia mbali vitabu.
 
Kwa kifupi sisi ni mabwege fulani hivi na ndio maana dunia inadhani Kiswahili ni cha Kenya.
 
Matinyi.
 

 

Date: Thu, 29 Nov 2012 07:06:21 -0800
Subject: Re: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] MJADALA SASA UMENOGA: Ushahidi mwingine
From: tmagobe@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Mimi naamini kitu kilichosaidia nchi zinazotumia lugha zao si mijadala ya lugha gani itumike bali ni uwezekezaji katika lugha zao. Hata sisi kitakachotusaidia kukuza Kiswahili si mijadala hata kidogo. Ni utuganji wa vitabu vingi ikiwa ni pamoja na matumizi mazuri ya misemo mbalimbali kama vile nahau, methali nk kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mijadala itaishia tu kusema "Kiingereza ni lugha ya kikoloni" na "Kiswahili ni lugha yetu ya taifa" basi, kitu ambacho hakitatusaidia sana. Naungana na hoja za Dk Kitila kwamba lolote tutakaloamua kufanya tujue lina gharama zake. Vitabu vikisha kuwa vingi na matumizi ya Kiswahili yakiongezeka, lugha itakuwa tu bila hata ya kuipigia debe.


2012/11/29 Aldin Mutembei <mutembei@yahoo.com>
Haya

Ngalieni ushahidi huu mpya, hasa Sayansi. Je, bado mtasema kuhusu sisi.

Imeandikwa na Chipila kwa UDASA kuhusiana na Ripoti ya kuwa UK imekuwa ya 6 katika mchuano wa masuala ya elimu duniani. Angalia wavuti hii, na uangalie maoni ya Chipila hapa chini
> http://uk.lifestyle.yahoo.com/uk-education-comes-sixth-global-league-table-130000692.html

Thursday, November 29, 2012 12:15 PM
Wana-UDASA,
Kuhusiana na ripoti hii, jicho langu limenasa kwenye aya hii:

"For educational attainment, based on literacy and graduation rates from
schools and colleges, the UK is second only to South Korea, while Finland,
Singapore, Hong Kong, South Korea and Japan were ranked highly in the
cognitive ability category based on international tests in maths, reading
and science."

Hapa inaonyesha kuwa nchi zinazoongoza kwa wanafunzi wake kuwa na
utambuzi, ufahamu, na ujuzi zote hazitumii Kiingereza kama lugha ya
kufundishia bali lugha zao. Uingereza inaongoza kwa "kufuta ujinga" (kujua
kusoma na kuandika), na kuhitimisha wanafunzi. Jambo la kufurahisha hapa
ni kuwa elimu ya Uingereza inamwezesha tu mwanafunzi kujua kusoma na
kuandika na kuhakikisha kuwa anahitimu wakati Finland, Singapore, Hong
Kong, South Korea na Japansi zinamwezesha mwanafunzi kupata utambuzi,
ufahamu, na ujuzi. Je, lengo la elimu tangu enzi za akina Socrates na
Plato ni nini? Kujua kusoma na kuandika au utambuzi, ufahamu, na ujuzi?

Isitoshe, katika orodha ya nchi 20 bora kwa elimu, nchi zinazotumia
Kiingereza ni 5 tu (mbili kati ya hizo hazitumii Kiingereza pekee (New
Zealand - Kiingereza na Maori, na Canada - Kiingereza na Kifaransa).
Zaidi, hata hizi tano, zenyewe zimeanzia nafasi ya sita.

Ripoti hii ni ushahidi mwingine kuwa Kiingereza si sawa na maarifa. Na
wala elimu bora haipatikani kwa Kiingerza pekee bali kwa lugha yoyote
anayoimudu mwanafunzi na mwalimu. Ile hoja kuwa Kiingereza ni lugha ya
elimu, sayansi, na teknolojia imejibiwa hapa. Ukiangalia ripoti mbalimbali
za nchi zinazoongoza kwa uvumbuzi na ugunduzi wa kisayansi na teknolojia,
kwa mara nyingine tena, kati ya nchi 10 bora, zinazotumia Kiingereza ni
nne tu (Marekani - ya 2, Uingereza  - ya 7, Canada - ya 9, na Australia -
ya 10), zingine zote ni zile zinazotumia lugha tofauti na Kiingereza. Na
usishangae pia kuona kuwa nchi nne zilizojichomeka katika orodha hii,
zimeingia kutokana na nguvu zake za kisiasa, ukiongeza na uporaji wa
bongo.

Tuhusishe ripoti hii na mjadala wa lugha ya elimu nchini Tanzania.

Dunia Duru!


Chipila

 
Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>


From: godfrey moshi <moshiwiner@yahoo.com>
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Thursday, November 29, 2012 9:53 AM
Subject: Re: [Wanazuoni] MJADALA SASA UMENOGA

 
Daktari Aldin na wengine,

Mjadala kweli umenoga! Nimeufuatilia kwa muda, nikisoma hoja mbali mbali za wachangiaji mbali mbali. Ninafurahia kwamba wapo ambao kwa uchungu wanatamani maendelea ya nchi hii. Na wapo ambao wanaelewa vizuri sana taabu na huzuni inayompata mtoto wa kitanzania anayetoka shule ya msingi kuingia ya upili. Laiti (hasa hawa wanaojaribu kutazama kwa makengeza) wangebahatika kama mimi kuingia katika darasa la wanafunzi wa kidato cha kwanza wangeelewa huzuni ninayoizungumzia.

Kuna masikitiko makubwa, kwa mwanafunzi ambaye kwa miaka saba amefundishwa kwa kutumia kiswahili halafu ghafla anakutana na kugha ya kiingereza ikiwa ndiyo ya kufundishia! Unapoingia unaona wazi wazi huzuni na woga uliogubika nyuso zao. Ni wanafunzi wenye hofu kubwa, na mashaka mengi yakiwa nyusoni mwao, si kwa maarifa mapya, bali kwa sababu ya lugha inayotumika kuingiza hayo maarifa.

Mwisho naomba kueleweshwa, inasemekana kuna mkono wa mataifa makubwa (kama Uingereza) kuhakikisha hatutumii kiswahili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?


Moshi.


 
Bwana Yona, Matinyi na Dkt. Kitila

Pamoja na majibu yenu na kuendeleza mjadala, kuna mambo ambayo ningelipenda tushirikiane kuyaelewa.

Kwa maoni yangu bado kuna kuchanganya hoja. Naomba kurudia.
Hoja moja, ni: watu kuwa na uwezo wa kuongea, kuandika na kufikiri kwa Kiingereza.
Hoja ya pili, watu kutumia lugha fulani KUFUNDISHIA, au kutolea elimu.

Hoja hizi mbili, ingawa zinaukaribu si sawasawa.

Mimi ninasimamia ile hoja ya pili: lugha ya kufundishia.

Nianze kuziangalia hoja za Kitila na za Matinyi, kabla ya kugusia "kukunwa" anakokusema Yona.

Kuhusu gharama. Ni kweli, hakuna kitu chochote cha maana ambacho hakina gharama. Kitu kizuri ni lazima kiwe na gharama. Ila mbona watu wanasema kama kwamba TUMESHITUKIZWA?

Suala hili limo katika TUME ZOTE. Tume zoote ambazo zimelishughulikia kwa kulitafiti na kulitolea maandishi zimezungumzia suala la gharama na kulitolea majibu. Tangu mwaka 1971, ambayo sasa ni Taasisi ya Elimu ilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu. Ilianzishwa hapo pamoja na shughuli nyingine, kukabiliana na suala la gharama pale ambapo Tanzania ilikuwa imeamua kwa dhati kutafsiri vitabu vya sayansi toka Lugha za Kiingereza na Kifaransa kuingia ktk Kiswahili. Baadhi ya Maprofesa ambao sasa ni wastaafu hapa Chuo, waliletwa kuja kufanya kazi hiyo.
Ni kwanini leo tulizungumzie na kuzidi kuvuta miaka? Tukiogopa gharama leo, basi tuujaribu ujinga wa muda mrefu na kuona ni kipi cha gharama zaidi.

Pili, NA HII INA MAANA ZAIDI. Ngoja niwape UZOEFU WETU hapa Kiswahili.

Tangu mwaka 1964 kilipoanzishwa Kitivo cha Sayansi za Jamii, somo la Kiswahili lilikuwa likifundishwa chini ya Idara ya Lugha na Isimu ambayo lugha ya kufundishia ilikuwa Kiingereza. Hata hivyo, tangu mwaka 1970 ilipoanzishwa Idara ya Kiswahili UAMUZI ULITOLEWA kuwa lugha ya kufundishia iwe ni Kiswahili tu.

Ikumbukwe kuwa, katika Vyuo vingine mbalimbali, walimu wanafundisha Kiswahili KWA KIINGEREZA. Na hapa CKD, ulifanyika uamuzi kufundisha masomo YOTE kwa Kiswahili. Ngoja niwaeleze masomo hayo kwa kifupi.
Somo la Isimu (linguistics); Fonolojia, Mofolojia, Sintaksia, Semantiki n.k Yote haya YANA VITABU KATIKA KIINGEREZA, na sisi tunayafundisha kwa Kiswahili. Wanafunzi wanafanya marejeleo kwa Kiingereza. Wanasoma vitabu vya Kiingereza kwa Kiingereza, na wanafundishwa taaluma hizo kwa Kiswahili.

Mimi hufundisha masomo ya Fasihi na Falsafa. Vitabu vingi vimo katika lugha ya Kiingereza. Vitabu vya Nadharia za Fasihi (literary theories) vingi vimeandikwa kwa Kiingereza. Vitabu karibu vyote vya Falsafa na hasa somo la lazima la Falsafa ya Kiafrika, VIMEANDIKWA KWA KIINGEREZA. Na wanafunzi wetu wanavisoma, na tunaendelea kujadiliana kwa Kiswahili. WANAELEWA, WANAJADILIANA  na kuandika Mitihani kwa Kiswahili.

Ndivyo walivyofanya walimu wangu akina Prof. Kezilahabi, Prof. Senkoro, Prof. Mulokozi, Prof. Kahigi, Prof. Madumulla na wengine. Katika isimu, ndivyo wanavyofanya akina Prof. Khamis, Massamba, Mkude n.k.
WANAFUNZI WANAELEWA.

Kwa hiyo, kusema kuwa NI LAZIMA KUTAFSIRI VITABU VYOOOOOOTE vilivyo na maarifa ambayo mwanafunzi anayahitaji, na hivyo kusema kuwa ITAKUWA GHARAMA KUBWA - si sahihi sana.

Tunachohitaji, ni watu waelewe na kupata maarifa kupitia lugha inayowazunguka.
Tunachosema ni kuwa, mtu afundishwe vizuri Kiingereza, akifahamu na kujiamini, lakini isiwe lugha ya kumfundishia maarifa mengine.

Mwaka 1970, waliogopa gharama.
Mwaka 79, wakaogopa gharama, mwaka 1982 (Makweta) ilizungumziwa gharama, na leo bado watu wanajadili gharama.
Yona, hili si suala la ushabiki, ni suala la kuinusuru Jamii ili ipige hatua YA KUJIAMINI, KUJIKOMBOA. Jamii ya Wanasayansi iweze kuwa na akili ya ugunduzi, udadisi na ubunifu. Si ushabiki. Ni jambo lililofanyiwa utafiti na ni jambo la zamani sana.

Wakati tunaendelea kulumbana, kumbuka, Waingereza wanatoa fedha nyingi kukiendeleza Kiingereza na KUINUA UCHUMI. Mashirika ya Uchapishaji kama Oxford (University Press) , yanazidi kuimarika, wakati mashirika yetu (Dar es salaam University Press) yanaporomoka na kufa. TPH, ipo ICU, n.k

SUALA SI GHARAMA. Ni Utashi na Uamuzi wa Kisiasa. Suala si Utaalamu, kuwa Je tutaweza? Suala ni Utashi na Uamuzi wa Kisiasa. Mashirika haya, leo hii yangelikuwa mbali kibiashara ikiwa Uamuzi ungelitolewa miaka ya 70.

Leo hii, hizi hoja zisingelikuwapo.

HATA HIVYO, KINACHONIFURAHISHA NA KUNIFANYA NITEMBEE KIFUA MBELE, ni kuendelea na kuenea kwa Kiswahili kwa KASI SANA SEHEMU NYINGI ZA AFRIKA.
Niliwaeleza kuwa Juzi nilikuwa Brazzavile. Ni nani angelifikiria nchi kama hizo, za Kifaransa, zingeliweza kukumbatia na kuamua kukitumia Kiswahili? Ninaelekea Senegal, ambapo tajiri Mkubwa katika nchi hiyo ameamua kuanzisha Taasisi ya Lugha na Umajumui wa Kiafrika (Language and Panafricanism) na uamuzi ni kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa YA LAZIMA.

Kiswahili, kilithubutu, kimeweza, na sasa kinasonga mbele kwa kasi. Iwe Isiwe. Watake wasitake.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki Waswahili, Mungu ubariki Umoja na Umajumui wa Afrika
na utuletee mabadiliko Ewe Mola wetu.
Tujalie tuone maendeleo ya kweli ya nchi zetu.

Amina

Aldin
 
Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>


From: Yona Tumaini <ytm2001uk@yahoo.co.uk>
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
Sent: Wednesday, November 28, 2012 3:58 PM
Subject: Re: [Wanazuoni] Jibu la Profesa Senkoro kuhusu Madai ya Dastan Kweka na "Mjadala haunogi" ya Kitila

 
Dkt Kitila na Matinyi mmenikuna akili, mmenena ukweli tupu,Kwakweli Mubarikiwe sana, ni vyema ifikie mahali Watanzania tuwe wakweli na tusichambue mambo kiushabiki.
 
YOM
DSM

From: Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
To: Kitila Mkumbo <kitilam00@gmail.com>
Cc: Wanazuoni@yahoogroups.com; Prof. Senkoro Fikeni E.M.K <femk.coded@gmail.com>
Sent: Wednesday, 28 November 2012, 0:57
Subject: Re: [Wanazuoni] Jibu la Profesa Senkoro kuhusu Madai ya Dastan Kweka na "Mjadala haunogi" ya Kitila

Dkt. Kitila,

Hoja yako imetulia vema na kuna mahali tunakubaliana vizuri sana.
Nadhani uliona pale niliposema kwamba hofu yangu mimi ni hapo kwenye
hilo zoezi la kuhamisha maarifa yaliyohifadhiwa kwa kutumia lugha ya
Kiingereza na kuyaweka katika Kiswahili, achilia mbali watu wetu
kukimudu Kiswahili cha kisomi na vigugumizi vya kutaka kufananisha
Kiswahili na Kiingereza katika kila kitu ambayo mimi huita kwamba ni
ulimbukeni tu.

Kwenye mjadala huu huu kwenye jukwaa jingine nimedokeza pia kwamba
tatizo letu kubwa, ambalo ninaamini ndilo limetufikisha hapa kwenye
mjadala kama huu na kilio kikuu cha kitaifa kuhusu ubora wa elimu
yetu, ni kuanguka kwa hiyo elimu yetu tangu miaka ile ya 1970 jumlisha
na athari za sera zetu za elimu wakati wa Nyerere ambazo - pamoja na
mambo mengine - zilibana idadi ya wasomi wa juu katika taifa letu.

Hatimaye hadithi inaishia kwamba tuko katika hali ngumu mno kielimu
kiasi kwamba kuupanda mlima wowote ule, uwe wa Kiswahili ama
Kiingereza, ni balaa. Na pengine hapo ndipo penye umuhimu wa kupima
machungu yapi yana ahueni. Binafsi, sina imani na kiwango cha
Kiswahili cha hivi sasa nchini mwetu ambapo wahariri na wasomi
wanaandika makosa kutokana na ushabiki wa kuiga miundo ya Kiingereza
kijinga kabisa. Tuna shida kubwa sana lakini kwa vyovyote
itakavyokuwa, sioni mantiki ya mtu kusingiziwa kwamba ana mapenzi au
kasumba na ukoloni ama kuulaumu ukoloni wenyewe au kuugopa. Haya mambo
ya lugha yanajitegemea na ni kweli kwamba zipo nchi tunazopaswa
kuziiga, hata kama hatutakubaliana kubadili kitu ama tukiamua
kubadili, mathalani, Waskandinavia walivyomudu lugha zao au Waafrika
wenzetu na Waasia walivyomudu lugha za Kiingereza na hata Kifaransa na
sisi kuishia njiani.

Shida ipo, tena kubwa tu!

Matinyi.

On 11/27/12, Kitila Mkumbo <kitilam00@gmail.com> wrote:
> Nakushukuruni Ndugu Mutembei na Matinyi,
>
>
> Muhimu kabisa katika mjadala huu ni kutambua kwamba njia yeyote
> tutakayochagua ina gharama zake. Tukichagua Kiswahili kuwa ndio lugha ya
> kufundishia ni muhimu tukajua kwamba haitakuwa mteremko. Tutahitaji
> kuwekeza katika kuhakikisha kwamba watu wetu wanakijua Kiswahili cha
> kitaaluma sawasawa na kwamba kutakuwa na gharama ya kuandaa vifundishio na
> vifunzio kwa lugha hii. Gharama yenyewe ni fedha na muda. Tukiamua
> Kiingereza kiindelee tujue vilevile kwamba kuna gharama ya kuwekeza katika
> kujifunza Kiingereza kizuri. Kwa hiyo mtu makini ataenda zaidi ya utamaduni
> na kuangalia ipi ni njia rahisi zaidi: kuwekeza katika kukifanya Kiswahili
> kiwe lugha ya kufundishia kama nilivyoeleza hapo juu au katika kuwekeza ili
> vijana wetu wajue Kiingereza vizuri kwa kiwango cha wenzetu kama Kenya,
> Uganda n.k.
>
> Mimi ninachokataa ni mambo matatu katika mjadala huu. Kwanza ni hii tabia
> ambayo imeibuka sasa katika kujaribu kuhalalisha matumizi ya Kiswahili kwa
> sababu tu baadhi ya watu, hata kama ni wengi, wanaonekana kutokuijua hii
> lugha. Mantiki ya namna ya hii inataka tuamini kwamba watanzania
> hawafundishiki linapokuja swala la lugha ya Kiingereza, jambo ambalo si
> kweli. Pili, nakataa vilevile kwamba tukiamua kuanza kutumia Kiswahili
> itakuwa rahisi na tupo tayari sasa hivi; tukiamua leo kesho tunaanza
> kutumia. Ninachojua mimi katika yote haya mawili hakuna njia ya
> mkato-utahitajika uwekezaji wa muda na fedha. Bahati mbaya hatujafanya
> mahesabu ya kiuchumi, kimuda na kisaikolojia kujua ipi ni rahisi zaidi na
> itakayochukua muda mfupi zaidi. Tutahitaji tukokotoe hili pia ili tuwekana
> sawa kimantiki na kisayanisi, zaidi ya kiutamaduni. Tatu, natakataa mantiki
> rahisi inayotaka watu waamini kwamba matatizo yetu ya elimu kwa sasa
> yanatokana na kuendelea kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia.
> Wataalamu wa elimu wamewahi kuchambua mchango wa aina mbalimbali za sababu
> zinachangia wanafunzi wafeli kidato cha nne kwa mfano. Sababu nyingi
> zilichaguliwa ikiwemo lugha, idadi, ubora na utayari wa walimu, vifaa vya
> kufunzia na kujifunzia, n.k. Ukweli ni kwamba, kitakwimu, mchango wa lugha
> japokuwa ni muhimu haukuwa mkubwa vile (yaani not statistically
> significant). Kwa hiyo si sawa kukibebesha Kiingereza matatizo yote ya
> elimu nchini.
>
> Kuna tabia pia ya kujaribu kuhalalisha matumizi ya Kiswahili kwa kutumia
> mifano ya nchi za Ulaya kama Norway, Uholanzi, Uswidi pamoja na nchi za
> Asia kama Japan, Malaysia, Singapore, n.k. Bahati mbaya watu wanaotoa hii
> mifano hawataki kabisa kutumia mifano ya hapa kwetu Afrika. Hawatuwambii,
> kwa mfano, inakuwaje Afrika Kusini wana lugha rasmi 11,  watoto huanza
> shule ya msingi kwa kutumia lugha lugha mama, kini mara waanzapo sekondari
> wote hulazimika kujifunza kwa lugha ya Kiingereza au Ki-Afrikaansa na
> kuweza kumudu lugha hizi vizuri tu? Kwa nini wataalamu wetu wa lugha mifano
> yao yote ni ya ulaya, lakini hawatuambii kwa nini Ghana, Kenya, Botwana,
> Namibia. Zambia, n.k., wanaweza kujifunza Kiingereza lakini sisi hatuwezi?
> Ninaogopa sana kwamba kwa jinsi mjdala unavyokwenda itafika mahala kuna
> watu wataanza kuaminiswa kwamba tatizo letu la kutokojua Kiingereza ni la
> kinasibu (genes) na si swala la mazingira, jambo ambalo ni hatari.
>
> Watetezi wa matumizi ya lugha ya Kiswahili wamefanikiwa mambo mawili mpaka
> sasa ambayo naamini hayakuwa malengo yao, ambayo ni hasi. Mosi, Vijana
> wengi sasa wameanza kuamini kwamba hakuna shida hata usipojua Kiingereza
> madamu unajua lugha ya taifa ya Kiswahili, usiwe na wasiwasi. Pili, ni kama
> vile sasa tumeahirisha kujifunza Kiingereza (we have taken a moratorium in
> learning English) kwa sababu kwa nini tuhangaike wakati Kiingereza sio
> muhimu vile na hivi karibuni tutaanza kutumia Kiswahili chetu. Haya ni
> matokeo hasi ya mjadala ambayo naamini hakuna aliyeyatarajia.
>
> Kosa lingine kubwa ambalo tumelifanya katika kukiponda Kiingereza ni kuiona
> lugha hii kwamba ni ya kikoloni, kitumwa, sio yetu. Ukweli ni kwamba
> Kiingereza ni zaidi lugha ya kikoloni. Kila lugha inachimbuka lake, na
> 'bahati mbaya' kwamba kina chimbuko lake huko kwa wakoloni wetu, kama
> ambavyo kuna watu wanakihusisha Kiswahili na uarabu. Na kwa sasa viingereza
> kibao duniani, na ndio maana Mwalimu Nyerere akasema kwamba Kiingereza ni
> Kiswahili cha dunia. Na tusisahau wa kwanza kabisa kwamba ni mwalimu
> huyuhuyu tunayemsifia kwa mambo mengi mazuri aliyoyafanya katika kuendeleza
> elimu yetu aliyekataa kutekeleza pendekezo la Makweta la kuifanya lugha ya
> Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia.
>
> Kuna tatizo lingine la kimantiki. Kwamba sasa hatuwezi kufundisha
> Kiingereza vizuri likiwa somo la kujifunzia lakini tutaweza litakapokuwa
> somo tu moja kama lugha-'The fallacy of less makes more and more makes
> less!'. Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi unaotolewa unaonyesha hili
> jambo ndivyo linavyopaswa kuwa.
>
> Kwa hiyo, kwa maoni yangu, mjadala wetu ujikite katika sababu za kisayansi
> zaidi kuliko sababu za kitamaduni na kizalendo kwa sababu kutumia tu
> Kiswahili hakukufanyi uwe mzalendo zaidi. Mimi nadhani tunahitaji kuzijua
> lugha zote hizi mbili-Kiingereza na Kiswahili na inawezekana. Na katika
> kujadili lugha gani inafaa kufundishia tupanue mjadala zaidi ya options
> mbili zilizopo mezani kwa sasa-Kiswahili au Kiingereza. Tuongeze option
> ingine kwamba watu wakifika ngazi fulani wachague kutumia Kiingereza au
> Kiswahili. Hii pia ni option na kuna nchi wanafanya hivi. Wenzetu Rwanda
> waliamua juzijuzi kuachana na Kifaransa na kuamua kuwekeza kujifunza
> Kiingereza na kwa sasa ndio hivyo tena ndio lugha yao katika kufundishia na
> wanaimudu. Tunaweza kujifunza na tukazijua hizi lugha 'zetu' zote mbili.
> Muhimu ni kuacha woga, uvivu na kuzomeana pale ambapo moja wetu anakuwa
> hajui lugha hii. Kujaribu kuhalalisha matumizi ya Kiswahili kwa sababu watu
> wengi wanaoenekana kutokimuda hii lugha mimi naiona kama ni kurahisisha mno
> mambo na haina tija yeyote katika kukipeleka Kiswahili mbele! Na wala
> kukizomea Kiingereza kama lugha ya kikoloni hakusaidii sana katika kukikuza
> Kiswahili. Tuwekeze watu wetu wazijue lugha hizi mbili kwa ufasaha, na
> kisha wajue pia angalau kidogokidogo lugha zingine kubwa Afrika kama vile
> Kikuyu, Kusukuma, Kiyoruba, kiyao, Kiafrikansa,  n.k.
>
> Inahitaji moyo kutoa mawazo tofauti hadharani kati jambo hili kama vile
> kutetea ujamaa! Najua ninaibua kasheshe na sasa hivi nitaambiwa
> nimeathirika na utumwa, ukoloni, n.k.. But simplicity is the enemy of
> truth.
>
> Kitila
>
>
> 2012/11/27 Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
>
>> Dkt. Mutembei,
>> Nashukuru kwa hoja zako zinazojibu hoja ya mwanasaikolojia ya elimu,
>> Dkt. Kitila.
>>
>> Naomba kuongezea kidogo:
>> Madai kwamba wanaotetea Kiswahili wanafanya hivyo kwa sababu za
>> kizalendo ama kuupinga/kuuchukia ukoloni yanaweza kuangushwa chini
>> puuu na kipande hiki cha historia:
>>
>> Kiswahili kilipewa hadhi ya kutumika kama lugha ya kufundishia kwa
>> mara ya kwanza kwenye enzi za karne ya 19 baada ya Wajerumani
>> kukabidhiwa rasmi koloni la Tanganyika kufuatia zoezi lile la mgawo wa
>> bara letu. Walihitaji wafanyakazi wa daraja la chini serikalini, na
>> hivyo wakaamua kuanzisha elimu ya darasa la kwanza hadi la nne. Hatua
>> hii ilikuja baada ya kwanza kumchukua Mtanganyika mwenyeji wa Bagamoyo
>> na kumpeleka Ujerumani kuwafundisha Kiswahili maofisa wa Ujerumani
>> waliokuwa wanatarajia kuja Tanganyika kuendesha koloni hili tajiri.
>> Pili, walitegemea msaada mkubwa wa wamisionari waliokuwa wameshajikita
>> kwenye lugha za kienyeji huku Kiswahili kikitamba zaidi kutokana na
>> sababu mbalimbali.
>>
>> Hivyo basi, kama tunaiheshimu historia hii, itabidi tuwe wazi kwamba
>> hata kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni kuendekeza
>> ukoloni na kukosa uzalendo kwa sababu tutakuwa tunaendelea maamuzi ya
>> wakoloni wa Kijerumani. Ndiyo, ni kweli kwamba Waingereza walirejea
>> kwenye kukifanya Kiingereza kama lugha ya kufundishia, lakini sisi
>> tulipopata uhuru wetu tulifanya uamuzi sahihi wa kukichukua tena
>> Kiswahili. Ninaamini sababu haikuwa kuwaiga Wajerumani.
>>
>> Kwa kuwa hili haliwezekani, basi inabidi tupate sababu nyingine na
>> hiyo ndiyo itakayokuwa ya kweli, hata kama sababu za Mwalimu Nyerere
>> hazina uzito leo.
>>
>> Mimi nadhani hofu ya kweli ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya
>> kufundishia tangu mtoto akiwa tumboni mwa mamaye hadi anapomaliza
>> masomo ya baada ya shahada yake ya udaktari wa falsafa (kama atapenda
>> kufika huko), ni kwamba tutakabiliwa na kazi kubwa sana ya kuyabadili
>> maarifa yaliyohifadhiwa kwenye Kiingereza (katika vitabu na machapisho
>> mengine halisi na ya kwenye Intaneti), na pengine kazi hiyo
>> haitafanyika kwa ufasaha ama haitakamilika kwa muda unaotakiwa au
>> itakwama kabisa. Hofu hii ndiyo inaweza kutubana lakini suala la
>> kwamba elimu itaanguka si la kutolewa na mwanazuoni yeyote, ama
>> kusingizia siasa/itikadi/ukoloni/n.k. haitakuwa sahihi. Nadhani wote
>> tunajua kwamba kuanguka kwa elimu yetu hakuna uhusiano wowote na
>> Kiswahili; ni sera zetu mbovu na utendaji dhaifu.
>>
>> Sisi ni waoga na wazembe tu, labda na maskini pia.
>>
>> Matinyi.
>>
>> On 11/26/12, Aldin Mutembei <mutembei@yahoo.com> wrote:
>> > Kitila
>> >
>> > Sidhani kama umewatendea haki wale wanaojadili suala hili, na sina
>> > hakika
>> > kama umejitendea haki wewe mwenyewe. Ninakuachia fikra kuwa mjadala
>> "umedoda
>> > na haunogi..." hizo utazidadavua mwenyewe.
>> >
>> > Lakini, hili la kusema wanaotetea Kiswahili "...hoja yao imejikita
>> > katika
>> > utamaduni, uzalendo..." si haki hata kidogo.
>> >
>> > Kwanza, tunaotetea Kiswahili HATUNA HOJA MOJA kama ambavyo unadai. Ziko
>> hoja
>> > nyingi na anuai.
>> > Pili, hoja ya uzalendo ni ndogo sana ambayo ninadhani ndiyo inayolenga
>> > kuwaponda wale wanaotetea Kiingereza kuwa wanasumbuliwa na ukoloni.
>> > Tatu, sidhani kwamba wanaotetea Kiingereza, umewatendea haki. Hukusema
>> wao
>> > WANASIMAMIA NINI. Umesema tu kuwa wanaotetea Kiingereza "kiendelee
>> wanakuwa
>> > 'labelled' kama watu wanaoendeleza uzungu....". Wao hoja zao za kutaka
>> > Kiingereza kiendelee kuwa lugha ya kutolea elimu ni nini hujaeleza. Na
>> bila
>> > kusahau historia, mjadala wenye wizani hautakosa kugusia suala la
>> ukoloni,
>> > maana Wakoloni walikuja lugha ya Kiingereza kama njia ya kupitishia
>> > utamaduni, mila na desturi zao.
>> > Wale waliotawaliwa na Ufaransa wanaelewa zaidi maana ya mtawala kuleta
>> kwa
>> > mtawaliwa lugha yek. Haiishii hapo tu.
>> >
>> >
>> > Kwa hiyo, unatutazamisha mahali unapotaka tutazame, na kutuwekea pazia
>> pale
>> > usipotaka tuangalie.
>> >
>> > Mwishoni mwa barua yako unauliza swali.
>> >
>> >
>> > Nina uhakika, unajua kabisa kuwa ziko sababu NYINGI nyuma ya pazia
>> > uliloliweka. Fungua tu utaziona na kuzisikia.
>> > Karibu kwenye mjadala.
>> >
>> > Watu wanachanganya mada mbili ambazo zinakaribiana na labda
>> > kuingiliana.
>> >
>> > Moja ni Umuhimu wa Lugha ya Kiingereza duniani.
>> > Ya pili ni Lugha ya Kiswahili kama lugha ya kutolea elimu Tanzania
>> >
>> > Ningelitarajia wewe mwana saikolojia ya elimu, uende mbele hatua walau
>> > chache tu, utueleze kwa mfano:
>> > Mayasia wamepoteza nini walipoacha lugha ya Kiingereza kama lugha ya
>> > kufundishia na kuanza kufundishia Kimalay. Je, elimu ya watoto wao
>> > imeathirika, imeshuka? Au watoto wamefaidi na kukua kisaikolojia na
>> > kimaarifa kwa kutumia Kimalay? (sio uzalendo)
>> > Je kuna uvumbuzi, ugunduzi na kukua kwa udadisi wowote ambao jamii ya
>> > Kimalay inayotumia Kimalay darasani imekuwa nao kutokana na kutumia
>> > lugha
>> > WANAYOIELEWA au la? (sio suala la utamaduni hapa)
>> >
>> > Na je, Watoto wa Kimalay, wanafahamu Kiingereza kiasi gani leo
>> (walipoamua
>> > kutumia Kimalay shuleni) ikilinganishwa na miaka ile walipokuwa
>> > wakitumia
>> > Kiingereza kama lugha ya kufundishia shuleni kama sisi leo? Kiingereza
>> chao
>> > leo kimeshuka au kuongezeka au vipi?
>> >
>> > Badala ya Malaysia, unaweza pia kuweka Thailand  (walipoamua kutumia Ki
>> > Thai) au Taiwan (walipoamua kutumia Mandarin) Taiwan ilikuwa koloni la
>> Japan
>> > na wote waliongea Kijapan kwa miaka zaidi ya 50. Lakini tangu 1945,
>> baada ya
>> > Vita ya dunia, iliamuriwa KiMandarin.
>> >
>> >
>> > Nimetoka Brazzaville Juzi katika mkutano wa kuangalia maendeleo ya
>> Kiswahili
>> > na Kilingala kama lugha zinazovuka mipaka ya kijiografia ya nchi zaidi
>> > ya
>> > moja.
>> > Nimeshangaa sana tulipotembezwa katika Jumba la Makumbusho ya Brazza.
>> > Mle
>> > ndani kuna kaburi lake, la mkewe na watoto wake wanne. Mabaki ya miili
>> yao
>> > yalichimbuliwa huko Algiers na kuzikwa kwa heshima yote juzi tu mwaka
>> 2006
>> > terehe 30 Septemba.
>> >
>> > Sherehe kubwa ilikuwa kwa "Brazza, mfaransa aliyeivumbua Kongo".
>> (alizikwa
>> > mara TATU. alizikwa Ufaransa, Mwili ukafukuliwa. Akazikwa Algiers,
>> > mwili
>> > ukafukuliwa. Na sasa amezikwa "mjini kwake" Brazzavile, Kongo.
>> >
>> > Nikamwuliza mwenyeji wetu, je habari za Mfalme Makoko wa Abateke
>> > aliyetia
>> > saini na Brazza habari zake ziko wapi? Kaburi lake Mkongo huyo liko
>> > wapi?
>> > Majibu yanakuonesha jinsi Wafaransa walivyofanikiwa kumwondolea
>> > Mwafrika
>> > utu, kujithamini na heshima yake.
>> >
>> >
>> > Kwa hiyo, ningelikuwa naangalia madhara ya Kifaransa nchini Kongo,
>> > nisingelisita kutaja ukoloni, kasumba na ujinga wa mwafrika.
>> > Hayo, Dakta Kitila, hayakwepeki.
>> > Labda ni kutokana na hasira dhidi ya wakoloni, na hasa huzuni kwa
>> Waafrika
>> > ambao wametekwa bakunja kama hawa ndugu zangu wa Kongo, ndio kunafanya
>> watu
>> > kuongea hayo unayoyaona hayanogeshi mjadala.
>> >
>> > Aldin
>> >
>> >
>> > Aldin K. Mutembei  (PhD)                        Aldin Mutembei (PhD)
>> > Mkurugenzi                                                  Director
>> > Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili
>> > Studies
>> > Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                  University of Dar es
>> Salaam,
>> > TANZANIA
>> > +255 222 410 757    [Ofisini]                    +255 222 410757 (Day
>> > time-Office)
>> > +255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162
>> > (Cell)
>> > b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail:
>> > <kaimutembei@gmail.com>
>> >
>> >
>> >
>> >
>> >>________________________________
>> >> From: Kitila Mkumbo <kitilam00@gmail.com>
>> >>To: Wanazuoni@yahoogroups.com
>> >>Sent: Monday, November 26, 2012 7:12 PM
>> >>Subject: Re: [Wanazuoni] Jibu la Profesa Senkoro kuhusu Madai ya Dastan
>> >> Kweka
>> >>
>> >>
>> >>
>> >>Mjadala kuhusu lugha ya kufundishia umedoda na haunogi kwa sababu
>> >> upande
>> wa
>> >> wale wanaotetea Kiingereza kiindelee wanakuwa 'labelled' kama watu
>> >> wanaoendekeza uzungu, ukoloni, utumwa na kwamba si wazalendo. Wengi wa
>> >> watu wanaotetea matumizi ya Kiswahili hoja yao imejikita katika
>> utamaduni,
>> >> uzalendo na wanaamini kwamba kutumia Kiswahili ndio uzaleno wenyewe.
>> >> Kwa
>> >> hiyo hatupati mtiririko mzuri wa mawazo wa upande wa pili kwa sababu
>> >> wanaogopa kushambuliwa. Na hii ni shida ya mijadala ya Tanzania-group
>> >> think-every is supposed to think alike. Ukienda pembeni kidogo unakuwa
>> >> msaliti, huna uzalendo, umeathiriwa na uzungu, hujaelimika?
>> >>
>> >>But are there no good reasons for 'defending' Kiswahili beyond cultural
>> >> romanticism?
>> >>
>> >>Kitila
>> >>
>> >>
>> >>2012/11/24 Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
>> >>
>> >>
>> >>>
>> >>>
>> >>>
>> >>>----- Forwarded Message -----
>> >>>>From: FEMK Senkoro <femk.coded@gmail.com>
>> >>>>To: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>; wanabidii@googlegroups.com;
>> >>>> "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>Sent: Friday, November 23, 2012 7:46 PM
>> >>>>Subject: Re: Baba Chichi
>> >>>>
>> >>>>
>> >>>>Dastan Kweka,
>> >>>>
>> >>>>Labda tusahihishane ndugu yangu. Huyo Profesa ni mimi, na sikusahau
>> hata
>> >>>> neno moja la Kiswahili. Soma wasilisho langu vizuri. Wasilisho lote
>> >>>> nililitoa kwa Kiingereza, na hatimaye nikasema kuwa najicheka kwa
>> >>>> nini
>> >>>> nimewasilisha kwa lugha hiyo wakati Chachage aliamua kwa makusudi
>> >>>> kabisa, kuandika riwaya zake kwa lugha ya Kiswahili itakayowafikia
>> wote.
>> >>>> Na kama kweli ulikuwepo na uliielewa kejeli iliyokuwepo katika
>> sentensi
>> >>>> yangu ya mwisho nadhani usingeandika hivi. Labda itakuwa vizuri
>> >>>> ukizingatia umakini zaidi katika maoni yako.
>> >>>>
>> >>>>Mwalimu Senkoro.
>> >>>>
>> >>>>
>> >>>>2012/11/15 Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
>> >>>>
>> >>>>----- Forwarded Message -----
>> >>>>>>From: Dan Kweka <kwekad@yahoo.co.uk>
>> >>>>>>To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>>>Sent: Thursday, November 15, 2012 12:54 AM
>> >>>>>>Subject: Re: [Wanazuoni] Mizengo Pinda: Tusilaumiane Kuhusu Kutumia
>> >>>>>> Kiswahili: KUMWELEWA WAZIRI MKUU
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>Ukweli ni kuwa hata wale tunaokipigania kiswahili bado tuna
>> >>>>>> wasiwasi
>> >>>>>> nacho. Moyoni mwetu hatujakikubali.  Ni Mtanzania gani wa tabaka
>> >>>>>> la
>> >>>>>> kati ambaye anampika mwanae awe mahiri katika lugha ya kiswahili
>> kabla
>> >>>>>> ya lugha ya kiingereza? Katika nchi hii,kiswahili kina hadhi
>> >>>>>> katika
>> >>>>>> taasisi za umma tuu. Sekta binafsi(rasmi) inatawaliwa na lugha
>> >>>>>> nyingine.
>> >>>>>>
>> >>>>>>Ukoloni ulipanda fikra ya kubagua na kupuuza lugha za wazawa.
>> >>>>>> Athari
>> ya
>> >>>>>> fikra hizo kwetu iko wazi.  Profesa mmoja(jina kapuni) wa
>> >>>>>> kiswahili
>> >>>>>> hapo UDSM alikua anahutubia mhadhara wa kumbukumbu ya chachage
>> >>>>>> alafu
>> >>>>>> `akashindwa` kusema jambo fulani kwa  kiswahili maana msamiati
>> >>>>>> wake
>> >>>>>> ulikuwa mbali,lakini akalikumbuka kwa kiingereza. Kisha
>> >>>>>> akajicheka.
>> >>>>>> Huyu ni nguli wa kiswahili.
>> >>>>>>
>> >>>>>>Dastan
>> >  Kweka
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>________________________________
>> >>>>>> From: Yona Tumaini <ytm2001uk@yahoo.co.uk>
>> >>>>>>To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>>>Sent: Thursday, 15 November 2012, 7:53
>> >>>>>>Subject: Re: [Wanazuoni] Mizengo Pinda: Tusilaumiane Kuhusu Kutumia
>> >>>>>> Kiswahili: KUMWELEWA WAZIRI MKUU
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>Mutembei Pamoja na taaluma mtanzania alionayo, ni vyema taaluma
>> >>>>>> kama
>> >>>>>> taaluma iambatane na Lugha ya wote. Unaweza kuwa na Taaluma yako
>> nzuri
>> >>>>>> lakini kama lugha ya wote huijui, ni kazi bure, ni vyema urudi
>> >>>>>> shule
>> >>>>>> ukajifunze lugha ya wote ili uendane na wakati. Swali kubwa ni
>> >>>>>> hili,
>> >>>>>> ninaomba kuwa uliza kwanini mnawapeleka watoto wenu wakasome shule
>> >>>>>> zinazofundisha Lugha ya wote? Kwanini msiwapeleke kwenye shule
>> >>>>>> zetu
>> za
>> >>>>>> kawaida ili wakajifunze kiswahili zaidi?
>> >>>>>>
>> >>>>>>YOM
>> >>>>>>DSM
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>From: Aldin Mutembei <mutembei@yahoo.com>
>> >>>>>>To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>>>Sent: Wednesday, 14 November 2012, 16:44
>> >>>>>>Subject: [Wanazuoni] Mizengo Pinda: Tusilaumiane Kuhusu Kutumia
>> >>>>>> Kiswahili: KUMWELEWA WAZIRI MKUU
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>Yona Unaajiriwa katika hayo makampuni ili ukaoneshe uwezo wako
>> >>>>>> kuhusu
>> >>>>>> lugha ya Kiingereza au utaalamu wako? Ikiwa unatarajia kupata
>> >>>>>> ajira
>> >>>>>> kutokana na umahiri wako wa lugha ya Kiingereza, basi rudi shule
>> upate
>> >>>>>> elimu. Ikiwa hukumwelewa vizuri Waziri Mkuu anachosisitiza ni
>> >>>>>> upatikanaji wa Maarifa na Elimu. Sio lugha kwa sababu ya lugha tu.
>> Na
>> >>>>>> ndicho kilio chetu. Kama hukumwelewa Waziri Mkuu, rudi shule,
>> ukapate
>> >>>>>> elimu. Ikiwa una Kiswahili kizuri, na kichwani hamna kitu, ni kazi
>> >>>>>> bure!! Na, ikiwa una Kiingereza kizuri, na kichwani hamna kitu,
>> >>>>>> huna
>> >>>>>> maarifa; unakwenda kujiaibisha mwenyewe katika hiyo ajira; na
>> >>>>>> hakika
>> >>>>>> utafukuzwa, ukae unazunguka mitaani na hiyo "lugha yako ya
>> kitaalamu"
>> >>>>>> Kwa ushauri mdogo tu.  Aldin
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>Aldin K. Mutembei  (PhD)                        Aldin Mutembei
>> >>>>>> (PhD)Mkurugenzi
>> >>>>>> DirectorTaasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute
>> of
>> >>>>>> Kiswahili StudiesChuo Kikuu cha Dar es Salaam
>> >>>>>> University of Dar es Salaam, TANZANIA+255 222 410 757
>> >>>>>> [Ofisini]
>> >>>>>>                    +255 222 410757 (Day time-Office)+255 715 426
>> >>>>>> 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162
>> >>>>>> (Cell)b-pepe:
>> >>>>>> kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail:
>> >>>>>> <kaimutembei@gmail.com>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>From: Yona Tumaini <ytm2001uk@yahoo.co.uk>
>> >>>>>>>To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>>>>Sent: Wednesday, November 14, 2012 12:44 PM
>> >>>>>>>Subject: Re: [Wanazuoni] Mizengo Pinda: Tusilaumiane Kuhusu
>> >>>>>>> Kutumia
>> >>>>>>> Kiswahili
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>Lugha ya kiswahili ni chanzo za kutufanya asilimia kubwa ya
>> watanzania
>> >>>>>>> tukose ajira kwenye makampuni ya kigeni. Wenzetu wanatumia lugha
>> >>>>>>> ya
>> >>>>>>> wote (English) sisi tuna ng'ang'ania kiswahili, je tutegemee
>> >>>>>>> kupata
>> >>>>>>> ajira hapo kweli?
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>YOM
>> >>>>>>>DSM
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>From: Dan Kweka <kwekad@yahoo.co.uk>
>> >>>>>>>To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>>>>Sent: Tuesday, 13 November 2012, 20:45
>> >>>>>>>Subject: Re: [Wanazuoni] Mizengo Pinda: Tusilaumiane Kuhusu
>> >>>>>>> Kutumia
>> >>>>>>> Kiswahili
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>Karibia kila mara ninaposoma hoja mbalimbali katika mjadala
>> >>>>>>> unaohusu
>> >>>>>>> matumizi ya kiswahili na jinsi serikali na  taasisi mbalimbali
>> >>>>>>> zikiwemo za elimu ya juu zinavyoshughulikia swala hili,hoja ya
>> >>>>>>> `umiliki` wa lugha ya kiswahili na jinsi umiliki huo
>> unavyotufaidisha
>> >>>>>>> linajitokeza.
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>Kwani hata wakenya wakijinoa na kufundisha kiswahili duniani kote
>> >>>>>>> ndiyo lugha ya kiswahili itakuwa yao? Kwani kiswahili ni milki ya
>> >>>>>>> nani? Leo hii kiingereza kinatumika dunia nzima na hata wapo
>> >>>>>>> waliodiriki kukiita `lugha ya wote`/isiyo na mwenyewe. Lakini
>> >>>>>>> mbali
>> >>>>>>> na kingereza kidogo ninachokifahamu,sioni fahari yoyote ya
>> kuhusishwa
>> >>>>>>> na lugha hiyo. Ina wenyewe. Anayedhani haina,awaulize
>> >>>>>>> wajerumani,waswedish,waitaliano n.k.
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>Ingawa ni muhumu kwa sisi kama Taifa kujihusisha na kuwa mstari wa
>> >>>>>>> mbele katika juhudi za kueneza lugha hii,kuenezwa kwake na watu
>> >>>>>>> wengine hakutufanyi tupoteze umiliki. Tunawahofia wakenya kwenye
>> >>>>>>> utalii na mlima(Kilimanjaro) ni wa kwetu,bado sasa tunawalaumu
>> kuhusu
>> >>>>>>> kiswahili wakati  kina wenyewe?
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>Dastan Kweka
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
>> >>>>>>>To: Wanazuoni - Informal Network of Tanzanian Intellectuals
>> >>>>>>> <wanazuoni@yahoogroups.com>
>> >>>>>>>Sent: Tuesday, 13 November 2012, 15:00
>> >>>>>>>Subject: [Wanazuoni] Mizengo Pinda: Tusilaumiane Kuhusu Kutumia
>> >>>>>>> Kiswahili
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>
>> >>>>>>>> Subject:[UDADISI: Rethinking in Action] Mizengo Pinda:
>> Tusilaumiane
>> >>>>>>>> Kuhusu Kiswahili
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>IV UENDELEZAJI WA LUGHA YA KISWAHILI
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>22. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu wa Bunge,
>> > Waheshimiwa Wabunge walipokea na kujadili pamoja na mambo mengine
>> Maazimio
>> > mbalimbali. Niruhusu nirejee Azimio lililonigusa sana kuhusu Uanzishaji
>> wa
>> > Kamisheni ya Lugha ya Kiswahili. Awali, Baraza la Kiswahili Tanzania
>> > (BAKITA), Chama cha Kiswahili Tanzania (CHAKITA) na Wawakilishi kutoka
>> > Uganda
>> > walianzisha wazo la kuwa na Mpango wa Kuundwa kwa Baraza la Kiswahili
>> > la
>> > Afrika Mashariki. Hata hivyo, Baraza hilo
>> > halikuanzishwa, badala yake ikapendekezwa kuanzisha Kamisheni ya Lugha
>> > ya
>> > Kiswahili. Azimio la Kuanzishwa kwa Kamisheni hiyo ya Lugha ya
>> > Kiswahili
>> > tumelipitisha katika Bunge hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana
>> > Waheshimiwa
>> > Wabunge kwa michango yao mizuri sana mliyoitoa.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>23. Mheshimiwa Spika, wakati wa mjadala kuhusu
>> > kuanzishwa kwa Kamisheni hiyo, michango mingi ya Waheshimiwa Wabunge
>> > imeonesha
>> > umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kwa Tanzania kuwa Dira, Mfano na
>> > Kitovu
>> > cha
>> > Lugha ya Kiswahili. Aidha, Waheshimiwa Wabunge walionesha umuhimu wa
>> > kutumia
>> > Kiswahili kama nguzo imara ya Mshikamano, Amani na Utulivu miongoni mwa
>> > Watanzania. Lakini pia majadiliano yamebaini Changamoto zilizopo.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Moja ya Changamoto hizo ni hoja ya Waheshimiwa Wabunge wengi
>> > kwamba, Nchi jirani ya Kenya inatumia fursa zilizopo za Lugha ya
>> Kiswahili
>> > vizuri zaidi kuliko sisi. Kutokana na uzito wa hoja hiyo, ndiyo maana
>> > ninapenda
>> > nami niseme machache.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>24. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni Mdau Mkuu wa
>> > Matumizi ya Kiswahili katika Afrika. Ziko taarifa kwamba Watanzania
>> > ndiyo
>> > walioanzisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Ghana, Chuo Kikuu cha Port
>> > Harcourt, Nigeria na Chuo Kikuu wa Sebha, Libya. Inawezekana upo ukweli
>> pia
>> > kwamba leo hii wengi walioko katika Vyuo hivyo ni kutoka Kenya. Japo
>> imekuwa
>> > vigumu
>> > kupata takwimu za Ajira ya Walimu wanaofundisha katika Nchi hizo
>> > kutokana
>> > na
>> > kwamba ajira iko katika Soko Huria. Hakuna Chombo maalum kinachoratibu
>> Ajira
>> > za
>> > Walimu hao kwenye Vyuo Vikuu. Nina hakika hii ni moja ya sababu
>> zilizofanya
>> > Wachangiaji wengi kutumia "Uzoefu" zaidi katika kujenga hoja hiyo
>> > kwamba
>> > Walimu wengi wanatoka Kenya. Wakati sasa umefika wa kuwa na Utaratibu
>> Maalum
>> > wa
>> > upatikanaji wa Walimu wa Kiswahili wenye sifa za kufundisha Nje ya
>> > Nchi.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>25. Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wameainisha
>> > mapungufu mbalimbali ambayo yanachangia katika tofauti iliyopo kati
>> > yetu
>> na
>> > jirani zetu wa Kenya. Pamoja na mapungufu hayo, bado Tanzania imekuwa
>> > Kitovu
>> > cha Lugha ya Kiswahili Duniani. Walimu wa Kiswahili Nchini Ujerumani,
>> > Hamburg,
>> > Berlin, Colon, Leipzig na Chuo cha INALCO Ufaransa, walifundishwa na
>> Walimu
>> > kutoka Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) Zanzibar na
>> Chuo
>> > Kikuu cha Dar es Salaam. Mwalimu wa Siku Nyingi wa Kiswahili katika
>> > Chuo
>> > Kikuu
>> > cha London (School of Oriental African Studies - SOAS) anatoka
>> > Tanzania,
>> > Prof. Farouk Topan ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa Kwanza wa Idara ya
>> > Kiswahili,
>> > Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Walimu wa Kiswahili hadi sasa kule Korea,
>> > katika
>> > Chuo Kikuu cha Hankuk wanatoka Tanzania. Walimu wa Osaka, Japan
>> > walitoka
>> > Tanzania, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Zanzibar.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>26. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, yapo mahitaji
>> > makubwa ya Lugha ya Kiswahili kwa sasa. Katika Afrika ya Mashariki peke
>> > yake,
>> > Uganda wanahitaji Walimu zaidi ya 10 kwa ajili ya Vyuo vyao Vikuu.
>> > Vilevile,
>> > wanataka Walimu katika Shule za Sekondari. Rwanda na Burundi wanahitaji
>> > Walimu
>> > na Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) wanahitaji Walimu kwa ajili ya Vyuo
>> vyao
>> > vya
>> > Lubumbashi na Kalemie. DRC wanahitaji pia Vitabu vya Kiswahili Sanifu.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>27. Mheshimiwa Spika, mahitaji ya Kiswahili yako
>> > katika Nchi nyingi. Chuo Kikuu cha Kwazulu, Natali, Afrika ya Kusini
>> > kimeanzisha masomo ya BA Kiswahili, hivyo, watahitaji Walimu. Chuo
>> > Kikuu
>> > cha Zimbabwe kinahitaji Walimu wa Kiswahili. Namibia wameomba Walimu
>> > kuanzisha
>> > Kiswahili katika Chuo chao Kikuu. Jamaica Wanahitaji Walimu wa
>> > kuanzisha
>> > masomo
>> > ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha West Indies. Baadhi ya Vyuo Vikuu
>> > vya
>> > Marekani kikiwemo Chuo Kikuu cha Lugha cha Monterey, California
>> wanahitaji
>> > Walimu wa Kiswahili. Hapa Nchini Vyuo Vikuu zaidi ya 20 kando ya Chuo
>> Kikuu
>> > cha
>> > Dar es Salaam vimeanzisha Masomo ya Kiswahili na vitahitaji Walimu
>> > wenye
>> > Shahada za Uzamili na Uzamivu katika Kiswahili. Hivyo, mahitaji ni
>> makubwa
>> > kupita kiasi na hivyo hii ni fursa kubwa kwa Watanzania wenye sifa
>> > kujipatia
>> > ajira.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>28. Mheshimiwa Spika, tarehe 30 Desemba 2005,
>> > Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
>> > Tanzania
>> > akifungua rasmi Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema
>> > na
>> > nanukuu:
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>"Lugha ya Kiswahili imeanza kupata umaarufu Afrika na
>> > Duniani. Umoja wa Afrika umekubali Kiswahili kuwa moja ya Lugha zake
>> > Kuu.
>> > Aidha, Nchi za Kanda ya Maziwa Makuu zimekubali kutumia na kuendeleza
>> > Kiswahili. Serikali ya Awamu ya Nne itahakikisha kuwa juhudi hizi
>> > zinaendelezwa
>> > na kuhakikisha kuwa Lugha ya Kiswahili inakua Nje ya Mipaka ya Afrika".
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Mwisho wa Kunukuu.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>29. Kwa maneno haya ya Mheshimiwa Rais, ni dhahiri kwamba,
>> > Serikali inajali umuhimu wa kuendeleza Lugha ya Kiswahili, kwa vile ina
>> > nafasi
>> > nzuri ya kupanuka na kushiriki katika ujenzi wa Jamii ya Watanzania na
>> > Jamii
>> > mpya ya Afrika ya Mashariki na hata Duniani kote.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>30. Mheshimiwa Spika, tunayo Changamoto ya kukifanya
>> > Kiswahili kiwe Lugha ya Dunia. Lakini pia tunalo jukumu la kuhakikisha
>> > kwamba
>> > Lugha ya Kiswahili inafundishwa na kutumika Mashuleni, ikiwa ni pamoja
>> > na
>> > Shule
>> > za Msingi, na kwamba inafundishwa katika Shule za Sekondari na Vyuo vya
>> > Elimu
>> > ya Juu. Aidha, tunahitaji kuhakikisha kwamba Lugha ya Kiswahili
>> > inatumika
>> > vizuri na kwa ufasaha katika Shughuli za Serikali, hapa Bungeni, katika
>> > Mahakamani na maeneo mengine kwa faida ya Wananchi wetu na Taifa kwa
>> > ujumla.
>> > Hata hivyo, pamoja na msisitizo huo, yapo maeneo ambayo tunahitaji
>> > kuyafanyia
>> > kazi zaidi. Kwa mfano:
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Moja: Bado kuna maeneo mengi yanayohusu Taaluma ya Kiswahili
>> >>>>>>>> ambayo
>> > hayajafanyiwa utafiti wa lugha. Utafiti ndio uhai wa Taaluma na
>> > chimbuko
>> la
>> > maarifa mapya. Ni kazi ya Wanataaluma wa Kiswahili kufanya tafiti za
>> > kina
>> > ambazo zitakifanya Kiswahili kitumiwe Kimataifa.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Pili: Vyuo Vikuu vilivyoanzishwa, pamoja na kuweza kufundisha
>> >>>>>>>> somo
>> >>>>>>>> la
>> > Kiswahili kwa Wanachuo wa Shahada ya Kwanza, bado havina Wahadhiri wa
>> > kutosha
>> > wa kufundisha mafunzo ya Uzamili na Uzamivu. Tunalo jukumu la Kuanzisha
>> > Programu za Shahada za Uzamili na Uzamivu zitakazokidhi mahitaji
>> > makubwa
>> ya
>> > uhaba wa Wataalamu wa Kiswahili Ndani na Nje ya Nchi.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Tatu: Hapa Nchini hakuna Chuo Kikuu kinachotoa mafunzo ya
>> Ukalimani.
>> >>>>>>>> Watu
>> > wanaohitaji stadi hii ya ukalimani wanalazimika kwenda kusomea katika
>> Vyuo
>> > Vikuu vya Nje ya Afrika Mashariki. Mimi najiuliza, hivi hili nalo
>> > tunalikubali
>> > wakati Lugha ni yetu? Ninaamini tunao uwezo wa kutumia Vyuo Vikuu na
>> > Vyuo
>> > vingine tulivyonavyo kufanya kazi hii ya kufundisha Wakalimani. Ni
>> > vizuri
>> > Vyuo
>> > vyetu Nchini vianzishe Idara za Mafunzo ya Ukalimani ili kupunguza
>> > tatizo
>> > hilo.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Nne: Imebainika pia kwamba, hata kama kukiwepo na Wakalimani,
>> >>>>>>>> bado
>> >>>>>>>> hakuna
>> > Kumbi za kisasa zenye vifaa vya kusikilizia Tafsiri za Lugha
>> > mbalimbali.
>> > Kumbi
>> > nyingi tunazofanyia Mikutano tukiacha Ukumbi wa Kimataifa wa Arusha
>> (AICC)
>> > hazina Vifaa hivyo. Changamoto tulio nayo kama Nchi na hasa Wawekezaji
>> > wa
>> > Kumbi
>> > za Mikutano ni kuhakikisha Kumbi zinazojengwa na zilizopo zinakuwa na
>> Vifaa
>> > vya
>> > kutoa huduma ya Ukalimani. Lengo ni kutumia fursa hiyo katika kukuza
>> Lugha
>> > yetu
>> > ya Kiswahili.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>31. Mheshimiwa Spika, mimi napata shida sana kuona
>> > Warsha yenye Wageni wasiozidi Kumi (10) na Waswahili 200 inaendeshwa
>> > kwa lugha ya Kiingereza, tena bila kujali kama Waswahili hao wanaelewa
>> > Kiingereza au la. Wanachojali ni kuwafurahisha Wageni wachache. Kwa
>> > maoni
>> > yangu hii ni kasumba isiyo na maelezo. Changamoto iliyo mbele yetu ni
>> > kuondoa
>> > kasumba hii kwa kupenda kutumia lugha yetu ya Kiswahili wakati wote.
>> > Tuondoe
>> > wasiwasi katika matumizi ya Lugha ya Kiswahili. Tumeshuhudia Kiswahili
>> > kikikuzwa na kutandazwa katika Mifumo ya Kompyuta ya Linux na
>> > Microsoft.
>> > Tumesikia pia kwamba, kama njia mojawapo ya kuboresha matumizi ya
>> Kiswahili
>> > sanifu, tayari Wataalamu wa lugha kwa kushirikiana na Wataalamu wa
>> Kompyuta
>> > wameweza kutengeneza Programu Maalum ya Kisahihishi cha Lugha ya
>> Kiswahili
>> > katika Kompyuta ambayo inatumiwa kusahihisha maneno ya Kiswahili. Haya
>> > ni
>> > maendeleo makubwa yaliyofikiwa ya kukiingiza Kiswahili katika
>> > Teknolojia
>> ya
>> > Habari na Mawasiliano Duniani.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>32. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba Lugha ya
>> > Kiswahili imekua sana. Wote ni mashahidi kwamba Mashirika makubwa ya
>> > Utangazaji
>> > Duniani yanatangaza Kiswahili. Tunajua sana Shirika la Utangazaji la
>> > Uingereza
>> > (BBC), Sauti ya America, Radio ya Ujerumani Deutsche -Well na Radio
>> France
>> > International. Wako pia Al Jazeera, Radio Vatican, Radio Japan na Radio
>> ya
>> > Umoja wa Mataifa. Aidha ziko Nchi zenye Vituo vya Radio vinavyotangaza
>> kwa
>> > lugha ya Kiswahili, kwa mfano, China, India, Syria, Misri, Sudan n.k.
>> > Hii
>> > pia
>> > ni ishara kwamba Kiswahili kinakua kwa kasi sana.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>33. Mheshimiwa Spika, tunaweza kuongea mengi ya
>> > nadharia kuhusu lugha yetu nzuri ya Kiswahili kwa muda mrefu.
>> > Tunatakiwa
>> > sasa
>> > tuanze kutekeleza hayo mengi kwa vitendo. Naomba kuhimiza Taasisi
>> > mbalimbali
>> > Nchini, ziweke juhudi zote katika kukuza Lugha ya Kiswahili ili iweze
>> > kutumika
>> > katika Nyanja zote za mawasiliano ikiwemo Sayansi na Teknolojia.
>> Vilevile,
>> > natoa Rai kwa Watanzania wote wakiwemo Waheshimiwa Wabunge kujitahidi
>> kila
>> > tunapozungumza Kiswahili kuepuka kuchanganya na maneno ya Lugha ya
>> > Kiingereza
>> > kwenye mazungumzo yetu.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>34. Baadhi yetu tunamkumbuka Mwandishi na Mshairi wa Riwaya
>> > Bwana Shaban Robert (1909 – 1962) ambaye aliandika kuhusu Lugha ya
>> Kiswahili
>> > na
>> > kukifananisha na ladha ya Titi la Mama. Katika moja ya Mashairi yake,
>> > aliandika
>> > na nanukuu:
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>"Titi la Mama litamu, hata likiwa la Mbwa, Kiswahili
>> > naazimu, sifayo iliyofumbwa, Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa,
>> > Toka
>> > kama
>> > mlizamu, funika palipozibwa, Titi la Mama litamu, jingine halishi hamu.
>> > Lugha
>> > yangu ya utoto, hata sasa nimekua, Tangu ulimi mzito, sasa kusema
>> > najua,
>> Ni
>> > sawa na manukato, moyoni mwangu na pua,Pori bahari na mto, napita
>> > nikitumia,
>> > Titi la Mama litamu, jingine halishi hamu".
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Mwisho wa Kunukuu.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>35. Anachosema Bwana Shaaban Robert ni kuonesha thamani ya
>> > Kiswahili jinsi kilivyo na utamu wa aina yake katika matumizi. Historia
>> ya
>> > Shaaban Robert, tunaambiwa alithubutu kulikataa kabila lake la Kiyao na
>> > kujiita
>> > Mswahili kuonesha jinsi alivyokipenda Kiswahili. Nasi tujivunie
>> Kiswahili,
>> > tukipende,
>> > tukitumie, tukienzi na tukithamini. Tukifanya hivyo, tutakuwa
>> > tumechangia
>> > katika kuendeleza Lugha ya Kiswahili.
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>36. Mheshimiwa
>> > Spika, Watanzania sasa si wakati wa kulalamikiana na kulaumiana juu ya
>> > Matumizi ya Lugha ya Kiswahili, bali sasa tushirikiane kujenga Lugha
>> > yetu
>> > ya
>> > Kiswahili. Njia iko wazi, nadhani sasa kazi kwetu!
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Hotuba:
>> >>>>>>>>
>> http://www.pmo.go.tz/docs/Hotuba_ya_Kufunga_Mkutano_wa_Tisa_wa_Bunge.pdf
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>
>> >>>>>>>>Picha:
>> >>>>>>>>
>> https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNi98kpKAxbvCfNBr8X3UG6VNm8vTFENi2YeqEk_pKTglfVoVjikRC95X5z-LEVFb9JnkENJ1-ghNxZq_xpstxpNDFPX9GGN1dseUe-XjCes2X0UdWklsa7CU8RneO4XJUmsa_3b6pBStQ/s640/Mizengo+Pinda.JPG
>> > --
>> > Posted By  Blogger  to UDADISI: Rethinking in Action at  11/13/2012
>> 02:36:00
>> > PM
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>>>
>> >>>>
>> >>>>
>> >>>>
>> >>
>> >>
>> >>
>> >>
>>
>


------------------------------------

Yahoo! Groups Links

<*> To visit your group on the web, go to:
    http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/

<*> Your email settings:
    Individual Email | Traditional

<*> To change settings online go to:
    http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/join
    (Yahoo! ID required)

<*> To change settings via email:
    Wanazuoni-digest@yahoogroups.com
    Wanazuoni-fullfeatured@yahoogroups.com

<*> To unsubscribe from this group, send an email to:
    Wanazuoni-unsubscribe@yahoogroups.com

<*> Your use of Yahoo! Groups is subject to:
    http://docs.yahoo.com/info/terms/







__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (17)
Recent Activity:
.

__,_._,___
...

[Message clipped]  


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment